إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ - Tawassul Za Shirki Kufru Na Bid’ah - Kutawassal Kwa 'Ahlul-Badr' Watu wa Badr
Baadhi
ya watu hutawassal kwa uradi unaojulikana katika jamii kama "albadiri"
au "halalbadri" kama wanavyotamka watu wengi wa kawaida.
Jina
lenyewe la tawassul hiyo laonesha wazi jinsi gani watu hawakufahamu
maana yake halisi kama ilivyokusudiwa katika lugha ya Kiarabu kwamba
maana yake ni: ‘Ahlul-Badr’ (Watu wa Badr).
Hao "Ahlul-Badr" ni Maswahaba waliopigana jihaad katika vita vya Badr Na Badr ni jina la mji ulio kiasi cha kilomita mia na khamsini mbali na mji wa Madiynah ambako Waislamu walipopigana vita vya kwanza na
washirikina wa Makkah. Vita hivyo viliongozwa na Nabiy (Swalla Allaahu
'alayhi wa aalihi wa sallam). Baadhi ya mapokezi yanaeleza kuwa walikuwa Waislamu mia tatu na kumi na tatu au kumi na nne na riwaya zingine zinasema kuwa walikuwa mia tatu na kumi na saba.
Hadiyth Ya Wiki
Hadiyth Arubaini: Imaam An-Nawawiy: 07 - Dini Ni Nasiha
Hadiyth Ya 7
الدِّينُ النَّصِيحَةُ
Dini Ni Nasiha
عن
أبي رُقَيَّةَ تَمِيمِ بنِ أوْسٍ الدَّارِيِّ رضي اللهُ عنه: أَنَّ
النَّبي صلى الله عليه وسلم قالَ:((الدِّينُ النَّصِيحَةُ)). قُلْنَا:
لِمَنْ؟ قالَ: ((للهِ، ولِكِتَابِهِ، ولِرَسُولِهِ، ولِلأَئِمةِ
المُسْلِمِينَ، وعامَّتِهِمْ)) رَوَاهُ مُسْلِمٌ
Imepokelewa kutoka kwa
Abuu Ruqayyah Tamiymiy bin Aws Ad-Daarriy (Radhwiya Allaahu 'anhu)
kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Dini
ni nasiha.” Tukauliza: Kwa nani? Akasema: “Kwa Allaah na Kitabu Chake,
na Rasuli Wake, na kwa viongozi wa Waislamu na watu wa kawaida.” [Muslim]
No comments:
Post a Comment