Saturday, 28 February 2015

15-Rasuli (Swalla Allaahu ‘Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam) Alitilia Umuhimu Mkubwa Kuhusu Tawhiyd

Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alithibitisha Tawhiyd akatoa mafunzo kwa Maswahaba tokea kutumwa kwake kama Rasuli mpaka kufariki kwake. Ikawa Tawhiyd ni jambo kuu akilingania na kupigana vita kwa ajili yake. Alipomtuma Mu’aadh bin Jabal (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa gavana wa Yemen na Qaadhwiy wao alimwambia: 
((إِنَّكَ تَأْتِي قَوْمًا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ, فَلْيَكُنْ أَوَّلَ مَا تَدْعُوهُمْ إِلَيْهِ شَهَادَةَ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اَللَّهُ))
((Unakwenda katika nchi ya watu wa Ahlul-Kitaab, kwa hiyo, jambo la kwanza walinganie katika shahada ya laa ilaaha illa Allaah)). [Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]

Akawafundisha Maswahaba wengineo:
عن أبي عَمْرو، وَقِيلَ: أبي عَمْرَةَ، سُفْيَانَ بْنِ عَبْدِ اللهِ  رَضيَ اللهُ عَنْهُ قَال: قُلْتُ: يا رَسُولَ الله، قُلْ لي في الإِسْلاَمِ قَوْلاً، لاَ أَسْأَلُ عَنْهُ أَحَداً غَيْرَكَ. قَال: ((قُلْ: آمَنْتُ باللهِ ثُمَّ اسْتَقِمْ)).  
Kutoka kwa Abu 'Amru vile vile (anajulikana kama) Abu 'Amrah Sufyaan bin ‘Abdillaah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: “Nilisema: Ee Rasuli wa Allaah, niambie kitu kuhusu Uislamu ambacho siwezi kumuuliza mtu yeyote isipokuwa wewe.  Akasema: ((Sema; Namuamini Allaah, kisha kuwa mwenye msimamo)). [Muslim]

Watoto pia aliwfundishwa Tawhiyd:

 

عَنْ أبي العَبَّاس عَبْدِ اللهِ بنِ عَبَّاسٍ رَضي اللهُ عنهما قال: كُنْتُ خَلْفَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم يًوْماً، فقال: ((يا غُلامُ، إنِّي أُعَلِّمُكَ كلِماتٍ: احْفَظِ اللهَ يَحْفَظْكَ، احْفَظِ اللهَ تَجِدْهُ تُجاهَك، إذا سأَلْتَ فاسْأَلِ اللهَ، وإذا اسْتَعنْتَ فاسْتَعِنْ باللهِ، واعْلَمْ أنَّ الأُمَّة  لَوِ اجْتَمَعَتْ على أَنْ يَنْفَعُـوكَ بِشَيءٍ لَمْ يَنْفَعُوكَ إلا بِشَيْءٍ قدْ كَتَبَهُ اللهُ لَكَ، وإن اجْتَمَعُوا على أن يَضُرَّوكَ بِشيءٍ لَمْ يَضُروكَ إلا بِشَيءٍ قَدْ كَتَبهُ اللهُ عَلَيْكَ، رُفِعَتِ الأقْلامُ وَجَفَّتِ الصُّحُفُ))
Kutoka kwa Abul ‘Abbaas ‘Abdullaah bin ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: “Siku moja nilikuwa nyuma ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaniambia: ((Ee kijana! Nitakufundisha maneno (yenye manufaa); Mhifadhi Allaah Atakuhifadhi. Muhifadhi Allaah na utamkuta mbele yako. Ukiomba, muombe Allaah, ukitafuta msaada tafuta kwa Allaah. Tambua kwamba, ikiwa ummah mzima utaungana kukunufaisha wewe kwa kitu, basi hutonufaika ila tu kwa kile Alichokwishakuandikia Allaah, na wakikusanyika kukudhuru kwa chochote, hotodhurika ila tu kwa kile Allaah Alichokwishakuandikia (kuwa kitakudhuru), kwani Kalamu zimeshanyanyuliwa na sahifa zimeshakauka (Majaaliwa yasiyobadilikika). [At-Tirmidhiy akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]   
 

Mpaka katika hali ya kufariki kwake alitilia umuhimu mkubwa Tawhiyd:

عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي مَرَضِهِ الَّذِي لَمْ يَقُمْ مِنْهُ: ((لَعَنَ اللَّهُ الْيَهُودَ وَالنَّصَارَى اتَّخَذُوا قُبُورَ أَنْبِيَائِهِمْ مَسَاجِدَ))
Kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema alipokuwa katika maradhi ambayo hakuinuka tena [alipokaribia kufariki]: ((Allaah Amewalaani Mayahudi na Manaswara wamegeuza makaburi ya Mitume yao kuwa Misikiti)). [Al-Bukhaariy na Muslim na wengineo]

Nabiy Ya’quwb (‘Alayhis-Salaam) naye pia aliwausia wanawe akiwa karibu ni kufariki kwake:

أَمْ كُنتُمْ شُهَدَاءَ إِذْ حَضَرَ يَعْقُوبَ الْمَوْتُ إِذْ قَالَ لِبَنِيهِ مَا تَعْبُدُونَ مِن بَعْدِي قَالُوا نَعْبُدُ إِلَـٰهَكَ وَإِلَـٰهَ آبَائِكَ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ إِلَـٰهًا وَاحِدًا وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ ﴿١٣٣﴾
Je, mlikuwa mashahidi wakati mauti yalipomfikia Ya’quwb alipowaambia wanawe: “Mtaabudu nini baada yangu?” Wakasema: “Tutamwabudu Ilaah (Muabudiwa wa haki) wako na Ilaaha wa baba zako, Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq; Ilaah Mmoja (Pekee) nasi Kwake tunajisalimisha (katika Uislamu).” [Al-Baqarah: 133]

No comments: