News

Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki yakutana na Gazeti la “Kisiwa”
Mjumbe wa Kamati ya Mawasiliano Hizb-ut Tahrir Afrika Mashariki Sheikh Mussa Kileo karibuni alikutana na gazeti la ‘Kisiwa’ linalotolewa na Waislamu na kuchapishwa kila wiki. Ziara hiyo ililenga mambo mawili makubwa: Moja, ni kutoa nasaha kwa gazeti hilo juu ya taarifa, ya moja ya gazeti lao la karibuni ukurasa wa mbele iliyohusiana na Hadd (adhabu) ya mzinifu. Katika kichwa cha habari cha gazeti hilo kilionesha kimakosa kwamba adhabu ya mzinifu ni kupigwa bastola. Gazeti hilo lilikiri kukosea, na kwa mujibu wa mhariri wa gazeti hilo walikusudia kuweka alama ya kuuliza mbele ya kichwa hicho cha habari lakini walisahau. Dhamira ya pili ya ujumbe huo ni ziara za kawaida kwa Hizb ut Tahrir Afrika Mashariki kuwazuru na kuwatembelea ndugu zetu Waislamu na taasisi mbalimbali za Kiislamu na kubadilishana nao mawazo juu ya dini yetu tukufu.        ****************************************************************************                  
Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki inalaani vikali  kitendo cha polisi cha kumuua  kijana Idris Mohammed  mwenye umri wa miaka 26 Muhammed nyumbani kwao Bondeni Mo kwa tuhuma za ugaidi!   Baada ya mauaji haya mkuu wa CID,Ndegwa Muhoro akasema kuwa serikali itafunga baadhi ya Misikiti kama hatua ya ‘kukabiliana na ugaidi’. Tungependa kuifafanua hali hii kama ifuatavyo:-
Ukatili na unyama wa kikosi cha polisi ambacho jukumu sio lake sio kuvuruga usalama  bali  ni kulinda usalama.   Kwa masikitiko makubwa katika  dhidi ya ‘ugaidi’ polisi bila hata amri ya mahkama   huvamia watu majumbani tena wakiwa usingizini  na kuwapiga risasi watuhumiwa  hata wanapojisalimisha!   Mauaji haya ambayo yamekuwa yakifanywa kila mara  tayari yameacha majumba mengi ya Waislamu kubakia pasina na vijana ambao ndio nguzo kubwa  kwa wazazi wao.

Cha kuzidisha mchanga maji serikali inanuia kufunga baadhi ya  misikiti eti kuwa inatoa mafunzo ya ugaidi!  Je hatua hiyo haigongani na katiba ya Kenya na hata hiyo iitwayo Demokrasia kuwa inalinda  majumba  ‘uhuru wa kuabudu’ . Hii ni dhulma nyengine kubwa inayofichua kuwa katiba  za nchi za  kidemokrasia pia hukiukwa kwenye vita dhidi ya Waislamu. Na ni nani dhalimu Mkubwa kuliko Yule anayezuia misikiti ya MwenyeziMungu kwamba humo lisitajwe jina la MwenyeziMungu na akajitahidi kuiharibu? [Baqara: 114]

Mateso haya dhidi ya Waislamu  wa Kenya  ni natija ya kanuni ‘Prevention of Terrorism Bill Act 2102’  iliopitishwa tena mbele ya wabunge wa Kiislamu mwezi Oktoba mwaka 2012.  Na  Hizb  yauliza je haya ndio maslahi ya Waislamu  ambayo  ‘ulamaa’ wanaopigia debe demokrasia na chaguzi zake kwa hoja ya kutetea maslahi ? Twasema kuwa ugaidi ni mmoja katika kampeni hatari inayotumiwa na  Marekani  kushambulia Uislamu na Waislamu.  Hivyo si kweli kuwa Uislamu  unahatarisha usalama bali sera mbovu za Ubepari ndio chanzo cha utovu wa usalama kote duniani na haya yako wazi kwa kila mwenye macho na masikio  moyo wa kufahamu.

Mwisho sisi twaamini kuwa Uislamu una hoja nzito zinazoweza kujieleza na kutawala maishani tena pasina kutumia matendo ya kinguvu na mabavu.  Na hii ndio njia ya kweli na ya kisheria ambayo sisi tunajifunga hadi pale Mola atakapotunusuru kwa nusra yake na nusra yake iko karibu inshallah.
KUMB: 23 / 1435 AH        Jumatano, 22nd Dhul Qiddah 1435 AH        17/09/2014 CE   
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki*****************************************************************************
Kama tulivyoonyesha katika sehemu ya pili ya makala yetu mgawiko wa hadithi kuegemea idadi ya wapokezi, tuangalie katika sehemu hii ya mwisho kugawika kwa hadithi kwa kimsingi wa kukubaliwa na kukataliwa.
Hadithi hugawika sampuli nne katika msingi huu nazo ni :-
1-Sahihi  (الصحيح)
2-Hasan   (الحسن)
3-,Dhaifu  (الضعيف)
4-Madhoo (الموضوع)
Hadithi Sahihi ni ile iliotimiza masharti yafuatayo:-
Kwanza: Kila mpokezi wake ameipokea kwa kuichukua moja kwa moja kwa aliemsimulia na kuendelea hivi hadi kufikia kwa Mtume SAAW. Hii ndio wasomi wa hadithi huita itiswal Sanad   اتصال السند
Pili: Wapokezi wawe ni waadilifu na maana ya uadilifu hapa ni kuwa na uovu. Hii inamaanisha kuwa Uislamu wake ni mzuri. Aidha mpokezi awe amebaleghe au kuvunja uongo(Mwanamke) na awe ni mwenye maadili mema.
Tatu:  Mpokezi asiwe na sifa ya kusahausahau na kutohifadhi maneno kwa uzuri.
Nne:  Isiwe na kasoro (illah) yoyote katika upande wa upokezi  سند wala katika upande wa maudhui (matn). Kwa mfano lau hadithi imepokelewa na mpokezi jina lake Abdalla bin Diinar ambalo ndio jina lake hasa kisha jina hili likabadilishwa na Amru bin Diinar tayari hii ni kasoro ya upokezi. Na  mfano wa upande wa Matn ni  La kuelewa hapa ni kuwa wasomi wametaja kuwa kasoro hizi yaani Isnad na Matn ziko zinazoweza kufanya hadithi isiwe sahihi au pia bado iwe ni sahihi. Asema Ibn Swaleh : ‘Kasoro kwenye wapokezi zaweza zikaitia doa hadithi au kutoitia halkadhalika katika  kasoro katika upande wa matn’. Kasoro hizi ni sharti zisiwe ni kwa wapokezi wote wa hadithi hiyo.
Masharti haya ndio hufanya hadithi ikaitwa sahihi. Mfano wa hadithi sahih ni ile inayosimuliwa na swahaba Jubair bin Mut’am kutoka kwa babake akisema  nilimsikia Mtume SAAW akisoma sura Tuur kwenye swala ya Maghribi.
 سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم قرأ في المغرب با الطور
Wapokezi wote hadithi ni watu wanaoaminika kuanzia swahaba hadi kwa aliekuja na hadithi naye ni Abdallah Bin Yusuf huyu ni mkweli naye akaipata kutoka kwa Maalik ambaye wanavyouni wanakubaliana kuwa Maalik ni Haafidh yaani mtu aliehifadhi hadithi laki moja kisanad na kimatn na kuelewa hali zake. Maalik akaipokea kutoka kwa  Ibn Hisham huyu ni Faqiih alieipokea kwa Muhamad ambaye ni thiqa mkweli ambaye naye aliipokea kwa swahaba Jubair Bin Mut’am. Hata hivyo hivyo ni muhimu kuelewa kusihi kwa hadithi haina maana kusihi kwake kidalili kwani yawezekana hadithi ni sahihi lakini imefutwa mansoukh
Tuje katika hadithi Hasan. Hii ni ile iliokosa moja wapo ya sharti ya hadithi sahihi tulizozitaja hapo juu. Kwa mfano ikipatikana kuwa mmoja ya wapokezi wa hadithi alikuwa na sifa ya kutodhibiti maneno au kuyahifadhi vizuri basi ndio huitwa ‘hadith Hasan’ Hadithi hasan ni nyingi mno moja wapo ni ile iliosimuliwa na Tirmidhiy kutoka kwa  Abdillah bin Amru RA Kuwa mtume SAAW alikataza kuimba mashairi misikitini na biashara ndani yake na tahaluq (mazungumzo) kabla ya swala ya ijumaa. Hadithi hii ina mmoja katika wapokezi wake ana kasoro katika kuhifadhi maneno.
 - أنَّ النبيَّ -صلَّى الله عليه وسلَّم- "نهى عن تناشُد الأشعار في المسجد، وعن البيعِ والشراء فيه، وأنْ يتحلَّق الناس يوم الجمعة قبل الصلاة
 Angalizo: Kuna baadhi ya Masheikh wanaitolea ushahidi hadithi hii kuharamisha nasaha au bayana zinazotolewa kwenye misikiti mingi kabla ya khutba na kuziita bida’a. Twasema ushahidi huu una makosa katika kufahamu maana ya hadithi hii  kama pia kutoelewa tahqiq –l manat. Tamko la Tahaluq  hapa sio mawaidha bali ni vika vya kuzungumzia mambo ya kidunia. Kiasili kuna dalili nyingi za kuhimiza watu kupeana nasaha na mawaidha na dalili hizi sio khasa bali ni amma.  Ama bayana na halaka za kielimu hili linafaa halina utata kama vile sio  mashairi yote yanayokatazwa bali yale ya miito ya  kijaahilia. Atwahaawi asema kuwa itakuwa makuru kufanya tahaluq ikiwa kutapelekea kuharibu safu lakini ama kinyume chake yafaa.
Ama hadithi Dhaif nayo ni ile iliokosa masharti ya hasan. Kwa hivyo hadithi yoyote ilio na kasoro kwa wapokezi wake wote na pia kwenye upande matn. Hata hivyo hadithi ili iitwe dhaif ni sharti kwamba hakuna Isnad yoyote ambayo haina kasoro. Inapokuja hadithi dhaifu kwa riwaya tofauti tofauti au njia mbalimbali basi huangaliwa njia hizo na huenda ikapanda daraja hadithi hiyo kuwa Hasan au sahii. Hii inategemea kuwa njia hizi hakuna katika wapokezi wake waliotuhumia na urongo au uovu. Lakini lau maana yaliyobebwa na hadithi dhaif yanapatikana kwa hadithi sahihi basi hufanyiwa kazi yale maana ya hadithi sahihi.
Ifahamike kuwa suala la kusahihisha hadithi na kudhoofisha ni suala la ijthadi hivyo upo uwezekano wa hadithi kudhoofishwa na mujtahidi na ikasahihishwa na mujtahidi mwengine.   Kwa hivyo sio  kila mtu adandie suala hili kama atakavyo.  Kwa bahati mbaya ni leo mujtahiduna leo ni wachache mno hali iliosababishwa na mitaala ya kielimu inayosimamiwa na serikali za Kiilmaania wanaoajiri masheikh wenye kutunga fiqhi mpya ya Kiislamu. Hali hii imefanya Waislamu wengi leo ni wafuasi tu bali vipofu wanaosoma maneno ya masheikh au wanafunzi wao. Masheikh hao hawafichi tu haki wamejitia uwezo wa kusahihisha na kudhoofisha sanad za  baadhi ya hadithi zinazosimuliwa na watu wanaotofautiana kirai. Kwa mfano Abu Haatim Al-Raazi mwanachuoni wa madhhabu ya Hanbali alidhoofisha riwaya anazosimulia Al-imam Bukhar kwa hoja kuwa ana msimamo juu ya kua Quran inaposomwa basi yale matamshi ya msomaji huwa ni kiumbe.
Sheikh Fauzan alimdhoofisha Al baihaqiy kwa kuwa alikuwa na msimamo wa kuzifanyia Taaweel sifa za Allah. Kivyovyote vile tunakariri kuwa suala la kusahihisha na kudhoofisha hadithi ni suala la Mujtahiiduna pekee.
Tumalize kwa kuingalia hadithi Maudhoo. Hii ni hadithi iliotungwa na kutajwa kuwa imepokelewa kutoka kwa Mtume SAAW. Nayo ni ima mtu kujitungia maneno au kuchukua maneno ya wenyehikma kisha akayanasibisha kwa Mtume SAAW.
Mmoja ya watu mashuhuri katika kitendo hiki cha kutunga hadithi ni Abu Ismah kisha akaeleza sababu yake ya  kutunga hadithi kuwa; ‘Nimeona watu wanaihama Quran (hawaisomi) na kujishughulisha zaidi na Fiqhi ya Abu Hanifa ,Maghaazi na  Muhammad bin Ishaq nami nikatunga hadithi..)
Kuna sababu kadhaa zilizochangia watu kutunga hadithi nazo ni kuutukana Uislamu na kunusuru madhhebu Fulani.

Angalizo Kuna baadhi ya masheikh hubadilisha sanad za hadithi au kuzikataa kabisa kwa hoja ya kugongana na fikra yake na jambo hili lipo sana katika hadithi zinazungumzia mitagaa ya itikadi. Kwa mfano,Hadithi isemayo من كنت مولاه فعلي مولاه  imekataliwa na baadhi ya masheikh akiwemo Ibn Taymia huku  Sheikh Albani ameikubali.
Riwaya nyingi zinazopokelewa kutoka kwa njia ya  Ubaiya bin Ka’ab na kutoka kwa Abu Isma kisha kuegemezwa kwa Ikrama kutoka kwa Ibn Ibn Abbas (Ra) huwa ni maaudhoo’
Maudhoo ni katika hadithi mbovu zaidi zisizofaa kabisa kutolewa ushahidi.
Hivi ndivyo vigawanyo vya hadithii kwa kuzingatia upande wa kuzikataa na kuzikubali.****************************

‘Kukomeshwa Adhabu Ya Kifo’: Dhihirisho La Mgongano Katika Mfumo Wa Kidemokrasia- 1


Masoud Msellem
Tangu mwaka 2003, siku ya tarehe 10 Oktoba ya kila mwaka imechaguliwa kimataifa kuwa siku ya kampeni ya kukomeshwa kwa adhabu ya kifo duniani. Kampeni hii hufanywa dunia nzima ikiungwa mkono na baadhi ya nchi, majukwaa ya haki za raia na taasisi mbali mbali hususan zinazoitwa na kujishughulisha na masuala ya ‘haki za binaadamu’. Dhamira ya kampeni hii ni kuhakikisha kwamba adhabu hiyo inafutwa kabisa katika uso wa dunia.
Adhabu hii ni miongoni mwa adhabu ya kale na imekuwepo tangu katika zama za sheria za mayunani (wagiriki) zilizobuniwa na Draco katika miaka ya 621 BC. Katika bara la Asia nchi kama China ilikuwa sheria maarufu hadi kusitishwa kwa muda katika zama za Utawala wa Tang (Tang Dynast) katika mwaka wa 747. Kwa upande wa baadhi ya nchi nyingine  za Ulaya ilitumika kiasi kwamba hata katika baadhi ya  mizozo yao ya  kikabila(vendetta) ikiwa kama chombo cha fidia au  njia ya utatuzi wa migogoro yao hususan  katika zama za Viking. Kwa upande wa dini, wakatoliki waliitumia sana kwa kufuata mafunzo ya Thomas Aquinas, hadi kufikia kuruka mipaka katika historia dhidi ya wanaopinga mafundisho ya kanisa hilo. Pia katika mfumo wa Uislamu ambao ndio mfumo wa haki na ambao sheria zake ni za wahyi nao umeweka adhabu ya kifo katika baadhi ya makosa ya ‘Hadd’ kama vile kwa anaeacha dini ya Uislamu na akakataa kutubu (murtad), mzinifu alieowa au kuolewa, vitendo vya liwati, ujambazi (ihrab), na mauwaji ya makusudi kama mawalii (ndugu) wa aliyeuliwa hawakusamehe au kukubali kulipwa fidia. Kadhalika adhabu hiyo inaweza kutumika katika upande wa adhabu za ‘Taazir’ kama itakuwa ipo haja ya kutoa adhabu hiyo kwa mujibu wa ‘ijtihadi’ ya kadhi. 
Adhabu ya kifo bado ilishika hatamu hata katika karne ya 18 na baada.  Kwa mfano, nchini Uingereza ilishtadi sana kati kati ya karne hiyo na baada, kiasi kwamba chini ya sheria yao iliyoitwa ‘Waltham Black Acts’ kwa kipindi cha karibu miaka mia kutoka 1740 mpaka mwaka 1834 iliwanyonga watu 8,753 katika England na Wales, huku idadi ya watu wao (population) kwa kipindi hicho ilikuwa haizidi watu Milioni  9. Urusi nayo iliwanyonga raia wake karibu 158,000 waliosaliti katika Vita vya kwanza vya dunia.***********************
******************************

Wanawake wa Kiislamu kamwe hawatopata hifadhi na ulinzi wao kutoka kwa yanayoitwa  Majeshi ya Kulinda Amani


Habari :
Mnamo tarehe 8 septemba 2014 Shirika la habari la Russia Today liliripoti matokeo ya utafiti  uliofanywa na Shirika la Haki za Binadamu la  Human Right Watch (HRW) juu ya matendo ya ubakaji  yanayotendwa na Vikosi vya Kulinda Amani vya Umoja wa Mataifa kwa wanawake wa kisomali pale wanapoomba misaada ikiwemo ya matibabu. Ripoti ya Shirika hilo ina anuani:  “Mabavu ya Wanaume hawa Juu Yetu: Udhalilishaji wa kijinsia na ushenzi wa Majeshi ya Umoja wa Afrika ndani ya Somalia”.
Ripoti hiyo imefichua wazi wazi  udhalilishaji na ushenzi wanaofanyiwa wanawake wa Somali wakiwemo watoto wa umri mdogo katika kambi mbili za majeshi ya Umoja wa Afrika (AMISOM) tangu mwaka 2013.
Katika utafiti huo, Shirika hilo la HRW liliongea na wahanga 21 waliofichua amma kubakwa au kudhalilishwa kijinsia. Misaada ya kibinadamu imekuwa ikitumika kama chombo cha  kuwalaghai wanawake hao na kuwatenza nguvu wakubwa na watoto kujihusisha na matendo ya ngono na wanajeshi hao wakati wakitafuta misaada ya madawa, maji na chakula.
Wahanga wa matukio hayo muda mwingi hubaki kimya kwa khofu ya kudhuriwa zaidi. Huku vikosi hivyo vikitamba kutokana na kinga inayowazuiya  kushtakiwa  na mahkama za ndani.
Maoni:
Ni jambo lililo wazi kwamba nchi za kibepari kamwe haziwezi kuwalinda wanawake. Na kimsingi wao ndio madhalimu wakubwa wa wanawake na wakiukaji wakubwa wa haki za wanawake na  heshima zao.
Linaloitwa Jeshi la Afrika la Kulinda Amani nchini Somalia ndio hao wanaosambaza vita na ufisadi nchini humo. Jeshi hilo limeundwa kutumikia maslahi ya madola ya magharibi hususan Marekani inayolenga kunyonya rasilimali za Somali na kupambana na Uislamu.
Uvamizi wa kigeni ndani ya  Somali umeleta majanga mengi kwa Waislamu wa Somalia na wakaazi jumla katika Ukanda wote wa Afrika Mashariki. Wakati matukio haya maovu na  ya kikatili  yakijiri, Umoja wa Afrika uko kimya kana kwamba hauoni yanayotendeka,  kwa kuwa ni Umoja wa kisanii  ulioundwa kwa ajili ya ajenda kutoka nje.
Muundo wa majeshi wa kimagharibi si zaidi ya mkusanyiko wa kundi la wabakaji wa wanawake wa Kiislamu kila wapaowakuta. Na hili ni kwa sababu wanawake wa Kiislamu wamekosa mlinzi na kinga tangu ilipoangushwa dola ya Kiislamu ya Khilafah. Tumeshashuhudia matukio kama hayo wakitendewa wanawake wa Kiislamu ndani ya Afghanistan, Bosnia, Iraki, Kashmir na maeneo mengi duniani.
Aina hii ya majeshi ni zao la nidhamu ya kidemokrasia ambayo ndio mvunjaji mkubwa wa heshima ya mwanamke kila mahala duniani. Na hii ni kwa kuwa haina khofu ya adhabu za Mwenyezi Mungu.
Ni Serikali ya Kiislamu ya Khilafah pekee ndio yenye uwezo wa kulinda na kuhifadhi heshima na hadhi ya wanawake wa Kiislamu na wasiokuwa Waislamu. Itakumbukwa namna Mtume Muhammad(SAAW) alivyowashughulikia wayahudi wa Bani Qainuka walipovunja heshima na hadhi  ya mwanamke wa Kiislamu. Aidha, tunakumbuka namna Khalifah Mu’tassim alivyowashughulikia Warumi pale walipomteka na kumdhalilisha mwanamke wa Kiislamu.
Imeandikwa kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir.
*********************

No comments: