SIFA TANO ZA MKE MWEMA..
Je, Mtume swalla llahu alleh wasalaaam ametufunfundisha nini kuhusu sifa njema za wake?
1-Ni watiifu kuwa waume zao: Abu Huraira alipokea kutoka kwa Mtume
swalla llahu alleh wasalaaam kwamba alisema: “Mke bora ni yule ambaye
ukimuangalia anakupendeza, ukimuarisha jambo anakutii na unapokuwa
haupo, analinda hadhi na mali yako.” [Ibn Jarir]
Amesema Allah
“…basi wanawake wema ni wale wenye kutii, wanaojifadhi wasipokuwapo
waume zao kwa kuwa Allah amewaamrisha wajifadhi.” [An-Nisaa: 34]
2- Wanazistitiri miili yao: Amesema Allah: “Ewe Mtume! Waambie wake zako, binti zako na wanawake wa Kiislamu wajiteremshie uzuri nguo zao. Kufanya hivyo kutapeleka upesi wajulikane kuwa ni watu wa heshima ili wasiudhiwe. Na Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu.” [Azhaab: 59]"
3-Hawaombi talaka bila sababu ya kisheria: Amesema Mtume swalla llahu alleh wasalam: “Mke yeyote atakayemuomba mumewe talaka pasina sababu ya kisheria, ataharamishwa pepo hata harufu ya pepo hatoisikia.” [Tirmidhi]
4-Wanasimamisha Swalaah: Amesema Mtume swalla llahu alleh wasalaaam: “Mwanamke akiswali swalah tano, akafunga saumu, akailinda tupu yake na kumtii mumewe, ataambiwa, ‘ingia peponi kwa mlango wowote uupendao.” [Imaam Ahmad]
5- Hawawakasirikii waume zao bure: Asema Mtume swalla llahu alleh wasalaaam: “Laana ya Allah iko juu ya mwanamke anaemkasirikia mumewe bila sababu,"