01 Wasiya Kumi Wa Allaah - Utangulizi-1
Idadi
ya hizi amri kumi ni sawa na idadi ya amri alizopewa Muusa
(‘Alayhis-Salaam) zinazojulikana kwa umaarufu katika lugha ya Kiingereza
‘The Ten Commandments”, ila zimetofuatiana katika amri zake zenyewe.
Kwetu sisi Waislamu hizi ni amri ambazo zinampasa kila mmoja wetu
ahakikishe kuwa anazitimiza kutokana na umuhimu wa maamrisho yake:
عَنْ
عُبَادَة بْن الصَّامِت قَالَ : قَالَ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه
عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ((أَيّكُمْ يُبَايِعنِي عَلَى ثَلَاث)) ثُمَّ تَلَا
رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ((قُلْ تَعَالَوْا أَتْلُ
مَا حَرَّمَ رَبّكُمْ عَلَيْكُمْ ...)) حَتَّى فَرَغَ مِنْ الْآيَات
((فَمَنْ وَفَى فَأَجْره عَلَى اللَّه وَمَنْ اِنْتَقَضَ مِنْهُنَّ شَيْئًا
فَأَدْرَكَهُ اللَّه بِهِ فِي الدُّنْيَا كَانَتْ عُقُوبَته وَمَنْ
أَخَّرَ إِلَى الْآخِرَة فَأَمْره إِلَى اللَّه إِنْ شَاءَ عَذَّبَهُ
وَإِنْ شَاءَ عَفَا عَنْهُ))
Kutoka
kwa ‘Ubaadah bin Swaamit ambaye amesema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi
wa aalihi wa sallam) amesema: ((Nani atakayefanya agano nami katika
matatu [Aayah tatu] Kisha akasoma hadi alipomaliza Aayah, akasema:
((Yeyote atakayetimiza (agano/ahadi hii) basi atapata thawabu zake
kutoka kwa Allaah, lakini yeyote atakayefanya
kasoro kwazo kisha Allaah Akamuadhibu duniani itakuwa ni malipo yake.
Yeyote ambaye Allaah Atamcheleweshea (adhabu yake) hadi Akhera, basi hii
ni amri ya Allaah. Akipenda Atamudhibu, na Akipenda Atamsamehe)) [Al-Haakim: 2:318]
Wasia hizi zilikuwa ni wasiya za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) za mwisho zenye muhuri wake.
عَنْ
اِبْن مَسْعُود رَضِيَ اللَّه عَنْهُ قَالَ : مَنْ أَرَادَ أَنْ يَنْظُر
إِلَى وَصِيَّة رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الَّتِي
عَلَيْهَا خَاتَمه فَلْيَقْرَأْ هَؤُلَاءِ الْآيَات ((قُلْ تَعَالَوْا أَتْلُ مَا حَرَّمَ رَبّكُمْ عَلَيْكُمْ أَلَّا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا)) - إِلَى قَوْله ((لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ))
Kutoka kwa Ibn Mas’uud (Radhiya Allaahu) ambaye amesema: “Anayetaka
kusoma wasiya wa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
ambao ulikuwa na muhuri wake, basi asome Aayah zifuatazo: ((Sema: Njooni
nikusomeeni Aliyokuharamishieni Mola wenu Mlezi. Nayo ni kuwa,
msimshirikishe Yeye na chochote …)) hadi kauli Yake: ((ili mpate kumcha
Mungu)) [Tuhfat Al-Ahwadhi]
Wasia
huo wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambao
unatokana na Qur-aan na ambao hauhusiani na mtu binafsi, kwani Mtume
(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuacha wasia kwa mtu
–hasa hasa kuhusu Ukhalifa - , bali ameleta yaleyale yaliyomo kwenye
Qur-aan ambazo zote zinapatikana katika Aayah tatu zifuatazo:
((قُلْ تَعَالَوْاْ أَتْلُ مَا حَرَّمَ رَبُّكُمْ عَلَيْكُمْ أَلاَّ تُشْرِكُواْ بِهِ شَيْئًا وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا وَلاَ تَقْتُلُواْ أَوْلاَدَكُم مِّنْ إمْلاَقٍ نَّحْنُ نَرْزُقُكُمْ وَإِيَّاهُمْ وَلاَ تَقْرَبُواْ الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَلاَ تَقْتُلُواْ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللّهُ إِلاَّ بِالْحَقِّ ذَلِكُمْ وَصَّاكُمْ بِهِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ))
((وَلاَ تَقْرَبُواْ مَالَ الْيَتِيمِ إِلاَّ بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ حَتَّى يَبْلُغَ أَشُدَّهُ وَأَوْفُواْ الْكَيْلَ وَالْمِيزَانَ بِالْقِسْطِ لاَ نُكَلِّفُ نَفْسًا إِلاَّ وُسْعَهَا وَإِذَا قُلْتُمْ فَاعْدِلُواْ وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَى وَبِعَهْدِ اللّهِ أَوْفُواْ ذَلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ))
((وَأَنَّ هَذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ وَلاَ تَتَّبِعُواْ السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ذَلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ))
((Sema:
Njooni nikusomeeni Aliyokuharamishieni Mola wenu Mlezi. Nayo ni kuwa,
msimshirikishe Yeye na chochote. Na wazazi wenu wafanyieni wema. Wala
msiwauwe watoto wenu kwa sababu ya umasikini. Sisi tunakuruzukuni nyinyi
na wao. Wala msikaribie mambo machafu, yanayoonekana, na
yanayofichikana. Wala msiuwe nafsi ambayo Allaah Ameharamisha kuiuwa,
ila ikiwa kwa haki. Hayo Amekuusieni ili myatie akilini))
((Wala msiyakaribie mali
ya yatima ila kwa njia ya wema kabisa, mpaka afikilie utu-uzima. Na
timizeni vipimo na mizani kwa uadilifu. Sisi Hatumkalifishi mtu ila kwa
kadiri ya uwezo wake. Na msemapo semeni kwa uadilifu ingawa ni jamaa. Na
ahadi ya Allaah itekelezeni. Hayo Amekuusieni ili mpate kukumbuka))
((Na
kwa hakika hii ndiyo Njia Yangu Iliyonyooka. Basi ifuateni, wala
msifuate njia nyingine, zikakutengeni na Njia Yake. Hayo Amekuusieni ili
mpate kumcha Mungu)) [Al-An’aam: 151-153]
02 Wasiya Kumi Wa Allaah - Utangulizi-2
Wasiya Kumi Wa Allaah
Utangulizi-2
Wasia
hizi zenye amri zimekuja baada ya kutangulia Aayah zinazoelezea madai
ya makafiri Quraysh kuharamisha baadhi ya wanyama na vyakula na
kuhusisha kwao vitu hivyo na masanamu yao, kuua watoto wao na kuzua mengi mengineyo yasiyokuwa katika sheria.
((وَجَعَلُواْ لِلّهِ مِمِّا ذَرَأَ مِنَ الْحَرْثِ وَالأَنْعَامِ نَصِيبًا فَقَالُواْ هَذَا لِلّهِ بِزَعْمِهِمْ وَهَذَا لِشُرَكَآئِنَا فَمَا كَانَ لِشُرَكَآئِهِمْ فَلاَ يَصِلُ إِلَى اللّهِ وَمَا كَانَ لِلّهِ فَهُوَ يَصِلُ إِلَى شُرَكَآئِهِمْ سَاء مَا يَحْكُمُونَ))
((Na wamemwekea sehemu Allaah katika mimea na wanyama Alioumba, nao husema: Hii ni sehemu ya Allaah - kwa madai yao - na hii ni ya miungu tunao washirikisha. Basi vile walivyo wakusudia miungu yao havimfikii Allaah na vilivyo kuwa vya Allaah huwafikia miungu yao. Ni uovu kabisa hayo wanayo yahukumu)) [Al-An’aam: 36]
(( وَكَذَلِكَ زَيَّنَ لِكَثِيرٍ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ قَتْلَ أَوْلاَدِهِمْ شُرَكَآؤُهُمْ لِيُرْدُوهُمْ وَلِيَلْبِسُواْ عَلَيْهِمْ دِينَهُمْ وَلَوْ شَاء اللّهُ مَا فَعَلُوهُ فَذَرْهُمْ وَمَا يَفْتَرُونَ))
(( وَقَالُواْ هَذِهِ أَنْعَامٌ وَحَرْثٌ حِجْرٌ لاَّ يَطْعَمُهَا إِلاَّ مَن نّشَاء بِزَعْمِهِمْ وَأَنْعَامٌ حُرِّمَتْ ظُهُورُهَا وَأَنْعَامٌ لاَّ يَذْكُرُونَ اسْمَ اللّهِ عَلَيْهَا افْتِرَاء عَلَيْهِ سَيَجْزِيهِم بِمَا كَانُواْ يَفْتَرُونَ))
(( وَقَالُواْ مَا فِي بُطُونِ هَذِهِ الأَنْعَامِ خَالِصَةٌ لِّذُكُورِنَا وَمُحَرَّمٌ عَلَى أَزْوَاجِنَا وَإِن يَكُن مَّيْتَةً فَهُمْ فِيهِ شُرَكَاء سَيَجْزِيهِمْ وَصْفَهُمْ إِنَّهُ حِكِيمٌ عَلِيمٌ))
(( قَدْ خَسِرَ الَّذِينَ قَتَلُواْ أَوْلاَدَهُمْ سَفَهًا بِغَيْرِ عِلْمٍ وَحَرَّمُواْ مَا رَزَقَهُمُ اللّهُ افْتِرَاء عَلَى اللّهِ قَدْ ضَلُّواْ وَمَا كَانُواْ مُهْتَدِينَ))
((Na kadhaalika hao washirika wao wamewapambia wengi katika washirikina kuwaua watoto wao ili kuwaangamiza na kuwavurugia dini yao. Na lau kuwa Allaah Angelipenda wasingefanya hayo. Basi waache na hayo wanayo yazua))
((Nao husema: Wanyama hawa na mimea hii ni mwiko. Hawatokula ila wale tuwapendao - kwa madai yao tu. Na wanyama hawa imeharimishwa migongo yao kupandwa. Na wanyama wengine hawalitaji jina la Allaah juu yao. Wanamzulia uwongo tu Allaah Atawalipa kwa hayo wanayomzulia))
((Na
husema: Waliomo matumboni mwa wanyama hawa ni kwa ajili ya wanaume wetu
tu, na wameharamishwa kwa wake zetu. Lakini ikiwa nyamafu basi
wanashirikiana. Allaah Atawalipa kwa maelezo yao hayo. Hakika Yeye ni Mwenye Hikma, Mwenye Kujua))
((Hakika
wamekhasirika wale ambao wamewaua watoto wao kwa upumbavu pasipo kujua,
na wakaharimisha alivyo waruzuku Allaah kwa kumzulia Allaah Hakika
wamepotea, wala hawakuwa wenye kuongoka)) [Al-An’aam: 137-140]
Kisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anawauliza na kuwakanusha:
((ثَمَانِيَةَ أَزْوَاجٍ مِّنَ الضَّأْنِ اثْنَيْنِ وَمِنَ الْمَعْزِ اثْنَيْنِ قُلْ آلذَّكَرَيْنِ حَرَّمَ أَمِ الأُنثَيَيْنِ أَمَّا اشْتَمَلَتْ عَلَيْهِ أَرْحَامُ الأُنثَيَيْنِ نَبِّؤُونِي بِعِلْمٍ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ))
(( وَمِنَ الإِبْلِ اثْنَيْنِ وَمِنَ الْبَقَرِ اثْنَيْنِ قُلْ آلذَّكَرَيْنِ حَرَّمَ أَمِ الأُنثَيَيْنِ أَمَّا اشْتَمَلَتْ عَلَيْهِ أَرْحَامُ الأُنثَيَيْنِ أَمْ كُنتُمْ شُهَدَاء إِذْ وَصَّاكُمُ اللّهُ بِهَذَا فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَى عَلَى اللّهِ كَذِبًا لِيُضِلَّ النَّاسَ بِغَيْرِ عِلْمٍ إِنَّ اللّهَ لاَ يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ))
((Amekuumbieni
namna nane za wanyama: Wawili katika kondoo, na wawili katika mbuzi.
Sema je, Ameharamisha yote madume wawili au majike wawili, au waliomo
matumboni mwa majike yote mawili? Niambieni kwa ilimu ikiwa nyinyi
mnasema kweli))
((Na
wawili katika ngamia, na wawili katika ng'ombe. Sema: Je, Ameharamisha
yote madume wawili au majike wawili, au waliomo matumboni mwa yote
majike? Au, nyinyi mlikuwapo Allaah Alipokuusieni haya? Basi ni nani
dhaalimu mkubwa kuliko yule aliyemzulia Allaah uongo, kwa ajili ya
kuwapoteza watu bila ya ilimu? Hakika Allaah Hawahidi watu madhaalimu)) [Al-an’aam: 143-144]
Ni ujinga, upotofu kutokana na akili na matamanio yao yaliyowafanya waweke madai kama hayo ya shirk na kufru.
Tunaelezea baadhi ya madai yao kwa ufupi:
- Baadhi ya vyakula na wanyama ni kwa ajili ya Allaah na wengine ni kwa ajili ya miungu yao (masanamu). Na hao wanyama walikuwa wakiachwa warande kwa uhuru bila ya kutumiliwa kwa kufaidika nao chochote ikiwa kuwapanda au kuwachinja. Wanyama walipewa majina ya masanamu yao Bahira, Saaibah, Waswiyla na Haam.
- Kichinjo chochote kilichohusishwa na Allaah, hakikuliwa isipokuwa kilichotaja majina ya masanamu yao wakati wa kuchinja. Ama walichokichinja kwa ajili ya masanamu yao, hawakuwa wakitaja jina la Allaah wakati wa kuchinja.
- Wanapogawa hivyo vitu na ikatokea kwamba kilichokuwa cha masanamu yao kimeharibika, hubadilisha na kile kitu walichomhusisha Allaah. Ama ikiwa kilichoharibika ni cha Allaah, basi hukiacha hivyo hivyo Kwake.
- Ikiwa ni wanyama, na mfano mnyama huyo amezaa watoto wane, hugawa wawili wa Allaah, na wawili wa masanamu yao. Pindi ikiwa wanyama waliowahusisha na Allaah, ni wenye nguvu kuliko wa masanamu yao, waliwabadilisha na kuwahusisha masanamu yao.
- Wanyama walipokuwa waja wazito, waliharamisha maziwa yao kunywewa na wanawake, wakaruhusu wanaume pekee wanywe.
- Kondoo alipozaa kondoo dume, walimchinja na nyama ilikuwa halaal kwa wanaume pekee, wanawake hawakuruhusiwa kuila.
- Kondoo dume anapozaa jike, hawakuwa wakimchinja. Lakini anapozaa mnyama asiyekamilika (still-born) walimchinja na kuwaruhusu wanawake wamle.
Funzo gani au faida gani tunapata baada ya kutambua upotofu na ujinga wa hao Washirikina na madai yao hayo? Jibu ni kwamba:
Kwanza:
Sisi Waislamu tumejaaliwa neema kubwa kuepukana na shirk kama
hizo. Hivyo inapasa tuwe tunamshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)
Kutuongoza katika Uislamu na kututoa katika kiza cha ujinga kama huo.
Pili:
Kuisoma
Qur-aan, kuifahamu maana yake, kujua sababu za kuteremshwa Aayah,
humzidishia mtu kuzidi kupenda kujifunza Qur-aan na kuzidi kutambua
neema za Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) juu yetu kama neema kubwa ya Uislamu na ndipo tutakapoweza kuithamini dini yetu na kuipenda.
03 Wasiya Kumi Wa Allaah - Utangulizi-3
Baada
ya Aayah za madai yao Washirikina na baada ya Allaah (Subhaanahu wa
Ta'ala) Kuwauliza madai yao, ndipo Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) katika Aayah
inayofuatia Anamwambia Mjumbe Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa
sallam) aseme kuwa hayo Hakuyaharamisha Yeye bali ni uzushi wao na
uongo wanaomzulia Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala). Ama Aliyoharamisha
yanayohusiana na wanyama ni yafuatayo:
((قُل لاَّ أَجِدُ فِي مَا أُوْحِيَ إِلَيَّ مُحَرَّمًا عَلَى طَاعِمٍ يَطْعَمُهُ إِلاَّ أَن يَكُونَ مَيْتَةً أَوْ دَمًا مَّسْفُوحًا أَوْ لَحْمَ خِنزِيرٍ فَإِنَّهُ رِجْسٌ أَوْ فِسْقًا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللّهِ بِهِ فَمَنِ اضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلاَ عَادٍ فَإِنَّ رَبَّكَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ))
((Sema:
Sioni katika yale niliyofunuliwa mimi kitu kilichoharamishwa kwa mlaji
kukila isipokuwa kiwe ni nyamafu, au damu inayomwagika, au nyama ya
nguruwe, kwani hiyo ni uchafu; au kwa upotofu kimechinjwa kwa jina la
asiyekuwa Allaah Lakini mwenye kushikwa na dharura, bila ya kutamani
wala kupita mipaka, basi hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye Kusamehe,
Mwenye Kurehemu)) [Al-An’aam: 45]
Baina
ya hizo Aayah Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ametaja Neema Zake na
mimea, matunda na wanyama kwamba vyote hivyo Ametuuumbia kwa ajili ya
manufaa yetu na Akatuonya tusifuate nyao za Shaytwaan akaja kutupotoa.
((وَهُوَ الَّذِي أَنشَأَ جَنَّاتٍ مَّعْرُوشَاتٍ وَغَيْرَ مَعْرُوشَاتٍ وَالنَّخْلَ وَالزَّرْعَ مُخْتَلِفًا أُكُلُهُ وَالزَّيْتُونَ وَالرُّمَّانَ مُتَشَابِهًا وَغَيْرَ مُتَشَابِهٍ كُلُواْ مِن ثَمَرِهِ إِذَا أَثْمَرَ وَآتُواْ حَقَّهُ يَوْمَ حَصَادِهِ وَلاَ تُسْرِفُواْ إِنَّهُ لاَ يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ))
(( وَمِنَ الأَنْعَامِ حَمُولَةً وَفَرْشًا كُلُواْ مِمَّا رَزَقَكُمُ اللّهُ وَلاَ تَتَّبِعُواْ خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ))
((Na
Yeye Ndiye Aliyeziumba bustani zenye kutambaa juu ya chanja, na
zisiotambaa, na mitende, na mimea yenye matunda mbalimbali, na mizaituni
na mikomamanga inayofanana na isiyofanana. Kuleni matunda yake
inapozaa, na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake. Wala msitumie kwa
fujo. Hakika Yeye Hawapendi watumiayo kwa fujo))
((Na
katika wanyama Amekujaalieni wenye kubeba mizigo na kutoa matandiko.
Kuleni katika Alivyokuruzukuni Allaah wala msifuate nyayo za Shaytwaan.
Hakika yeye ni adui yenu dhaahiri)) [Al-An’aam: 141-142]
Mwishowe ndipo Anapomwambia Mjumbe Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
((قُلْ تَعَالَوْاْ أَتْلُ مَا حَرَّمَ رَبُّكُمْ عَلَيْكُمْ...))
((Sema: Njooni nikusomeeni Aliyokuharamishieni Mola wenu Mlezi..)) hadi kumalizika hizo Aayah tatu zenye wasiya huu wa mambo kumi.
Zingatia kwamba katika kila mwisho wa Aayah hizo Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anataja kuwa ni Wasiya ili …..
((Hayo Amekuusieni ili myatie akilini))
((Hayo Amekuusieni ili mpate kukumbuka
((Hayo Amekuusieni ili mpate kumcha Mungu))
Tutaendelea kutaja
wasiya au amri zote kwa kuelezea moja moja kila wiki ili zifahamike
vizuri na kwa upana zaidi, hadi tuzimalize zote Inshaa-Allaah. Ni
matumaini yetu kuwa huu wasiya au hizi amri zitatekelezwa kama zllivyo maamrisho yake na kutegemea thawabu kutoka kwa Mola wetu Mtukufu.
Itaendelea InshaAllaah…/
No comments:
Post a Comment