035 - Hadiyth Ya 35: Katika Starehe Bora Kabisa Ya Dunia Ni Mke Mwema
عَنْ
عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو بْنِ الْعَاص (رضي الله عنهما) أَنَّ
رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((الدُّنْيَا
مَتَاعٌ, وَخَيْرُ مَتَاعِ الدُّنْيَا الْمَرْأَةُ الصَّالِحَة)) مسلم
Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amr bin Al-‘Aasw(رضي الله عنهما) kwamba Mtume wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Dunia ni starehe, na bora ya starehe zake ni mke mwema)).[1]
Mafunzo Na Al-manani:
- Umuhimu wa kuchagua mke mwema, mwenye taqwa. [Rejea Hadiyth namba 40].
- Sababu mojawapo ya furaha ya dunia na Aakhirah ni kuwa na mke mwema, mwenye taqwa.
- Fadhila za mwanamke mwema mwenye taqwa kufananishwa na starehe.
زُيِّنَ
لِلنَّاسِ حُبُّ الشَّهَوَاتِ مِنَ النِّسَاءِ وَالْبَنِينَ
وَالْقَنَاطِيرِ الْمُقَنطَرَةِ مِنَ الذَّهَبِ وَالْفِضَّةِ وَالْخَيْلِ
الْمُسَوَّمَةِ وَالْأَنْعَامِ وَالْحَرْثِ ۗ ذَٰلِكَ مَتَاعُ الْحَيَاةِ
الدُّنْيَا ۖ وَاللَّـهُ عِندَهُ حُسْنُ الْمَآبِ ﴿١٤﴾
Watu
wamepambiwa kupenda matamanio (miongoni mwake) wanawake, na watoto, na
mirundi ya mali iliyorundikwa ya dhahabu na fedha na farasi wenye chapa
(ya aina bora) na wanyama wa mifugo na mashamba. Hayo ni burudisho (liwazo) la maisha ya dunia, na Allaah Kwake kuna marejeo mazuri [2]
- Wema na taqwa ni miongoni mwa sifa njema anazopasa mwanamke wa Kiislamu kumiliki. [At-Tahriym 66: 11-12].
- Mume anayeruzukiwa mke mwema ni neema kwake. Inampasa ailinde neema kwa kukaa naye vyema na kuwa na huruma naye, mapenzi ili apate kudiriki starehe za dunia na Aakhirah. [Ar-Ruwm 30: 21, An-Nuwr 24: 26].
No comments:
Post a Comment