Namna Gani Dunia Inaendeshwa Kitaalamu?
Mnamo
Ogasti ya 2, 1990 majeshi ya Saddam Hussayn yalikwaruzana na vikosi vya
ulinzi vya Kuwaiti iliyo tajiri kwa mafuta kwa khofu ya Iraqi kuivamia
Saudi Arabia. Marekani na majeshi yake ya ushirika yalijimwaga ndani ya
eneo la Arabuni kutengeneza himaya itakayojulikana kwa jina la Ngome ya
Jangwani. Hayo yalipelekea kwenye meza ya mazungumzo ya kisiasa,
maelewano na majibu yake ambayo mara moja yaliporomoka na kutotarajia
lolote. Mnamo Ogasti ya 17, 1991 Ngome ya Jangwani ikawa ni Jangwa la
Makombora.
Migongano
hiyo ilishuhudiwa na mamilioni ya watu kupitia IF, CNN na BBC
zikionesha propaganda za mtindo wa kuondosha majeshi ya Saddam kwa
ushirikiano wa mataifa yaliyo juu kwenye teknolojia, kisiasa na nguvu za
kiuchumi. Hata hivyo, kisichoeleweka ni kwamba kuanzia muono wake wa
nje, vita hivyo vilitengenezwa, kuendeshwa na kufanyiwa hila na kundi
lililo werevu. Kundi ambalo limejitengeneza kiudanganyifu kama
mwanaadamu aliye na nguvu juu ya mamilioni ya majeshi yaliyo na nguvu
kwa hila za nuclear. Mtu ambaye amepata kushikilia 1/5 ya mafuta
yote duniani kwa usiku mmoja; hata hivyo, ukweli ni kwamba hakuwa
chochote isipokuwa alikuwa na duru yake kama walivyo wengine. Ni kama mfano wa kijibwa ndani ya mpango mkuu wa Vita vya Ughaibuni na pia kama
ni mpigaji filimbi. Wapigaji filimbi hao wa Vita hiyo sio kwamba
hawaeleweki katika kuendesha matokeo makuu Duniani. Ukweli ni kwamba
wamefanya hivyo kwa kipindi kirefu, sasa ni karne.
Kuanzia kujificha kwao katika kila vita vikuu wanavyoviongoza wao, mapinduzi na mgawanyo. Wana mikono yao
katika kila kitu unachosoma, kila kitu unachosikia na kila kitu
unachoona. Wamefanikiwa kuingiza ndani ya kila ubongo wa mtu aina za
fikra zao na kutumbukiza watu wao kwenye mamlaka za nchi zilizo muhimu
na ni kutokana na kivuli hichi wamekitumilia kuanzisha mfumo mpya wa
kisiasa, mfumo mpya wa kiuchumi na bila ya shaka mfumo wa dini ulio
sheheni dhambi. Lengo lao la moja kwa moja ni kuhodhi mamlaka ya
ulimwengu mzima na watafanya kila waliwezalo kuzuia chochote
kitakachokuwa ni kikwazo kufikia malengo yao. Shabaha ambayo imewekwa wazi ndani ya risala iliyotolewa na Raisi mstaafu wa Marekani, George Bush: "Kilicho mbele yenu ni zaidi ya nchi moja ndogo, ni fikra mpya na Mfumo Mpya Wa Ulimwengu".
Hata hivyo, asili ya mpango wa ulimwengu mzima haukuanzishwa ndani ya ofisi za White House. Ukweli ni kwamba, mizizi yake imeanzia kwenye vita vyengine, huko mwaka 1095 sehemu za Claremont – Ufaransa. Karne ya 11 ya Ulaya ilitawaliwa na kanisa ambalo liliwakamata barabara watu, kuanzia mioyo yao
hadi fikra zao. Nguvu hii ilimuwezesha Papa Erwin II kuanza vita
alivyoviita takatifu (crusade) dhidi ya Kiongozi wa Kiislamu kwa jina la
Vita Vya Msalaba kuikomboa ardhi ya Jerusalem.
Ardhi ambayo ilikuwa chini ya himaya ya Waislamu tokea mwaka 637,
lakini mwaka 1099 himaya hii ilikhitimishwa kwa umwagaji damu na ghafla
moja ikafikia tamati. Kwa jina la Msalaba, wanawake walibakwa na
kuuawa, watoto walikatwa mapanga na inasemekana kwamba damu iliogelea
kwenye mitaa hadi kufikia urefu wa goti la farasi. Nje ya ardhi hii
ya umwagaji damu kulikuwa na kundi linalotisha (terror) ambalo litafanya
lolote kupata wanalotaka hata kwa gharama yoyote. Miaka ishirini baada
ya kuchukuliwa Jerusalem, Baytul-Maqdis ilitekwa nyara na kundi la
wapiganaji waliookoka wanaojiita wenyewe Wapiganaji Wa Hekalu La Sulaymaan au kiufupi Wapiganaji Wa Hekalu.
Huko Jerusalem, Wapiganaji Wa Hekalu walianza kuachana na mafunzo ya Ukristo mbali zaidi na zaidi. Walijifunza siri za usanii wa Kabala na
mitindo ya kale ya uchawi wa Kiyahudi pamoja na miiko yake
isiyoeleweka. Mayahudi hao walijifunza usanifu wa kale wa kipagani
kutoka Misri kwenye kipindi cha utumwa chini ya Firauni na kuziendeleza
ndani ya Babylon
katika kipindi cha utawala wa Navakanazar. Mnamo mwaka 1307, Mfalme
Philip wa Ufaransa aliwatia hatiani kwa mashitaka ya kumkataa Kristo,
liwati na ibada za mizimu pamoja na uchawi. Mnamo mwaka 1314, Papa
Claymont V alitangaza kwamba Mahekalu yote ni ya urithi wa Ukristo na
kuamrisha kwa nguvu zote majengo hayo kushikiliwa. Kiongozi wao aitwae
Chekthemolay alitekwa nyara na kuchomwa.
Hekalu hilo
lilizungushiwa pembe zote na karibu ya kumaliza kazi hiyo itakayodumu
milele, matumaini yaliibuka lakini walihitajika kutafuta mshirika wa
usalama wao lakini sio kwa Ufaransa. Walihitaji nchi ambayo ipo kwenye
shauku kubwa ya kupigania uhuru dhidi ya Waingereza, nchi ya Scotland
ilifaa kwa hili. Nchi ambayo matumaini yake ya uhuru yalififia kutokana
na kifo cha William Wallace. Hata hivyo, kwa Mfalme wa Scotland, Robert
Bruce, kuwasili kwa Wapiganaji Wa Hekalu kulimpa zana ya siri mpya.
Uzoefu wao ulipatikana kwa zaidi ya miaka mia mbili ya kupigana dhidi ya
majeshi makubwa ya Uislamu, mapigano ambayo yaliwafanya kuwa wataalamu
katika kujihami na upiganaji kuliko mapigano yoyote ambayo yanaweza
kuletwa mbele yao.
Mnamo mwaka 1314, Wapiganaji Wa Hekalu waliungana na Robert Bruce na jeshi lake lilichukuwa
sehemu za Ballack Burn, wakiwa tayari kusubiri mapigano pamoja na
Waingereza. Uoni wa Robert Bruce kwenye pembe zote nne ulimuwezesha
kulipiga vibaya mno jeshi lenye wapiganaji 25,000 lililo na nguvu la
Muingereza dhidi ya wapiganaji 6,500 tu. Ndoto ya Scotland iliyo huru hatimaye ilifikiwa. Wapiganaji Wa Hekalu sasa wamerudi na hawatakuwa tayari tena kujikubalisha kushindwa.
Wakati huu, wataiendesha nchi hiyo kwa kuwadhibiti Wafalme wake na ili kuficha siri yao moja kati ya mawili lazima
yatendeke;ama wafe Wapiganaji
Wa Hekalu wote au jina lao life. Wapiganaji Wa Hekalu ambao walitoroka
Ulaya, hatimaye walizikwa huko Rovelin Chapel – Scotland (kama inavyoonekana kwenye picha hapo kushoto) jengo ambalo hadi leo linasimama kama ni alama ya kuwepo kwao nchini Uingereza. Vizazi vyao vilikuja kuwa na nguvu sahihi ya Scotland.
Kifo cha Malkia Elizabeth I mnamo mwaka 1603, kiliiacha Uingereza bila
ya mrithi wa kiti cha ufalme. Kwa mnasaba wa kizazi cha Mfalme James V
wa Scotland ndiye atakayekuwa Mfalme wa Uingereza, na kwa kufanya hivyo, Scotland na Uingereza walilazimika kujiunga pamoja kuunda utawala mpya. Na nguvu ambayo ilikuwa nayo Wapiganaji Wa Hekalu juu ya Scotland
iliwaenea kuwapa himaya thabiti ya Uingereza yote. Kwa zaidi ya miaka
mia moja, Wapiganaji Wa Hekalu walizificha shughuli zao chinichini hadi
walipojulikana kwa uchache na kukumbukwa kidogo. Hata hivyo,
hawakusimama kukamata himaya thabiti ya Uingereza.
Kipindi
chote hicho walikuwa wakipanga na kujipangua na kujiingiza ndani ya
uongozi katika pembe zote za utawala. Mwaka 1717, Wapiganaji Wa Hekalu
walijitokeza tena Uingereza wakiwa wengi na nguvu zaidi, na sasa wakiwa
tayari kujibadilisha utambulisho wao utakaokuwa mbali na sifa yao
ya hapo nyuma. Hawakupata hadhi isipokuwa kwa wakuu na watawala wa
Uingereza na jina walilolijichagulia lilikuwa ni jina litakalojulikana
na wengi lakini litakaloeleweka na wachache. [Sikubaliani na jina la
"freemasons" linalotokana na Kifaransa "frerés masons" yaani ndugu wa
Kimasoni. Ni Waingereza wasioelewa ndio waliolibadilisha kuwa
Freemasons].
Utambulisho
huo mpya kwa wajumbe wenye mamlaka za kuamrisha mambo uliwawezesha
Wamasoni kuwa na sifa na heshima. Mwanachama wa mwanzo wa Kimasoni
kimataifa alikuwa ni Frederick, Mtoto wa Mfalme wa Wales. Mwanachama
wa hivi karibuni ni Phillip, Mtoto wa Mfalme wa Duke wa Edinburgh na
mwandani wa karibu wa Malkia wa leo wa Uingereza Bibi Elizabeth II
ambaye yeye mwenyewe ni mlezi wa zamani wa Wamasoni. Hata hivyo, nyuma
ya milango iliyofungwa, Wamasoni walikuwa huru kujihusisha na maadili na
kanuni za siri zilizokabidhiwa kwao na wazee wao, na hizi zikaja kuwa
ni msingi wa kiwango cha uwanachama kiitwacho Degree. Wamasoni
hawakujihusisha tu na mfumo wa Uingereza peke yake, mawazo yao
yalikuwa mbali ya hapo. Miaka inayokuja badaye, wakati ambao Dunia na
Marekani zitatumbukizwa kwenye vita na mapinduzi zaidi na zaidi, mmoja
kumshinda mwenziwe. Hata hivyo, hayakuwa haya ni malengo makuu
yaliyokuwa yakiaminika kuwa na athari kwa wenye kuonewa. Lakini ukweli
ni kwamba mipango ilibuniwa na watu wachache maalumu, waliokuwa na njaa
ya uongozi katika kila kitu. Yote haya yatatokea ndani ya nchi zao
walizozikimbia kwa karne zilizopita na nchi hizi zitakuwa ni msingi wa
Kuutawala Ulimwengu Mzima.
Katika
karne ya 18, idadi kubwa ya Wafaransa walikuwa ni masikini wakati koo
za kifalme na zile zinazojiweza zikiishi kwa starehe na ubadhirifu,
kukaibuka tofauti kubwa baina ya matabaka haya mawili. Wamasoni
watatumia hili kushurutisha madaraka juu yao
na hivyo kusababisha mgongano mkubwa katika historia ya Ufaransa.
Wamasoni wakachukua nafasi hiyo ya hali mbaya iliyojaa ghadhabu miongoni
mwa Wafaransa na wakatumia hilo kufanikisha malengo yao
kwa kupanga vizuri vita vya propaganda. Walivihodhi vyombo vyote vya
habari kisawasawa na walivitumia kuyapinda maoni ya walio wengi.
Magazeti yalitezwa nguvu kutangaza mwisho wa utawala wa kifalme na
kuanzisha jamii inayofuata uhuru, usawa na ushurutishwaji.
Mamilioni
ya fedha yalitumika kuweka chini ya uangalizi hali ya kisiasa ya
Ufaransa. Wanasiasa wanaofadhiliwa na Wamasoni walihamasisha dhana ya
Kimasoni, siri zilizojikita za Wamasoni zilifunguliwa kwa wajumbe wa
jeshi la Ufaransa, maofisa wa juu na makamanda waliendeshwa kwa kutumia
mawazo ya Wamasoni. Wamasoni walifanya kila jitihada kuwatawala
wanasiasa na majeshi ya Ufaransa chini ya Umasoni. Ilipofika tarehe 14
Julai 1789, kundi la watu lilivamia jela ya Basteel, Paris. Alama za
upinzani uliojikita dhidi ya watawala wa Ufaransa hapo zilidhihirika kwa
watu wengi kujitokeza sehemu tofauti nchini Ufaransa.
Huko
vijijini na mijini, watu walitoa mawazo yao yaliyojaa chuki dhidi ya
utawala wa kifalme. Lakini chuki hizo za Wafaransa hazikuweza kuzimwa
moto hadi kufikia mwaka 1793. Mnamo tarehe 21 Januari ya mwaka huo huo,
Mfalme Louis XVI alikatwa kichwa mbele ya umati wa watu na kuwa ni
sababu ya kufikia kikomo utawala wa Kifalme wa Kifaransa na kusafisha
njia ya taifa jengine la Kimasoni barani Ulaya. Kutokana na ufalme huo
kuondoka, ilionekana kana kwamba hakuna kitakachowazuia Wamasoni
kuitawala Ufaransa kisawasawa. Hata hivyo, kilichotokezea badaye
kitawaacha Wamasoni katika kilema kibaya na kitakachotokezea badaye
hakika hakikuwa ni kwa mujibu wa mipango ya Kimasoni.
Kijana
mmoja kwa jina la Napoleon Bonarparte alikuwa ni askari. Yeye alikosea
kidogo kuipeleka Ufaransa kwenye vita vibaya kabisa pamoja na Ulaya pale
alipoacha kuufuata muziki wa Kimasoni. Napoleon alijitangaza mwenyewe
kwamba yeye ndie Mtawala wa milele wa Ufaransa. Napoleon alilazimishwa
kuachana na ufalme huo mnamo mwaka 1814 na alihamishwa kisiwani Corsica.
Hata hivyo, mwaka 1815 Napoleon alitokeza kwa mara nyengine tena Paris
akihamasisha jeshi jipya likiwa tayari na vita vipya huko Ulaya. Hapo
Wamasoni walikuwa na tatizo kubwa mikononi mwao. Uingereza na washirika
wake wa Kimasoni hawakuweza kufadhili vita virefu dhidi ya Napoleon bila
ya kukaribia kufilisika.
Msaada ulikuja kutoka kwa mtu asiye marufu kabisa. Nathan Rothschild alikuwa ni mkuu akiongoza benki ya kifamilia, lakini kwasababu ya hadhi yao
ya Uyahudi, walilazimishwa kufanya kazi kwa kutumia kivuli cha watu
wengine. Rothschild alihakikisha kutumia nafasi ya kuwakomboa watu wake
na mara nyingi mwenyewe peke yake akidai kurudishwa utambulisho wa
Wayahudi kama ni watu walio sawa ndani ya Ulaya, wakiwa nao wana haki ya kufanya biashara wazi wazi. Na kama Wamasoni watazikataa fedha zao mara zote zitaenda kwa Napoleon.
Wamasoni
hawakuwa na khiyari isipokuwa kukubali, na biashara ya mkopo
ikakamilishwa. Mnamo mwaka 1815 askari wa Kiingereza, Kidachi na Kirusi
walikanyaga ardhi ya Waterloo
nchini Ubelgiji ambapo walikutana na vikosi vya Napoleon na kuwashinda.
Napoleon mara hii alikamatwa na kutorudi tena Ufaransa ambayo hatimaye
sasa ilikuwa chini ya muongozo wa Wamasoni. Ingawa wanahistoira wametaja
machache katika mahusiano ya Wamasoni ndani ya mapinduzi, Wamasoni
wenyewe walilazimika kudhihirisha utambulisho wao wakati wa kipindi
hichi muhimu katika historia. Mnamo mwaka 1904 Marc Vadourasambo akiwa ni Mmasoni alitangaza waraka wa makubaliano: "Wamasoni
wamefanya (mapinduzi) kwa kujificha lakini kwa namna madhubuti ya
kutayarisha mapinduzi, hivyo tupo na makubaliano ya moja kwa moja,
Wamasoni wakiwa ndio waanzilishi wa mapinduzi na sifa nilizozipata
kutoka kushoto na ambazo nimeridhika nazo zinaonesha kwamba nyinyi
waungwana mnakubaliana na mimi kwamba walikuwa ni Wamasoni waliofanya
Mapinduzi ya Ufaransa."
Wavumbuzi wa taifa la Marekani walipokanyaga mguu katika jabali la Plymouth,
sio tu kwamba walileta watu wasio na haki ya uraia bali pia walileta
fikra za Kimasoni za Ulaya. Yale madhila yaliyokimbiwa Ulaya na hao
wavumbuzi wa Marekani pia yaliweza kuonekana ndani ya ardhi mpya kwenye
mfumo wa utawala wa kibabe wa Kiingereza. Ili kudhibiti na kuendesha
katika hali zote taifa hilo jipya la Marekani, Wamasoni walitumia njia zile zile walizotumia kuiteka Ufaransa.
Ingawa
ufalme wa Uingereza ulikuwa ukiongozwa na Wamasoni, vita vya Marekani
vya kudai uhuru wa Marekani vilihitajika. Na watu walioshiriki ndani ya
vita hivyo waligharamika kutimiza ndoto za Wamasoni. Hisia za watu
ziliharibiwa katika hamaki na kama
zilivyo ghadhabu za Ufaransa zilisababisha vita. Hata hivyo, wakati huu
makosa yaliyofanywa huko nyuma hayatarudiwa. Ushindani waliokutana nao
Wamasoni dhidi ya Napoleon na jeshi lake huko
Ulaya uliwafunza adabu Wamasoni. Kiongozi yeyote wa upinzani
anayefuatia ni lazima atekeleze matakwa ya Kimasoni na njia bora ya
kufanya hilo ni kuhakikisha kiongozi mwenyewe ni Mmasoni. Na kiongozi aliyepigana dhidi ya Waingereza hakuwa mwengine isipokuwa ni George Washington.
Mnamo tarehe 4 ya Julai mwaka 1776, tamko la uhuru lilitangazwa. Tarehe 17 Oktoba 1781, hatimaye Waingereza walishindwa na kuyasalimisha makoloni kwa Wamarekani na Taifa la mwanzo la Kimasoni likazaliwa, taifa litakalowakilisha Umasoni katika kila njia. Alama
ya kuwepo Umasoni ndani ya Marekani inaonekana wazi kwenye sarafu ya
dola ambayo inabeba picha ya raisi wa mwanzo wa Kimasoni George
Washington ndani ya ulimwengu, na picha ya alama ya Kimasoni iitwayo "Jicho Moja Linaloona Kila Kitu."
Kumbukumbu
zinaonesha kwamba udhibiti na uharibifu wa maoni ya kisiasa ni zana kuu
inayotumiwa na Wamasoni katika kushikilia nchi na mataifa. Pale tu
watawala na wanasiasa wa nchi wanapodhibitiwa, basi sheria na mfumo wa
siasa unaweza mara moja kubadilishwa kwa mujibu wa matakwa yao. Hata hivyo, kuutawala mwili haina maana kwamba umeitawala akili.
Wamasoni wanaelewa kwamba mipango yao ya Serikali Moja inafungamana moja kwa moja na kuwalainisha watu katika matakwa yao na hivyo kudhibiti
upinzani kutokana na yale wanayoyafanya na tishio kubwa dhidi ya
mipango yao ni akili iliyo na fikra huru. Hili kwao ni tishio kubwa
kuliko hata jeshi au sheria. Ili kudhibiti tishio hili na kufanikisha
malengo yao,
Wamasoni wametengeneza mpango wa hatari usiowahi kutengenezwa hapo
kabla. Mpango ambao utatawala kila nyanja ya mwanadamu, maisha yako na
zana wanazotumia dhidi yako zipo ndani ya nyumba yako mwenyewe,
zikikuburudisha wewe pamoja na watoto wako na kidogo kidogo zikikutawala
bila ya wewe mwenyewe kulitambua hilo.
Ndani ya jamii ya leo, watu wanatumia muda zaidi na zaidi katika vyombo
vya kisasa. Luninga, Sinema, Michezo ya Kompyuta, Tovuti, Michezo na
vipindi vya ulaghai na Miziki iliyoenea imeganda ndani ya maisha yao.
Na
kweli vitu hivi vinasababisha upanuzi wa haraka wa habari ambazo wewe
unachukua ndani ya akili yako aidha kwa kutambua ama bila ya kutambua.
Habari ndani ya jamii zinaoneshwa katika maadili na tamaduni, tofauti ya
zuri na baya hadi namna ya jamii na uchumi unavyotakiwa kutengenezwa.
Haya yote yapo mbele ya macho yako katika kila siku ya maisha yako.
Vyombo
hivi vya habari, kwa nafasi kubwa vinatumika katika kuweka msingi wa
kuamua uoni wa mtu kwa Ulimwengu na kila kitu kilicho mbele yake. Hivyo,
kila mtu anapodhibitiwa na vyombo vya habari kama
hivi bila ya shaka ataathirika na nguvu za kutawaliwa, na kwa kweli
idadi kubwa ya watu duniani inaathirika na fikra zao, na hili hakika
ndilo Wamasoni wanaloendelea kuvumbua.
Hakika
Wamasoni wanatumia vyombo vya starehe kushurutisha watu katika namna
zao za fikra ima wazi wazi au kwa kujificha. Taratibu wanazotumia
zinatofautiana lakini lengo lao ni hilo hilo kuingiza imani zao, fikra
zao na madhumuni yao kwako wewe katika namna ambayo unaanza kuwafikiria
kama ni watu wako. Ushahidi wa kuwepo kwao ndani ya starehe marufu
umeenea kila pahala. Ushirikishwaji wa Wamasoni ndani ya uzalishaji huu
sio jambo geni. Hail ni miongoni mwa watunzi wa zamani, Wolf Gang
Amadeus, Mozart ambaye yeye mwenyewe ni Mmasoni ametengeneza muziki
ambao ulikuwa na uonekano wa wazi wa Umasoni. Muziki huo umetungwa
kutokana na hadithi iliyochukuliwa kutoka kwa Wamisri wa kale Avysus na
Cyrus. Haki za wapagani katika hadithi za kutungwa za kale za Misri za
Kabala ni miongoni mwa sifa kuu za Kimasoni. Ni kutokana na asili ya
upagani huu wa Kimisri ndio ikapatikana alama ya Shina La Jicho Moja.
Ushahidi
wa kuwepo kwa Wamasoni pia unapatikana sana ndani ya miziki marufu ya
sasa. Kwa mfano Michael Jackson ambaye anatambulika kama ni mfalme wa pop
na anasifika kuwa ni mburudishaji wa wakati huu (wakati huo
ilipoandikwa makala hii). Pia anazalisha na kuuza albamu nyingi tu
duniani kote, lakini pia anaweza kuunganishwa na Umasoni. Gamba la
albamu lake la "Dangerous" lina sifa ya kushangaza kwa kuwa na alama ya
Jicho Moja, na pia kuna picha ya mfano wa maji ya mto yanayowaka kwa
moto. Inaonesha wazi kwamba yeyote anayeingia ndani ya maji hakika
atatumbukia ndani ya moto. Gamba pia lina fumbo ya picha ya mtu mwenye
kipara kama ni Alistair Crowley. Yeye mwenyewe alikuwa ni Mmasoni na
badaye akawa Mlokole na kuandika kitabu cha "Sheria Mpya Ya Mwanadamu"
ambacho kimeeleza ndani yake kwamba siku moja kitachukua nafasi ya
Qur-aan kama ni sheria ya mwanadamu.
Ulinganisho
huo baina ya Umasoni na fumbo hauishii hapo. Uzalishaji wa miziki
inayodhibitiwa na Wamasoni inaingizwa vitendawili vyenye ujumbe wa
kishetani. Uchezeshwaji wa kuanza mwisho kuja mwanzo (back tracking) ni
njama zinazotumiwa katika kuhifadhi ujumbe ili kuufanya kuwa ni sauti ya
muziki katika namna ambayo zinatambuliwa pale tu zinapochezeshwa kwa
mtindo wa mwisho kuja mwanzo. Pale inapochezeshwa kwenda mbele,
msikilizaji hataelewa hata kidogo ujumbe unaochezeshwa.
Ingawa msikilizaji hatakuwa makini kwamba akili yake inakamata ujumbe asiouelewa, lakini katika siku za mbele ujumbe kama
huu unaweza kuhifadhiwa ndani ya akili ya mtu na unaweza kuathiri tabia
za mtu ama maamuzi yake. Katika namna nyingi, uchezeshwaji wa muziki wa
kuanza mwisho kuja mwanzo ni mfumo wa kumfanya mtu atende mambo bila ya
kujitambua na ni mfumo wenye kuharibu mara moja. Mfano wa mwanzo wa
uchezeshwaji huu ni kutoka kwa msanii wa kike aitwaye Madonna.
Unapatikana katika albamu yake marufu kwenye nyimbo ya "Like a Prayer."
Hata hivyo, kama utakavyosikia sio
mungu anayeonekana kuombwa katika nyimbo hiyo bali ni shetani.
Inapochezeshwa kwa mtindo wa mwisho kuja mwanzo maneno ya "Ah shetani
tuitikie" yanasikika wazi wazi. Pia alama ya Jicho Moja imetumika
miongoni mwa video za nyimbo zake Madonna. Ambapo jicho moja linaonekana
likitoka katika kichwa chake. Pia anaonekana ndani ya video ambapo
amesimama katika maandishi, uchunguzi wa karibu unaonesha kwamba
maandishi haya ni ya Kiarabu katika lugha ya Qur-aan.
Mfano mwengine wa uchezeshwaji huu unapatikana katika kundi la "The Eagles" na nyimbo yao
inayoitwa "Hotel California". Maneno haya yanapochezeshwa kwa mtindo wa
mwisho kuja mwanzo yanasikika maneno haya kwa uwazi "Ndio shetani". Na
pia hadithi yake wenyewe ni ya kishetani. California ya hapo sio hoteli bali ni mtaa ndani ya Marekani unaoitwa California.
Ni katika mtaa huu ambapo makao makuu ya kanisa yalipatikana, lakini
sio aina ya kanisa ambalo mtu anaweza kufikiria, bali ni kanisa ambalo
baadhi wameliita "Kanisa la shetani." Lililo ongozwa na kuanzishwa na
Anthony Sans Delivy, muandishi wa Biblia ya Kishetani. Inaonesha
mafundisho ya kanisa hili yamekuwa ndio imani ya watu marufu katika
uzalishaji wa bidhaa za starehe kwa waimbaji wote, kuanzia rock hadi main streams,
wengine wamefikia hatua ya kushajiisha imani za kanisa hili. Miongoni
mwa mjumbe anayetuhumiwa kuhusika na kanisa hili ni mwimbaji wa Rolling Stones
anayeitwa Mick Jagger aliyeandika nyimbo ya "Sympathy for the Devil".
Inaonesha kwamba kile kilichoanza kama ni Jumuiya ya Wakristo badaye
ikabadilika na kuwa ni dini iliyorithiwa hata kwa Wakristo na sasa ina
sifa za kishetani zilizochanganywa ndani yake. Ulimwengu wote wa
burudani umegandana na ushahidi wa kuwepo kwa Wamasoni wazi wazi au
kuzitangaza imani zao kwa fahari kabisa.
(Tanbihi:
Mwandishi wa makala hii kutoa mifano ya hiyo miziki, haina maana kuwa
miziki inakubalika katika Uislamu, bali ni njia ya kuonyesha upotofu na
ushetani wa mielekeo hiyo na inayoambatana nayo. Muziki ni haramu katika
Uislamu, na zaidi msomaji asome na asikilize humu:
Hili linadhihirishwa zaidi ndani ya filamu marufu katika big screen au small screen, kwa gharama kubwa za filamu za Hollywood hadi cartoons
za kawaida. Wamasoni hawakuacha kuingiza hamasa zao katika kitu
chochote ili kushajihisha ujumbe wao wa serikali moja. Matt Growning
ambaye ni mtengenezaji wa kipindi cha cartoon marufu katika historia ya luninga. "The Simpsons" ni cartoon
inayotaka uhuru wa madaraka. Matt Growming mwenyewe kwa uwazi kabisa
ametangaza kwamba anataka kuziweka fikra zake za kisiasa ndani ya kazi
zake. Lakini anataka kufanya hivi katika namna ambayo watu watakubaliana
kwa urahisi na mawazo yake. Na njia aliyotumia kulifanya hili ni cartoon
ya kitalamu inayoitwa "The Simpsons". Sasa nini haswa hakika Simpsons
inatufunza sisi na watoto wetu? Kuna mafunzo mengi (mabaya)
yanayofundishwa kwetu, haya yanahusu kutotii utawala aidha ikiwa ni wa
mzazi au wa serikali. Tabia mbaya na kutofuata amri ni njia ambazo
zinatumika kupata hadhi miongoni mwa watu na kwamba ujahili ni sifa
nzuri wakati elimu ni kitu kilichopitwa na wakati. Hata hivyo, kitu
kinachotisha haswa ni mambo yaliyojificha chini ndani ya miongoni mwa
vipindi vyake.
Kipindi ambacho baba mtu wa familia anayeitwa Homer Simpson anawahamakia kundi linaloitwa stone cutters. Alipojiunga na kundi hilo,
wafuasi wenziwe wanatambua alama ya kuzaliwa inayofanya kundi lote
kumtangaza kuwa ni aliyechaguliwa lakini kwa hadhi yake na tabia zake
yeye Homer Simpson anajidanganya mwenyewe kwa kujidhania kwamba yeye ni
mungu. Mtu anaweza kulidharau hilo na kuelewa kwamba jambo hilo ni la cartoon
ya kitoto, burudani na kitu kisicho na dhara. Lakini nguvu iliyokuwa
nayo kwa watazamaji inafanya kuwa ni njia ya kuathiri watu kwa
kuwabadilisha bila ya wenyewe kujitambua. Watengenezaji wake wanakiri
kwamba wanaingiza propaganda zao za fikra za kisiasa kwa watazamaji
katika njia iliyojificha. Fikra zinazoenezwa kupitia luninga ya nyumbani
zinasambaa mbali sana kuliko michezo inayooneshwa sinema. Na ni kupitia vyombo hivi kwamba dhana mpya inawasilishwa. Nayo ni dhana ya kiongozi mmoja kwa ulimwengu mzima.
1 comment:
duh dunia imeisha
Post a Comment