TAQABBALA ALLAAHU MINNAA WA MINKUM - FAIDA MBALIMBALI ZA RAMADHWAAN
Assalaamu 'alaykum wa RahmatuLLaahi wa Barakaatuh, 
ALHIDAAYA
 inawaombea Ramadhwaan ya kheri na Baraka nyingi, mchume thawabu tele, 
Swawm zikubaliwe, dhambi zighufuriwe, na Allaah Atutakabalie 'amali 
zetu.  
Tusiache kuwaombea du’aa ndugu zetu Waislam popote
 walipo ulimwenguni walio katika dhiki za ukandamizwaji, vita, njaa na 
machafuko. Na pia tukumbukane kwa du’aa kwani Mtume Swalla-Allaahu 
alayhi wa aalihi wa sallam amesema katika Hadiyth kutoka kwa Ummu Dardaa
 Radhwiya-Allaahu ‘anhaa: ((Atakayemuombea ndugu yake kwa siri Malaika aliyewakilishwa kwake husema: “Aamiyn nawe pia upate mfano wake)) (wa kama unayomuombea) [Muslim]  
Kwa
 Munaasabah wa mwezi mtukufu wa Ramadhwaan, Alhidaaya imewaekea 
tayari mafundisho mbalimbali yenye manufaa katika kuongeza elimu na 
kuimarisha 'ibaadah zenu ili muweze kuchuma mema mengi na muweze kufikia
 kuipata taqwaa ambayo ndio lengo kuu la Swawm. 
No comments:
Post a Comment