Kuna Dalili Yoyote Katika Qur-aan au Sunnah Kuhusu Global Warming?
SWALI
Assalaam aleykum.
Baada
 ya salam naomba kuuliza kuwa “Global warming” imetajwa katika Qur-an 
tukufu au japo katika hadithi za Mtume Salla Llaahu alayh wa sallam? 
Nahisi ni moja kati ya dalili za kiama, je ni kweli?
Natanguliza shukrani zangu, jazaakumullaahu khair.
JIBU:
Sifa
 zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote,
 Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu
 ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu Global warming.
 Global warming ni ile hali ya dunia kupata joto na uharara wa juu zaidi
 kuliko ilivyokuwa hapo awali. Sababu kubwa ni matumizi makubwa ya vifaa
 vya petroli, ongezeko la viwanda ambavyo vinajaza uchafu wa moshi 
angani na matumizi ya magari na ongezeko lake. Uchafu unaotokana na 
vifaa hivyo na vinginevyo vinasababisha kulika lile tabaka la Ozoni 
(Ozone layer – O3).
 Na kwa sababu hiyo ulimwengu leo unapata uharara mwingi zaidi kuliko 
awali kwani tabaka ambalo lilikuwa linachuja miale ya jua haitekelezi 
jambo hilo kwa njia nzuri kwa kulika tabaka hilo.
Allaah Aliyetukuka Anatueleza: 
“Je!
 Hawakuona kwamba Tunaifikia ardhi Tukiipunguza nchani mwake? Na Allaah 
huhukumu, na hapana wa kupinga hukumu yake, naye ni Mwepesi wa kuhisabu” (13: 41). 
Na pia, 
“Bali
 tuliwastarehesha hawa na baba zao mpaka umri ukawa mrefu kwao. Je, 
hawaoni ya kwamba Sisi tunaifikia ardhi tukiipunguza ncha zake? Basi je!
 Hao ni wenye kushinda?” (21: 44).
Aayah hizo mbili tulizonukuu hapo juu ni dalili ya global warming. Na kwa ajili hiyo ndio kukaribia Qiyaama.
 
No comments:
Post a Comment