Wednesday 15 February 2017

Ipi hekma ya kulala upande wa kulia kamaalivyofundisha Mtume Muhamady

Nini Hikma Ya Kulala Upande Wa Kulia Kama Alivyotufundisha Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ?

Yote tunayoyapata kutoka katika Sunnah ya mwalimu wetu, Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni mafunzo yenye faida kwetu ima faida ya nafsi zetu au faida katika mwili wetu au faida katika maisha yetu na kwa ujumla, bali kuna hikma kubwa kwenye mafunzo hayo:
عن البراء بن عازب رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه و قال صلى الله عليه وسلم : ((إذا أتيت مضجعك فتوضأ وضوءك للصلاة ثم ثم اضطجع على شقك الأيمن ثم قل :  أللهم  أَسْـلَمْتُ نَفْـسي إِلَـيْكَ، وَفَوَّضْـتُ أَمْـري إِلَـيْكَ، وَوَجَّـهْتُ وَجْـهي إِلَـيْكَ، وَأَلْـجَـاْتُ ظَهـري إِلَـيْكَ، رَغْبَـةً وَرَهْـبَةً إِلَـيْكَ، لا مَلْجَـأَ وَلا مَنْـجـا مِنْـكَ إِلاّ إِلَـيْكَ، آمَنْـتُ بِكِتـابِكَ الّـذي أَنْزَلْـتَ وَبِنَبِـيِّـكَ الّـذي أَرْسَلْـت"   واجعلهن آخر كلامك فإن مت مت على الفطرة)) – البخاري و مسلم
Kutoka kwa Al-Baraa Bin 'Aazib رضي الله عنهما kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kasema; utakapofika wakati wa kulala, tawadha kama wudhuu wa Swalah, kisha lala upande wako wa kulia, kisha sema:  "Allaahumma aslamtu nafsiy Ilayka, wa fawwadhwtu amriy Ilayka, wa wajjahtu wajhiya Ilayka, wa aljaatu dhwahriy Ilayka, raghbatan wa rahbatan Ilayka, laa maljaa wa laa manjaa Minka illa Ilayka, aamantu bi-Kitaabikal-ladhiy Anzalta, wa bi-Nabiyyikal-ladhiy Arsalta"
[Ewe Allaah,  nimeisalimisha nafsi yangu Kwako, na nimekuachia mambo yangu Wewe na nimeuelekeza uso wangu Kwako na nimeutegemeza mgongo wangu Kwako, kwa matajarajio na kwa kukuogopa, hapana sehemu ya kukimbilia wala ya kujiokoa ila Kwako, nimekiamini kitabu Chako Ulichokiteremsha na Mtume Wako Uliyemtuma] Na fanya hivyo iwe ni maneno yako ya mwisho kwani utakapokufa utakufa katika Fitwrah [(Uislamu]))  [Al-Bukhaariy na Muslim] 
Hatuna shaka na tunaamini  na kuyafuata  mafunzo yake kadiri tuwezavyo  kwani nani msemaye kweli kuliko Allaah (Subhanaahu wa Ta’ala) na Mjumbe Wake Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)? Mjumbe ambaye hasemi kwa matamanio yake ila ni wahyi utokao kwa Mola wetu Muumba Anayesema:
((وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَى))  (( إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَى))
((Wala hatamki kwa matamanio)) ((Hayakuwa haya ila ni ufunuo ulio funuliwa)) [An-Najm: 3-4]

Basi hebu tuone hikma ya kutufunza kulala upande wa kulia.



  

Ubongo (Brain)

 
Ubongo sehemu yake huwa upande wa kulia na ndio ambao unauongoza Moyo ulioko upande wa kushoto.


Mapafu (Lungs)



Pafu la upande wa kulia wa mwili ni kubwa kuliko pafu la upande wa kushoto, kwa kuwa pafu la upande wa kulia lina sehemu 3 wakati ambapo la upande wa kushoto lina sehemu 2 tu.
Ini (Liver)

   
Ini liko upande wa kulia na ndilo tezi (gland) kubwa kubwa kabisa mwilini.


Nyongo (Gall Bladder)


 
Nyongo nayo nipo upande wa kulia na ina majukumu ya kutengeneza utomvu ambao unameng’enyua (digest) mafuta.

 
 
Matumbo (Intestines)


 

Matumbo (Intestines) Na Sehemu Ya Mwisho Wa Utumbo (colon)

 


Sehemu ya 'mwisho wa Utumbo mkubwa' (colon) na mwisho wa matumbo (intestines) yako upande wa kulia. (Appendix) 
 
 
Moyo 
 

Moyo uko upande wa kushoto na ndio pampu la taratibu ya mzungukuo(circulatory system)
Tumeona kwamba  kwamba viungo vya mwili vikubwa viko upande wa kulia katika mwili, kwa hiyo mtu anapolala upande wa kushoto, huathiri viungo hivi na huleta madhara katika siha ya Binaadamu. Na juu ya hivyo mtu anapolala upande wa kulia huwa haileti shinikizo katika vyumba vya mapumziko ya moyo ambazo hufanya wepesi kazi ya Taratibu ya Mzunguko (circulatory cycle).
Kwa hiyo mtu anayelala upande wa kulia anapoamka asubuhi huamka akiwa mwenye nguvu na  mchangamfu.
Hadiyth za  Mtume صلى الله عليه وآله وسلم tulizoamrishwa na mapendekezo ya kulala upande wa kulia

عن أبي  هريرة رضي الله عنه قال :" رأى رسول الله صلى الله عليه و سلم رجلاً مضطجعاً على بطنه فقال ((إن هذه ضجعة يبغضها الله و رسوله))". رواه الترمذي  .
Imetoka kwa Abu Hurayrah رضي الله عنه ambaye kasema: Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alimuona mtu amelala kifudifudi, akasema: ((Kulala huku kunachukizwa na Allaah سبحانه وتعالى na Mtume Wake)) [At-Tirmidhy]

  عن  عائشة أن رسول الله  صلى الله عليه وسلم   "كان   إذاصلى  ركعتي    الفجر    (يعني سنتها)  اضطجع على شقه   الأيمن"  - صحيح البخاري
Imetoka kwa mama wa waumini 'Aaishah رضي الله عنها  kwamba "Mtume صلى الله عليه وآله وسلم  akishaswali rakaa mbili za Alfajiri, [yaani Sunnah za Alfajiri]  hulala upande wa kulia" [al-Bukhaariy] 
  


عن أبي أمامة قال: مر النبي صلى الله عليه وسلم على رجل نائم في المسجد منبطح على وجهه فضربه برجله وقال: (( قم أو اقعد فإنها نومة جهنمية))
 مسند أحمد وسنن ابن ماجه
Kutoka kwa Abu Amaamah kasema; alipita Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kwa mtu mmoja ambaye alikuwa amelala kifudifudi  msikitini akampiga hivi (teke) kwa mguu akasema: ((Inuka au kaa kwani kulala huku ni kama kulala kwa watu wa motoni))   [Musnad Ahmad na Sunan Ibn Maajah]

وعن حفصة رضي الله عنها قالت:" كان النبي صلى الله عليه وسلم إذا أخذ مضجعه جعل يده اليمنى تحت خده الأيمن" رواه الطبراني، صحيح الجامع  
Kutoka kwa mama wa waumini Hafswah رضي الله عنها   ambaye kasema: "Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alikuwa anapotaka kulala huweka mkono wake katika shavu la kulia" [At-Twabraaniy katika Swahiyh al-Jaami'y]
Amesema Imaam Ibn al-Qayyim (Allaah Amrehemu): "Kulala kwake Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa ubavu wake wa kulia kuna siri, nayo ni kuwa Moyo unakuwa juu kwa upande wa kushoto, kwa hivyo, ikiwa atalalia ubavu wake wa kushoto basi usingizi utakuwa mzito; kwani atakuwa katika hali ya utulivu na ushwari na hivyo kuwa usingizi wake ni mzito. Na kama atalala kwa upande wa ubavu wake wa kulia, basi atakuwa katika hali ya wasiwasi na usingizi wake utakuwa si mzito kwa kuwa moyo utakuwa katika hali ya wasiwasi na atahitajia utulie na moyo kupondokeka kwake.

Uharamu wa Valentine day

Valentine (Siku Ya Wapendanao) Na Hukumu Ya Kuisherehekea


BismiLLaah wa AlhamduliLLaah was-Swalaatu was Salaamu ‘alaa Muhammad wa ‘alaa ‘Aalihi wa Aswhaabihil Kiraam, wa Ba’ad,

Allaah سبحانه وتعالى Ametuchagulia Dini ya Kiislamu, Dini ya haki na Hatokubali dini yoyote nyingine. Anasema: 
((وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الإِسْلاَمِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ))  
((Na yeyote anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislaam basi haitokubaliwa kwake; naye katika Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika)) [Al-'Imraan: 85]

Na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ametuambia kuwa kutakua na makundi katika ummah wake ambao watawafuata maadui wa Allaah سبحانه وتعالى katika desturi na mila zao: 
((ستتبعون سنن من كان قبلكم شبراً بشبر وذراعاً بذراع حتى لو دخلوا جحر ضب لدخلتموه)) قالوا: أتراهم اليهود والنصارى؟ قال: ((فمن إذن؟)) البخاري ومسلم
((Mtafuata nyendo  za wale waliokuja  kabla yenu  hatua kwa hatua mpaka itafika hadi wakiingia katika shimo la kenge, na nyinyi mtaingia pia)) Wakasema (Maswahaba):  Ee Mtume! Je, unamaanisha Mayahudi na Manaswara? Akasema: ((Hivyo nani basi mwengine?)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

Maneno hayo aliyoyasema Mtume صلى الله عليه وآله وسلم hakika yamethibiti kwa sababu imedhihirika Waislamu kuigizia mila, desturi na tabia za makafiri na kuzisherehekea kama mfano siku hii inayoitwa 'Valentine day' (Siku ya Wapendanao).

Na baya zaidi na la kusikitisha sana ni kwamba sherehe hizi zinaenezwa katika njia mbali mbali za mawasiliano kama kutumiana kadi, barua pepe (e-mail), salamu katika simu za mkono. Hakika fitnah hii humfanya Muislamu aharibu 'Aqiydah (Iymaan) yake kwa kudhani kuwa anafanya jambo la kawaida na hali ni jambo lisilo katika shariy'ah ya dini yetu bali ni shirki kubwa na upotofu wa kufuata wanayoamini makafiri.


Historia Ya Sherehe Ya Siku Ya Valentine

Sherehe hii ya wapendanao ni sherehe ya wapagani  wa Kirumi wakati dini yao ya upagani ilikuwa ni dini iliyotapakaa kwa Warumi karne zaidi ya kumi na saba zilizopita.  Na fikra zao ilikuwa ni kuelezea hisia ya 'mapenzi ya kiroho'.

Kulikuwa na visasili (uongo) zilizohusishwa na sherehe hii ya upagani ya Warumi ambao umeendelea kutoka warithi wa Kikiristo. Miongoni mwa uongo huo ni kuamini kwao Warumi kuwa Romulus, aliyevumbua Rome, alinyonyeshwa siku moja na mbwa mwitu mwanamke, hivyo akampa nguvu na hikmah.

Warumi walikuwa wakisherehekea tukio hili katikati ya Februari kila mwaka kwa kufanya sherehe kubwa. Na mojawapo ya tambiko katika sherehe hii ni kuchinja mbwa au mbuzi. Vijana wawili wenye nguvu hujipaka damu ya mbwa au ya mbuzi katika miili yao, kisha huiosha damu hiyo kwa maziwa. Baada ya hapo, watu hufanya gwaride wakiwa vijana hawa wawilii wako mbele wakiongoza gwaride iliyokuwa ikitembea barabarani. Vijana hao wawili walikuwa wakichukua vipande vya ngozi ambavyo waliwapigia watu wanaowavuka. Wanawake wa kirumi walikuwa wakipokea mapigo hayo wakiamini kuwa yatawahifadhi na kutibu utasa.


Kuungamana Baina Mtakatifu Valentine (Saint Valentine) Na Sherehe Hii

Mtakatifu Valentine (Saint Valentine) ni jina waliopewa mashujaa wawili wakongwe waliokufa ambao ni wana wa kanisa la kikiristo. Inasemekena kwamba walikuwa ni wawili au mmoja tu. Huyo mmoja alikufa Rome kutokana na mateso ya kiongozi wa Kigothi aliyeitwa Claudius. Kanisa la Saint Valentine lilijengwa kwa ajili ya kudumisha kumbukumbu yake.

Warumi walipoingia ukristo, wakaendelea kusherehekea sikukuu ya wapendanao (valentine day) lakini wakabadilisha kutoka fikra ya upagani ya 'mapenzi ya kiroho' (spiritual love) na kuleta fikra nyingine iliyojulikana kama ni 'mapenzi ya mashujaa' yaliyowakilishwa na Saint Valentine ambaye aliuliwa kwa ajili ya kutetea mapenzi na amani. Vile vile ikajulikana ni sikukuu ya wapenzi, na Saint Valentine alifanywa kuwa ni mlezi wa mapenzi ya mtakatifu.

Miongoni mwa imani yao inayoambatana na sherehe hii ni kwamba majina ya wasichana waliofika umri wa kuolewa yaliandikwa katika vikaratasi vidogo vilivyokunjwa mviringo kisha vikawekwa katika chombo juu ya meza. Kisha wavulana waliotaka kuoa waliitwa na kila mmoja huchagua karatasi moja ikiwa na jina la msichana. Kisha hujiambatanisha naye huyo msichana aliyempata kutokana na kura hiyo aliyochagua kwa muda wa mwaka ili wajuane vizuri kisha tena hufunga ndoa, au kama hawakuelewana hurudia tena kufanya kura inapofika siku hiyo mwaka unaofatia.   

Vile vile imesemekana kwamba chanzo cha sikukuu hii, ni kwamba warumi walipokuwa wakristo baada ya ukristo kutapakaa, Mfalme wa Kirumi Claudius II alitoa hukumu katika karne ya tatu kwamba askari wasioe kwa sababu kuoa kwao kutawashughulisha na vita walivyokuwa wakipigana. Hukumu hiyo ilipingwa na Saint Valentine ambaye alianzisha kuozesha maaskari kwa siri. Alipokuja kujua mfalme, alimfunga jela na akamhukumu kuuliwa. Huko jela akapendana na mtoto wa mkuu wa jela, lakini ikawa ni siri kwani kutokana na sheria ya ukristo, mapadri na makasisi wameharamishwa kuoa au kupenda.
Hata hivyo alipewa heshima yake na wakristo kwa sababu ya kushikilia na kujikita imara katika ukristo wakati mfalme alipotaka kumsamehe kwa sharti aache ukristo na kuabudu miungu ya Kirumi ili awe msiri wake na awe mkwe wake. Lakini Saint Valentine alikataa ahadi hiyo na akapendelea ukristo, kwa hiyo akauliwa siku ya tarehe 14 Februari 270 M. Ndio ikaitwa siku hii kwa jina la huyo mtakatifu (Valentine).

Papa (Pope) naye akaifanya siku hiyo ya kufa Saint Valentine tarehe 14 Februari 270 M kuwa ni sikukuu ya mapenzi. Na ni nani alikuwa Papa huyo? Ni Askofu mkuu wa kanisa la 'universal church', ambaye ni mrithi wa mtakatifu Peter.

Ndugu Waislamu tazameni vipi huyo askofu anavyohusika katika kuadhimisha sikukuu hii ambayo ni uzushi katika dini yao ya Kikiristo. Hii itukumbushe kauli ya Allaah سبحانه وتعالى:
((اتَّخَذُواْ أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللّهِ))
((Wamewafanya Wanavyuoni wao mafuqahaa wa dini na Wamonaki wao kuwa ni miola badala ya Allaah)) [At-Tawbah: 31]


Matendo Yanayotakiwa Kujiepusha Nayo Ambayo Yanayofanyika Katika Sikukuu Hii   
1.     Kuonyeshana bashasha na furaha kama ilivyo katika sikukuu zao nyingine.

2.     Kupeana mawaridi mekundu (Red Roses) ambayo ni alama ya kuelezea mapenzi, 'mapenzi ya kiroho' ya wapagani au 'mapenzi' ya Wakristo. Hivyo inajulikana kuwa ni 'Sikukuu Ya Wapendanao'.

3.     Kupelekeana kadi. Na kadi nyingine zina picha za 'mungu wa mapenzi wa kirumi' ambaye ana mbawa mbili, akiwa amekamata upinde na mshale. Huyu ndio mungu wa mapenzi wa wapagani warumi. Shirk iliyoje hii ndugu Waislamu?

4.     Kubadilishana maneno ya mapenzi na matamanio katika kadi wanazopelekeana, yakiwa katika mfumo wa kimashairi, tenzi na sentensi fupi fupi. Kadi nyingine zina picha za kimzaha na maneno ya kuchekesha, na mara nyingi zina maneno ya kusema 'Kuwa Valentine wangu'. Hii inaashiria maana ya kikiristo ya sikukuu hii baada ya kuwa asili yake ni kutokana na fikra za upagani.

5.     Katika nchi nyingi za kimagharibi, hufanyika sherehe siku hiyo ambayo kunakuweko kuchanganyika wanaume na wanawake, kuimba, na kucheza dansi. Na wengi wanapelekeana zawadi kama mawaridi, maboksi ya chokoleti kwa wake zao, marafiki na wanaowapenda.

Kutokana na maelezo yote hayo ya chanzo cha sikukuu hii, tunaona kwamba siku hiyo haina uhusiano wowote katika Uislamu, bali yana uhusiano na washirikina mapagani, hata wakristo katika dini yao nao pia ni uzushi, sasa itakuwaje sisi Waislamu tuwaigize kusherehekea? 

Basi ndugu Waislamu tutambue kuwa jambo hili ni ovu mno, haimpasi Muislamu kuharibu 'Aqiydah (iymaan) yake kwani kuna hatari kubwa kushiriki katika sherehe hii nayo ni kuingia katika kumshirikisha Allaah سبحانه وتعالى, na kama tunavyojua kuwa Allaah سبحانه وتعالى Hamsamehe mtu anayefanya shirki pindi akifariki bila ya kutubu kama ilivyo katika aya ifuatayo: 
 ((إِنَّ اللّهَ لاَ يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَلِكَ لِمَن يَشَاء وَمَن يُشْرِكْ بِاللّهِ فَقَدِ افْتَرَى إِثْمًا عَظِيمًا))
((Hakika Allaah Haghufuri kushirikishwa; lakini Anaghufuria yasiyokuwa hayo kwa Amtakae.  Na yeyote atakayemshirikisha Allaah basi kwa yakini amebuni dhambi kuu)) [An-Nisaa: 48]

Hivyo ni kuharamishwa na Pepo na kupata makazi ya moto, tunajikinga na Allaah kwa hayo.

((إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللّهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللّهُ عَلَيهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَار))
((Hakika mwenye kumshirikisha Allaah bila shaka Allaah Atamharamishia Jannah, na makazi yake yatakuwa ni motoni. Na madhalimu hawatopata yeyote mwenye kunusuru)) [Al-Maaidah: 72]

Tunamuomba Allaah سبحانه وتعالى Atuepushe na kila aina ya shirk na Atuoneshe yaliyo ya haki tuyafuate, na yaliyo ya batili tujiepushe nayo na Atuajaalie ni miongoni mwa wale wanaosikiliza kauli (nyingi) wakafuata zile zilizo njema. Aamiyn


إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ - Tawassul Za Shirki Kufru Na Bid’ah - Kutawassal Kwa 'Ahlul-Badr' Watu wa Badr

Baadhi ya watu hutawassal kwa uradi unaojulikana katika jamii kama "albadiri" au "halalbadri" kama wanavyotamka watu wengi wa kawaida.
Jina lenyewe la tawassul hiyo laonesha wazi jinsi gani watu hawakufahamu maana yake halisi kama ilivyokusudiwa katika lugha ya Kiarabu kwamba maana yake ni: ‘Ahlul-Badr’ (Watu wa Badr). 
Hao "Ahlul-Badr" ni Maswahaba waliopigana jihaad katika vita vya Badr Na Badr ni jina la mji ulio kiasi cha kilomita mia na khamsini mbali na mji wa Madiynah ambako Waislamu walipopigana vita vya kwanza na washirikina wa Makkah. Vita hivyo viliongozwa na  Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Baadhi ya mapokezi yanaeleza kuwa walikuwa Waislamu mia tatu na kumi na tatu au kumi na nne na riwaya zingine zinasema kuwa walikuwa mia tatu na kumi na saba.

Hadiyth Ya Wiki

Hadiyth Arubaini: Imaam An-Nawawiy: 07 - Dini Ni Nasiha

Hadiyth Ya 7
الدِّينُ النَّصِيحَةُ
Dini Ni Nasiha
عن أبي رُقَيَّةَ تَمِيمِ بنِ أوْسٍ الدَّارِيِّ رضي اللهُ عنه: أَنَّ النَّبي صلى الله عليه وسلم قالَ:((الدِّينُ النَّصِيحَةُ)). قُلْنَا: لِمَنْ؟ قالَ: ((للهِ، ولِكِتَابِهِ، ولِرَسُولِهِ، ولِلأَئِمةِ المُسْلِمِينَ، وعامَّتِهِمْ)) رَوَاهُ مُسْلِمٌ    
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Ruqayyah Tamiymiy bin Aws Ad-Daarriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Dini ni nasiha.” Tukauliza: Kwa nani? Akasema: “Kwa Allaah na Kitabu Chake, na Rasuli Wake, na kwa viongozi wa Waislamu na watu wa kawaida.” [Muslim]