Wednesday, 12 October 2016

Ukumbusho Wa Kukithirisha Swawm Mwezi Wa Muharram Na Swawm Za Ayyaamul-Biydhw

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: 
((أَفْضَلُ الصِّيَامِ بَعْدَ رَمَضَانَ شَهْرُ اللَّهِ الْمُحَرَّمُ)) رواه مسلم
Swiyaam (funga) bora kabisa baada ya Ramadhwaan ni swawm ya mwezi wa Allaah wa Muharram [Muslim]
Pia, tunapenda kuwakumbusha swawm za Ayyaamul-Biydhw (masiku meupe) ambayo ni tarehe 13, 14, 15 katika kila mwezi wa Kiislaam (Hijriyyah). Masiku hayo mwezi huu wa Muharram 1438H, yataangukia tarehe 14, 15, 16 Oktoba (Ijumaa, Jumamosi, Jumapili). 
عَنْ أَبي ذَرٍّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيهِ وَسَلَّمَ:((مَنْ صَامَ مِنْ كُلِّ شَهْرٍ ثَلاثَةَ أَيَّامٍ فَذَلِكَ صِيَامُ الدَّهْرِ)) فَأَنْزَلَ اللهُ تُصْدِيقَ ذَلِكَ في كِتَابِهِ الْكَرِيمِ: ((مَنْ جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا))، الْيَوْمُ بِعَشَرَةِ أَيّامٍ. أخرجه أحمد والترمذي وقال حديث حسن ، والنسائي وابن ماجه وابن خزيمة
Imepokelewa kutoka kwa Abu Dharr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam amesema: ((Yeyote atakaye swawm kila mwezi siku tatu, ni sawa na swawm ya milele)) Kisha Allaah Akateremsha Aayah ithibitishayo hayo: “Atakayekuja kwa amali nzuri basi atapata (thawabu) kumi mfano wa hiyo.”  Siku moja kwa malipo ya siku kumi. [Imepokewa na At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Hasan, An Nasaaiy na Ibn Maajah, Ibn Khuzaymah na ameisahihisha Shaykh Al-Albaaniy katika Al-Irwaa (4/102)]. Aayah: Suwrat Al-An’aam (160)]
Bonyeza: 'Endelea' upate faida nyenginezo.

Nasiha Za Wiki

إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ --- Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! 23- Sihri (Uchawi) Na Michezo Ya Mazingaombwe

Neno “As-Sihr” (uchawi) maana yake ni kitendo cha kujikurubisha na shaytwaan na kwa msaada wake (shaytwaan) na uchawi ni kulibadilisha jambo mbali na uhakika wake, nako ni kuwadhihirishia watu jambo lisilo la kweli wakaliona kuwa ni la kweli.” [Lisaan Al-‘Arab]
Na Sihri ni tendo la kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa kuwa linahusiana na shaytwaan 'aaswi mwenye kumkufuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):   
وَاتَّبَعُوا مَا تَتْلُو الشَّيَاطِينُ عَلَىٰ مُلْكِ سُلَيْمَانَ ۖ وَمَا كَفَرَ سُلَيْمَانُ وَلَـٰكِنَّ الشَّيَاطِينَ كَفَرُوا يُعَلِّمُونَ النَّاسَ السِّحْرَ وَمَا أُنزِلَ عَلَى الْمَلَكَيْنِ بِبَابِلَ هَارُوتَ وَمَارُوتَ ۚ وَمَا يُعَلِّمَانِ مِنْ أَحَدٍ حَتَّىٰ يَقُولَا إِنَّمَا نَحْنُ فِتْنَةٌ فَلَا تَكْفُرْ ۖ فَيَتَعَلَّمُونَ مِنْهُمَا مَا يُفَرِّقُونَ بِهِ بَيْنَ الْمَرْءِ وَزَوْجِهِ ۚ وَمَا هُم بِضَارِّينَ بِهِ مِنْ أَحَدٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ وَيَتَعَلَّمُونَ مَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ ۚ وَلَقَدْ عَلِمُوا لَمَنِ اشْتَرَاهُ مَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِنْ خَلَاقٍ ۚ وَلَبِئْسَ مَا شَرَوْا بِهِ أَنفُسَهُمْ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿١٠٢﴾
Na wakafuata yale waliyoyasoma mashaytwaan juu ya ufalme wa Sulaymaan; na Sulaymaan hakukufuru lakini mashaytwaan ndio waliokufuru; wanafundisha watu sihri na yaliyoteremshwa kwa Malaika wawili katika (mji wa) Baabil; Haaruwt na Maaruwt. Nao wawili hawamfundishi yeyote mpaka waseme: “Hakika sisi ni mtihani, basi usikufuru.” Kisha wakajifunza kutoka kwa hao wawili yenye kupelekea kufarikisha kwayo baina ya mtu na mkewe. Na wao hawawezi kamwe kumdhuru yeyote kwayo isipokuwa kwa idhini ya Allaah; na wanajifunza yanayowadhuru na wala hayawanufaishi; na kwa yakini walijua kwamba atakayeinunua (sihiri) hatopata katika Aakhirah fungu lolote, na ni ubaya ulioje walichouzia kwayo nafsi zao, lau wangelikuwa wanajua. [Al-Baqarah: 102]
Pia, sihri ni miongoni mwa Al-Kabaair (madhambi makubwa) na ni miongoni mwa ambayo yanamuangamiza mtu kwa dalili ya Hadiyth:

No comments: