Mjumbe wa Kamati ya Mawasiliano Hizb-ut Tahrir Afrika Mashariki Sheikh Mussa Kileo karibuni alikutana na gazeti la ‘Kisiwa’ linalotolewa na Waislamu na kuchapishwa kila wiki. Ziara hiyo ililenga mambo mawili makubwa: Moja, ni kutoa nasaha kwa gazeti hilo juu ya taarifa, ya moja ya gazeti lao la karibuni ukurasa wa mbele iliyohusiana na Hadd (adhabu) ya mzinifu. Katika kichwa cha habari cha gazeti hilo kilionesha kimakosa kwamba adhabu ya mzinifu ni kupigwa bastola. Gazeti hilo lilikiri kukosea, na kwa mujibu wa mhariri wa gazeti hilo walikusudia kuweka alama ya kuuliza mbele ya kichwa hicho cha habari lakini walisahau. Dhamira ya pili ya ujumbe huo ni ziara za kawaida kwa Hizb ut Tahrir Afrika Mashariki kuwazuru na kuwatembelea ndugu zetu Waislamu na taasisi mbalimbali za Kiislamu na kubadilishana nao mawazo juu ya dini yetu tukufu. ****************************************************************************
Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki inalaani
vikali kitendo cha polisi cha kumuua kijana Idris Mohammed mwenye
umri wa miaka 26 Muhammed nyumbani kwao Bondeni Mo kwa tuhuma za
ugaidi! Baada ya mauaji haya mkuu wa CID,Ndegwa Muhoro akasema kuwa
serikali itafunga baadhi ya Misikiti kama hatua ya ‘kukabiliana na
ugaidi’. Tungependa kuifafanua hali hii kama ifuatavyo:-
Ukatili na unyama wa kikosi cha polisi
ambacho jukumu sio lake sio kuvuruga usalama bali ni kulinda
usalama. Kwa masikitiko makubwa katika dhidi ya ‘ugaidi’ polisi bila
hata amri ya mahkama huvamia watu majumbani tena wakiwa usingizini na
kuwapiga risasi watuhumiwa hata wanapojisalimisha! Mauaji haya
ambayo yamekuwa yakifanywa kila mara tayari yameacha majumba mengi ya
Waislamu kubakia pasina na vijana ambao ndio nguzo kubwa kwa wazazi
wao.
Cha kuzidisha mchanga maji serikali inanuia kufunga baadhi ya misikiti eti kuwa inatoa mafunzo ya ugaidi! Je hatua hiyo haigongani na katiba ya Kenya na hata hiyo iitwayo Demokrasia kuwa inalinda majumba ‘uhuru wa kuabudu’ . Hii ni dhulma nyengine kubwa inayofichua kuwa katiba za nchi za kidemokrasia pia hukiukwa kwenye vita dhidi ya Waislamu. Na ni nani dhalimu Mkubwa kuliko Yule anayezuia misikiti ya MwenyeziMungu kwamba humo lisitajwe jina la MwenyeziMungu na akajitahidi kuiharibu? [Baqara: 114]
Mateso haya dhidi ya Waislamu wa Kenya ni natija ya kanuni ‘Prevention of Terrorism Bill Act 2102’ iliopitishwa tena mbele ya wabunge wa Kiislamu mwezi Oktoba mwaka 2012. Na Hizb yauliza je haya ndio maslahi ya Waislamu ambayo ‘ulamaa’ wanaopigia debe demokrasia na chaguzi zake kwa hoja ya kutetea maslahi ? Twasema kuwa ugaidi ni mmoja katika kampeni hatari inayotumiwa na Marekani kushambulia Uislamu na Waislamu. Hivyo si kweli kuwa Uislamu unahatarisha usalama bali sera mbovu za Ubepari ndio chanzo cha utovu wa usalama kote duniani na haya yako wazi kwa kila mwenye macho na masikio moyo wa kufahamu.
Mwisho sisi twaamini kuwa Uislamu una hoja nzito zinazoweza kujieleza na kutawala maishani tena pasina kutumia matendo ya kinguvu na mabavu. Na hii ndio njia ya kweli na ya kisheria ambayo sisi tunajifunga hadi pale Mola atakapotunusuru kwa nusra yake na nusra yake iko karibu inshallah.
Cha kuzidisha mchanga maji serikali inanuia kufunga baadhi ya misikiti eti kuwa inatoa mafunzo ya ugaidi! Je hatua hiyo haigongani na katiba ya Kenya na hata hiyo iitwayo Demokrasia kuwa inalinda majumba ‘uhuru wa kuabudu’ . Hii ni dhulma nyengine kubwa inayofichua kuwa katiba za nchi za kidemokrasia pia hukiukwa kwenye vita dhidi ya Waislamu. Na ni nani dhalimu Mkubwa kuliko Yule anayezuia misikiti ya MwenyeziMungu kwamba humo lisitajwe jina la MwenyeziMungu na akajitahidi kuiharibu? [Baqara: 114]
Mateso haya dhidi ya Waislamu wa Kenya ni natija ya kanuni ‘Prevention of Terrorism Bill Act 2102’ iliopitishwa tena mbele ya wabunge wa Kiislamu mwezi Oktoba mwaka 2012. Na Hizb yauliza je haya ndio maslahi ya Waislamu ambayo ‘ulamaa’ wanaopigia debe demokrasia na chaguzi zake kwa hoja ya kutetea maslahi ? Twasema kuwa ugaidi ni mmoja katika kampeni hatari inayotumiwa na Marekani kushambulia Uislamu na Waislamu. Hivyo si kweli kuwa Uislamu unahatarisha usalama bali sera mbovu za Ubepari ndio chanzo cha utovu wa usalama kote duniani na haya yako wazi kwa kila mwenye macho na masikio moyo wa kufahamu.
Mwisho sisi twaamini kuwa Uislamu una hoja nzito zinazoweza kujieleza na kutawala maishani tena pasina kutumia matendo ya kinguvu na mabavu. Na hii ndio njia ya kweli na ya kisheria ambayo sisi tunajifunga hadi pale Mola atakapotunusuru kwa nusra yake na nusra yake iko karibu inshallah.
KUMB: 23 / 1435 AH Jumatano, 22nd Dhul Qiddah 1435 AH 17/09/2014 CE
Shabani MwalimuMwakilishi kwa Vyombo Vya Habari Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki*****************************************************************************
Kama tulivyoonyesha katika sehemu ya
pili ya makala yetu mgawiko wa hadithi kuegemea idadi ya wapokezi,
tuangalie katika sehemu hii ya mwisho kugawika kwa hadithi kwa kimsingi
wa kukubaliwa na kukataliwa.
Hadithi hugawika sampuli nne katika msingi huu nazo ni :-1-Sahihi (الصحيح)
2-Hasan (الحسن)
3-,Dhaifu (الضعيف)
4-Madhoo (الموضوع)
Hadithi Sahihi ni ile iliotimiza masharti yafuatayo:-
Kwanza: Kila mpokezi
wake ameipokea kwa kuichukua moja kwa moja kwa aliemsimulia na kuendelea
hivi hadi kufikia kwa Mtume SAAW. Hii ndio wasomi wa hadithi huita
itiswal Sanad اتصال السند
Pili: Wapokezi wawe ni
waadilifu na maana ya uadilifu hapa ni kuwa na uovu. Hii inamaanisha
kuwa Uislamu wake ni mzuri. Aidha mpokezi awe amebaleghe au kuvunja
uongo(Mwanamke) na awe ni mwenye maadili mema.
Tatu: Mpokezi asiwe na sifa ya kusahausahau na kutohifadhi maneno kwa uzuri.
Nne: Isiwe na kasoro
(illah) yoyote katika upande wa upokezi سند wala katika upande wa
maudhui (matn). Kwa mfano lau hadithi imepokelewa na mpokezi jina lake
Abdalla bin Diinar ambalo ndio jina lake hasa kisha jina hili
likabadilishwa na Amru bin Diinar tayari hii ni kasoro ya upokezi. Na
mfano wa upande wa Matn ni La kuelewa hapa ni kuwa wasomi wametaja kuwa
kasoro hizi yaani Isnad na Matn ziko zinazoweza kufanya hadithi isiwe
sahihi au pia bado iwe ni sahihi. Asema Ibn Swaleh : ‘Kasoro kwenye wapokezi zaweza zikaitia doa hadithi au kutoitia halkadhalika katika kasoro katika upande wa matn’. Kasoro hizi ni sharti zisiwe ni kwa wapokezi wote wa hadithi hiyo.
Masharti haya ndio hufanya hadithi
ikaitwa sahihi. Mfano wa hadithi sahih ni ile inayosimuliwa na swahaba
Jubair bin Mut’am kutoka kwa babake akisema nilimsikia Mtume SAAW
akisoma sura Tuur kwenye swala ya Maghribi.
سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم قرأ في المغرب با الطور
Wapokezi wote hadithi ni watu
wanaoaminika kuanzia swahaba hadi kwa aliekuja na hadithi naye ni
Abdallah Bin Yusuf huyu ni mkweli naye akaipata kutoka kwa Maalik ambaye
wanavyouni wanakubaliana kuwa Maalik ni Haafidh yaani mtu aliehifadhi
hadithi laki moja kisanad na kimatn na kuelewa hali zake. Maalik
akaipokea kutoka kwa Ibn Hisham huyu ni Faqiih alieipokea kwa Muhamad
ambaye ni thiqa mkweli ambaye naye aliipokea kwa swahaba Jubair Bin
Mut’am. Hata hivyo hivyo ni muhimu kuelewa kusihi kwa hadithi haina
maana kusihi kwake kidalili kwani yawezekana hadithi ni sahihi lakini
imefutwa mansoukh
Tuje katika hadithi Hasan. Hii ni ile
iliokosa moja wapo ya sharti ya hadithi sahihi tulizozitaja hapo juu.
Kwa mfano ikipatikana kuwa mmoja ya wapokezi wa hadithi alikuwa na sifa
ya kutodhibiti maneno au kuyahifadhi vizuri basi ndio
huitwa ‘hadith Hasan’ Hadithi hasan ni nyingi mno moja wapo ni ile
iliosimuliwa na Tirmidhiy kutoka kwa Abdillah bin Amru RA Kuwa mtume
SAAW alikataza kuimba mashairi misikitini na biashara ndani yake na
tahaluq (mazungumzo) kabla ya swala ya ijumaa. Hadithi hii ina mmoja
katika wapokezi wake ana kasoro katika kuhifadhi maneno.
-
أنَّ النبيَّ -صلَّى الله عليه وسلَّم- "نهى عن تناشُد الأشعار في المسجد،
وعن البيعِ والشراء فيه، وأنْ يتحلَّق الناس يوم الجمعة قبل الصلاة
Angalizo: Kuna baadhi
ya Masheikh wanaitolea ushahidi hadithi hii kuharamisha nasaha au bayana
zinazotolewa kwenye misikiti mingi kabla ya khutba na kuziita bida’a.
Twasema ushahidi huu una makosa katika kufahamu maana ya hadithi hii
kama pia kutoelewa tahqiq –l manat. Tamko la Tahaluq
hapa sio mawaidha bali ni vika vya kuzungumzia mambo ya kidunia. Kiasili
kuna dalili nyingi za kuhimiza watu kupeana nasaha na mawaidha na
dalili hizi sio khasa bali ni amma. Ama bayana na halaka za kielimu
hili linafaa halina utata kama vile sio mashairi yote yanayokatazwa
bali yale ya miito ya kijaahilia. Atwahaawi asema kuwa itakuwa makuru
kufanya tahaluq ikiwa kutapelekea kuharibu safu lakini ama kinyume chake
yafaa.
Ama hadithi Dhaif nayo ni ile iliokosa
masharti ya hasan. Kwa hivyo hadithi yoyote ilio na kasoro kwa wapokezi
wake wote na pia kwenye upande matn. Hata hivyo hadithi ili iitwe dhaif ni sharti kwamba hakuna Isnad yoyote ambayo haina kasoro. Inapokuja hadithi dhaifu
kwa riwaya tofauti tofauti au njia mbalimbali basi huangaliwa njia hizo
na huenda ikapanda daraja hadithi hiyo kuwa Hasan au sahii. Hii
inategemea kuwa njia hizi hakuna katika wapokezi wake waliotuhumia na
urongo au uovu. Lakini lau maana yaliyobebwa na hadithi dhaif yanapatikana kwa hadithi sahihi basi hufanyiwa kazi yale maana ya hadithi sahihi.
Ifahamike kuwa suala la kusahihisha
hadithi na kudhoofisha ni suala la ijthadi hivyo upo uwezekano wa
hadithi kudhoofishwa na mujtahidi na ikasahihishwa na mujtahidi
mwengine. Kwa hivyo sio kila mtu adandie suala hili kama atakavyo.
Kwa bahati mbaya ni leo mujtahiduna leo ni wachache mno hali
iliosababishwa na mitaala ya kielimu inayosimamiwa na serikali za
Kiilmaania wanaoajiri masheikh wenye kutunga fiqhi mpya ya Kiislamu.
Hali hii imefanya Waislamu wengi leo ni wafuasi tu bali vipofu wanaosoma
maneno ya masheikh au wanafunzi wao. Masheikh hao hawafichi tu haki
wamejitia uwezo wa kusahihisha na kudhoofisha sanad za baadhi ya
hadithi zinazosimuliwa na watu wanaotofautiana kirai. Kwa mfano Abu
Haatim Al-Raazi mwanachuoni wa madhhabu ya Hanbali alidhoofisha riwaya
anazosimulia Al-imam Bukhar kwa hoja kuwa ana msimamo juu ya kua Quran
inaposomwa basi yale matamshi ya msomaji huwa ni kiumbe.
Sheikh Fauzan alimdhoofisha Al baihaqiy
kwa kuwa alikuwa na msimamo wa kuzifanyia Taaweel sifa za Allah.
Kivyovyote vile tunakariri kuwa suala la kusahihisha na kudhoofisha
hadithi ni suala la Mujtahiiduna pekee.
Tumalize kwa kuingalia hadithi Maudhoo. Hii
ni hadithi iliotungwa na kutajwa kuwa imepokelewa kutoka kwa Mtume
SAAW. Nayo ni ima mtu kujitungia maneno au kuchukua maneno ya wenyehikma
kisha akayanasibisha kwa Mtume SAAW.
Mmoja ya watu mashuhuri katika kitendo hiki
cha kutunga hadithi ni Abu Ismah kisha akaeleza sababu yake ya kutunga
hadithi kuwa; ‘Nimeona watu wanaihama Quran (hawaisomi) na
kujishughulisha zaidi na Fiqhi ya Abu Hanifa ,Maghaazi na Muhammad bin
Ishaq nami nikatunga hadithi..)
Kuna sababu kadhaa zilizochangia watu kutunga hadithi nazo ni kuutukana Uislamu na kunusuru madhhebu Fulani.
Angalizo Kuna baadhi ya masheikh hubadilisha sanad za hadithi au kuzikataa kabisa kwa hoja ya kugongana na fikra yake na jambo hili lipo sana katika hadithi zinazungumzia mitagaa ya itikadi. Kwa mfano,Hadithi isemayo من كنت مولاه فعلي مولاه imekataliwa na baadhi ya masheikh akiwemo Ibn Taymia huku Sheikh Albani ameikubali.
Riwaya nyingi zinazopokelewa kutoka kwa
njia ya Ubaiya bin Ka’ab na kutoka kwa Abu Isma kisha kuegemezwa kwa
Ikrama kutoka kwa Ibn Ibn Abbas (Ra) huwa ni maaudhoo’
Maudhoo ni katika hadithi mbovu zaidi zisizofaa kabisa kutolewa ushahidi.
Hivi ndivyo vigawanyo vya hadithii kwa kuzingatia upande wa kuzikataa na kuzikubali.****************************
‘Kukomeshwa Adhabu Ya Kifo’: Dhihirisho La Mgongano Katika Mfumo Wa Kidemokrasia- 1
Masoud Msellem
Tangu mwaka 2003, siku ya tarehe 10
Oktoba ya kila mwaka imechaguliwa kimataifa kuwa siku ya kampeni ya
kukomeshwa kwa adhabu ya kifo duniani. Kampeni hii hufanywa dunia nzima
ikiungwa mkono na baadhi ya nchi, majukwaa ya haki za raia na taasisi
mbali mbali hususan zinazoitwa na kujishughulisha na masuala ya ‘haki za
binaadamu’. Dhamira ya kampeni hii ni kuhakikisha kwamba adhabu hiyo
inafutwa kabisa katika uso wa dunia.
Adhabu hii ni miongoni mwa adhabu ya
kale na imekuwepo tangu katika zama za sheria za mayunani (wagiriki)
zilizobuniwa na Draco katika miaka ya 621 BC. Katika bara la Asia nchi
kama China ilikuwa sheria maarufu hadi kusitishwa kwa muda katika zama
za Utawala wa Tang (Tang Dynast) katika mwaka wa 747. Kwa upande wa
baadhi ya nchi nyingine za Ulaya ilitumika kiasi kwamba hata katika
baadhi ya mizozo yao ya kikabila(vendetta) ikiwa kama chombo cha fidia
au njia ya utatuzi wa migogoro yao hususan katika zama za Viking. Kwa
upande wa dini, wakatoliki waliitumia sana kwa kufuata mafunzo ya
Thomas Aquinas, hadi kufikia kuruka mipaka katika historia dhidi ya
wanaopinga mafundisho ya kanisa hilo. Pia katika mfumo wa Uislamu ambao
ndio mfumo wa haki na ambao sheria zake ni za wahyi nao umeweka adhabu
ya kifo katika baadhi ya makosa ya ‘Hadd’ kama vile kwa anaeacha dini ya
Uislamu na akakataa kutubu (murtad), mzinifu alieowa au kuolewa,
vitendo vya liwati, ujambazi (ihrab), na mauwaji ya makusudi kama
mawalii (ndugu) wa aliyeuliwa hawakusamehe au kukubali kulipwa fidia.
Kadhalika adhabu hiyo inaweza kutumika katika upande wa adhabu za
‘Taazir’ kama itakuwa ipo haja ya kutoa adhabu hiyo kwa mujibu wa
‘ijtihadi’ ya kadhi.
Adhabu ya kifo bado ilishika hatamu hata
katika karne ya 18 na baada. Kwa mfano, nchini Uingereza ilishtadi
sana kati kati ya karne hiyo na baada, kiasi kwamba chini ya sheria yao
iliyoitwa ‘Waltham Black Acts’ kwa kipindi cha karibu miaka mia kutoka
1740 mpaka mwaka 1834 iliwanyonga watu 8,753 katika England na Wales,
huku idadi ya watu wao (population) kwa kipindi hicho ilikuwa haizidi
watu Milioni 9. Urusi nayo iliwanyonga raia wake karibu 158,000
waliosaliti katika Vita vya kwanza vya dunia.***********************
******************************
Wanawake wa Kiislamu kamwe hawatopata hifadhi na ulinzi wao kutoka kwa yanayoitwa Majeshi ya Kulinda Amani
Habari :
Mnamo tarehe 8 septemba 2014 Shirika la
habari la Russia Today liliripoti matokeo ya utafiti uliofanywa na
Shirika la Haki za Binadamu la Human Right Watch (HRW) juu ya matendo
ya ubakaji yanayotendwa na Vikosi vya Kulinda Amani vya Umoja wa
Mataifa kwa wanawake wa kisomali pale wanapoomba misaada ikiwemo ya
matibabu. Ripoti ya Shirika hilo ina anuani: “Mabavu ya Wanaume hawa Juu Yetu: Udhalilishaji wa kijinsia na ushenzi wa Majeshi ya Umoja wa Afrika ndani ya Somalia”.
Ripoti hiyo imefichua wazi wazi
udhalilishaji na ushenzi wanaofanyiwa wanawake wa Somali wakiwemo watoto
wa umri mdogo katika kambi mbili za majeshi ya Umoja wa Afrika (AMISOM)
tangu mwaka 2013.
Katika utafiti huo, Shirika hilo la HRW
liliongea na wahanga 21 waliofichua amma kubakwa au kudhalilishwa
kijinsia. Misaada ya kibinadamu imekuwa ikitumika kama chombo cha
kuwalaghai wanawake hao na kuwatenza nguvu wakubwa na watoto kujihusisha
na matendo ya ngono na wanajeshi hao wakati wakitafuta misaada ya
madawa, maji na chakula.
Wahanga wa matukio hayo muda mwingi
hubaki kimya kwa khofu ya kudhuriwa zaidi. Huku vikosi hivyo vikitamba
kutokana na kinga inayowazuiya kushtakiwa na mahkama za ndani.
Maoni:
Ni jambo lililo wazi kwamba nchi za
kibepari kamwe haziwezi kuwalinda wanawake. Na kimsingi wao ndio
madhalimu wakubwa wa wanawake na wakiukaji wakubwa wa haki za wanawake
na heshima zao.
Linaloitwa Jeshi la Afrika la Kulinda
Amani nchini Somalia ndio hao wanaosambaza vita na ufisadi nchini humo.
Jeshi hilo limeundwa kutumikia maslahi ya madola ya magharibi hususan
Marekani inayolenga kunyonya rasilimali za Somali na kupambana na
Uislamu.
Uvamizi wa kigeni ndani ya Somali
umeleta majanga mengi kwa Waislamu wa Somalia na wakaazi jumla katika
Ukanda wote wa Afrika Mashariki. Wakati matukio haya maovu na ya
kikatili yakijiri, Umoja wa Afrika uko kimya kana kwamba hauoni
yanayotendeka, kwa kuwa ni Umoja wa kisanii ulioundwa kwa ajili ya
ajenda kutoka nje.
Muundo wa majeshi wa kimagharibi si
zaidi ya mkusanyiko wa kundi la wabakaji wa wanawake wa Kiislamu kila
wapaowakuta. Na hili ni kwa sababu wanawake wa Kiislamu wamekosa mlinzi
na kinga tangu ilipoangushwa dola ya Kiislamu ya Khilafah.
Tumeshashuhudia matukio kama hayo wakitendewa wanawake wa Kiislamu ndani
ya Afghanistan, Bosnia, Iraki, Kashmir na maeneo mengi duniani.
Aina hii ya majeshi ni zao la nidhamu ya
kidemokrasia ambayo ndio mvunjaji mkubwa wa heshima ya mwanamke kila
mahala duniani. Na hii ni kwa kuwa haina khofu ya adhabu za Mwenyezi
Mungu.
Ni Serikali ya Kiislamu ya Khilafah
pekee ndio yenye uwezo wa kulinda na kuhifadhi heshima na hadhi ya
wanawake wa Kiislamu na wasiokuwa Waislamu. Itakumbukwa namna Mtume
Muhammad(SAAW) alivyowashughulikia wayahudi wa Bani Qainuka walipovunja
heshima na hadhi ya mwanamke wa Kiislamu. Aidha, tunakumbuka namna
Khalifah Mu’tassim alivyowashughulikia Warumi pale walipomteka na
kumdhalilisha mwanamke wa Kiislamu.
Imeandikwa kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir.
*********************
No comments:
Post a Comment