Kufanya Zinaa Na Kumuoa Mwanamke Aliyeshika Mimba
SWALI:
Assalaam aleikum,
Baada ya salam na kumshukuru Mwenyezimungu kwa rehma zake na Mtume 
wetu mohammad ninapenda kutowa shukran zangu za dhati kwa waendeshaji wa
 tovuti hii ya AL HIDAAYA,kwa kazi hii tukufu munayoifanya kuelemisha 
ummah. Allah wataala ndiye ataokulipeni ujira wenu.Halafu tafadhali napenda kuuliza ikiwa mwanamme na mwanamke wamefanya zinaa na wanataka kuowana. Huyo mwanamke anahitajika kushufu kipindi cha kusubiri kusafisha tumbo lake la uzazi kabla ya huyo mwanamme kumuowa? Jee ikiwa ana mimba? Anaweza kumuowa wakati yupo katika mimba na kumwita huyo mtoto wake mwenyewe?
Ndugi zangu suali hili ni muhimu sana kwangu kwa hiyo Inshallah nategemeya majibu karibu kutoka kwenu.
Shukran
JIBU:
Sifa
 zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)  Aliyetukuka Mola 
Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume
 (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya 
Allahu 'anhum jamiy'an) na watangu wema mpaka Siku ya Qiyaamah. 
Kwanza
 tunapenda na sisi kutoa shukurani kwa du'aa zenu nzuri mnazotuombea 
nyote mnaotuma maswali yenu pamoja na wengineo wanaoingia ALHIDAAYA 
 kutafuta faida mbali mbali. Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)  
Atutakabalie hizo du'aa na Atuzidishie uwezo wa kuelimishana kwa kadiri 
Anavyotujaalia. Aamiyn
Shukran
 kwa muulizaji swali hili. Na inaonyesha kuwa mas-ala haya ya uasherati 
au mafungamano ya kimwili baina ya mume na mke yamekithiri. Inatakiwa 
tuwe ni wenye kumcha Allah (Subhaanahu
 wa Ta'ala) popote tulipo na kila wakati. Na kama ilivyo kawaida, sisi 
wanaadamu huwa tunakosea, hivyo tunapokosea au kufanya dhambi basi hapo 
hapo turudi kwa Allah (Subhaanahu
 wa Ta'ala) kwa kumuomba msamaha na kutubia toba ya kweli kweli. Na pia 
tufanye mambo mema ili yafute hayo mabaya ya madhambi.
Mwanzo inatakiwa tufahamu kuwa zinaa ni kitendo kibaya sana kilichokatazwa na Allah (Subhaanahu
 wa Ta'ala) na Mtume Wake (Swalla Llaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). 
Na yeyote mwenye kufanya amali hiyo basi angefaa apatiwe adhabu ya 
kisheria hapa. Adhabu yenyewe ni kama ifuatavyo:
Ikiwa
 ni mwanamume au mwanamke waliokuwa hawakuoa/kuolewa bado, na ni watu 
huru, wenye akili timamu, basi ni kupigwa mijeledi (bakora) mia na 
ishuhudiwe hiyo adhabu hadharani na kundi la watu. Kisha ni kuhamishwa 
mbali mwanamume ahame huo mji aliokuwa akiishi kwa muda wa mwaka mmoja. 
Ikiwa
 mwanamume na mwanamke waliozini au mmoja wao ni mtu huru (sio mtumwa), 
mwenye akili timamu, na amefanya zinaa wakati tayari yumo katika 
fungamano la ndoa, basi adhabu yake ni kupigwa mawe hadi mauti yawafike.
 
Dalili ya hayo ni Hadiyth ifuatayo: 
فِي
 الصَّحِيحَيْنِ مِنْ رِوَايَة الزُّهْرِيّ عَنْ عُبَيْد اللَّه بْن عَبْد 
اللَّه بْن عُتْبَة بْن مَسْعُود عَنْ أَبِي هُرَيْرَة وَزَيْد بْن خَالِد 
الْجُهَنِيّ فِي الْأَعْرَابِيَّيْنِ اللَّذَيْنِ أَتَيَا رَسُول اللَّه 
صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ أَحَدهمَا : يَا رَسُول اللَّه 
إِنَّ اِبْنِي هَذَا كَانَ عَسِيفًا - يَعْنِي أَجِيرًا - عَلَى هَذَا 
فَزَنَى بِامْرَأَتِهِ فَافْتَدَيْت اِبْنِي مِنْهُ بِمِائَةِ شَاة 
وَوَلِيدَة فَسَأَلْت أَهْل الْعِلْم فَأَخْبَرُونِي أَنَّ عَلَى اِبْنِي 
جَلْد مِائَة وَتَغْرِيب عَام وَأَنَّ عَلَى اِمْرَأَة هَذَا : الرَّجْم 
فَقَالَ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((وَاَلَّذِي 
نَفْسِي بِيَدِهِ لَأَقْضِيَنَّ بَيْنكُمَا بِكِتَابِ اللَّه تَعَالَى 
الْوَلِيدَة وَالْغَنَم رَدّ عَلَيْك وَعَلَى اِبْنك مِائَة جَلْدَة 
وَتَغْرِيب عَام . وَاغْدُ يَا أُنَيْس - لِرَجُلٍ مِنْ أَسْلَم - إِلَى 
اِمْرَأَة هَذَا فَإِنْ اِعْتَرَفَتْ فَارْجُمْهَا))  فَغَدَا عَلَيْهَا 
فَاعْتَرَفَتْ فَرَجَمَهَا      البخاري  و مسلم 
Katika
 Swahihayn kutoka  kwa Abu Hurayrah na Zayd bin Khaalid Al-Juhani 
(Radhiya Allahu 'anhum) katika  kisa cha Mabedui wawili waliokuja kwa 
Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa  sallam).  Mmoja alisema: "Ewe
 Mjume wa Allaah, mwanangu (wa kiume) aliajiriwa na  bwana huyu kisha 
akafanya zinaa na mke wake. Nimemlipa fidia kwa ajili ya  mwanangu kwa 
kumpa kondoo mia moja na mtumwa mwanamke. Lakini nilipowauliza watu  
wenye elimu, wamesema kwamba mwanangu apigwe mijeledi mia na ahamishwe 
mji kwa  muda wa mwaka na mke wa huyu bwana apigwe mawe hadi afariki".  
Mtume (Swalla  Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Naapa kwa
 Yule Ambaye nafsi  yangu imo Mikononi Mwake, nitahukumu baina yenu 
wawili kutokana na kitabu cha  Allaah. Rudisha mtumwa mwanamke na 
kondoo  na mwanao apigwe bakora mia kisha  mwanao ahamishwe mbali kwa 
muda wa mwaka. Nenda Ewe Unays! )) Alimwambia mtu  katika kabila la 
Aslam, ((Nenda kwa mke wa huyu bwana na akikiri makosa yake,  basi mpige
 mawe hadi mauti [yamfike])) Unays akamuendea na akakiri makosa yake,  
kwa hiyo akampiga mawe hadi mauti. [Al-Bukhaariy na Muslim]
قال
 الإمام مالك أن عمر، رضي الله عنه، قام فحمد الله وأثنى عليه، ثم قال: أما
 بعد، أيها الناس، فإن الله بعث محمدًا بالحق، وأنـزل عليه الكتاب، فكان 
فيما أنـزل عليه آية الرجم، فقرأناها وَوَعَيْناها، وَرَجمَ رسول الله صلى 
الله عليه وسلم وَرَجمْنا بعده، فأخشى أن يطول بالناس زمان أن يقول قائل: 
لا نجد آية الرجم في كتاب الله، فيضلوا بترك فريضة قد أنـزلها الله، فالرجم
 في كتاب الله حق على من زنى، إذا أحصن، من الرجال والنساء، إذا قامت 
البينة، أو الحبل، أو الاعتراف. (  الموطأ و البخاري و مسلم   )
Imaam
 Maalik amerikodi kwamba 'Umar (Radhiya Allahu 'anhu) alisimama na 
kumsifu na kumtukuza Allah, kisha akasema: "Enyi watu! Allah Amemtuma 
Muhammad (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa haki na 
Amemfunulia Kitabu Chake. Jambo moja alilofunuliwa ni Aayah ya kupigwa 
mawe hadi mauti ambayo tumeisoma na kuifahamu. Mjumbe wa Allaah 
(Subhaanahu wa Ta'ala) ameitimiza adhabu hii ya kupigwa mawe na baada 
yake pia sisi tumeitimiza. Lakini nakhofu kuwa muda (miaka) utakapopita 
wengine watakuja kusema kuwa hawakuiona hii Aayah ya kupigwa mawe katika
 Kitabu cha Allah, na watapotoka kwa sababu ya kuacha moja ya wajibu wa 
kisheria iliyofunuliwa katika Kitabu cha Allah kwa mwanamume au mwanamke
 watakaofanya zinaa, ikiwa mmojawapo ameoa au ameolewa, na ushahidi 
ukipatikana au mimba ikidhihirika kutokana   na kitendo hicho, au 
akikiri mmojawao. [Al-Muwattwaa, Al-Bukhaariy na Muslim]  
Hivyo
 tunaona jinsi gani adhabu kali ilivyoweka hukumu yake katika jambo hili
 ovu la zinaa, na lau ingelikuwa hukumu hii inatekelezwa katika dola za 
Kiislamu au kwa kila Muislamu anayetenda kitendo hiki, basi hakika 
hakuna mtu yeyote angelithubutu kutenda kitendo hiki kiovu kabisa. Ni 
jambo la kusitisha sana kuona kitendo hiki hakichukuliwi kuwa ni dhambi 
kubwa ambayo adhabu yake ni kali kama hiyo. Mara kwa mara tunapata 
maswali kama haya, na mara kwa mara tunasikia kitendo hiki kutendekea 
katika Jamii yetu na Jamii nyingine pia hadi tumefika kuwa kama makafiri
 wanaoishi kama wanyama na kuingiliana bila ya khofu yoyote. 
Lakini
 kwa kuwa hakuna dola ya Kiislamu kwa wakati huu na nchi nyingi 
tunazoishi si za Kiislamu wala Waislamu wengi, anatakiwa mkosa afanye 
toba ya sawasawa pamoja na kufanya mema mengi kadri ya uwezo wake. 
Jambo hili Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Amelikanya na kutuonya hata tusilikaribie kabisa: 
((وَلاَ تَقْرَبُواْ الزِّنَى إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَسَاء سَبِيلاً)) 
((Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya)) [Al-Israa:32] 
Ikiwa watu hao wawili wamefanya zinaa wanaweza
 kuoana kisheria baada ya kutenganishwa kwa muda. Muda huu ni wa 
kuhakikisha kuwa yule mwanamke hana mimba. Muda unaweza kuanzia miezi 
mitatu au kutegemea uamuzi wa Qadhi ikiwa katika sehemu hiyo yupo mmoja.
 Na ikiwa mwanamke ana mimba basi hawatafaa kuoana mpaka yule mwanamke 
azae kwa sababu Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) 
amekataza kumwaga mbegu za uzazi juu ya mbegu nyingine kama ilivyo 
katika Hadiyth ifuatayo: 
 ((لا يحل لامرئ يؤمن بالله واليوم الآخر أن يسقي ماءه زرع غيره)) ابن حبان  
((Haimpasi mtu mwenye kumuamini Allah na Siku ya Mwisho amwage maji (ya uzazi) juu ya mbegu aliyootesha mwingine)) [Ibn Hibbaan] 
Kwa
 hiyo baada ya kuzaa ndio wanaweza kuoana baada ya wote kufanya toba ya 
kweli kabisa. Na huu ndio msimamo sahihi (Wa Allahu A'alam) kulinganisha
 na ule wa wale wanaokataza wasioane hata baada ya toba. Matokeo yake 
watu wanaendelea kufanya zinaa maadam wamependana na hawawezi kuwa 
mbali.
Ifahamike
 kuwa yule mtoto hatokuwa wa baba yule na hawatariathiana kisheria baina
 yao. Baba hatarithi anachoacha mtoto, wala mtoto kutoka kwa baba.  
Na Allah Anajua zaidi
No comments:
Post a Comment