Nini Hikma Ya Kulala Upande Wa Kulia Kama Alivyotufundisha Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ?
Yote
tunayoyapata kutoka katika Sunnah ya mwalimu wetu, Mtume (Swalla
Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni mafunzo yenye faida kwetu ima
faida ya nafsi zetu au faida katika mwili wetu au faida katika maisha
yetu na kwa ujumla, bali kuna hikma kubwa kwenye mafunzo hayo:
عن
البراء بن عازب رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه و قال صلى الله
عليه وسلم : ((إذا أتيت مضجعك فتوضأ وضوءك للصلاة ثم ثم اضطجع على شقك
الأيمن ثم قل : أللهم أَسْـلَمْتُ نَفْـسي إِلَـيْكَ،
وَفَوَّضْـتُ أَمْـري إِلَـيْكَ، وَوَجَّـهْتُ وَجْـهي إِلَـيْكَ،
وَأَلْـجَـاْتُ ظَهـري إِلَـيْكَ، رَغْبَـةً وَرَهْـبَةً إِلَـيْكَ، لا
مَلْجَـأَ وَلا مَنْـجـا مِنْـكَ إِلاّ إِلَـيْكَ، آمَنْـتُ بِكِتـابِكَ
الّـذي أَنْزَلْـتَ وَبِنَبِـيِّـكَ الّـذي أَرْسَلْـت" واجعلهن آخر
كلامك فإن مت مت على الفطرة)) – البخاري و مسلم
Kutoka kwa Al-Baraa Bin 'Aazib رضي الله عنهما kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kasema; utakapofika wakati wa kulala, tawadha kama wudhuu wa Swalah, kisha lala upande wako wa kulia, kisha sema: "Allaahumma
aslamtu nafsiy Ilayka, wa fawwadhwtu amriy Ilayka, wa wajjahtu wajhiya
Ilayka, wa aljaatu dhwahriy Ilayka, raghbatan wa rahbatan Ilayka, laa
maljaa wa laa manjaa Minka illa Ilayka, aamantu bi-Kitaabikal-ladhiy Anzalta, wa bi-Nabiyyikal-ladhiy Arsalta"
[Ewe
Allaah, nimeisalimisha nafsi yangu Kwako, na nimekuachia mambo yangu
Wewe na nimeuelekeza uso wangu Kwako na nimeutegemeza mgongo wangu
Kwako, kwa matajarajio na kwa kukuogopa, hapana sehemu ya kukimbilia
wala ya kujiokoa ila Kwako, nimekiamini kitabu Chako Ulichokiteremsha na
Mtume Wako Uliyemtuma] Na fanya hivyo iwe ni maneno yako ya mwisho kwani utakapokufa utakufa katika Fitwrah [(Uislamu])) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hatuna
shaka na tunaamini na kuyafuata mafunzo yake kadiri tuwezavyo kwani
nani msemaye kweli kuliko Allaah (Subhanaahu wa Ta’ala) na Mjumbe Wake
Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)? Mjumbe ambaye
hasemi kwa matamanio yake ila ni wahyi utokao kwa Mola wetu Muumba
Anayesema:
((وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَى)) (( إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَى))
Basi hebu tuone hikma ya kutufunza kulala upande wa kulia.
Ubongo (Brain)
Ubongo sehemu yake huwa upande wa kulia na ndio ambao unauongoza Moyo ulioko upande wa kushoto.
Mapafu (Lungs)
Pafu
la upande wa kulia wa mwili ni kubwa kuliko pafu la upande wa kushoto,
kwa kuwa pafu la upande wa kulia lina sehemu 3 wakati ambapo la upande
wa kushoto lina sehemu 2 tu.
Ini (Liver)
Ini liko upande wa kulia na ndilo tezi (gland) kubwa kubwa kabisa mwilini.
Nyongo (Gall Bladder)
Nyongo nayo nipo upande wa kulia na ina majukumu ya kutengeneza utomvu ambao unameng’enyua (digest) mafuta.
Matumbo (Intestines)
Matumbo (Intestines) Na Sehemu Ya Mwisho Wa Utumbo (colon)
Sehemu ya 'mwisho wa Utumbo mkubwa' (colon) na mwisho wa matumbo (intestines) yako upande wa kulia. (Appendix)
Moyo
Moyo uko upande wa kushoto na ndio pampu la taratibu ya mzungukuo(circulatory system)
Tumeona kwamba kwamba viungo vya mwili vikubwa viko upande wa
kulia katika mwili, kwa hiyo mtu anapolala upande wa kushoto, huathiri
viungo hivi na huleta madhara katika siha ya Binaadamu. Na juu ya hivyo
mtu anapolala upande wa kulia huwa haileti shinikizo katika vyumba vya
mapumziko ya moyo ambazo hufanya wepesi kazi ya Taratibu ya Mzunguko
(circulatory cycle).
Kwa hiyo mtu anayelala upande wa kulia anapoamka asubuhi huamka akiwa mwenye nguvu na mchangamfu.
Hadiyth za Mtume صلى الله عليه وآله وسلم tulizoamrishwa na mapendekezo ya kulala upande wa kulia
عن
أبي هريرة رضي الله عنه قال :" رأى رسول الله صلى الله عليه و سلم رجلاً
مضطجعاً على بطنه فقال ((إن هذه ضجعة يبغضها الله و رسوله))". رواه الترمذي .
Imetoka kwa Abu Hurayrah رضي الله عنه ambaye kasema: Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alimuona mtu amelala kifudifudi, akasema: ((Kulala huku kunachukizwa na Allaah سبحانه وتعالى na Mtume Wake)) [At-Tirmidhy]
عن عائشة أن رسول الله صلى الله عليه وسلم "كان إذاصلى ركعتي الفجر (يعني سنتها) اضطجع على شقه الأيمن" - صحيح البخاري
Imetoka kwa mama wa waumini 'Aaishah رضي الله عنها kwamba "Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akishaswali rakaa mbili za Alfajiri, [yaani Sunnah za Alfajiri] hulala upande wa kulia" [al-Bukhaariy]
عن أبي أمامة قال: مر النبي صلى الله عليه وسلم على رجل نائم في المسجد منبطح على وجهه فضربه برجله وقال: (( قم أو اقعد فإنها نومة جهنمية))
مسند أحمد وسنن ابن ماجه
Kutoka kwa Abu Amaamah kasema; alipita Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kwa
mtu mmoja ambaye alikuwa amelala kifudifudi msikitini akampiga hivi
(teke) kwa mguu akasema: ((Inuka au kaa kwani kulala huku ni kama kulala
kwa watu wa motoni)) [Musnad Ahmad na Sunan Ibn Maajah]
وعن حفصة رضي الله عنها قالت:" كان النبي صلى الله عليه وسلم إذا أخذ مضجعه جعل يده اليمنى تحت خده الأيمن" رواه الطبراني، صحيح الجامع
Kutoka kwa mama wa waumini Hafswah رضي الله عنها ambaye kasema: "Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alikuwa anapotaka kulala huweka mkono wake katika shavu la kulia" [At-Twabraaniy katika Swahiyh al-Jaami'y]
Amesema Imaam Ibn al-Qayyim (Allaah Amrehemu): "Kulala kwake Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa ubavu wake wa kulia kuna siri, nayo ni kuwa Moyo unakuwa juu kwa upande wa kushoto, kwa hivyo, ikiwa atalalia ubavu wake wa kushoto basi usingizi utakuwa mzito; kwani atakuwa katika hali ya utulivu na ushwari na hivyo kuwa usingizi wake ni mzito. Na kama atalala kwa upande wa ubavu wake wa kulia, basi atakuwa katika hali ya wasiwasi na usingizi wake utakuwa si mzito kwa kuwa moyo utakuwa katika hali ya wasiwasi na atahitajia utulie na moyo kupondokeka kwake.