Majina Ya Mitume 25 Kama Walivyotajwa Katika Qur-aan Na Mpangilio Wao
SWALI:
Kama nilivyo sema hapo juu mimi naomba majina ya mitume 25 walivyo kuja kwa utaratibu na unaweza kunichambuli vyema kama huyu ni baba wa huyu wabilahi tawfiq asalamaalaykum
JIBU:
Sifa
zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote,
Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu
'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa ndugu yetu kwa swali lako.
Pamoja na kwamba
inasemwa kuwa idadi ya Mitume wanafika hadi 124,000 kutokana na baadhi
ya mapokezi, lakini Hadiyth hizo zimedhoofishwa na hivyo hatuwezi
kuzitegemea, ila kuna Hadiyth ambayo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa
aalihi wa sallam) iliyosimuliwa na Abu Dhar ambayo alimuuliza Mtume
(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) idadi ya Mitume (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na akamjibu kuwa ni mia tatu na
makumi kadhaa. Hadiyth hiyo imeelezwa usahihi wake na Imaam Al-Albaaniy
kama ilivyo hapa chini:
عن أبي ذر ، قال : قلت : يا رسول الله ! أي الأنبياء كان أول ؟ ! قال : آدم ، قلت : يا رسول الله ! ونبي كان ؟ ! قال : نعم نبي مكلم ، قلت : يا رسول الله : كم المرسلون ؟ ! قال : ثلاث مئة وبضعة عشر ؛ جما غفيرا .
الراوي: أبو ذر الغفاري - خلاصة الدرجة: صحيح - المحدث: الألباني - المصدر: مشكاة المصابيح - الصفحة أو الرقم: 5669
الراوي: أبو ذر الغفاري - خلاصة الدرجة: صحيح - المحدث: الألباني - المصدر: مشكاة المصابيح - الصفحة أو الرقم: 5669
Kutoka
kwa Abu Dhar ambaye amesema: Nilisema: Ee Mjumbe wa Allaah, Nabii yupi
wa mwanzo? Akasema: ((Aadam)). Nikasema: Ee Mjumbe wa Allaah, alikuwa ni
Nabii? Akasema: ((Ndio Mtume aliyesemeshwa)) Nikasema: Ee Mjumbe wa
Allaah. Wapo Mitume wangapi? Akasema: ((Mia tatu na makumi kidogo)) [Mishkaat Al-Maswaabiyh ikiwa na daraja ya Swahiyh]
Hata hivyo idadi iliyotajwa katika Qur-aan ni Mitume 25 pekee na dalili ni kauli ya (Subhaanahu wa Ta'ala):
وَرُسُلاً قَدْ قَصَصْنَاهُمْ عَلَيْكَ مِن قَبْلُ وَرُسُلاً لَّمْ نَقْصُصْهُمْ عَلَيْك
((Na Mitume tuliokwisha kukuhadithia kabla yake, na Mitume wengine hatukukuhadithia)) [An-Nisaa: 164]
Mitume 18 wametajwa kwa pamoja katika Aayah 4 zifuatazo zinazofuatana:
((وَتِلْكَ حُجَّتُنَا آتَيْنَاهَا إِبْرَاهِيمَ عَلَى قَوْمِهِ نَرْفَعُ دَرَجَاتٍ مَّن نَّشَاء إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٌ)) (( وَوَهَبْنَا لَهُ إِسْحَقَ وَيَعْقُوبَ كُلاًّ هَدَيْنَا وَنُوحًا هَدَيْنَا مِن قَبْلُ وَمِن ذُرِّيَّتِهِ دَاوُودَ وَسُلَيْمَانَ وَأَيُّوبَ وَيُوسُفَ وَمُوسَى وَهَارُونَ وَكَذَلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ)) ((وَزَكَرِيَّا وَيَحْيَى وَعِيسَى وَإِلْيَاسَ كُلٌّ مِّنَ الصَّالِحِينَ)) ((وَإِسْمَاعِيلَ وَالْيَسَعَ وَيُونُسَ وَلُوطًا وَكُلاًّ فضَّلْنَا عَلَى الْعَالَمِينَ))
((Na hiyo ndio hoja Yetu Tuliyompa Ibraahiym juu ya watu wake. Tunampandisha cheo Tumtakaye. Hakika Mola wako ni Hakiymun-‘Aliym (Mwenye hikmah wa yote daima - Mjuzi wa yote daima)).
((Na
Tukamtunukia (Ibraahiym mwana anayeitwa) Is-haaq, na (mjukuu) Ya’quwb.
Wote Tukawaongoa. Na Nuwh Tulimuongoa kabla (zamani kabla ya Nabii
Ibraahiym). Na katika dhuria wake Daawuwd, na Sulaymaan, na Ayyuwb, na
Yuwsuf, na Muwsaa, na Haaruwn. Na hivyo ndivyo Tulipavyo watenda wema))
((Na Ismaa’iyl, na Al-Yasa’a na Yuwnus, na Luwtw. Na wote Tuliwafadhilisha juu ya walimwengu)) [Al-An’aam: 83-86]
Manabii na Mitume waliotajwa katika Qur-aan kwa mpangio wa ujio ni kama ifutavyo:
1. Aadam
2. Idriys
3. Nuwh
4. Huwd
5. Swaalih
6. Ibraahiym
7. Luutw
8. Ismaa'iyl bin Ibraahiym
9. Is-haaq bin Ibraahiym
10. Ya'quwb bin Is-haaq bin Ibraahiym
11. Yuwsuf bin Ya'quwb bin Is-haaq bin Ibraahiym
12. Shu'ayb
13. Ayyuwb
14. Dhul Kifl
15. Muwsaa
16. Haaruwn nduguye Muwsaa
17. Daawuwd
18. Sulaymaan bin Daawuwd
19. Ilyaas
20. Alyasaa'
21. Yuwnus
22. Zakariyyaa
23. Yahyaa bin Zakariyyaa
24. 'Iysaa bin Maryam
25. Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhim wa sallam)
2 comments:
ndo hao hao au kuna zaid ya hao?
mitume wako zaid ya hao ila wanaojulikana zaid ndio hao shekhe
Post a Comment