Thursday, 13 October 2016

035 - Hadiyth Ya 35: Katika Starehe Bora Kabisa Ya Dunia Ni Mke Mwema



عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو بْنِ الْعَاص (رضي الله عنهما)  أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:  ((الدُّنْيَا مَتَاعٌ, وَخَيْرُ مَتَاعِ الدُّنْيَا الْمَرْأَةُ الصَّالِحَة)) مسلم
 
Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amr bin Al-‘Aasw(رضي الله عنهما)  kwamba Mtume wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Dunia ni starehe, na bora ya starehe zake ni mke mwema)).[1]
 
Mafunzo Na Al-manani:
 
  1. Umuhimu wa kuchagua mke mwema, mwenye taqwa. [Rejea Hadiyth namba 40].


  1. Sababu mojawapo ya furaha ya dunia na Aakhirah ni kuwa na mke mwema, mwenye taqwa.
 
  1. Fadhila za mwanamke mwema mwenye taqwa kufananishwa na starehe. 
 
 زُيِّنَ لِلنَّاسِ حُبُّ الشَّهَوَاتِ مِنَ النِّسَاءِ وَالْبَنِينَ وَالْقَنَاطِيرِ الْمُقَنطَرَةِ مِنَ الذَّهَبِ وَالْفِضَّةِ وَالْخَيْلِ الْمُسَوَّمَةِ وَالْأَنْعَامِ وَالْحَرْثِ ۗ ذَٰلِكَ مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَاللَّـهُ عِندَهُ حُسْنُ الْمَآبِ ﴿١٤﴾
 
Watu wamepambiwa kupenda matamanio (miongoni mwake) wanawake, na watoto, na mirundi ya mali iliyorundikwa ya dhahabu na fedha na farasi wenye chapa (ya aina bora) na wanyama wa mifugo na mashamba. Hayo ni burudisho (liwazo) la maisha ya dunia, na Allaah Kwake kuna marejeo mazuri [2]
 
 
  1. Wema na taqwa ni miongoni mwa sifa njema anazopasa mwanamke wa Kiislamu kumiliki. [At-Tahriym 66: 11-12].
 
  1. Mume anayeruzukiwa mke mwema ni neema kwake. Inampasa ailinde neema kwa kukaa naye vyema na kuwa na huruma naye, mapenzi ili apate kudiriki starehe za dunia na Aakhirah. [Ar-Ruwm 30: 21, An-Nuwr 24: 26].
 

Wednesday, 12 October 2016

Hiswnul Muslim - Du'aa Na Adhkaar Mbalimbali Kutoka Katika Qur-aan, Sunnah Na Athar


بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمن الرَّحيم
Kwa Jina La Allaah Mwingi Wa Rehema (Duniani) Mwenye Kurehemu (Akhera)

UTANGULIZI
Hakika sifa njema zote ni za Allaah, tunamsifu, tunamuomba msaada na tunamuomba maghfirah, tunamuomba Atuhifadhi na shari za nafsi zetu, na maovu ya matendo yetu. Anayemuongoza Allaah hapana wa kumpoteza, na Anayempoteza, hapana wa wa kumuongoza.  Nakiri kwamba, hapana apasaye kuabudiwa ila Allaah, hali ya kuwa peke Yake, hana mshirika, na ninakiri kwamba Muhammad ni mja Wake na ni Mtume Wake. Allaah Amrehemu na Awarehemu jamaa zake na Maswahaba zake na wanaowafuata hao kwa wema mpaka siku ya malipo na Amsalimishe kwa amani nyingi.
Baada ya yaliyotangulia huu ni ufupi (Mukhtasar) wa kitabu changu  kiitwacho “HISWN AL-MUSLIM MIN ADHKAAR AL-KITAAB WA SUNNAH
Ninamuomba Allaah kwa majina Yake mazuri, na sifa Zake zilizo juu, Ajaaliye kazi hii kuwa, imesafika  lengo lake, kwa kutaka radhi zake Allaah Mtukufu, na Aninufaishe kwa hayo katika uhai wangu huu, na baada ya kufa, na Amnufaishe atakayekisoma, kukichapisha, au aliyekuwa ni sababu ya kukitawanya, hakika  Yeye  Allaah Ndiye  Muweza.
Allaah Amrehemu Mtume wetu Muhammad صلى الله عليه وسلم na Aali zake na Maswahaba wake na wanaowafuata hao, kwa wema mpaka siku ya malipo.
                                      






01 Fadhila Za Kumtaja Allaah




 Amesema Allaah سبحانه وتعالى
:{ فَاذْكُرُونِي أَذْكُرْكُمْ وَاشْكُرُواْ لِي وَلاَ تَكْفُرُونِ }
“Nitajeni nami nitawataja, na nishukuruni na wala msinikufuru (Suratul Baqaraha 152)
Na akasema:
 { يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا اللَّهَ ذِكْراً كَثِيراً}
“Enyi mlioamini mtajeni Mwenyezi Mungu sana” (Suratul Ahzaab 41 )
Akasema tena:
 { وَالذَّاكِرِينَ اللَّهَ كَثِيراً وَالذَّاكِرَاتِ أَعَدَّ اللَّهُ لَهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْراً عَظِيماً}
“Nawasifu wanaume wanaomtaja Mwenyezi Mungu sana na nawasifu wanawake wanaomtaja, Mwenyezi Mungu   kawaandalia wote hao msamaha na malipo makubwa” (Suratul Ahzaab 35 )
Akasema tena :
{ وَاذْكُر رَّبَّكَ فِي نَفْسِكَ تَضَرُّعاً وَخِيفَةً وَدُونَ الْجَهْرِ مِنَ الْقَوْلِ بِالْغُدُوِّ وَالآصَالِ وَلاَ تَكُن مِّنَ الْغَافِلِينَ }
“Mtaje Mola wako  moyoni mwako kwa  unyenyekevu  na kwa uwoga, pasina kudhihirisha sauti, mtaje asubuhi  na jioni, nawala usiwe nikatika wenye kughafilika” (Suratul A’raaf 205)
Mtume صلى الله عليه وسلم amesema :
 }  وقال صلى الله عليه وسلم :" مثل الذي يذكر ربه والذي لا يذكر ربه مثل الحي والميت {
{Mfano wa anaemtaja Mola wake na asiyemtaja ni mfano wa alie hai na maiti }
Na akasema Mtume صلى الله عليه وسلم
وقال صلى الله عليه وسلم :" ألا أنبئكم بخير أعمالكم , وأزكاها عند مليككم، وأرفعها في درجاتكم ، وخير لكم من إنفاق الذهب والورق ، وخير لكم من أن تلقوا عدوكم فتضربوا أعناقهم ويضربوا أعناقكم ؟" قالوا بلى .قال : "ذكر الله تعالى
{Hivi niwaambieni khabari  yamatendo yenu bora, na ambayo ni masafi mno, mbele ya Mola wenu, na ambayo ni yajuu mno katika daraja zenu, na ambayo ni bora kwenu kuliko kutoa  dhahabu na fedha, na ambayo ni bora kuliko  kukutana  na adui zenu, mkawapiga shingo zao, nao wakakupigeni shingo zenu?))  Wakasema masahaba; Ndio . Akasema  Mtume صلى الله عليه وسلم  ((Ni kumtaja Mwenyezi Mungu))
وقال صلى الله عليه وسلم :" يقول الله تعالى : أنا عند ظن عبدي بي ، وأنا معه إذا ذكرني ، فإن ذكرني في نفسه ذكرتهُ في نفسي ، وإن ذكرني في ملأ ذكرته في ملأ خير منهم ،وإن تقرب إلى شبراً تقربت إليه ذراعاً ،وإن تقرب إلي ذراعاً تقربت إليه باعاً ، وإن أتاني يمشي أتيتهُ هرولة "
Amesema Mtume صلى الله عليه وسلم Mwenyezi Mungu  anasema “Mimi niko mbele ya dhana ya mja wangu kwangu, akinitaja moyoni nami ninamtaja moyoni  na akinitaja katika  kundi, nami namtaja  katika kundi bora zaidi ya hilo lake, na akijikurubisha kwangu paa moja, basi mimi najikurubisha kwake kiasi cha dhiraa, na akijikurubisha  kwangu kiasi cha dhiraa, basi mimi nitajikurubisha  kwake kiasi chakuyoosha mkono hadi kati ya kifuwa, na akinijia kwa mwendo mdogo basi nami nitamjia kwa mwendo wa kasi. 
وعن عبد الله بن بسرٍ رضي الله عنهُ أن رجلاً قال : يا رسول الله إن شرائع الإسلام قد كثرت علي فأخبرني بشيءٍ أتشبث به. قال :" لا يزال لسانك رطباً من ذكر الله  
Imepokelewa kutoka kwa Abdalla Bin Busr رضى الله عنه   kwamba mtu mmoja alisema :
“Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ibada za dini zimekuwa nyingi kwangu, basi nieleze kitu  ambacho nitaweza  kudumu nacho.   Mtume صلى الله عليه وسلم  akamwambia : Ulimi wako utaendelea kuwa rutuba  (yaani sio ukavu ) kwakumtaja Mwenyezi Mungu  .
وقال صلى الله عليه وسلم:" من قرأ حرفاً من كتاب الله به حسنة ،والحسنة بعشر أمثالها ، لا أقول : {الم } حرف؛ ولكن : ألف حرف ،ولام حرف ،وميم حرف
Na amesema tena Mtume صلى الله عليه وسلم  “Anaesoma harufu moja katika kitabu cha Mwenyezi Mungu  basi anapata thawabu za jema moja na jema ni kwa mema kumi, sisemi kuwa ‘Alif Laam Miim’ ni harufu moja lakini ni kwamba ‘Alif’ peke yake ni harufu moja, na ‘Laam’ ni harufu , na ‘Miim’ ni harufu”
وعن عقبة بن عامر رضي الله عنه قال : خرج رسول الله صلى الله عليه وسلم ونحن في الصفة فقال :" أيكم يحب أن يغدو كل يوم إلى بطحان أو إلى العقيق فيأتي منه بناقتين كوماوين في غير إثم ولا قطيعة رحم ؟" فقلنا : يا رسول الله نحب ذلك . قال :" أفلا يغدو أحدكم إلى المسجد فيعلم ، أو يقرأ آيتين من كتاب الله عز وجل خير له من ناقتين ، وثلاث خير لهُ من ثلاث ٍ، وأربع خير لهُ من أربع ، ومن أعدادهن من الإبل
Imepokelewa kutoka kwa Uqbah bin Aamir رضى الله عنه   amesema :  ‘Ametoka Mtume wa Mwenyezi Mungu   na sisi tuko sehemu iitwayo Assufah, akasema “Nani kati yenu anapenda aende kila siku sehemu iitwayo But-haan au Aqiq aje na ngamia  wawili walio  nenepa pasi na dhambi wala kukata udugu?”  Wakasema  maswahaba “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu tunapenda hivyo’ akasema Mtume صلى الله عليه وسلم  “Hivi haendi (asubuhi ) mmoja wenu msikitini  akajuwa  au akasoma Aya mbili, za kitabu cha Mwenyezi Mungu?    Hizo aya mbili  ni bora kwake kuliko  kupata ngamia wawili, na endapo atasoma aya tatu zitakuwa  ni bora   kwake  kuliko ngamia watatu, na aya nne ni bora kwake kuliko ngamia wanne, na vilevile zaidi ya hapo.  Aya zozote atakazo zisoma  basi ni bora kwake kuliko hisabu  yake kwa ngamia”
وقال صلى الله عليه وسلم:" من قعد مقعداً لك يذكر الله فيه كانت عليه من الله ترة ومن اضطجع مضجعاً لم يذكر الله فيه كانت عليه من الله ترة
Na Anasema Mtume صلى الله عليه وسلم  “Anaekaa kikao chochote  kile asimtaje Mwenyezi Mungu  katika kikao hicho basi ana dhambi kutoka kwa Mwenyezi Mungu,  na anaelala sehemu yeyote ile kisha asimtaje Mwenyezi Mungu   wakati wakuinuka sehemu hiyo basi ana dhambi kwa Mwenyezi Mungu” 
وقال صلى الله عليه وسلم : " ما جلس قوم مجلساً لم يذكروا الله فيه ، ولم يصلوا على نبيهم إلا كان عليهم ترة ، فإن شاء عذبهم وإن شاء غفر لهم
Amesema Mtume صلى الله عليه وسلم Hapana watu wowote  wale, wanaokaa kikao kisha wasimtaje Mwenyezi Mungu humo, wala wasimswalie Mtume wao  ila  watakuwa wana dhambi. Akipenda Atawaadhibu na Akipenda Atawaghufuria.  
وقال صلى الله عليه وسلم :" ما من قوم يقومون من مجلس لا يذكرون الله فيه إلا قاموا عن مثل جيفة حمار وكان لهم حسرة
Amesema Mtume صلى الله عليه وسلم Hapana watu wowote wale  wanaosimama katika kikao walichokaa, kisha wasimtaje  Mwenyezi Mungu  ila watakuwa wanasimama kama  mzoga wa punda, na watakuja juta kwa kutomtaja Mwenyezi Mungu”
















02 Kuamka Kutoka Usingizini

(1)
  الحَمْـدُ لِلّهِ الّذي أَحْـيانا بَعْـدَ ما أَماتَـنا وَإليه النُّـشور
“Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu  ambae ametupa uhai baada ya kutufisha na ni Kwake tu kufufuliwa “
Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu  “Mwenye kushutuka usingizini usiku akasema
 (2):
ُ لا شَـريكَ له، لهُ المُلـكُ ولهُ الحَمـد، وهوَ على كلّ شيءٍ قدير، سُـبْحانَ اللهِ، والحمْـدُ لله ، ولا إلهَ إلاّ اللهُ
   لا إلهَ إلاّ اللّهُ وَحْـدَه واللهُ أكبَر، وَلا حَولَ وَلا قوّة إلاّ باللّهِ العليّ العظيم, رب اغْفِرْ لي
“Hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu, na hali ya kuwa peke yake hana mshirika, ni Wake ufalme, na ni Zake sifa njema, na Yeye juu ya kila kitu ni muweza, Ametakasika Mwenyezi Mungu  na sifa njema zote ni zake, na hapana Mola apasae  kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu , na Mwenyezi Mungu  ni mkubwa, na hapana uwezo wala nguvu, isipokuwa vyote vinatokana na Mwenyezi Mungu aliyejuu, aliyemtukufu, Ewe Mola (Mwenyezi Mungu) nisamehe :
basi atasamhewa na kama atasimama akaenda kutawadha, akaswali, basi swala yake atakubaliwa :
(3)
الحمدُ للهِ الذي عَافانِي فِي جَسَدي وَرَدّ عَليّ رُْوحِي وَأَذِنَ لِي بِذِكْرِه
“Sifa njema zote ni Zake Mwenyezi Mungu  ambae amenipa uzima wa mwili wangu, na akanirudishia  roho yangu, na akaniruhusu kumtaja”
(4)
) إِنّ فِي خَلْقِ السّمَوَاتِ وَالأرْضِ واخْتِـلافِ اللّيلِ والنّهارِ لآياتٍ لأُولي الألباب (…
(سورة آل عمران 190-200






03 Dua'a Ya Kuvaa Nguo


(5)
الْحَمْدُ للهِ الّذِي كََسَانِي هَذا (الثّوب) وَرَزَقَنِيهِ مِنْ غَـيـْرِ حَولٍ مِنّي وَلا قُوَّة
“Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu  ambae amenivisha nguo hii, na kuniruzuku pasina uwezo kutoka kwangu wala nguvu” 





04 Dua'a Ya Kuvaa Nguo Mpya

(6) 
اللّهُـمَّ لَـكَ الحَـمْـدُ أنْـتَ كَسَـوْتَنيهِ، أََسْأََلُـكَ مِـنْ خَـيرِهِ وَخَـيْرِ مَا صُنِعَ لَـه، وَأَعوذُ بِكَ مِـنْ شَـرِّهِ وَشَـرِّ مـا صُنِعَ لَـهُ.
“Ewe Mwenyezi Mungu , sifa njema ni zako, wewe ndie ulienivisha, nakuomba kheri ya nguo hii, na kheri ya kila ambacho nguo hii imetengenezewa, na najilinda Kwako kutokana na shari yake, na shari ambayo nguo hii imetengenezewa”itaendelea**************


001-Asmaa Wa Swifaat (Majina Na Sifa Za) Allaah: ALLAAH

Asmaa Wa Swifaat (Majina Na Sifa Za) Allaah
الله
001-ALLAAH

Allaah: Mwenye Uluwhiyyah (Mwenye Uungu) na Al-‘Ubuwdiyyah (Mwenye kustahiki kuabudiwa kwa haki na viumbe vyote). Mwenye kustahiki kupwekeshwa katika kuabudiwa kwa Alivyojisifu kwa Sifa za Uwluwhiyyah nazo ni Sifa za ukamilifu.
Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Mwenye Kustahiki kurejewa kwa mapenzi, kwa unyeyenyekevu, kwa khofu, matumaini, matarajio, kuadhimishwa na kutiiwa. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):
اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ ۚ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ ۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ ۚ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۖ وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا ۚ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ ﴿٢٥٥﴾
Allaah, hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye, Aliyehai daima, Msimamia kila kitu. Haumchukui usingizi wala kulala. Ni Vyake pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Nani huyu ambaye anashufai mbele Yake bila ya idhini Yake. Anajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawawezi kuzunguka chochote katika elimu Yake isipokuwa kwa Alitakalo. Imeenea Kursiyy Yake mbingu na ardhi. Wala hakumchoshi kuvihifadhi viwili hivyo. Naye ni Mwenye Uluwa, Ametukuka, Adhimu; Mkuu kabisa. [Al-Baqarah 2: 255]
Maana ya Allaah kilugha:  Allaah; Asili yake ni Al-Ilaah, na Al-Ilaah katika lugha ya Kiarabu ina maana nne:
Kwanza:  Al-Ma’buwd:  Mwenye kuabudiwa. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):
وَهُوَ الَّذِي فِي السَّمَاءِ إِلَـٰهٌ وَفِي الْأَرْضِ إِلَـٰهٌ ۚ  
Na Yeye Ndiye Muabudiwa wa haki mbinguni na ardhini  [Az-Zukhruf 43: 84]
Pili:  Mwenye kukimbiliwa katika hali ya khofu:
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):
وَاتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ آلِهَةً لَّعَلَّهُمْ يُنصَرُونَ ﴿٧٤﴾
Na wamejichukulia badala ya Allaah miungu (ya uongo) ili (wakitumaini) watawanusuru! [Yaasiyn 36: 74]
Yaani; Wanategemea wawanusuru dhidi ya maadui wao, Waarabu wakawa wanaelekea miungu yao kuomba nusra.
Tatu:  Al-Mahbuwb Al-Mu’adhwam – Mpendwa Mtukuzwa.
Waarabu wakawa wanapenda miungu yao na wakiitukuza Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):
وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللَّـهِ أَندَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّـهِ ۖ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَشَدُّ حُبًّا لِّلَّـهِ ۗ
Na miongoni mwa watu wako wenye kuchukua asiyekuwa Allaah na kuwafanya kuwa ni wanaolingana (na Allaah) wanawapenda kama mapenzi (yapasavyo) ya kumpenda Allaah. Na wale walioamini wana mapenzi zaidi kwa Allaah. [Al-Baqarah 2: 165]  

Nne:  Ambaye kwayo akili zinakanganyika
Yaani: zinakanganya nyoyo zinapotafakari utukufu Wake (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kisha zikashindwa kufikia ufahamu wa dhati ya Ujalali Wake na Utukufu Wake (‘Azza wa Jalla).
Jina hili ni Jina tukufu kabisa kuliko yote miongoni mwa Asmaul-Husnaa, na ni lilotukuka zaidi na lililojumuisha maana za Majina Yake yote. Allaah (Tabaaraka wa Ta’aalaa) Amejipwekesha Kwalo kutokana na walimwengu wote. Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Akazitia khofu nyoyo za majahili na ndimi zao zikatamka bila kipingamizi wala taradadi. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):
وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ ۚ
Na ukiwauliza: “Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi?” bila shaka watasema: “Allaah.” [Luqmaan 31: 21]

Jina hili ni Ambalo linalokusanya Majina Mazuri yote na Sifa tukufu za Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa). Mja anapoomba husema “Allaahumma” hivyo atakuwa ameomba kwa kila Majina Mazuri na Sifa Zake tukufu [Madaarij As-Saalikiyn (1/32)]  Ndio maana Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anaongezea Jina hili Tukufu katika Al-Asmaaul-Husnaa yote mfano kauli Yake:
وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا
Na Allaah Ana Majina Mazuri kabisa, basi muombeni kwayo [Al-A’raaf 7: 180]

Na ndio maana pia baadhi ya ‘Ulamaa wakaona kuwa Jina hili la Allaah Ndilo Jina tukufu kabisa ambalo likiombwa kwalo du’aa hutakabaliwa.
Na husemwa Ar-Rahmaan na Ar-Rahiym, Al-Qudduws, As-Salaam, Al-‘Aziyz, Al-Hakiym kuwa ni miongoni mwa Asmaaul-Husnaa wala haisemwi “Allaah” ni miongoni mwa Majina ya Ar-Rahmaan wala miongoni mwa Majina ya Al-‘Aziyz n.k, na ndipo Anaposema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):
 هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ ۖ هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ ﴿٢٢﴾
  Yeye ni Allaah, Ambaye hakuna Muabudiwa wa haki  ila Yeye. Mjuzi wa ghayb na ya dhahiri, Yeye Ndiye Mwingi wa rahmah, Mwenye kurehemu.

 هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْمَلِكُ الْقُدُّوسُ السَّلَامُ الْمُؤْمِنُ الْمُهَيْمِنُ الْعَزِيزُ الْجَبَّارُ الْمُتَكَبِّرُ ۚ سُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٢٣﴾
Yeye Ndiye Allaah Ambaye hakuna Muabudiwa wa haki  ila Yeye. Mfalme, Mtakatifu Ametakasika na sifa zote hasi, Mwenye kusalimisha, Amesalimika na kasoro zote, Mwenye kusadikisha ahadi, Mwenye kuaminisha, Mwenye kutawalia, kuchunga na kuhifadhi, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Jabari, Asiyeshindwa kufanya Atakalo, Mwenye kutakabari dhidi ya dhulma nk, Yuko juu ya viumbe, Utakasifu ni wa Allaah! kutokana na ambayo wanamshirikisha.

 هُوَ اللَّـهُ الْخَالِقُ الْبَارِئُ الْمُصَوِّرُ ۖ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ يُسَبِّحُ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٢٤﴾
Yeye Ndiye Allaah, Muumbaji, Mwanzishi viumbe bila kasoro, Muundaji sura na umbile, Ana Majina Mazuri kabisa, kinamsabbih Pekee kila kilichokuweko katika mbingu na ardhi, Naye Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [Al-Hashr 59: 22-24]

Jina hili ndio asili ya Majina ya Majina ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na yanayofuatia mengine yote yamejumuika ndani Yake.  

Jina la Allaah linamhusu Yeye Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa). Anasema (Subhaanahu wa Ta’aalaa):
رَّبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا فَاعْبُدْهُ وَاصْطَبِرْ لِعِبَادَتِهِ ۚ هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا ﴿٦٥﴾
Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake; basi mwabudu Yeye tu na dumisha subira katika ‘ibaadah Yake. Je, unamjua mwenye Jina kama Lake (Allaah)? [Maryam 19: 65]

000-Asmaa Wa Swifaat (Majina Na Sifa Za) Allaah: Utangulizi

Asmaa Wa Swifaat (Majina Na Sifa Za)  Allaah

000-Utangulizi
بِسْمِ الله الرَّحْمنِ الرَّحِيم
الْحمْدُ لِلَّه وَالصَّلاةُ وَالسِّلامُ عَلى خَاتم الأنْبِيَاء وَالْمُرْسَلِين، الْمَبْعُوثُ رَحْمَةً لِلْعَالَمِين، مُحَمَّد وَعَلى آلِه وَأصْحابِه أجْمَعِين وَمَنْ تَبِعَهُمْ بِإِحْسَانٍ إِلَى يَوْمِ الدِّينِ.
Himdi zote Anastahiki Allaah, Swalaah na Salaam ziwe juu ya Nabiy na Rasuli wa mwisho, aliyetumwa awe rahmah kwa walimwengu, Muhammad, pamoja na ahli zake na Maswahaba zake wote, na wanaowafuata kwa ihsaan mpaka Siku ya Malipo.
Al-Asmaaul-Husnaa imetajwa mara nne katika Qur-aan katika kauli zifuatazo za Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):
قُلِ ادْعُوا اللَّـهَ أَوِ ادْعُوا الرَّحْمَـٰنَ ۖ أَيًّا مَّا تَدْعُوا فَلَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ
Sema; “Muiteni Allaah au muiteni Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rahmah). Vyovyote mtakavyomwita basi Yeye Ana Majina Mazuri kabisa. [Al-Israa 17: 110]

Na pia:
اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ﴿٨﴾
Allaah, hapana ilaaha (muabudiwa wa haki) ila Yeye. Anayo Majina Mazuri kabisa.[Twaahaa 20: 7-8]
Na:
وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا ۖ وَذَرُوا الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي أَسْمَائِهِ ۚ سَيُجْزَوْنَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٨٠﴾
Na Allaah Ana Majina Mazuri kabisa, basi muombeni kwayo. Na waacheni wale wanaopotoa katika Majina Yake, watalipwa yale waliyokuwa wakiyatenda. [Al-A’raaf 7: 180]

Na pia:
هُوَ اللَّـهُ الْخَالِقُ الْبَارِئُ الْمُصَوِّرُ ۖ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ يُسَبِّحُ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٢٤﴾
Yeye Ndiye Allaah, Muumbaji, Mwanzishi viumbe bila kasoro, Muundaji sura na umbile, Ana Majina Mazuri kabisa, kinamsabbih Pekee viliyoko katika mbingu na ardhi, Naye Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.  [Al-Hashr (59:22-24)]

Kumpwekesha Allaah Katika Majina Yake Na Kuthibitisha Sifa Za Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):
‘Aqiydah ya Ahlus-Sunnah wal-Jamaa’ah kuhusiana na Majina Mazuri kabisa ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na Sifa Zake ni tawqifiyyah; yanathibitishwa Aliyoyathibitisha Mwenyewe Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) katika Qur-aan na Sunnah  bila ya ta-awiyl (kukwepesha maana yake ya kihakika kwa kuipa maana ndogo; ishara ambayo ni tofauti na maana ya juu, ni kukanusha maana) wala tashbiyh (kushabihisha; kuanzisha mfananisho) wala tamthiyl (kumithilisha; kulinganisha, kufananisha) wala takyiyf (kuainisha maana na kuziulizia namna yake au kuuliza ni vipi Sifa hiyo ipo, kuchunguza ni kwa “namna gani” zimefungamana au kuambatana na Allaah) wala tah-riyf (kubadilisha maana, kupotosha Sifa ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa kutoa maana isiyo sahihi). Allaah Anaposema kuwa Ana Qudra (uwezo), na sisi tunaamini kuwa Anao Uwezo. Anaposema Yeye ni Qawiyy (Mwenye nguvu), na sisi tunaamini kuwa Ana nguvu. Anaposema kuwa Anaona, na sisi tunaamini kuwa Anaona. Anaposema kuwa Anasikia, na sisi tunaamini kuwa Anasikia. Lakini kuona Kwake au kusikia Kwake si kama kuona au kusikia kwa kiumbe chochote kile! Na Anaposema kuwa Anayo Macho, na sisi tunaamini kuwa Anayo Macho. Na Anaposema kuwa Anayo Mikono na sisi tunaamini kuwa Anayo Mikono, na Anaposema kuwa Anao Wajihi, na sisi tunaamini kuwa Anao Wajihi. Lakini Uwezo Wake, au Nguvu Zake, au Macho Yake au Masikio Yake au Wajihi Wake, hakuna mfano wowote na kitu chochote wala kiumbe chochote kile kama Anavyosema:
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ ﴿١١﴾
Hakuna chochote kinachofanana Naye, Naye Ndiye Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote. [Ash-Shuwraa 42: 11]

Kwa hiyo Anapotujulisha kuwa Yeye ni Al-‘Aliym (Mjuzi wa yote daima), hatuwezi kusema hivyo kwa bin Aadam. Na kadhalika hatuwezi pia kufananisha Sifa Zake nyinginezo kwa kiumbe chochote kile. Anasema (Subhaanahu wa Ta’aalaa):
فَلَا تَضْرِبُوا لِلَّـهِ الْأَمْثَالَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿٧٤﴾
Basi msimpigie mifano Allaah! Hakika Allaah Anajua nanyi hamjui. [An-Nahl 16: 74]

Kutokuzithibitisha sifa ambazo Mwenyewe Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Amejipa ni kuzigeuza na kuzipotoa; Anaonya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):
وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا ۖ وَذَرُوا الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي أَسْمَائِهِ ۚ سَيُجْزَوْنَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٨٠﴾
Na Allaah Ana Majina Mazuri kabisa, basi muombeni kwayo. Na waacheni wale wanaopotoa katika Majina Yake, watalipwa yale waliyokuwa wakiyatenda. [Al-A’raaf 7: 180]
Hiyo ndiyo ‘Aqiydah sahihi kabisa waliyoitakidi Salaf wa ummah na ndivyo ipasavyo kuzikubali Sifa zote za Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) bila ya kukisia kwa akili zetu namna yake au mfano wake, wala kuogopa kuzithibitisha zilivyo kwa kukhofia kufananisha na viumbe. Kuzithibitisha vile vile zilivyokuja kutoka katika Kitabu Chake kama Alivyoziita Mwenyewe (‘Azza wa Jalla) na Alivyotaka Yeye, hiyo ndio salama kwetu. Tujisalimishe na Alivyojithibitishia Mwenyewe na alivyothibitisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwani akili zetu haziwezi kufikia upeo wa utambuzi na ujuzi wa Sifa Zake (‘Azza wa Jalla).
Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema:
وَلَا تَقْفُ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ ۚ إِنَّ السَّمْعَ وَالْبَصَرَ وَالْفُؤَادَ كُلُّ أُولَـٰئِكَ كَانَ عَنْهُ مَسْئُولًا ﴿٣٦﴾
Na wala usiyafuate (kusema au kushuhudia) yale usiyokuwa nayo elimu. Hakika masikio na macho na moyo; vyote hivyo vitakuwa vya kuulizwa (Siku ya Qiyaamah). [Al-Israa 17:36]

Na Anasema pia (Subhaanahu wa Ta’aalaa):
يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلَا يُحِيطُونَ بِهِ عِلْمًا ﴿١١٠﴾
Anajua yale yaliyoko mbele yao, na yale yaliyoko nyuma yao, na wala hawawezi kuzunguka elimu Yake. [Twaahaa 20: 110]

Umuhimu wa kuyajua na kujifunza Majina Mazuri kabisa ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na Sifa Zake:
1.      ’Ilmu kuhusu Asmaa na Swifaat za Allaah ni kumtambua Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na kutambua Utukufu Wake.
Unapotaka kutaamali na mtu, hakuna shaka kuwa utataka kujua jina lake, kun-yah yake na kuulizia khabari zake upate ufahamu bayana kumhusu yeye hata uridhike unapotaamali naye. Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Ametuumba na Ndiye Anayeturuzuku kila kitu na tunakhofia ghadhabu Zake na tunataraji rahmah Zake Atughufurie madhambi yetu Asituadhibu. Kwa hiyo, hakuna budi kutambua yanayomridhia ili Naye Aridhike na sisi, na pia kutambua yanayomghadhibisha ili tujiepushe nayo. Kama vile ambavyo huwezi kumpenda usiyemjua, hali kadhaalika huwezi kumkhofu na kumpenda Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa haki apasayo kukhofiwa na kupendwa isipokuwa kwa kumtambua Utukufu Wake, na njia mojawapo ni kutambua Majina Yake Mazuri kabisa na Sifa Zake. Usipomtambua ukampenda, Naye Hatokutambua wala kukujali.
Anasema (Subhaanahu wa Ta’aalaa):
وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ نَسُوا اللَّـهَ فَأَنسَاهُمْ أَنفُسَهُمْ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ﴿١٩﴾
Na wala msiwe kama wale waliomsahau Allaah, Naye (Allaah) Akawasahaulisha nafsi zao, hao ndio mafasiki. [Al-Hashr 59: 19]

Hivyo, kumtambua Allaah kunapelekea katika kumpenda, na kumkhofu, na kutawakali Kwake, na kumsafishia niyyah (ikhlaasw) katika matendo na kutaraji rahmah Yake.

2.      ’Ilmu Ya Asmaa na Swifaat Za Allaah ni ’Ilmu ya asasi.

’Ilmu kuhusu Asmaa na Swifaat za Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) ni’ilmu ya asasi, kwani ni aina ya tatu ya Tawhiyd. Na tawhiyd ndio jambo kuu walilokuja nalo Rusuli wote katika ulinganiaji wao. Na ni ’ilmu bora na tukufu kabisa kuitambua. Na ndio lengo kuu na kuumbwa kwa kumpwekesha Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) katika ’ibaadah.

3.      ’Ilmu Ya Asmaa na Swifaat Za Allaah Inazidisha Iymaan.

 ’Ilmu kuhusu Asmaa na Swifaat za Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) ni sababu ya kuzidisha iymaan kama alivyosema Imaam As-Sa’dy (Rahimahu Allaah): “Hakika kuamini Asmaa Allaah Al-Husnaa na utambuzi wake, inajumuisha aina tatu za tawhiyd; Tawhiyd Ar-Rubuwbiyyah, Tawhiyd Al-’Uluwhiyyah (’Ibaadah) na Tawhiyd Asmaa wasw-Swifaat. Na aina hizi ndio roho ya iymaan na ndio furaha halisi na kitulizo cha dhiki za moyo, na ndio asili yake na lengo lake. Basi kila mja anapozidi kutambua maarifa ya Asmaa Allaah na Sifa Zake ndipo inapozidi iymaan yake na kuthibitika yakini yake. [At-Tawdhiwyh Wal-Bayaan Lishajaratil-Iymaan Lis-Sa’dy, uk. 41]

4.      ’Ilmu kuhusu Asmaa na Swifaat za Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) ni sababu ya kupata Jannah:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((إِنَّ لِلَّهِ تِسْعَةً وَتِسْعِينَ اسْمًا مِائَةً إِلا وَاحِدًا مَنْ أَحْصَاهَا دَخَلَ الْجَنَّةَ))
Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ’anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakika Allaah Ana Majina tisini na tisa, atakayejifunza moyoni ataingia Jannah.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Ahswaahaa imekusudiwa: Kuyafahamu maana Zake, kuyahifadhi, kufanyia kazi, kuomba du’aa kuyatumia kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):
وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا ۖ
Na Allaah Ana Majina Mazuri kabisa, basi muombeni kwayo. [Al-A’raaf 7: 180]

Imaam Ibn ’Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema: Ahswaahaa haimaanishi kuwa ni kuyaandika Majina ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwenye karatasi na kuyakariri mpaka mtu aweze kuyahifadhi bali inamaanisha:
  • Kujifunza kuyatamka.
  • Kufahamu maana Zake.
  • Kumwabudu Allaah kwayo, kwa njia mbili:
Kwanza:  Kumuomba du’aa kwayo kwa sababu Allaah Anasema:
وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا ۖ
Na Allaah Ana Majina Mazuri kabisa, basi muombeni kwayo. [Al-A’raaf 7: 180]
Kwa hivyo, uyafanye kuwa ni wasiylah (kurubisho) ya du’aa yako, hivyo utachagua Jina linalowafikiana na haja yako. Unapotaka  kuomba maghfirah useme: ”Yaa Ghafuwru nighufurie.” Na si kusema: ”Yaa Shadiyd Al-’Iqaab Ighfir-liy (Ee Mkali wa kuakibu nighufurie!)” kwani hii inakuwa kama ni istihzaa. Linalopasa (ikiwa utamwita Allaah hivyo) useme ”Ee Mkali wa kuakibu, Niepushe na ikabu Yako.”
Pili:  Katika ’ibaadah zako, vitendo viashirie  Majina Yake. Kama Ar-Rahiym (Mwenye kurehemu) kusudio lake ni rahmah, basi fanya vitendo vyema vitakavyosababisha kupata rahmah ya Allaah.
Hiyo ndio maana ya ahswaahaa. Basi itakapotekelezwa hayo ndipo itakapostahiki kuingizwa Jannah.” [Majmuw’ Fataawa wa Rasaail Ibn ’Uthaymiyn (1/74)]
’Ulamaa wamekubaliana kwamba Majina ya Allaah si tisini na tisa pekee bali yako zaidi ya hayo kwa dalili ya Hadiyth:
عن عَبْدِ اللَّهِ بن مسعود قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((مَا أَصَابَ أَحَدًا قَطُّ هَمٌّ وَلا حَزَنٌ فَقَالَ: اللَّهُمَّ إِنِّي عَبْدُكَ، وَابْنُ عَبْدِكَ، وَابْنُ أَمَتِكَ، نَاصِيَتِي بِيَدِكَ، مَاضٍ فِيَّ حُكْمُكَ، عَدْلٌ فِيَّ قَضَاؤُكَ، أَسْأَلُكَ بِكُلِّ اسْمٍ هُوَ لَكَ سَمَّيْتَ بِهِ نَفْسَكَ، أَوْ عَلَّمْتَهُ أَحَدًا مِنْ خَلْقِكَ، أَوْ أَنْزَلْتَهُ فِي كِتَابِكَ، أَوْ اسْتَأْثَرْتَ بِهِ فِي عِلْمِ الْغَيْبِ عِنْدَكَ، أَنْ تَجْعَلَ الْقُرْآنَ رَبِيعَ قَلْبِي، وَنُورَ صَدْرِي، وَجِلَاءَ حُزْنِي، وَذَهَابَ هَمِّي، إِلا أَذْهَبَ اللَّهُ هَمَّهُ وَحُزْنَهُ وَأَبْدَلَهُ مَكَانَهُ فَرَجًا)) فَقِيلَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَلا نَتَعَلَّمُهَا؟ فَقَالَ: ((بَلَى يَنْبَغِي لِمَنْ سَمِعَهَا أَنْ يَتَعَلَّمَهَا)) صححه الألباني في السلسلة الصحيحة (199)
Ibn Mas’uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Yeyote atakayefikiwa na dhiki na huzuni kisha akasema:
Allaahumma inniy ‘abduka, ibnu-‘abdika, ibnu-amatika, naaswiyaatiy Biyadika, maadhwin fiyya hukmuka, ‘adlun fiyya qadhwaauka, as-aluka bikullismin huwa Laka, sammayta bihi Nafsaka aw Anzaltahu fiy Kitaabika, aw ‘Allamtahu ahadan min Khalqika, awis-staa-tharta bihi fiy ‘ilmil-ghaybi  ‘Indaka, an Taj-’alal-Qur-aana rabiy’a qalbiy, wanuwra swadriy, wajalaa-a huzniy, wadhahaaba hammiy.
Ee Allaah hakika mimi ni mtumwa Wako, mtoto wa mtumwa Wako, mtoto wa kijakazi Chako, utosi wangu uko Mikononi Mwako, yaliyopita kwangu yako katika hukumu Yako, ni usawa kwangu kunihukumu Kwako, nakuomba kwa kila Jina ambalo ni Lako Ulilojiita Kwako Mwenyewe au Uliloliteremsha katika Kitabu Chako, au Ulilomfundisha yeyote yule kati ya viumbe Vyako, au Ulilolihifadhi Wewe mwenyewe (na kujihusisha kulijua) katika ’ilmu ya ghayb Kwako, nakuomba Ujaalie (uifanye) Qur-aan kuwa ni raha na uchanuzi wa moyo wangu na nuru ya kifua changu, na utatuzi wa  huzuni yangu, na sababu ya kuondoka majonzi yangu - Akisema hivyo hakuna isipokuwa Allaah Atamuondoshea dhiki na huzuni na Atambadilisha badala yake faraja.” Ikasemwa: Ee Rasuli wa Allaah! Je tujifunze? Akasema: ”Ndio, inampasa kwa mwenye kuisikia kujifunza.” [Ameipokea Ahmad (1/391) [452], Al-Haakim (1/509) na ameisahihisha Al-Albaaniy katika As-Silsilah Asw-Swahiyhah (199) na Al-Kalimi Atw-Twayyib (124)]
Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:
“Hii (du’aa katika Hadiyth hiyo) ni dalili kwamba Allaah Ana Majina zaidi ya tisini na tisa.” [Majmu’w Al-Fataawa (6/374)]
Na Imaam Ibn ’Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema alipoulizwa kuhusu idadi ya Majina ya Allaah:
“Majina ya Allaah hayana idadi maalumu. Na dalili ni kauli ya (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika Hadiyth Swahiyh:
((Ee Allaah hakika mimi ni mtumwa Wako, mtoto wa mtumwa Wako, mtoto wa kijakazi Chako, utosi wangu uko Mikononi Mwako, yaliyopita kwangu yako katika hukumu Yako, ni usawa kwangu kunihukumu Kwako, nakuomba kwa kila Jina ambalo ni Lako Ulilojiita Kwako Mwenyewe au Uliloliteremsha katika Kitabu Chako, au Ulilomfundisha yeyote yule kati ya viumbe Vyako, au Ulilolihifadhi Wewe mwenyewe (na kujihusisha kulijua) katika ’ilmu ya ghayb Kwako)).
Basi ambayo Aliyoyahifadhi Allaah katika ’ilmu ya ghayb hayawezi kujulikana, na ambayo hayajulikani hayawezi kuhesabika. Ama kauli ya (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
”Hakika Allaah Ana Majina tisini na tisa, atakayejifunza moyoni ataingia Jannah.”
Haimaanishi kuwa Hana isipokuwa Majina haya tu. Lakini inayokusudiwa ni kwamba atakayehifadhi Majina haya tisini na tisa basi ataingia Jannah. Kauli yake: Man Ahswaahaa (atakayejifunza kwa moyo) ni kamilisho la sentensi ya mwanzo na si kiendelezo kilichojitenga, ni kama vile Waarabu wanaposema: “Nina farasi mia ambao nimewaandaa kwa jihaad kwa ajili ya Allaah”; Hii haimaanishi kwamba msemaji ana farasi mia tu bali hawa mia ndio aliowaandaa kwa ajili ya jambo hili.” [Majmuw’ Fataawa Ibn ‘Uthaymiyn (1/122)]
Kazi hii ya ku-tarjam na kuelezea Asmaa na Swifaat za Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) tulizozikusanya humu hakika ni mukhtasari tu kwa sababu ’ilmu yake ni pana mno haiwezekani kuijumuisha kwa makala fupi kama hizi. Lakini tunatumai kuwa mukhtasari huu utatoa maarifa ya kumtoshelezea kiasi msomaji kutambua maana za msingi za Majina na Sifa za Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa).
Haya ndio Ambayo Allaah Ametuwezesha kwa tawfiyq Yake, huku tukimuomba Ajaalie kazi hii iwe yenye ikhlaasw Kwake na ilete manufaa kwa jamii na Atutakabalie. Aamiyn.
Alhidaaya.com

Ukumbusho Wa Kukithirisha Swawm Mwezi Wa Muharram Na Swawm Za Ayyaamul-Biydhw

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: 
((أَفْضَلُ الصِّيَامِ بَعْدَ رَمَضَانَ شَهْرُ اللَّهِ الْمُحَرَّمُ)) رواه مسلم
Swiyaam (funga) bora kabisa baada ya Ramadhwaan ni swawm ya mwezi wa Allaah wa Muharram [Muslim]
Pia, tunapenda kuwakumbusha swawm za Ayyaamul-Biydhw (masiku meupe) ambayo ni tarehe 13, 14, 15 katika kila mwezi wa Kiislaam (Hijriyyah). Masiku hayo mwezi huu wa Muharram 1438H, yataangukia tarehe 14, 15, 16 Oktoba (Ijumaa, Jumamosi, Jumapili). 
عَنْ أَبي ذَرٍّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيهِ وَسَلَّمَ:((مَنْ صَامَ مِنْ كُلِّ شَهْرٍ ثَلاثَةَ أَيَّامٍ فَذَلِكَ صِيَامُ الدَّهْرِ)) فَأَنْزَلَ اللهُ تُصْدِيقَ ذَلِكَ في كِتَابِهِ الْكَرِيمِ: ((مَنْ جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا))، الْيَوْمُ بِعَشَرَةِ أَيّامٍ. أخرجه أحمد والترمذي وقال حديث حسن ، والنسائي وابن ماجه وابن خزيمة
Imepokelewa kutoka kwa Abu Dharr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam amesema: ((Yeyote atakaye swawm kila mwezi siku tatu, ni sawa na swawm ya milele)) Kisha Allaah Akateremsha Aayah ithibitishayo hayo: “Atakayekuja kwa amali nzuri basi atapata (thawabu) kumi mfano wa hiyo.”  Siku moja kwa malipo ya siku kumi. [Imepokewa na At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Hasan, An Nasaaiy na Ibn Maajah, Ibn Khuzaymah na ameisahihisha Shaykh Al-Albaaniy katika Al-Irwaa (4/102)]. Aayah: Suwrat Al-An’aam (160)]
Bonyeza: 'Endelea' upate faida nyenginezo.

Nasiha Za Wiki

إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ --- Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! 23- Sihri (Uchawi) Na Michezo Ya Mazingaombwe

Neno “As-Sihr” (uchawi) maana yake ni kitendo cha kujikurubisha na shaytwaan na kwa msaada wake (shaytwaan) na uchawi ni kulibadilisha jambo mbali na uhakika wake, nako ni kuwadhihirishia watu jambo lisilo la kweli wakaliona kuwa ni la kweli.” [Lisaan Al-‘Arab]
Na Sihri ni tendo la kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa kuwa linahusiana na shaytwaan 'aaswi mwenye kumkufuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):   
وَاتَّبَعُوا مَا تَتْلُو الشَّيَاطِينُ عَلَىٰ مُلْكِ سُلَيْمَانَ ۖ وَمَا كَفَرَ سُلَيْمَانُ وَلَـٰكِنَّ الشَّيَاطِينَ كَفَرُوا يُعَلِّمُونَ النَّاسَ السِّحْرَ وَمَا أُنزِلَ عَلَى الْمَلَكَيْنِ بِبَابِلَ هَارُوتَ وَمَارُوتَ ۚ وَمَا يُعَلِّمَانِ مِنْ أَحَدٍ حَتَّىٰ يَقُولَا إِنَّمَا نَحْنُ فِتْنَةٌ فَلَا تَكْفُرْ ۖ فَيَتَعَلَّمُونَ مِنْهُمَا مَا يُفَرِّقُونَ بِهِ بَيْنَ الْمَرْءِ وَزَوْجِهِ ۚ وَمَا هُم بِضَارِّينَ بِهِ مِنْ أَحَدٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ وَيَتَعَلَّمُونَ مَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ ۚ وَلَقَدْ عَلِمُوا لَمَنِ اشْتَرَاهُ مَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِنْ خَلَاقٍ ۚ وَلَبِئْسَ مَا شَرَوْا بِهِ أَنفُسَهُمْ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿١٠٢﴾
Na wakafuata yale waliyoyasoma mashaytwaan juu ya ufalme wa Sulaymaan; na Sulaymaan hakukufuru lakini mashaytwaan ndio waliokufuru; wanafundisha watu sihri na yaliyoteremshwa kwa Malaika wawili katika (mji wa) Baabil; Haaruwt na Maaruwt. Nao wawili hawamfundishi yeyote mpaka waseme: “Hakika sisi ni mtihani, basi usikufuru.” Kisha wakajifunza kutoka kwa hao wawili yenye kupelekea kufarikisha kwayo baina ya mtu na mkewe. Na wao hawawezi kamwe kumdhuru yeyote kwayo isipokuwa kwa idhini ya Allaah; na wanajifunza yanayowadhuru na wala hayawanufaishi; na kwa yakini walijua kwamba atakayeinunua (sihiri) hatopata katika Aakhirah fungu lolote, na ni ubaya ulioje walichouzia kwayo nafsi zao, lau wangelikuwa wanajua. [Al-Baqarah: 102]
Pia, sihri ni miongoni mwa Al-Kabaair (madhambi makubwa) na ni miongoni mwa ambayo yanamuangamiza mtu kwa dalili ya Hadiyth: