Thursday, 30 December 2021

HAYA NDIO MAISHA YA MUISLAMU WA KWELI. 1. TUZUNGUMZE KIISLAM Muislam wa kweli ni lazima awe ni mkweli, hatakiwi kuzua uongo, kufitinisha, kusengenya wala kuzungumza kwa sauti ya juu. Haya tunayapata ndani ya Qur-aan: {{Na uteremshe sauti yako; bila shaka sauti ya punda ni mbaya kuliko sauti zote (kwa makelele yake ya bure).}} [Surat Luqmaan: 19] Pia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametuhimiza sana kushikamana katika kusema ukweli: “Shikamaneni na ukweli, kwani ukweli unapeleka katika wema, na wema unapeleka Peponi.” [Muslim] *2. TULE KIISLAM* Muislam anatakiwa ale kilicho mbele yake kwa kutumia mkono wa kulia na asiwe na papara ya kusukuma tonge namna ya kima anavyokula. Aanze kula kwa kusema “BismiLlaah” na amalize kwa kusema “AlhamduliLlaahilladhi atwa'amani haadha ttwa'am warazaqanihi min ghairi hauli minni walaquwwa”. Chakula cha Muislam ni lazima kiwe ni cha halali, hatakiwi kula ovyo ovyo kama wanavyofanya wasiokuwa Waislam. Anapokula aligawe tumbo lake kwenye thuluthi tatu. Thuluthi moja ni ya chakula, nyengine ni ya maji na mwisho ni hewa. Hii ni kwa mujibu wa dalili ya Hadityh: "Kama ukilazimika kula hakikisha theluthi moja ya tumbo lako unaijaza chakula, theluthi moja maji na acha theluthi moja kwa ajili ya hewa (yaani iache tupu)” (At-Tirmidhiy). *3. TUSIKILIZE KIISLAMU* Muziki ni haramu na haifai kwa Muislam kuutengeneza, kutengenezewa, kuimba, kuimbiwa, kuutangaza, kuupeleka muziki, kuuza, kula thamani yake, kununua na kuuza. Muziki umekuwa ni tatizo kubwa kwa Waislam kwani wengine hata usingizi hawapati bila ya kusikiliza muziki. Nyumba za Kiislam sasa zimekuwa sawa na magofu kwa kutopatikana maadili ya Kiislam. Kwani wengi wanaishi tofauti na mafundisho ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Ni muhimu kwa Waislam wakawa wanasoma Qur-aan kila siku kwa sauti na kwa kusikilizana kwa mtindo wa dawaar (mmoja baada ya mwengine). Tuzibadilishe nyumba zetu kwa kusikiliza idhaa za Kiislam zisizokuwa na mambo ya uchafu na uzushi. {{Na soma Qur-aan kwa utaratibu na utungo.}} [Al-Muzammil 73: 4] Muislam anayesoma Qur-aan atakuwa pamoja na Malaika na Mitume (‘Alayhi swalaatu was-salaam). Hata yule asiyejua kusoma Qur-aan ni vyema akawa na jitihada ya kujifundisha ilhali anakosea au hata kuchekwa. Amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Yule ambaye kwamba anasoma Qur-aan naye ni mjuzi (hana shida aina yoyote) atakuwa pamoja na Malaika na Mitume (‘Alayhi swalaatu was-salaam) na watiifu. Na yule ambaye kwamba anarudia pamoja na kuwa na shida katika kusoma basi atakuwa na ujira mara mbili )) [al-Bukhaariy, Muslim, Tirmidhy na Ibn Maajah kutoka kwa ‘Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha)] *4. TUVAE NA TUTEMBEE KIISLAM* Maringo ya kutembea bila ya shaka yanatokana na mtu kuvaa nguo za kifakhari ambazo hazitakiwi kuvaliwa kwa Muislam. Muislam wa kiume anatakiwa avae nguo zisizoburura. Mwanamke hatakiwi kuonekana zaidi ya viganja vya mikono na kipaji cha sura yake. Mapambo yote ni halali kwa mumewe na walio Maharimu wake. Haitakikani Muislam kutembea kwa kujivuna, kujifakharisha na maringo. Hivi sivyo Uislam unavyotufundisha kuishi. Qur-aan inasema: {{Wala usitembee katika ardhi kwa maringo. Hakika wewe huwezi kuipasua ardhi wala huwezi kufikia urefu wa milima}} [Surat Israa: 37] Usiwaangalie watu kwa jeuri au kwa upande mmoja wa uso. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema: {{Wala usiwatazame (usiwafanyie watu jeuri), kwa upande mmoja wa uso, wala usende katika ardhi kwa maringo, hakika Allaah hampendi kila ajivunaye, ajifaharishaye.}} [Surat Luqmaan:18] *5. TUJENGE URAFIKI WA KIISLAM* Miongoni mwa matatizo makubwa ya vijana wetu pamoja na Waislam kukosa maadili ya Kiislam ni kuwa na marafiki wasiokuwa na maadili mema. Ni vyema Muislam akawa hana rafiki hata mmoja kuliko kuwa na marafiki kumi wasioishi Kiislam. Kuishi Kiislam yatakikana juhudi na inaanza kwa kuwa na rafiki mwema atakayekukemea unapofanya kosa na kukupa maneno ya subra wakati wa huzuni. Lazima tuchague marafiki ambao wako radhi na dini yetu na tuepukane na wale ambao hawako radhi na dini yetu. Na tukiona marafiki zetu matendo yao sio mazuri, ni lazima tuepukane nao kwa sababu tunaweza tukaiga tabia zao ambazo zinakwenda kinyume na diyn yetu. Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mtu yamkini kufuata dini ya rafiki yake, kwa hivyo muangalie unayemfanya rafiki.” (Abuu Daawuud na At-Tirmidhiy) *6. TULALE KIISLAM* Tumalizie kwa kuona namna anavyotakiwa Muislam kuimaliza siku yake kwa kujipumzisha Kiislam. Muislam anatakiwa atie wudhuu kabla ya kulala, wudhuu unaendana na Sunnah ya kupiga mswaki. Ni vizuri ukaswali rakaa tatu za witri (kwa wasioamka usiku). Alikuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akienda kulala usiku anakusanya viganja vyake kisha akivipuliza na akivisomea Suratul-Ikhlaas, na Suratul-Falaq, na Suratun-Naas, kisha akipangusa kwa hivyo viganja vyake kiasi anachoweza katika mwili wake, akianza kichwani na usoni na mbele (akifanya hivyo mara tatu). Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Ukienda kulala soma Ayatul-Kursiy mpaka uimalize kwani Allaah Ataendelea kukuhifadhi wala hakukaribii shaytwaan mpaka asubuhi” Unapolala ulaze ubavu kwa upande wa kulia na usome du’aa ifuatayo: ﺍﻟﻠّﻬُـﻢَّ ﺃَﺳْـﻠَﻤْﺖُ ﻧَﻔْـﺴﻲ ﺇِﻟَـﻴْﻚَ، ﻭَﻓَﻮَّﺿْـﺖُ ﺃَﻣْـﺮﻱ ﺇِﻟَـﻴْﻚَ، ﻭَﻭَﺟَّـﻬْﺖُ ﻭﺍ ﺟْـﻬﻲ ﺇِﻟَـﻴْﻚَ، ﻭَﺃَﻟْـﺠَـﺎْﺕُ ﻇَﻬـﺮﻱ ﺇِﻟَـﻴْﻚَ، ﺭَﻏْﺒَـﺔً ﻭَﺭَﻫْـﺒَﺔً ﺇِﻟَـﻴْﻚَ، ﻻ ﻣَﻠْﺠَـﺄَ ﻭَﻻ ﻣَﻨْـﺠـﺎ ﻣِﻨْـﻚَ ﺇِﻻّ ﺇِﻟَـﻴْﻚَ، ﺁﻣَﻨْـﺖُ ﺑِﻜِﺘـﺎﺑِﻚَ ﺍﻟّـﺬﻱ ﺃَﻧْﺰَﻟْـﺖَ ﻭَﺑِﻨَﺒِـﻴِّـﻚَ ﺍﻟّـﺬﻱ ﺃَﺭْﺳَﻠْـﺖ “Ewe Allaah nimeisalimisha nafsi yangu kwako, na nimekuachia mambo yangu Wewe na nimeuelekeza uso wangu kwako na nimeutegemeza mgongo wangu kwako, kwa matarajio na kwa kukuogopa, hapana sehemu ya kukimbilia wala ya kujiokoa ila kwako, nimekiamini kitabu chako ulichokiteremsha na Mtume wako uliyemtuma”. Na hizi hapa ni Nyiradi za kulala. Bila ya shaka tutakapoishi Kiislam tutakuwa mbali na wasiokuwa Waislam. Hivyo maisha yetu yatakuwa hakika ni ya Kiislam. Kila kitu yatakikana juhudi na inaanza kwa nafsi kujifunga kukubali mafundisho ya Kiislam. Inawezekana kubadilika kwa kuishi Kiislam. Anza sasa, katu usichelewe. **** Jiunge nasi katika Ukurasa wetu wa Uislamu Dini Yangu kwa Kubonyeza kitufe cha "Like" uwe mmoja wa ndugu walio katika ukurasa huu...

Thursday, 15 October 2020

SIFA TANO ZA MKE MWEMA..

Je, Mtume swalla llahu alleh wasalaaam ametufunfundisha nini kuhusu sifa njema za wake?

1-Ni watiifu kuwa waume zao: Abu Huraira alipokea kutoka kwa Mtume swalla llahu alleh wasalaaam kwamba alisema: “Mke bora ni yule ambaye ukimuangalia anakupendeza, ukimuarisha jambo anakutii na unapokuwa haupo, analinda hadhi na mali yako.” [Ibn Jarir]
Amesema Allah “…basi wanawake wema ni wale wenye kutii, wanaojifadhi wasipokuwapo waume zao kwa kuwa Allah amewaamrisha wajifadhi.” [An-Nisaa: 34]

2- Wanazistitiri miili yao: Amesema Allah: “Ewe Mtume! Waambie wake zako, binti zako na wanawake wa Kiislamu wajiteremshie uzuri nguo zao. Kufanya hivyo kutapeleka upesi wajulikane kuwa ni watu wa heshima ili wasiudhiwe. Na Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu.” [Azhaab: 59]"

3-Hawaombi talaka bila sababu ya kisheria: Amesema Mtume swalla llahu alleh wasalam: “Mke yeyote atakayemuomba mumewe talaka pasina sababu ya kisheria, ataharamishwa pepo hata harufu ya pepo hatoisikia.” [Tirmidhi]

4-Wanasimamisha Swalaah: Amesema Mtume swalla llahu alleh wasalaaam: “Mwanamke akiswali swalah tano, akafunga saumu, akailinda tupu yake na kumtii mumewe, ataambiwa, ‘ingia peponi kwa mlango wowote uupendao.” [Imaam Ahmad]

5- Hawawakasirikii waume zao bure: Asema Mtume swalla llahu alleh wasalaaam: “Laana ya Allah iko juu ya mwanamke anaemkasirikia mumewe bila sababu,"

Uislamu Dini Yangu

Maelezo ya picha hayapo.

 

Wednesday, 15 February 2017

Ipi hekma ya kulala upande wa kulia kamaalivyofundisha Mtume Muhamady

Nini Hikma Ya Kulala Upande Wa Kulia Kama Alivyotufundisha Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ?

Yote tunayoyapata kutoka katika Sunnah ya mwalimu wetu, Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni mafunzo yenye faida kwetu ima faida ya nafsi zetu au faida katika mwili wetu au faida katika maisha yetu na kwa ujumla, bali kuna hikma kubwa kwenye mafunzo hayo:
عن البراء بن عازب رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه و قال صلى الله عليه وسلم : ((إذا أتيت مضجعك فتوضأ وضوءك للصلاة ثم ثم اضطجع على شقك الأيمن ثم قل :  أللهم  أَسْـلَمْتُ نَفْـسي إِلَـيْكَ، وَفَوَّضْـتُ أَمْـري إِلَـيْكَ، وَوَجَّـهْتُ وَجْـهي إِلَـيْكَ، وَأَلْـجَـاْتُ ظَهـري إِلَـيْكَ، رَغْبَـةً وَرَهْـبَةً إِلَـيْكَ، لا مَلْجَـأَ وَلا مَنْـجـا مِنْـكَ إِلاّ إِلَـيْكَ، آمَنْـتُ بِكِتـابِكَ الّـذي أَنْزَلْـتَ وَبِنَبِـيِّـكَ الّـذي أَرْسَلْـت"   واجعلهن آخر كلامك فإن مت مت على الفطرة)) – البخاري و مسلم
Kutoka kwa Al-Baraa Bin 'Aazib رضي الله عنهما kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kasema; utakapofika wakati wa kulala, tawadha kama wudhuu wa Swalah, kisha lala upande wako wa kulia, kisha sema:  "Allaahumma aslamtu nafsiy Ilayka, wa fawwadhwtu amriy Ilayka, wa wajjahtu wajhiya Ilayka, wa aljaatu dhwahriy Ilayka, raghbatan wa rahbatan Ilayka, laa maljaa wa laa manjaa Minka illa Ilayka, aamantu bi-Kitaabikal-ladhiy Anzalta, wa bi-Nabiyyikal-ladhiy Arsalta"
[Ewe Allaah,  nimeisalimisha nafsi yangu Kwako, na nimekuachia mambo yangu Wewe na nimeuelekeza uso wangu Kwako na nimeutegemeza mgongo wangu Kwako, kwa matajarajio na kwa kukuogopa, hapana sehemu ya kukimbilia wala ya kujiokoa ila Kwako, nimekiamini kitabu Chako Ulichokiteremsha na Mtume Wako Uliyemtuma] Na fanya hivyo iwe ni maneno yako ya mwisho kwani utakapokufa utakufa katika Fitwrah [(Uislamu]))  [Al-Bukhaariy na Muslim] 
Hatuna shaka na tunaamini  na kuyafuata  mafunzo yake kadiri tuwezavyo  kwani nani msemaye kweli kuliko Allaah (Subhanaahu wa Ta’ala) na Mjumbe Wake Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)? Mjumbe ambaye hasemi kwa matamanio yake ila ni wahyi utokao kwa Mola wetu Muumba Anayesema:
((وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَى))  (( إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَى))
((Wala hatamki kwa matamanio)) ((Hayakuwa haya ila ni ufunuo ulio funuliwa)) [An-Najm: 3-4]

Basi hebu tuone hikma ya kutufunza kulala upande wa kulia.



  

Ubongo (Brain)

 
Ubongo sehemu yake huwa upande wa kulia na ndio ambao unauongoza Moyo ulioko upande wa kushoto.


Mapafu (Lungs)



Pafu la upande wa kulia wa mwili ni kubwa kuliko pafu la upande wa kushoto, kwa kuwa pafu la upande wa kulia lina sehemu 3 wakati ambapo la upande wa kushoto lina sehemu 2 tu.
Ini (Liver)

   
Ini liko upande wa kulia na ndilo tezi (gland) kubwa kubwa kabisa mwilini.


Nyongo (Gall Bladder)


 
Nyongo nayo nipo upande wa kulia na ina majukumu ya kutengeneza utomvu ambao unameng’enyua (digest) mafuta.

 
 
Matumbo (Intestines)


 

Matumbo (Intestines) Na Sehemu Ya Mwisho Wa Utumbo (colon)

 


Sehemu ya 'mwisho wa Utumbo mkubwa' (colon) na mwisho wa matumbo (intestines) yako upande wa kulia. (Appendix) 
 
 
Moyo 
 

Moyo uko upande wa kushoto na ndio pampu la taratibu ya mzungukuo(circulatory system)
Tumeona kwamba  kwamba viungo vya mwili vikubwa viko upande wa kulia katika mwili, kwa hiyo mtu anapolala upande wa kushoto, huathiri viungo hivi na huleta madhara katika siha ya Binaadamu. Na juu ya hivyo mtu anapolala upande wa kulia huwa haileti shinikizo katika vyumba vya mapumziko ya moyo ambazo hufanya wepesi kazi ya Taratibu ya Mzunguko (circulatory cycle).
Kwa hiyo mtu anayelala upande wa kulia anapoamka asubuhi huamka akiwa mwenye nguvu na  mchangamfu.
Hadiyth za  Mtume صلى الله عليه وآله وسلم tulizoamrishwa na mapendekezo ya kulala upande wa kulia

عن أبي  هريرة رضي الله عنه قال :" رأى رسول الله صلى الله عليه و سلم رجلاً مضطجعاً على بطنه فقال ((إن هذه ضجعة يبغضها الله و رسوله))". رواه الترمذي  .
Imetoka kwa Abu Hurayrah رضي الله عنه ambaye kasema: Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alimuona mtu amelala kifudifudi, akasema: ((Kulala huku kunachukizwa na Allaah سبحانه وتعالى na Mtume Wake)) [At-Tirmidhy]

  عن  عائشة أن رسول الله  صلى الله عليه وسلم   "كان   إذاصلى  ركعتي    الفجر    (يعني سنتها)  اضطجع على شقه   الأيمن"  - صحيح البخاري
Imetoka kwa mama wa waumini 'Aaishah رضي الله عنها  kwamba "Mtume صلى الله عليه وآله وسلم  akishaswali rakaa mbili za Alfajiri, [yaani Sunnah za Alfajiri]  hulala upande wa kulia" [al-Bukhaariy] 
  


عن أبي أمامة قال: مر النبي صلى الله عليه وسلم على رجل نائم في المسجد منبطح على وجهه فضربه برجله وقال: (( قم أو اقعد فإنها نومة جهنمية))
 مسند أحمد وسنن ابن ماجه
Kutoka kwa Abu Amaamah kasema; alipita Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kwa mtu mmoja ambaye alikuwa amelala kifudifudi  msikitini akampiga hivi (teke) kwa mguu akasema: ((Inuka au kaa kwani kulala huku ni kama kulala kwa watu wa motoni))   [Musnad Ahmad na Sunan Ibn Maajah]

وعن حفصة رضي الله عنها قالت:" كان النبي صلى الله عليه وسلم إذا أخذ مضجعه جعل يده اليمنى تحت خده الأيمن" رواه الطبراني، صحيح الجامع  
Kutoka kwa mama wa waumini Hafswah رضي الله عنها   ambaye kasema: "Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alikuwa anapotaka kulala huweka mkono wake katika shavu la kulia" [At-Twabraaniy katika Swahiyh al-Jaami'y]
Amesema Imaam Ibn al-Qayyim (Allaah Amrehemu): "Kulala kwake Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa ubavu wake wa kulia kuna siri, nayo ni kuwa Moyo unakuwa juu kwa upande wa kushoto, kwa hivyo, ikiwa atalalia ubavu wake wa kushoto basi usingizi utakuwa mzito; kwani atakuwa katika hali ya utulivu na ushwari na hivyo kuwa usingizi wake ni mzito. Na kama atalala kwa upande wa ubavu wake wa kulia, basi atakuwa katika hali ya wasiwasi na usingizi wake utakuwa si mzito kwa kuwa moyo utakuwa katika hali ya wasiwasi na atahitajia utulie na moyo kupondokeka kwake.

Uharamu wa Valentine day

Valentine (Siku Ya Wapendanao) Na Hukumu Ya Kuisherehekea


BismiLLaah wa AlhamduliLLaah was-Swalaatu was Salaamu ‘alaa Muhammad wa ‘alaa ‘Aalihi wa Aswhaabihil Kiraam, wa Ba’ad,

Allaah سبحانه وتعالى Ametuchagulia Dini ya Kiislamu, Dini ya haki na Hatokubali dini yoyote nyingine. Anasema: 
((وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الإِسْلاَمِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ))  
((Na yeyote anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislaam basi haitokubaliwa kwake; naye katika Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika)) [Al-'Imraan: 85]

Na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ametuambia kuwa kutakua na makundi katika ummah wake ambao watawafuata maadui wa Allaah سبحانه وتعالى katika desturi na mila zao: 
((ستتبعون سنن من كان قبلكم شبراً بشبر وذراعاً بذراع حتى لو دخلوا جحر ضب لدخلتموه)) قالوا: أتراهم اليهود والنصارى؟ قال: ((فمن إذن؟)) البخاري ومسلم
((Mtafuata nyendo  za wale waliokuja  kabla yenu  hatua kwa hatua mpaka itafika hadi wakiingia katika shimo la kenge, na nyinyi mtaingia pia)) Wakasema (Maswahaba):  Ee Mtume! Je, unamaanisha Mayahudi na Manaswara? Akasema: ((Hivyo nani basi mwengine?)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

Maneno hayo aliyoyasema Mtume صلى الله عليه وآله وسلم hakika yamethibiti kwa sababu imedhihirika Waislamu kuigizia mila, desturi na tabia za makafiri na kuzisherehekea kama mfano siku hii inayoitwa 'Valentine day' (Siku ya Wapendanao).

Na baya zaidi na la kusikitisha sana ni kwamba sherehe hizi zinaenezwa katika njia mbali mbali za mawasiliano kama kutumiana kadi, barua pepe (e-mail), salamu katika simu za mkono. Hakika fitnah hii humfanya Muislamu aharibu 'Aqiydah (Iymaan) yake kwa kudhani kuwa anafanya jambo la kawaida na hali ni jambo lisilo katika shariy'ah ya dini yetu bali ni shirki kubwa na upotofu wa kufuata wanayoamini makafiri.


Historia Ya Sherehe Ya Siku Ya Valentine

Sherehe hii ya wapendanao ni sherehe ya wapagani  wa Kirumi wakati dini yao ya upagani ilikuwa ni dini iliyotapakaa kwa Warumi karne zaidi ya kumi na saba zilizopita.  Na fikra zao ilikuwa ni kuelezea hisia ya 'mapenzi ya kiroho'.

Kulikuwa na visasili (uongo) zilizohusishwa na sherehe hii ya upagani ya Warumi ambao umeendelea kutoka warithi wa Kikiristo. Miongoni mwa uongo huo ni kuamini kwao Warumi kuwa Romulus, aliyevumbua Rome, alinyonyeshwa siku moja na mbwa mwitu mwanamke, hivyo akampa nguvu na hikmah.

Warumi walikuwa wakisherehekea tukio hili katikati ya Februari kila mwaka kwa kufanya sherehe kubwa. Na mojawapo ya tambiko katika sherehe hii ni kuchinja mbwa au mbuzi. Vijana wawili wenye nguvu hujipaka damu ya mbwa au ya mbuzi katika miili yao, kisha huiosha damu hiyo kwa maziwa. Baada ya hapo, watu hufanya gwaride wakiwa vijana hawa wawilii wako mbele wakiongoza gwaride iliyokuwa ikitembea barabarani. Vijana hao wawili walikuwa wakichukua vipande vya ngozi ambavyo waliwapigia watu wanaowavuka. Wanawake wa kirumi walikuwa wakipokea mapigo hayo wakiamini kuwa yatawahifadhi na kutibu utasa.


Kuungamana Baina Mtakatifu Valentine (Saint Valentine) Na Sherehe Hii

Mtakatifu Valentine (Saint Valentine) ni jina waliopewa mashujaa wawili wakongwe waliokufa ambao ni wana wa kanisa la kikiristo. Inasemekena kwamba walikuwa ni wawili au mmoja tu. Huyo mmoja alikufa Rome kutokana na mateso ya kiongozi wa Kigothi aliyeitwa Claudius. Kanisa la Saint Valentine lilijengwa kwa ajili ya kudumisha kumbukumbu yake.

Warumi walipoingia ukristo, wakaendelea kusherehekea sikukuu ya wapendanao (valentine day) lakini wakabadilisha kutoka fikra ya upagani ya 'mapenzi ya kiroho' (spiritual love) na kuleta fikra nyingine iliyojulikana kama ni 'mapenzi ya mashujaa' yaliyowakilishwa na Saint Valentine ambaye aliuliwa kwa ajili ya kutetea mapenzi na amani. Vile vile ikajulikana ni sikukuu ya wapenzi, na Saint Valentine alifanywa kuwa ni mlezi wa mapenzi ya mtakatifu.

Miongoni mwa imani yao inayoambatana na sherehe hii ni kwamba majina ya wasichana waliofika umri wa kuolewa yaliandikwa katika vikaratasi vidogo vilivyokunjwa mviringo kisha vikawekwa katika chombo juu ya meza. Kisha wavulana waliotaka kuoa waliitwa na kila mmoja huchagua karatasi moja ikiwa na jina la msichana. Kisha hujiambatanisha naye huyo msichana aliyempata kutokana na kura hiyo aliyochagua kwa muda wa mwaka ili wajuane vizuri kisha tena hufunga ndoa, au kama hawakuelewana hurudia tena kufanya kura inapofika siku hiyo mwaka unaofatia.   

Vile vile imesemekana kwamba chanzo cha sikukuu hii, ni kwamba warumi walipokuwa wakristo baada ya ukristo kutapakaa, Mfalme wa Kirumi Claudius II alitoa hukumu katika karne ya tatu kwamba askari wasioe kwa sababu kuoa kwao kutawashughulisha na vita walivyokuwa wakipigana. Hukumu hiyo ilipingwa na Saint Valentine ambaye alianzisha kuozesha maaskari kwa siri. Alipokuja kujua mfalme, alimfunga jela na akamhukumu kuuliwa. Huko jela akapendana na mtoto wa mkuu wa jela, lakini ikawa ni siri kwani kutokana na sheria ya ukristo, mapadri na makasisi wameharamishwa kuoa au kupenda.
Hata hivyo alipewa heshima yake na wakristo kwa sababu ya kushikilia na kujikita imara katika ukristo wakati mfalme alipotaka kumsamehe kwa sharti aache ukristo na kuabudu miungu ya Kirumi ili awe msiri wake na awe mkwe wake. Lakini Saint Valentine alikataa ahadi hiyo na akapendelea ukristo, kwa hiyo akauliwa siku ya tarehe 14 Februari 270 M. Ndio ikaitwa siku hii kwa jina la huyo mtakatifu (Valentine).

Papa (Pope) naye akaifanya siku hiyo ya kufa Saint Valentine tarehe 14 Februari 270 M kuwa ni sikukuu ya mapenzi. Na ni nani alikuwa Papa huyo? Ni Askofu mkuu wa kanisa la 'universal church', ambaye ni mrithi wa mtakatifu Peter.

Ndugu Waislamu tazameni vipi huyo askofu anavyohusika katika kuadhimisha sikukuu hii ambayo ni uzushi katika dini yao ya Kikiristo. Hii itukumbushe kauli ya Allaah سبحانه وتعالى:
((اتَّخَذُواْ أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللّهِ))
((Wamewafanya Wanavyuoni wao mafuqahaa wa dini na Wamonaki wao kuwa ni miola badala ya Allaah)) [At-Tawbah: 31]


Matendo Yanayotakiwa Kujiepusha Nayo Ambayo Yanayofanyika Katika Sikukuu Hii   
1.     Kuonyeshana bashasha na furaha kama ilivyo katika sikukuu zao nyingine.

2.     Kupeana mawaridi mekundu (Red Roses) ambayo ni alama ya kuelezea mapenzi, 'mapenzi ya kiroho' ya wapagani au 'mapenzi' ya Wakristo. Hivyo inajulikana kuwa ni 'Sikukuu Ya Wapendanao'.

3.     Kupelekeana kadi. Na kadi nyingine zina picha za 'mungu wa mapenzi wa kirumi' ambaye ana mbawa mbili, akiwa amekamata upinde na mshale. Huyu ndio mungu wa mapenzi wa wapagani warumi. Shirk iliyoje hii ndugu Waislamu?

4.     Kubadilishana maneno ya mapenzi na matamanio katika kadi wanazopelekeana, yakiwa katika mfumo wa kimashairi, tenzi na sentensi fupi fupi. Kadi nyingine zina picha za kimzaha na maneno ya kuchekesha, na mara nyingi zina maneno ya kusema 'Kuwa Valentine wangu'. Hii inaashiria maana ya kikiristo ya sikukuu hii baada ya kuwa asili yake ni kutokana na fikra za upagani.

5.     Katika nchi nyingi za kimagharibi, hufanyika sherehe siku hiyo ambayo kunakuweko kuchanganyika wanaume na wanawake, kuimba, na kucheza dansi. Na wengi wanapelekeana zawadi kama mawaridi, maboksi ya chokoleti kwa wake zao, marafiki na wanaowapenda.

Kutokana na maelezo yote hayo ya chanzo cha sikukuu hii, tunaona kwamba siku hiyo haina uhusiano wowote katika Uislamu, bali yana uhusiano na washirikina mapagani, hata wakristo katika dini yao nao pia ni uzushi, sasa itakuwaje sisi Waislamu tuwaigize kusherehekea? 

Basi ndugu Waislamu tutambue kuwa jambo hili ni ovu mno, haimpasi Muislamu kuharibu 'Aqiydah (iymaan) yake kwani kuna hatari kubwa kushiriki katika sherehe hii nayo ni kuingia katika kumshirikisha Allaah سبحانه وتعالى, na kama tunavyojua kuwa Allaah سبحانه وتعالى Hamsamehe mtu anayefanya shirki pindi akifariki bila ya kutubu kama ilivyo katika aya ifuatayo: 
 ((إِنَّ اللّهَ لاَ يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَلِكَ لِمَن يَشَاء وَمَن يُشْرِكْ بِاللّهِ فَقَدِ افْتَرَى إِثْمًا عَظِيمًا))
((Hakika Allaah Haghufuri kushirikishwa; lakini Anaghufuria yasiyokuwa hayo kwa Amtakae.  Na yeyote atakayemshirikisha Allaah basi kwa yakini amebuni dhambi kuu)) [An-Nisaa: 48]

Hivyo ni kuharamishwa na Pepo na kupata makazi ya moto, tunajikinga na Allaah kwa hayo.

((إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللّهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللّهُ عَلَيهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَار))
((Hakika mwenye kumshirikisha Allaah bila shaka Allaah Atamharamishia Jannah, na makazi yake yatakuwa ni motoni. Na madhalimu hawatopata yeyote mwenye kunusuru)) [Al-Maaidah: 72]

Tunamuomba Allaah سبحانه وتعالى Atuepushe na kila aina ya shirk na Atuoneshe yaliyo ya haki tuyafuate, na yaliyo ya batili tujiepushe nayo na Atuajaalie ni miongoni mwa wale wanaosikiliza kauli (nyingi) wakafuata zile zilizo njema. Aamiyn


إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ - Tawassul Za Shirki Kufru Na Bid’ah - Kutawassal Kwa 'Ahlul-Badr' Watu wa Badr

Baadhi ya watu hutawassal kwa uradi unaojulikana katika jamii kama "albadiri" au "halalbadri" kama wanavyotamka watu wengi wa kawaida.
Jina lenyewe la tawassul hiyo laonesha wazi jinsi gani watu hawakufahamu maana yake halisi kama ilivyokusudiwa katika lugha ya Kiarabu kwamba maana yake ni: ‘Ahlul-Badr’ (Watu wa Badr). 
Hao "Ahlul-Badr" ni Maswahaba waliopigana jihaad katika vita vya Badr Na Badr ni jina la mji ulio kiasi cha kilomita mia na khamsini mbali na mji wa Madiynah ambako Waislamu walipopigana vita vya kwanza na washirikina wa Makkah. Vita hivyo viliongozwa na  Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Baadhi ya mapokezi yanaeleza kuwa walikuwa Waislamu mia tatu na kumi na tatu au kumi na nne na riwaya zingine zinasema kuwa walikuwa mia tatu na kumi na saba.

Hadiyth Ya Wiki

Hadiyth Arubaini: Imaam An-Nawawiy: 07 - Dini Ni Nasiha

Hadiyth Ya 7
الدِّينُ النَّصِيحَةُ
Dini Ni Nasiha
عن أبي رُقَيَّةَ تَمِيمِ بنِ أوْسٍ الدَّارِيِّ رضي اللهُ عنه: أَنَّ النَّبي صلى الله عليه وسلم قالَ:((الدِّينُ النَّصِيحَةُ)). قُلْنَا: لِمَنْ؟ قالَ: ((للهِ، ولِكِتَابِهِ، ولِرَسُولِهِ، ولِلأَئِمةِ المُسْلِمِينَ، وعامَّتِهِمْ)) رَوَاهُ مُسْلِمٌ    
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Ruqayyah Tamiymiy bin Aws Ad-Daarriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Dini ni nasiha.” Tukauliza: Kwa nani? Akasema: “Kwa Allaah na Kitabu Chake, na Rasuli Wake, na kwa viongozi wa Waislamu na watu wa kawaida.” [Muslim]

Thursday, 13 October 2016

035 - Hadiyth Ya 35: Katika Starehe Bora Kabisa Ya Dunia Ni Mke Mwema



عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو بْنِ الْعَاص (رضي الله عنهما)  أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:  ((الدُّنْيَا مَتَاعٌ, وَخَيْرُ مَتَاعِ الدُّنْيَا الْمَرْأَةُ الصَّالِحَة)) مسلم
 
Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amr bin Al-‘Aasw(رضي الله عنهما)  kwamba Mtume wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Dunia ni starehe, na bora ya starehe zake ni mke mwema)).[1]
 
Mafunzo Na Al-manani:
 
  1. Umuhimu wa kuchagua mke mwema, mwenye taqwa. [Rejea Hadiyth namba 40].


  1. Sababu mojawapo ya furaha ya dunia na Aakhirah ni kuwa na mke mwema, mwenye taqwa.
 
  1. Fadhila za mwanamke mwema mwenye taqwa kufananishwa na starehe. 
 
 زُيِّنَ لِلنَّاسِ حُبُّ الشَّهَوَاتِ مِنَ النِّسَاءِ وَالْبَنِينَ وَالْقَنَاطِيرِ الْمُقَنطَرَةِ مِنَ الذَّهَبِ وَالْفِضَّةِ وَالْخَيْلِ الْمُسَوَّمَةِ وَالْأَنْعَامِ وَالْحَرْثِ ۗ ذَٰلِكَ مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَاللَّـهُ عِندَهُ حُسْنُ الْمَآبِ ﴿١٤﴾
 
Watu wamepambiwa kupenda matamanio (miongoni mwake) wanawake, na watoto, na mirundi ya mali iliyorundikwa ya dhahabu na fedha na farasi wenye chapa (ya aina bora) na wanyama wa mifugo na mashamba. Hayo ni burudisho (liwazo) la maisha ya dunia, na Allaah Kwake kuna marejeo mazuri [2]
 
 
  1. Wema na taqwa ni miongoni mwa sifa njema anazopasa mwanamke wa Kiislamu kumiliki. [At-Tahriym 66: 11-12].
 
  1. Mume anayeruzukiwa mke mwema ni neema kwake. Inampasa ailinde neema kwa kukaa naye vyema na kuwa na huruma naye, mapenzi ili apate kudiriki starehe za dunia na Aakhirah. [Ar-Ruwm 30: 21, An-Nuwr 24: 26].
 

Wednesday, 12 October 2016

Hiswnul Muslim - Du'aa Na Adhkaar Mbalimbali Kutoka Katika Qur-aan, Sunnah Na Athar


بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمن الرَّحيم
Kwa Jina La Allaah Mwingi Wa Rehema (Duniani) Mwenye Kurehemu (Akhera)

UTANGULIZI
Hakika sifa njema zote ni za Allaah, tunamsifu, tunamuomba msaada na tunamuomba maghfirah, tunamuomba Atuhifadhi na shari za nafsi zetu, na maovu ya matendo yetu. Anayemuongoza Allaah hapana wa kumpoteza, na Anayempoteza, hapana wa wa kumuongoza.  Nakiri kwamba, hapana apasaye kuabudiwa ila Allaah, hali ya kuwa peke Yake, hana mshirika, na ninakiri kwamba Muhammad ni mja Wake na ni Mtume Wake. Allaah Amrehemu na Awarehemu jamaa zake na Maswahaba zake na wanaowafuata hao kwa wema mpaka siku ya malipo na Amsalimishe kwa amani nyingi.
Baada ya yaliyotangulia huu ni ufupi (Mukhtasar) wa kitabu changu  kiitwacho “HISWN AL-MUSLIM MIN ADHKAAR AL-KITAAB WA SUNNAH
Ninamuomba Allaah kwa majina Yake mazuri, na sifa Zake zilizo juu, Ajaaliye kazi hii kuwa, imesafika  lengo lake, kwa kutaka radhi zake Allaah Mtukufu, na Aninufaishe kwa hayo katika uhai wangu huu, na baada ya kufa, na Amnufaishe atakayekisoma, kukichapisha, au aliyekuwa ni sababu ya kukitawanya, hakika  Yeye  Allaah Ndiye  Muweza.
Allaah Amrehemu Mtume wetu Muhammad صلى الله عليه وسلم na Aali zake na Maswahaba wake na wanaowafuata hao, kwa wema mpaka siku ya malipo.
                                      






01 Fadhila Za Kumtaja Allaah




 Amesema Allaah سبحانه وتعالى
:{ فَاذْكُرُونِي أَذْكُرْكُمْ وَاشْكُرُواْ لِي وَلاَ تَكْفُرُونِ }
“Nitajeni nami nitawataja, na nishukuruni na wala msinikufuru (Suratul Baqaraha 152)
Na akasema:
 { يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا اللَّهَ ذِكْراً كَثِيراً}
“Enyi mlioamini mtajeni Mwenyezi Mungu sana” (Suratul Ahzaab 41 )
Akasema tena:
 { وَالذَّاكِرِينَ اللَّهَ كَثِيراً وَالذَّاكِرَاتِ أَعَدَّ اللَّهُ لَهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْراً عَظِيماً}
“Nawasifu wanaume wanaomtaja Mwenyezi Mungu sana na nawasifu wanawake wanaomtaja, Mwenyezi Mungu   kawaandalia wote hao msamaha na malipo makubwa” (Suratul Ahzaab 35 )
Akasema tena :
{ وَاذْكُر رَّبَّكَ فِي نَفْسِكَ تَضَرُّعاً وَخِيفَةً وَدُونَ الْجَهْرِ مِنَ الْقَوْلِ بِالْغُدُوِّ وَالآصَالِ وَلاَ تَكُن مِّنَ الْغَافِلِينَ }
“Mtaje Mola wako  moyoni mwako kwa  unyenyekevu  na kwa uwoga, pasina kudhihirisha sauti, mtaje asubuhi  na jioni, nawala usiwe nikatika wenye kughafilika” (Suratul A’raaf 205)
Mtume صلى الله عليه وسلم amesema :
 }  وقال صلى الله عليه وسلم :" مثل الذي يذكر ربه والذي لا يذكر ربه مثل الحي والميت {
{Mfano wa anaemtaja Mola wake na asiyemtaja ni mfano wa alie hai na maiti }
Na akasema Mtume صلى الله عليه وسلم
وقال صلى الله عليه وسلم :" ألا أنبئكم بخير أعمالكم , وأزكاها عند مليككم، وأرفعها في درجاتكم ، وخير لكم من إنفاق الذهب والورق ، وخير لكم من أن تلقوا عدوكم فتضربوا أعناقهم ويضربوا أعناقكم ؟" قالوا بلى .قال : "ذكر الله تعالى
{Hivi niwaambieni khabari  yamatendo yenu bora, na ambayo ni masafi mno, mbele ya Mola wenu, na ambayo ni yajuu mno katika daraja zenu, na ambayo ni bora kwenu kuliko kutoa  dhahabu na fedha, na ambayo ni bora kuliko  kukutana  na adui zenu, mkawapiga shingo zao, nao wakakupigeni shingo zenu?))  Wakasema masahaba; Ndio . Akasema  Mtume صلى الله عليه وسلم  ((Ni kumtaja Mwenyezi Mungu))
وقال صلى الله عليه وسلم :" يقول الله تعالى : أنا عند ظن عبدي بي ، وأنا معه إذا ذكرني ، فإن ذكرني في نفسه ذكرتهُ في نفسي ، وإن ذكرني في ملأ ذكرته في ملأ خير منهم ،وإن تقرب إلى شبراً تقربت إليه ذراعاً ،وإن تقرب إلي ذراعاً تقربت إليه باعاً ، وإن أتاني يمشي أتيتهُ هرولة "
Amesema Mtume صلى الله عليه وسلم Mwenyezi Mungu  anasema “Mimi niko mbele ya dhana ya mja wangu kwangu, akinitaja moyoni nami ninamtaja moyoni  na akinitaja katika  kundi, nami namtaja  katika kundi bora zaidi ya hilo lake, na akijikurubisha kwangu paa moja, basi mimi najikurubisha kwake kiasi cha dhiraa, na akijikurubisha  kwangu kiasi cha dhiraa, basi mimi nitajikurubisha  kwake kiasi chakuyoosha mkono hadi kati ya kifuwa, na akinijia kwa mwendo mdogo basi nami nitamjia kwa mwendo wa kasi. 
وعن عبد الله بن بسرٍ رضي الله عنهُ أن رجلاً قال : يا رسول الله إن شرائع الإسلام قد كثرت علي فأخبرني بشيءٍ أتشبث به. قال :" لا يزال لسانك رطباً من ذكر الله  
Imepokelewa kutoka kwa Abdalla Bin Busr رضى الله عنه   kwamba mtu mmoja alisema :
“Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ibada za dini zimekuwa nyingi kwangu, basi nieleze kitu  ambacho nitaweza  kudumu nacho.   Mtume صلى الله عليه وسلم  akamwambia : Ulimi wako utaendelea kuwa rutuba  (yaani sio ukavu ) kwakumtaja Mwenyezi Mungu  .
وقال صلى الله عليه وسلم:" من قرأ حرفاً من كتاب الله به حسنة ،والحسنة بعشر أمثالها ، لا أقول : {الم } حرف؛ ولكن : ألف حرف ،ولام حرف ،وميم حرف
Na amesema tena Mtume صلى الله عليه وسلم  “Anaesoma harufu moja katika kitabu cha Mwenyezi Mungu  basi anapata thawabu za jema moja na jema ni kwa mema kumi, sisemi kuwa ‘Alif Laam Miim’ ni harufu moja lakini ni kwamba ‘Alif’ peke yake ni harufu moja, na ‘Laam’ ni harufu , na ‘Miim’ ni harufu”
وعن عقبة بن عامر رضي الله عنه قال : خرج رسول الله صلى الله عليه وسلم ونحن في الصفة فقال :" أيكم يحب أن يغدو كل يوم إلى بطحان أو إلى العقيق فيأتي منه بناقتين كوماوين في غير إثم ولا قطيعة رحم ؟" فقلنا : يا رسول الله نحب ذلك . قال :" أفلا يغدو أحدكم إلى المسجد فيعلم ، أو يقرأ آيتين من كتاب الله عز وجل خير له من ناقتين ، وثلاث خير لهُ من ثلاث ٍ، وأربع خير لهُ من أربع ، ومن أعدادهن من الإبل
Imepokelewa kutoka kwa Uqbah bin Aamir رضى الله عنه   amesema :  ‘Ametoka Mtume wa Mwenyezi Mungu   na sisi tuko sehemu iitwayo Assufah, akasema “Nani kati yenu anapenda aende kila siku sehemu iitwayo But-haan au Aqiq aje na ngamia  wawili walio  nenepa pasi na dhambi wala kukata udugu?”  Wakasema  maswahaba “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu tunapenda hivyo’ akasema Mtume صلى الله عليه وسلم  “Hivi haendi (asubuhi ) mmoja wenu msikitini  akajuwa  au akasoma Aya mbili, za kitabu cha Mwenyezi Mungu?    Hizo aya mbili  ni bora kwake kuliko  kupata ngamia wawili, na endapo atasoma aya tatu zitakuwa  ni bora   kwake  kuliko ngamia watatu, na aya nne ni bora kwake kuliko ngamia wanne, na vilevile zaidi ya hapo.  Aya zozote atakazo zisoma  basi ni bora kwake kuliko hisabu  yake kwa ngamia”
وقال صلى الله عليه وسلم:" من قعد مقعداً لك يذكر الله فيه كانت عليه من الله ترة ومن اضطجع مضجعاً لم يذكر الله فيه كانت عليه من الله ترة
Na Anasema Mtume صلى الله عليه وسلم  “Anaekaa kikao chochote  kile asimtaje Mwenyezi Mungu  katika kikao hicho basi ana dhambi kutoka kwa Mwenyezi Mungu,  na anaelala sehemu yeyote ile kisha asimtaje Mwenyezi Mungu   wakati wakuinuka sehemu hiyo basi ana dhambi kwa Mwenyezi Mungu” 
وقال صلى الله عليه وسلم : " ما جلس قوم مجلساً لم يذكروا الله فيه ، ولم يصلوا على نبيهم إلا كان عليهم ترة ، فإن شاء عذبهم وإن شاء غفر لهم
Amesema Mtume صلى الله عليه وسلم Hapana watu wowote  wale, wanaokaa kikao kisha wasimtaje Mwenyezi Mungu humo, wala wasimswalie Mtume wao  ila  watakuwa wana dhambi. Akipenda Atawaadhibu na Akipenda Atawaghufuria.  
وقال صلى الله عليه وسلم :" ما من قوم يقومون من مجلس لا يذكرون الله فيه إلا قاموا عن مثل جيفة حمار وكان لهم حسرة
Amesema Mtume صلى الله عليه وسلم Hapana watu wowote wale  wanaosimama katika kikao walichokaa, kisha wasimtaje  Mwenyezi Mungu  ila watakuwa wanasimama kama  mzoga wa punda, na watakuja juta kwa kutomtaja Mwenyezi Mungu”
















02 Kuamka Kutoka Usingizini

(1)
  الحَمْـدُ لِلّهِ الّذي أَحْـيانا بَعْـدَ ما أَماتَـنا وَإليه النُّـشور
“Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu  ambae ametupa uhai baada ya kutufisha na ni Kwake tu kufufuliwa “
Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu  “Mwenye kushutuka usingizini usiku akasema
 (2):
ُ لا شَـريكَ له، لهُ المُلـكُ ولهُ الحَمـد، وهوَ على كلّ شيءٍ قدير، سُـبْحانَ اللهِ، والحمْـدُ لله ، ولا إلهَ إلاّ اللهُ
   لا إلهَ إلاّ اللّهُ وَحْـدَه واللهُ أكبَر، وَلا حَولَ وَلا قوّة إلاّ باللّهِ العليّ العظيم, رب اغْفِرْ لي
“Hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu, na hali ya kuwa peke yake hana mshirika, ni Wake ufalme, na ni Zake sifa njema, na Yeye juu ya kila kitu ni muweza, Ametakasika Mwenyezi Mungu  na sifa njema zote ni zake, na hapana Mola apasae  kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu , na Mwenyezi Mungu  ni mkubwa, na hapana uwezo wala nguvu, isipokuwa vyote vinatokana na Mwenyezi Mungu aliyejuu, aliyemtukufu, Ewe Mola (Mwenyezi Mungu) nisamehe :
basi atasamhewa na kama atasimama akaenda kutawadha, akaswali, basi swala yake atakubaliwa :
(3)
الحمدُ للهِ الذي عَافانِي فِي جَسَدي وَرَدّ عَليّ رُْوحِي وَأَذِنَ لِي بِذِكْرِه
“Sifa njema zote ni Zake Mwenyezi Mungu  ambae amenipa uzima wa mwili wangu, na akanirudishia  roho yangu, na akaniruhusu kumtaja”
(4)
) إِنّ فِي خَلْقِ السّمَوَاتِ وَالأرْضِ واخْتِـلافِ اللّيلِ والنّهارِ لآياتٍ لأُولي الألباب (…
(سورة آل عمران 190-200






03 Dua'a Ya Kuvaa Nguo


(5)
الْحَمْدُ للهِ الّذِي كََسَانِي هَذا (الثّوب) وَرَزَقَنِيهِ مِنْ غَـيـْرِ حَولٍ مِنّي وَلا قُوَّة
“Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu  ambae amenivisha nguo hii, na kuniruzuku pasina uwezo kutoka kwangu wala nguvu” 





04 Dua'a Ya Kuvaa Nguo Mpya

(6) 
اللّهُـمَّ لَـكَ الحَـمْـدُ أنْـتَ كَسَـوْتَنيهِ، أََسْأََلُـكَ مِـنْ خَـيرِهِ وَخَـيْرِ مَا صُنِعَ لَـه، وَأَعوذُ بِكَ مِـنْ شَـرِّهِ وَشَـرِّ مـا صُنِعَ لَـهُ.
“Ewe Mwenyezi Mungu , sifa njema ni zako, wewe ndie ulienivisha, nakuomba kheri ya nguo hii, na kheri ya kila ambacho nguo hii imetengenezewa, na najilinda Kwako kutokana na shari yake, na shari ambayo nguo hii imetengenezewa”itaendelea**************


001-Asmaa Wa Swifaat (Majina Na Sifa Za) Allaah: ALLAAH

Asmaa Wa Swifaat (Majina Na Sifa Za) Allaah
الله
001-ALLAAH

Allaah: Mwenye Uluwhiyyah (Mwenye Uungu) na Al-‘Ubuwdiyyah (Mwenye kustahiki kuabudiwa kwa haki na viumbe vyote). Mwenye kustahiki kupwekeshwa katika kuabudiwa kwa Alivyojisifu kwa Sifa za Uwluwhiyyah nazo ni Sifa za ukamilifu.
Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Mwenye Kustahiki kurejewa kwa mapenzi, kwa unyeyenyekevu, kwa khofu, matumaini, matarajio, kuadhimishwa na kutiiwa. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):
اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ ۚ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ ۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ ۚ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۖ وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا ۚ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ ﴿٢٥٥﴾
Allaah, hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye, Aliyehai daima, Msimamia kila kitu. Haumchukui usingizi wala kulala. Ni Vyake pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Nani huyu ambaye anashufai mbele Yake bila ya idhini Yake. Anajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawawezi kuzunguka chochote katika elimu Yake isipokuwa kwa Alitakalo. Imeenea Kursiyy Yake mbingu na ardhi. Wala hakumchoshi kuvihifadhi viwili hivyo. Naye ni Mwenye Uluwa, Ametukuka, Adhimu; Mkuu kabisa. [Al-Baqarah 2: 255]
Maana ya Allaah kilugha:  Allaah; Asili yake ni Al-Ilaah, na Al-Ilaah katika lugha ya Kiarabu ina maana nne:
Kwanza:  Al-Ma’buwd:  Mwenye kuabudiwa. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):
وَهُوَ الَّذِي فِي السَّمَاءِ إِلَـٰهٌ وَفِي الْأَرْضِ إِلَـٰهٌ ۚ  
Na Yeye Ndiye Muabudiwa wa haki mbinguni na ardhini  [Az-Zukhruf 43: 84]
Pili:  Mwenye kukimbiliwa katika hali ya khofu:
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):
وَاتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ آلِهَةً لَّعَلَّهُمْ يُنصَرُونَ ﴿٧٤﴾
Na wamejichukulia badala ya Allaah miungu (ya uongo) ili (wakitumaini) watawanusuru! [Yaasiyn 36: 74]
Yaani; Wanategemea wawanusuru dhidi ya maadui wao, Waarabu wakawa wanaelekea miungu yao kuomba nusra.
Tatu:  Al-Mahbuwb Al-Mu’adhwam – Mpendwa Mtukuzwa.
Waarabu wakawa wanapenda miungu yao na wakiitukuza Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):
وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللَّـهِ أَندَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّـهِ ۖ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَشَدُّ حُبًّا لِّلَّـهِ ۗ
Na miongoni mwa watu wako wenye kuchukua asiyekuwa Allaah na kuwafanya kuwa ni wanaolingana (na Allaah) wanawapenda kama mapenzi (yapasavyo) ya kumpenda Allaah. Na wale walioamini wana mapenzi zaidi kwa Allaah. [Al-Baqarah 2: 165]  

Nne:  Ambaye kwayo akili zinakanganyika
Yaani: zinakanganya nyoyo zinapotafakari utukufu Wake (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kisha zikashindwa kufikia ufahamu wa dhati ya Ujalali Wake na Utukufu Wake (‘Azza wa Jalla).
Jina hili ni Jina tukufu kabisa kuliko yote miongoni mwa Asmaul-Husnaa, na ni lilotukuka zaidi na lililojumuisha maana za Majina Yake yote. Allaah (Tabaaraka wa Ta’aalaa) Amejipwekesha Kwalo kutokana na walimwengu wote. Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Akazitia khofu nyoyo za majahili na ndimi zao zikatamka bila kipingamizi wala taradadi. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):
وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ ۚ
Na ukiwauliza: “Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi?” bila shaka watasema: “Allaah.” [Luqmaan 31: 21]

Jina hili ni Ambalo linalokusanya Majina Mazuri yote na Sifa tukufu za Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa). Mja anapoomba husema “Allaahumma” hivyo atakuwa ameomba kwa kila Majina Mazuri na Sifa Zake tukufu [Madaarij As-Saalikiyn (1/32)]  Ndio maana Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anaongezea Jina hili Tukufu katika Al-Asmaaul-Husnaa yote mfano kauli Yake:
وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا
Na Allaah Ana Majina Mazuri kabisa, basi muombeni kwayo [Al-A’raaf 7: 180]

Na ndio maana pia baadhi ya ‘Ulamaa wakaona kuwa Jina hili la Allaah Ndilo Jina tukufu kabisa ambalo likiombwa kwalo du’aa hutakabaliwa.
Na husemwa Ar-Rahmaan na Ar-Rahiym, Al-Qudduws, As-Salaam, Al-‘Aziyz, Al-Hakiym kuwa ni miongoni mwa Asmaaul-Husnaa wala haisemwi “Allaah” ni miongoni mwa Majina ya Ar-Rahmaan wala miongoni mwa Majina ya Al-‘Aziyz n.k, na ndipo Anaposema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):
 هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ ۖ هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ ﴿٢٢﴾
  Yeye ni Allaah, Ambaye hakuna Muabudiwa wa haki  ila Yeye. Mjuzi wa ghayb na ya dhahiri, Yeye Ndiye Mwingi wa rahmah, Mwenye kurehemu.

 هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْمَلِكُ الْقُدُّوسُ السَّلَامُ الْمُؤْمِنُ الْمُهَيْمِنُ الْعَزِيزُ الْجَبَّارُ الْمُتَكَبِّرُ ۚ سُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٢٣﴾
Yeye Ndiye Allaah Ambaye hakuna Muabudiwa wa haki  ila Yeye. Mfalme, Mtakatifu Ametakasika na sifa zote hasi, Mwenye kusalimisha, Amesalimika na kasoro zote, Mwenye kusadikisha ahadi, Mwenye kuaminisha, Mwenye kutawalia, kuchunga na kuhifadhi, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Jabari, Asiyeshindwa kufanya Atakalo, Mwenye kutakabari dhidi ya dhulma nk, Yuko juu ya viumbe, Utakasifu ni wa Allaah! kutokana na ambayo wanamshirikisha.

 هُوَ اللَّـهُ الْخَالِقُ الْبَارِئُ الْمُصَوِّرُ ۖ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ يُسَبِّحُ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٢٤﴾
Yeye Ndiye Allaah, Muumbaji, Mwanzishi viumbe bila kasoro, Muundaji sura na umbile, Ana Majina Mazuri kabisa, kinamsabbih Pekee kila kilichokuweko katika mbingu na ardhi, Naye Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [Al-Hashr 59: 22-24]

Jina hili ndio asili ya Majina ya Majina ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na yanayofuatia mengine yote yamejumuika ndani Yake.  

Jina la Allaah linamhusu Yeye Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa). Anasema (Subhaanahu wa Ta’aalaa):
رَّبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا فَاعْبُدْهُ وَاصْطَبِرْ لِعِبَادَتِهِ ۚ هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا ﴿٦٥﴾
Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake; basi mwabudu Yeye tu na dumisha subira katika ‘ibaadah Yake. Je, unamjua mwenye Jina kama Lake (Allaah)? [Maryam 19: 65]