Saturday, 28 February 2015

Mambo Matano Uwezayo Kuwafanyia Wazazi Waliofariki Kama Kwamba Wako Hai-1



 Wazazi wetu ni sababu ya kuweko kwetu duniani kwa idhini ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala), na kupata radhi zao ni sababu ya kuingizwa kwetu Peponi. Je, anapofariki mmoja wao au wote wawili, ndio mwisho wa kuwatendea wema?
Jibu ni kwamba tunaweza kuendelea kuwatendea wema kama kwamba wako hai tukipata thawabu zetu na wao pia. Baadhi ya amali za kuwatendea zimetajwa katika Hadiyth ifuatayo:
 عن أبي أسيد مالك بن ربيعة رضي الله عنه قال:  بينا نحن جلوس عند رسول الله صلى الله عليه وسلم إذا جاءه رجل من بني سلمة فقال يا رسول الله هل بقي من بر أبوي شيء أبرهما به بعد موتهما ؟ قال: ((نعم! الصلاة عليهما والاستغفار لهما وإنفاذ عهدهما من بعدهما وصلة الرحم التي لا توصل إلا بهما وإكرام صديقهما)) رواه ابن حبان في صحيحه  أبو داود وابن ماجه
Kutoka kwa Abu Asyad Maalik bin Rabiy’ah (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Tulipokuwa tumekaa pamoja na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi   wa sallam) alikuja mtu kutoka [kabila la] Bani Salamah akasema: Ee Mtume Allaah, ‘Je, kuna kilichobakia katika wema ninaoweza kuwafanyia wazazi wangu baada ya kifo chao? Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa Sallam) akajibu, ((Ndio; kuwaswalia [yaani kuwaombea du’aa] kuwaombea maghfirah, kuwalipa deni [au ahadi] zao, na kuunga ukoo ambao hauungiki ila kutokana nao, na kuwakirimu rafiki zao)) [Ibn Hibbaan katika Swahiyh yake, Abu Daawuud na Ibn Maajah]

1-Kuwaswalia (kuwaombea du’aa):
Ni miongoni mwa amali tatu ambazo zinaendelea kumfikia mzazi aliyefariki kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam):
 ((إذا مات إبن آدم إنقطع عمله إلا من ثلاث: صدقة جارية  أو علم ينتفع به أو ولدٌ صالح يدعوا له))  مسلم
((Anapokufa mja, hukatika amali zake zote isipokuwa mambo matatu, swadaqah inayoendelea, au elimu yenye kunufaikiwa, au mtoto mwema anayemuombea)) [Muslim]
Ni amri pia kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anaposema:
 ((وَقُل رَّبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرًا))
((Na useme: Mola wangu! Warehemu kama walivyonilea utotoni)) [Al-Israa: 23-24]

Hii ni du’aa mojawapo inayopasa kuwaombea, kwa sharti kuwaombea kipekee na si kwa mkusanyiko wa watu. 

Du’aa za kuwaombea wazazi waliofariki kama zilivyokuja katika Qur-aan na Sunnah:

Katika Qur-aan:

 رَّبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرًا
Rabbir-Hamhumaa kamaa Rabbayaaniy Swaghiyraa.
Mola wangu! Warehemu kama walivyonilea utotoni. [Al-Israa: 24]

رَبَّنَا اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِلْمُؤْمِنِينَ يَوْمَ يَقُومُ الْحِسَاب  
Rabbanagh-fir-liy wa liwaalidayya walil Mu-uminiyna yawma Yaquwmul hisaab.
Mola wetu! Unighufirie mimi na wazazi wangu wote wawili, na Waumini, siku ya kusimama hisabu. [Ibraahiym: 41]
رَبِّ اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ  
Rabbigh-fir-liy waliwaalidayya  
Mola wangu! Nighufirie mimi na wazazi wangu. [Nuuh 28]
 رَبِّ اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِمَن دَخَلَ بَيْتِيَ مُؤْمِنًا وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ  
Rabbigh-fir-liy wa liwaalidayya waliman dakhala baytiya Mu-uminan wa lil Mu-uminiyna wal Mu-uminaati 
Mola wangu! Nighufirie mimi na wazazi wangu, na kila aliye ingia nyumbani mwangu kuwa ni mwenye kuamini, na Waumini wote wanaume, na Waumini wanawake [Nuuh: 28]

Katika Sunnah wanaposaliwa Swalaah ya Janaazah:
Maiti mwanamume
اللهُـمِّ اغْفِـرْ لَهُ وَارْحَمْـه، وَعافِهِ وَاعْفُ عَنْـه، وَأَكْـرِمْ نُزُلَـه، وَوَسِّـعْ مُدْخَـلَه، وَاغْسِلْـهُ بِالْمـاءِ وَالثَّـلْجِ وَالْبَـرَدْ، وَنَقِّـهِ مِنَ الْخطـايا كَما يُنَقَّ الـثَّوْبُ الأَبْيَـضُ مِنَ الدَّنَـسْ، وَأَبْـدِلْهُ داراً خَـيْراً مِنْ دارِه، وَأَهْلاً خَـيْراً مِنْ أَهْلِـه، وَزَوْجَـاً خَـيْراً مِنْ زَوْجِه،  وَأَدْخِـلْهُ الْجَـنَّة، وَأَعِـذْهُ مِنْ عَذابِ القَـبْر وَعَذابِ النّـار
Allaahumma-Ghfir-lahu warhamhu, wa 'aafihi wa’afu 'anhu, wa akrim nuzulahu, wawassi' mudkhalahu, waghsilhu bilmaai wath-thalji walbaradi, wanaqqihi minal-khatwaayaa kamaa yunaqqath-thawbul abyadhwu minad-danas, wa abdilhu daaran khayran min daarihi, wa ahlan khayran min ahlihi, wazawjan khayran min zawjihi, wa adkhilhul-Jannah, wa a’idh-hu min ‘adhaabil-qabri, wa ‘adhaabin-naar  
Eee Allaah, Mghufurie na Mrehemu, na Muafu na Msamehe na Mtukuze kushuka kwake (kaburini) na Mpanulie kuingia kwake, na Muoshe na maji na kwa theluji na barafu na Mtakase na makosa kama inavyotakaswa nguo nyeupe kutokana na uchafu, na Mbadilishie nyumba bora kuliko nyumba yake na jamaa bora kuliko jamaa zake, na mke bora kuliko mke wake, na Muingize Peponi na Mkinge na adhabu ya kaburi (na adhabu ya moto)

Maiti mwanamke:
اللهُـمِّ اغْفِـرْ لَهُا وَارْحَمْـها، وَعافِهاِ وَاعْفُ عَنْـها، وَأَكْـرِمْ نُزُلَـها، وَوَسِّـعْ مُدْخَـلَها، وَاغْسِلْـهُا بِالْمـاءِ وَالثَّـلْجِ وَالْبَـرَدْ، وَنَقِّـهِا مِنَ الْخطـايا كَما يُنَقَّ الـثَّوْبُ الأَبْيَـضُ مِنَ الدَّنَـسْ، وَأَبْـدِلْهُا داراً خَـيْراً مِنْ دارِها، وَأَهْلاً خَـيْراً مِنْ أَهْلِـها، وَزَوْجَـاً خَـيْراً مِنْ زَوْجِها،  وَأَدْخِـلْهُا الْجَـنَّة، وَأَعِـذْهُا مِنْ عَذابِ القَـبْر وَعَذابِ النّـار
Allaahumma-Ghfir lahaa warhamhaa, wa 'aafihaa wa’fu 'anhaa, wa akrim nuzulahaa, wawassi' mudkhalahaa, waghsilhaa bilmaai wath-thalji walbarad, wanaqqiha minal-khatwaayaa kamaa yunaqqath-thawbul abyadhwu minad-danas, wa abdilhaa daaran khayran min daarihaa, wa ahlan khayran min ahlihaa, wazawjan khayran min zawjihaa, wa adkhilhal-jannah, waa’idh-haa min ‘adhaabil-qabri, wa ‘adhaabin-naar

Kuwaombea wazazi wawili:
اللهُـمِّ اغْفِـرْ لَهُما وَارْحَمْـهما، وَعافِهِما وَاعْفُ عَنْـهما، وَأَكْـرِمْ نُزُلَـهما، وَوَسِّـعْ مُدْخَـلَهما، وَاغْسِلْـهُما بِالْمـاءِ وَالثَّـلْجِ وَالْبَـرَدْ، وَنَقِّـهِما مِنَ الْخطـايا كَما يُنَقَّ الـثَّوْبُ الأَبْيَـضُ مِنَ الدَّنَـسْ، وَأَبْـدِلْهُما داراً خَـيْراً مِنْ دارِهما، وَأَهْلاً خَـيْراً مِنْ أَهْلِـهما، وأَزَوْاجَـاً خَـيْراً مِنْ اَزْوَاجِهِما  وَأَدْخِـلْهُما الْجَـنَّة، وَأَعِـذْهُما مِنْ عَذابِ القَـبْر وَعَذابِ النّـار
Allaahumma-Ghfir lahumaa warhamhumaa, wa 'aafihimaa wa’fu 'anhumaa, wa akrim nuzulahumaa, wa wassi' mudkhalahumaa, waghsilhumaa bil maai wath-thalji wal barad, wanaqqihimaa minal khatwaayaa kamaa yunaqqa-th-thawbul abyadhw minad-danas, wa abdilhumaa daaran khayran min daarihimaa, wa ahlan khayran min ahlihimaa, wa azwaajan khayran min azwaajihimaa, wa adkhilhumaal-Jannah, wa a’idh-humaa min ‘adhaabil qabri, wa ‘adhaabin-naar
Maiti zaidi ya wawili
اللهُـمِّ اغْفِـرْ لَهُم وَارْحَمْـهم، وَعافِهِم وَاعْفُ عَنْـهم، وَأَكْـرِمْ نُزُلَـهم، وَوَسِّـعْ مُدْخَـلَهم، وَاغْسِلْـهُم بِالْمـاءِ وَالثَّـلْجِ وَالْبَـرَدْ، وَنَقِّـهِم مِنَ الْخطـايا كَما يُنَقََّ الـثَّوْبُ الأَبْيَـضُ مِنَ الدَّنَـسْ، وَأَبْـدِلْهُم داراً خَـيْراً مِنْ دارِهم، وَأَهْلاً خَـيْراً مِنْ أَهْلِـهم، وأَزَوْاجَـاً خَـيْراً مِنْ اَزْوَاجِهِم  وَأَدْخِـلْهُم الْجَـنَّة، وَأَعِـذْهُم مِنْ عَذابِ القَـبْر وَعَذابِ النّـار
Allaahumma-Ghfir lahum warhamhum, wa 'aafihim wa’fu 'anhum, wa akrim nuzulahum, wawassi' mudkhalahum, waghsilhum bilmaai wath-thalji walbarad, wanaqqihim minal-khatwaayaa kamaa yunaqqath-thawbul abyadhwu minad-danas, wa abdilhum daaran khayran min daarihim, wa ahlan khayran min ahlihim, wa azwaajan khayran min azwaajihim, waadkhilhumul-Jannah, wa a’idh-hum min ‘adhaabil-qabri, wa  ‘adhaabin-naar

Baadhi ya Wema Waliotangulia wametaja kwamba “Atakayewaombea wazazi wake kila siku mara tano (baada ya Swalah za fardhi) atakuwa ametimiza haki zao kutokana na kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
أَنِ اشْكُرْ لِي وَلِوَالِدَيْكَ إِلَيَّ الْمَصِيرُ
((Nishukuru Mimi na wazazi wako. Ni Kwangu Mimi ndiyo marudio)) [Luqmaan: 14]

Na Allaah Anajua zaidi.

2-Kuwaombea maghfirah:
Kila unapowaombea maghfirah wao hupandishwa daraja Peponi:

عن أبي هريرة رضي الله عنه ، قال : قال رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّه عَلَيْه ِ وَ سَلَّمَ: ((إِنَّ الرَّجُلَ لَتُرْفَعُ دَرَجَتُهُ فِي الْجَنَّةِ فَيَقُولُ : أَنَّى هَذَا ؟ فَيُقَالُ :باسْتِغْفَارِ وَلَدِكَ لَكَ)) لإمام أحمد  و في سنن ابن ماجة أيضاً بإسنادٍ صحيح  
Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema: ((Hakika mtu hupandishwa daraja yake Peponi. Kisha huuliza: Kwa ajili ya nini? [huku kupandishwa kwangu daraja?] Huambiwa: Kwa ajili ya kuombewa maghfirah na mtoto wako)) Ahmad, na katika Sunan Ibn Maajah ikiwa na isnaad Swahiyh]

Inaendelea…

No comments: