Ayyuwb: Mfano Katika Imani Na Subira (Ustahimilivu)
Imetafsiriwa na Ukht Haliymah ‘Abdullaah
Historia ya Ayyuwb (katika ujira) inawapa faraja wale wote ambao ni wagonjwa au walionyimwa mali au watoto.
Malaika walikuwa wanajadili hali ya binaadamu, utiifu na uasi wao. 
Mmoja wao akasema kwamba Ayyuwb ndio mbora wa watu ulimwenguni. Alikuwa Muumin mtiifu, daima akiswali kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Alimbariki kwa kuwa tajiri miaka themanini. Muda wote huu hakusahau kumuabudu au kumshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Alishirikiana katika utajiri wake na maskini na kuwavisha walio uchi.
Mmoja wao akasema kwamba Ayyuwb ndio mbora wa watu ulimwenguni. Alikuwa Muumin mtiifu, daima akiswali kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Alimbariki kwa kuwa tajiri miaka themanini. Muda wote huu hakusahau kumuabudu au kumshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Alishirikiana katika utajiri wake na maskini na kuwavisha walio uchi.
Shaytwaan
 hakuamini kwamba kuna mtumishi mkweli kama Ayyuwb. Shaytwaan alifikiri 
kwamba utajiri wake ndio sababu ya ukweli wake, kwa hiyo akamuomba 
Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kwa uwezo Wake amuondoshee Ayyuwb utajiri 
kwa nia mbaya ya kumpotosha. Allaah Akamuondoshea kumpima Nabii Wake.
Akaonyesha
 kutokana na upotevu huo kwa kusema utajiri ni wa Allaah (Subhaanahu wa 
Ta’ala) na namshukuru kwa Aliyoniruzuku na namshukuru kwa Aliyochukua. 
Akashuka chini kwa kusujudu. Hili lilimfanya Shaytwaan akasirike.
Shaytwaan
 alijaribu mara mbili kumpoteza Ayyuwb baada ya kukosa utajiri wake kwa 
kumuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kwa nguvu zake kumuondoshea 
watoto na afya. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Alisema nitakupa uwezo 
katika mwili wake, lakini nakutahadharisha kuifikia roho yake, ulimi, 
moyo, kwa sababu ndani yake inasema uongo kuhusu Imaan ya kweli. Ayyuwb 
akaonyesha mwenendo alioufuata wakati alipochukuliwa utajiri wake.
Shaytwaan
 aligundua kwamba hawezi kumpoteza Ayyuwb, hivyo alimwendea mkewe 
kumpoteza (kumdanganya), kwa kumkumbusha maisha yao ya zamani (ya 
utajiri). Shaytwaan alifanikiwa katika kumdanganya mkewe. Hilo 
lilimpelekea kumlalamikia Ayyuwb kuhusu hali waliyo nayo sasa. Hili 
lilimfanya Ayyuwb kuapa kwamba atampiga viboko 100 ikiwa Allaah 
(Subhaanahu wa Ta’ala ) Atamrudishia afya yake.  
Shaytwaan
 hakufanikiwa katika kumpoteza Ayyuwb. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) 
Akarudishia vyote Alivyopoteza. Ikabakia kwa Ayyuwb sasa kutimiza kiapo 
chake cha kumpiga fimbo mkewe.
Allaah
 (Subhaanahu wa Ta’ala) Akamuagiza kumpiga mkewe kwa mara moja fimbo 100
 za mianzi, kwa Kumuonea huruma huyo mama. Kweli Allaah (Subhaanahu wa 
Ta’ala) ni mwingi wa rehema.
Kisa
 cha Ayyuwb kitakuwa daima ni ukumbusho kwetu sote. Inatakiwa tusome 
kisa hiki mara kwa mara kwa ajili ya kujikumbusha. Wengi wetu 
tunalalamika kwa kitu kidogo katika maisha. Allaah (Subhaanahu wa 
Ta’ala) Alimpa mtihani Ayyuwb kwa namna ambayo kweli inatakiwa 
tujihusishe nayo.
Imani
 yake na uvumilivu ni kitu ambacho kama sisi ni Waumini wa Kiislamu wa 
kweli tujaribu na kutekeleza katika maisha yetu, wakati Akitupa mtihani 
katika hali hizi. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) katika Qur-aan:
“…Bila shaka tulimkuta ni mwenye subira, mja mwema, kwa hakika alikuwa mnyenyekevu sana.” Swaad: 44
Wakati huu ni lazima tumkumbuke Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) zaidi, kufanya ibaada kwa bidii, na kuwa wenye kushukuru sana badala ya kutoridhika na hali zetu. Inabidi Tumtukuze na Tumshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kwa kila hali Atakayotupa majaribio. Kama tunavyojua huu ni wakati ambao Shaytwaan anajaribu kuchezea akili zetu, hisia, na udhaifu wetu. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Hawezi kusahau kamwe kumlipa mwenye kumtumikia kwa hiyo kazi kubwa.
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Na (Mtaje) Ayyuwb alipomwita Mola wake (akasema) Mimi imenipata dhara Nawe Ndiye Unayerehemu kuliko wote wanaorehemu.
“Basi
 tukamkubalia (wito wake) na tukamuondolea dhara aliyokuwa nayo, na 
tukampa watu wake na mfano wao pamoja nao. Ni rehma inayotoka Kwetu, na 
ukumbusho (mzuri) kwa wafanyao ibaada) Al-Anbiyaa: 83-84. 
Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Atupe imaan na uvumilivu wakati wa mitihani, Aamiyn.
No comments:
Post a Comment