Imesimuliwa ya kwamba kulikuwa na mcha Mungu aliyependwa sana na watu wa wakati wake akiitwa Wadd. Alipofariki, swahiba zake walilizunguka kaburi lake huko Babylon kwa masikitiko makubwa. Ibilisi alipoona hilo, aliwashauri kumtengenezea sanamu ili wapate kumkumbuka.
Walikubaliana na hilo,
hivyo likatengenezwa na kuwekwa mbele ya umma wa watu. Kizazi
kilipokuja kuona namna sanamu la Wadd linavyotukuzwa, wakaamua kuweka
sanamu hilo
ndani ya kila nyumba. Baada ya kupita muda mrefu na pia kuondoka elimu
ya Dini, watoto wa hao watu walikuja kuabudia masanamu hayo.
Kisa
cha Wadd kinatudhihirishia ya kwamba hawakuanza kuabudia masanamu kwa
ghafla moja tu. Walianza kidogo kidogo hadi kuingia kwenye shirki moja
kwa moja. Na kisa hichi kinadhihirisha Qawl ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kwamba Ibilisi ni adui aliye wazi kabisa:
{{Hakika Shaytwaan kwa mwanadamu ni adui aliye dhahiri}} [17:53]
Ibilisi
hana haraka ya kuwavuta viumbe na wala hakati tamaa, huanza kidogo
kidogo na hatimaye kuwatumbukiza ndani ya dimbwi la maasi bila ya
kujijua. Mfano mwengine ni wa Muislamu mwenye kusimamisha Swalah tano.
Ibilisi huanza kumuondoshea hamu ya kufika Masjid mapema, baadaye
humshughulisha ili asipate kuswali, huendelea kwa kuswali nyumbani na
hatimaye huacha kabisa.
Maandishi
ya SW kusimama kwa Subhaanahu Wa Ta’ala na SAW kuelezea Swalla Allaahu
‘alayhi wa sallam ni mambo mengine ambayo hapana budi kuyafikiria
vizuri. Kwa hali hii, haitokuwa ajabu kuona kizazi kinachofuata
kikitamka: Allaah Ess Dabal Yuu (SW) au Mtume Ess Eee Dabal Yuu (SAW).
Halikadhalika, mambo ya kusherehekea birthday hayana mnasaba ndani ya Diyn hii tukufu. Wanaswara wanayo birthday ya Yesu (Krismasi), Waislamu nao wakaweka birthday ya Mtume! Laa hawla! Jina la birthday
likabadilishwa ili lipate lafdhi zile za Kiarabu na kuitwa Mawlid. Kwa
mtindo huu, ndio tunaona sasa hata Waislamu hawaelewi kufunga Jumatatu
wala Alkhamisi, Sunnah za Swalah ya dhuhaa na witri zote kaachiwa
mwenyewe Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Wanasubiri
Mfunguo sita waende kusoma hayo Mawlidi wakielewa kuwa ndio kumtukuza
kipenzi chetu.
Yeye
Ibilisi hamuachi mtu hadi mauti yamfike. Hivyo, haifai kusema kwamba
‘nitatubu baadaye’ au ‘nitaanza kuvaa hijabu nikifika umri kadhaa’.
Kwani tunashuhudia ndani ya jamii zetu kizee cha kupindukia miaka 85
kikiwa kinaimba kwa matusi ya juu na kunywa pombe mithili ya kijana wa
miaka 20!
Vipi tutaepukana naye?
Kuna njia mbili kuu za kuepukana na Ibilisi ambazo ni:
Kwanza
ni kufuata amri za Allaah. Hii ni pamoja na kukumbuka wasia wa Mola
Mlezi wa kutomfuata Ibilisi na badala yake kumuabudia Yeye pekee kwani
hii ndiyo njia iliyonyoka:
{{Je,
Sikukuagizeni (Sikukuusieni) enyi wanaadamu kuwa msimuabudu Shaytwaan?
Hakika yeye ni adui aliye dhahiri kwenu. Na ya kwamba niabuduni Mimi.
Hii ndiyo njia iliyonyoka.}} [36:60-61]
Pili ni kushikamana kwa hali zote katika mwendo wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pamoja na Makhalifa wake waadilifu:
"...
Basi shikamaneni na Sunnah zangu na Sunnah za Makhalifa wangu waongofu,
kamataneni nazo kwa magego (shikamaneni nazo kwa nguvu zote)" [Abu Daawuud 4607, At-Tirmidhy 2676 Nayo ni Hadiyth Nzuri Sahihi]
Huyo
ndie Ibilisi ambaye Radhi za Allaah zipo mbali na yeye. Athari ya
kumfuata Ibilisi ni mbaya mno, kwani hutuwekea kizuizi baina yetu na
Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Na kila mwenye kumfuata yeye ataelekea kwenye njia potofu.
No comments:
Post a Comment