Wednesday, 29 July 2015

Ayyuwb: Mfano Katika Imani Na Subira (Ustahimilivu)


Imetafsiriwa na Ukht Haliymah ‘Abdullaah

Historia ya Ayyuwb (katika ujira) inawapa faraja wale wote ambao ni wagonjwa au walionyimwa mali au watoto.
Malaika walikuwa wanajadili hali ya binaadamu, utiifu na uasi wao.
Mmoja wao akasema kwamba Ayyuwb ndio mbora wa watu ulimwenguni. Alikuwa Muumin mtiifu, daima akiswali kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Alimbariki kwa kuwa tajiri miaka themanini. Muda wote huu hakusahau kumuabudu au kumshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Alishirikiana katika utajiri wake na maskini na kuwavisha walio uchi.
Shaytwaan hakuamini kwamba kuna mtumishi mkweli kama Ayyuwb. Shaytwaan alifikiri kwamba utajiri wake ndio sababu ya ukweli wake, kwa hiyo akamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kwa uwezo Wake amuondoshee Ayyuwb utajiri kwa nia mbaya ya kumpotosha. Allaah Akamuondoshea kumpima Nabii Wake.
Akaonyesha kutokana na upotevu huo kwa kusema utajiri ni wa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) na namshukuru kwa Aliyoniruzuku na namshukuru kwa Aliyochukua. Akashuka chini kwa kusujudu. Hili lilimfanya Shaytwaan akasirike.
Shaytwaan alijaribu mara mbili kumpoteza Ayyuwb baada ya kukosa utajiri wake kwa kumuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kwa nguvu zake kumuondoshea watoto na afya. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Alisema nitakupa uwezo katika mwili wake, lakini nakutahadharisha kuifikia roho yake, ulimi, moyo, kwa sababu ndani yake inasema uongo kuhusu Imaan ya kweli. Ayyuwb akaonyesha mwenendo alioufuata wakati alipochukuliwa utajiri wake.
Shaytwaan aligundua kwamba hawezi kumpoteza Ayyuwb, hivyo alimwendea mkewe kumpoteza (kumdanganya), kwa kumkumbusha maisha yao ya zamani (ya utajiri). Shaytwaan alifanikiwa katika kumdanganya mkewe. Hilo lilimpelekea kumlalamikia Ayyuwb kuhusu hali waliyo nayo sasa. Hili lilimfanya Ayyuwb kuapa kwamba atampiga viboko 100 ikiwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala ) Atamrudishia afya yake. 
Shaytwaan hakufanikiwa katika kumpoteza Ayyuwb. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Akarudishia vyote Alivyopoteza. Ikabakia kwa Ayyuwb sasa kutimiza kiapo chake cha kumpiga fimbo mkewe.
Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Akamuagiza kumpiga mkewe kwa mara moja fimbo 100 za mianzi, kwa Kumuonea huruma huyo mama. Kweli Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) ni mwingi wa rehema.
Kisa cha Ayyuwb kitakuwa daima ni ukumbusho kwetu sote. Inatakiwa tusome kisa hiki mara kwa mara kwa ajili ya kujikumbusha. Wengi wetu tunalalamika kwa kitu kidogo katika maisha. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Alimpa mtihani Ayyuwb kwa namna ambayo kweli inatakiwa tujihusishe nayo.
Imani yake na uvumilivu ni kitu ambacho kama sisi ni Waumini wa Kiislamu wa kweli tujaribu na kutekeleza katika maisha yetu, wakati Akitupa mtihani katika hali hizi. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) katika Qur-aan:
“…Bila shaka tulimkuta ni mwenye subira, mja mwema, kwa hakika alikuwa mnyenyekevu sana.” Swaad: 44

Wakati huu ni lazima tumkumbuke Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) zaidi, kufanya ibaada kwa bidii, na kuwa wenye kushukuru sana badala ya kutoridhika na hali zetu. Inabidi Tumtukuze na Tumshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kwa kila hali Atakayotupa majaribio. Kama tunavyojua huu ni wakati ambao Shaytwaan anajaribu kuchezea akili zetu, hisia, na udhaifu wetu. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Hawezi kusahau kamwe kumlipa mwenye kumtumikia kwa hiyo kazi kubwa.



Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Na (Mtaje) Ayyuwb alipomwita Mola wake (akasema) Mimi imenipata dhara Nawe Ndiye Unayerehemu kuliko wote wanaorehemu.
“Basi tukamkubalia (wito wake) na tukamuondolea dhara aliyokuwa nayo, na tukampa watu wake na mfano wao pamoja nao. Ni rehma inayotoka Kwetu, na ukumbusho (mzuri) kwa wafanyao ibaada) Al-Anbiyaa: 83-84.
Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Atupe imaan na uvumilivu wakati wa mitihani, Aamiyn.

No comments: