Ukumbusho Wa Kukithirisha Swawm Mwezi Wa Muharram Na Swawm Za Ayyaamul-Biydhw
Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:  
Pia, tunapenda kuwakumbusha swawm za Ayyaamul-Biydhw (masiku meupe) ambayo ni tarehe 13, 14, 15 katika kila mwezi wa Kiislaam (Hijriyyah). Masiku hayo mwezi huu wa Muharram 1438H, yataangukia tarehe 14, 15, 16 Oktoba (Ijumaa, Jumamosi, Jumapili).
Bonyeza: 'Endelea' upate faida nyenginezo.
((أَفْضَلُ الصِّيَامِ بَعْدَ رَمَضَانَ شَهْرُ اللَّهِ الْمُحَرَّمُ)) رواه مسلم 
Swiyaam (funga) bora kabisa baada ya Ramadhwaan ni swawm ya mwezi wa Allaah wa Muharram [Muslim]Pia, tunapenda kuwakumbusha swawm za Ayyaamul-Biydhw (masiku meupe) ambayo ni tarehe 13, 14, 15 katika kila mwezi wa Kiislaam (Hijriyyah). Masiku hayo mwezi huu wa Muharram 1438H, yataangukia tarehe 14, 15, 16 Oktoba (Ijumaa, Jumamosi, Jumapili).
عَنْ
 أَبي ذَرٍّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ 
عَلَيهِ وَسَلَّمَ:((مَنْ صَامَ مِنْ كُلِّ شَهْرٍ ثَلاثَةَ أَيَّامٍ 
فَذَلِكَ صِيَامُ الدَّهْرِ)) فَأَنْزَلَ اللهُ تُصْدِيقَ ذَلِكَ في 
كِتَابِهِ الْكَرِيمِ: ((مَنْ جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا))، الْيَوْمُ بِعَشَرَةِ أَيّامٍ. أخرجه أحمد والترمذي وقال حديث حسن ، والنسائي وابن ماجه وابن خزيمة 
Imepokelewa
 kutoka kwa Abu Dharr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah 
Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam amesema: ((Yeyote atakaye 
swawm kila mwezi siku tatu, ni sawa na swawm ya milele)) Kisha Allaah 
Akateremsha Aayah ithibitishayo hayo: “Atakayekuja kwa amali nzuri basi atapata (thawabu) kumi mfano wa hiyo.”  Siku moja kwa malipo ya siku kumi.
 [Imepokewa na At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Hasan, An Nasaaiy na Ibn 
Maajah, Ibn Khuzaymah na ameisahihisha Shaykh Al-Albaaniy katika 
Al-Irwaa (4/102)]. Aayah: Suwrat Al-An’aam (160)]Bonyeza: 'Endelea' upate faida nyenginezo.
» 
Nasiha Za Wiki
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ --- Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! 23- Sihri (Uchawi) Na Michezo Ya Mazingaombwe
Neno
 “As-Sihr” (uchawi) maana yake ni kitendo cha kujikurubisha na shaytwaan
 na kwa msaada wake (shaytwaan) na uchawi ni kulibadilisha jambo mbali 
na uhakika wake, nako ni kuwadhihirishia watu jambo lisilo la kweli 
wakaliona kuwa ni la kweli.” [Lisaan Al-‘Arab]
Na Sihri ni tendo la kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa kuwa linahusiana na shaytwaan 'aaswi mwenye kumkufuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
Pia, sihri ni miongoni mwa Al-Kabaair (madhambi makubwa) na ni miongoni mwa ambayo yanamuangamiza mtu kwa dalili ya Hadiyth:
Na Sihri ni tendo la kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa kuwa linahusiana na shaytwaan 'aaswi mwenye kumkufuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
وَاتَّبَعُوا
 مَا تَتْلُو الشَّيَاطِينُ عَلَىٰ مُلْكِ سُلَيْمَانَ ۖ وَمَا كَفَرَ 
سُلَيْمَانُ وَلَـٰكِنَّ الشَّيَاطِينَ كَفَرُوا يُعَلِّمُونَ النَّاسَ 
السِّحْرَ وَمَا أُنزِلَ عَلَى الْمَلَكَيْنِ بِبَابِلَ هَارُوتَ 
وَمَارُوتَ ۚ وَمَا يُعَلِّمَانِ مِنْ أَحَدٍ حَتَّىٰ يَقُولَا إِنَّمَا 
نَحْنُ فِتْنَةٌ فَلَا تَكْفُرْ ۖ فَيَتَعَلَّمُونَ مِنْهُمَا مَا 
يُفَرِّقُونَ بِهِ بَيْنَ الْمَرْءِ وَزَوْجِهِ ۚ وَمَا هُم بِضَارِّينَ 
بِهِ مِنْ أَحَدٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ وَيَتَعَلَّمُونَ مَا 
يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ ۚ وَلَقَدْ عَلِمُوا لَمَنِ اشْتَرَاهُ مَا 
لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِنْ خَلَاقٍ ۚ وَلَبِئْسَ مَا شَرَوْا بِهِ 
أَنفُسَهُمْ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿١٠٢﴾
Na wakafuata 
yale waliyoyasoma mashaytwaan juu ya ufalme wa Sulaymaan; na Sulaymaan 
hakukufuru lakini mashaytwaan ndio waliokufuru; wanafundisha watu sihri 
na yaliyoteremshwa kwa Malaika wawili katika (mji wa) Baabil; Haaruwt na
 Maaruwt. Nao wawili hawamfundishi yeyote mpaka waseme: “Hakika sisi ni 
mtihani, basi usikufuru.” Kisha wakajifunza kutoka kwa hao wawili yenye 
kupelekea kufarikisha kwayo baina ya mtu na mkewe. Na wao hawawezi kamwe
 kumdhuru yeyote kwayo isipokuwa kwa idhini ya Allaah; na wanajifunza 
yanayowadhuru na wala hayawanufaishi; na kwa yakini walijua kwamba 
atakayeinunua (sihiri) hatopata katika Aakhirah fungu lolote, na ni 
ubaya ulioje walichouzia kwayo nafsi zao, lau wangelikuwa wanajua. [Al-Baqarah: 102]Pia, sihri ni miongoni mwa Al-Kabaair (madhambi makubwa) na ni miongoni mwa ambayo yanamuangamiza mtu kwa dalili ya Hadiyth:
No comments:
Post a Comment