Saturday 11 April 2015

Nani Aliyepanga Surah, Aayah Na Nani Aliyetoa Majina ya Surah?

SWALI:
Swali La Kwanza: 
Asslaam aleykum,
Ni nani aliezipanga sura za Qur-an katika mpango tunaouona sasa. Ni kwa nini na kuna hikma gani. Ikiwa Suratul Baqra imeteremshwa Madina kwa nini iwe ya pili katika msahafu na isiwe ya 86, kwani za mwanzo zilianza kuteremshwa Makkah?
Swali La Pili:
Shekh, naomba tafadhali maelezo nani aliyetoa majina ya sura za qurani?  Vipi zimepangwa aya ikiwa Qurani imeteremshwa kidogo kidogo kuanzia iqra hadi aya za mwisho kabla kufa Mtume maana naona imeanza Alhamdu na kumalizikia Qul-audhu. 
 
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu upangaji wa surah za Qur-aan. Ni jambo linaloeleweka kuwa hakuna jambo lolote la Uislamu isipokuwa lina hekima kubwa ni sawa tunazijua hizo hekima au la.
 
Mpangilio wa Qur-aan na majina yake yamepangwa na Yeye Mwenyewe Allaah Mwenye hekima na busara kubwa. Tufahamu kuwa Qur-aan yote ilikuwa imehifadhiwa na Allaah Aliyetukuka katika sehemu inayoitwa Lawhul Mahfuudh na kisha kuteremshwa yote usiku wa al-Qadr katika mwezi wa Ramadhaan hadi wingu wa duniani. Kutoka hapo Jibriyl ('Alayhis Salaam) akawa ni mwenye kupatiwa amri na Aliyetukuka kumteremshia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'Alayhi wa aalihi wa sallam) kidogo kidogo kwa miaka 23 kulingana na mahitajio.
 
Kila ilipokuwa inateremshwa Surah au baadhi ya Aayah Jibriyl ('Alayhis Salaam) kwa maagizo kutoka kwa Allaah Aliyetukuka alikuwa akimuamuru Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi wa aalihi wa sallam) aiweke mahali kadhaa na jina la Surah liwe kadhaa. Baada ya kuhama Madiynah, Jibriyl alikuwa akija kila Ramadhaan kumsikiliza Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi wa aalihi wa sallam) kisomo cha Qur-aan. Na ule mwaka aliokufa, Jibriyl alikuja mara mbili na mara ya mwisho Zayd bin Thaabit (Radhiya Allaahu 'anhu) alikuwepo.
Hivyo, alivyoaga dunia (Swalla Allaahu 'Alayhi wa aalihi wa sallam), Maswahaba (Radhiya Allaahu 'anhum) waliandika Qur-aan kama walivyofundishwa na kuagiziwa na Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi wa aalihi wa sallam). Hata wale waandishi wa Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi wa aalihi wa sallam) walikuwa wakipatiwa maagizo hayo.
Ama kuhusu Suratul Baqarah kuwa ni ya 86 si kweli na huenda kuwa ndugu yetu akawa amekosea katika ubinaadamu wake. Na hilo si la ajabu. Hakika ni kuwa Suratul Baqarah ni Surah ya 87 kuteremshwa na ya kwanza kuteremka Madiynah. Surah ya mwisho kuteremshwa Makkah ilikuwa ni ya 86 nayo ni Suratul Mutwaffifiyn (83).
 
Na Allaah Anajua zaidi
 
Pesa Anazopewa Za Ukimbizi Zinafaa Ajenge Msikiti Au Atoe Sadaka Kwa Waislamu?

SWALI:
 
Asalam aleykum warahmatulahi, mimi nauliza je inaswihi mtu kudanganya yeye ni mkimbizi kutoka nchi zenye vita hali ya kuwa si kweli na akapewa mahitaji yote kama kweli yeye ni mkimbizi nachotaka kujua ni kwamba akipewa hizo hela kwa matumizi yake ya chakula na mahitaji mengine itaswihi au itakuwa hela ni ya haramu kwa sababu amedanganya pia akitoa kiasi hicho cha fedha akajengea msikiti au akatoa sadaka kwa Waislamu wengine itaswihi?
 
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu udanganyifu wa ukimbizi. Hakika hili leo limekuwa ni tatizo kubwa sana. Mara nyingi huwa tunafanya jambo bila kutizama hatima yake. Wapo wengi waliodanganya kuhusu suala hilo mpaka wakawa ni wenye kubadilisha majina ili wapate wasiyokuwa na haki nayo kuyapata.
 
Allaah Aliyetukuka Anasema:
Enyi Mlioamini! Mcheni Allaah na kuweni pamoja na wakweli” (9: 119).
Hapa tunaamriwa tuwe na wakweli kumaanisha kuwa nasi pia tunafaa tujipambe na tabia ya ukweli katika kila hali. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anatuhimiza kusema ukweli na Muumini hasemi uongo. Anatueleza (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa Muumini anaweza kuwa muoga, bakhili lakini hawezi kuwa muongo hasa kwa kupata kisichokuwa haki yake. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Anayetudanganya si katika sisi (Waislamu)” (Muslim).
 
Hivyo, huko ni kama kuiba kutoka kwa serikali. Inatakiwa ufanye juhudi upate kazi ya halali ili uweze kujikimu kimaisha na kujenga Msikiti na kutoa sadaka kwa pesa zako na sio pesa za wizi ambazo unazipata kwa ulaghai na hila.
Misikiti haijengwi ila na pesa za halali hata Waarabu wakati wa ujahiliya kabla ya kutumilizwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) walijua hilo. Walipotaka kuijenga Ka‘bah baada kuvunjika kwa mvua kubwa walitoa masharti kuwa isiingie pesa ya haramu katika hilo.
 
Na Allaah Anajua zaidi

Kuna Dalili Yoyote Katika Qur-aan au Sunnah Kuhusu Global Warming?

SWALI
Assalaam aleykum.
Baada ya salam naomba kuuliza kuwa “Global warming” imetajwa katika Qur-an tukufu au japo katika hadithi za Mtume Salla Llaahu alayh wa sallam? Nahisi ni moja kati ya dalili za kiama, je ni kweli?
Natanguliza shukrani zangu, jazaakumullaahu khair.

JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu Global warming. Global warming ni ile hali ya dunia kupata joto na uharara wa juu zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali. Sababu kubwa ni matumizi makubwa ya vifaa vya petroli, ongezeko la viwanda ambavyo vinajaza uchafu wa moshi angani na matumizi ya magari na ongezeko lake. Uchafu unaotokana na vifaa hivyo na vinginevyo vinasababisha kulika lile tabaka la Ozoni (Ozone layer – O3). Na kwa sababu hiyo ulimwengu leo unapata uharara mwingi zaidi kuliko awali kwani tabaka ambalo lilikuwa linachuja miale ya jua haitekelezi jambo hilo kwa njia nzuri kwa kulika tabaka hilo.

Allaah Aliyetukuka Anatueleza:

Je! Hawakuona kwamba Tunaifikia ardhi Tukiipunguza nchani mwake? Na Allaah huhukumu, na hapana wa kupinga hukumu yake, naye ni Mwepesi wa kuhisabu” (13: 41).
Na pia,

Bali tuliwastarehesha hawa na baba zao mpaka umri ukawa mrefu kwao. Je, hawaoni ya kwamba Sisi tunaifikia ardhi tukiipunguza ncha zake? Basi je! Hao ni wenye kushinda?” (21: 44).

Aayah hizo mbili tulizonukuu hapo juu ni dalili ya global warming. Na kwa ajili hiyo ndio kukaribia Qiyaama.

Na Allaah Anajua zaidi

Vipi Aswali Tarawiyh Akiwa Safarini?

SWALI:
Assalam alaykum warahmatullah,baada ya salam ya kheri na baraka,nilikua naomba kufaham namna ya kuswali taraweh nikiwa safarini,nawatakieni wepesi katika kazi zenu,Allah awalipe pepo,amin

JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Muislamu anapokuwa safarini ameruhusiwa kupunguza Swalah zake za fardhi, kwa hiyo hata Swalah za Sunnah anaweza kuziacha. Yote inategemea na hali yake ilivyo huko safarini. Ikiwa unahisi kuwa huwezi kuswali basi ni ruhusa kwako, ama ikiwa unao uwezo wa kuswali basi ni vyema kuzitekeleza ili upate fadhila na thawabu zake.

Na Allaah Anajua zaidi

Anajitegeme Mwenyewe, Anachangia Katika Futari, Je Anawajibika Kutoa Zakaatul-Fitwr?

SWALI:
salam alaykum.
Swali langu ni kwamba. Mimi nataka kutoa zaka ni msichana ninae jitegemea lakini nimekua nafturu kwa ndugu tofauti mwezi mzima. Na pia huko ninako enda kufuturu nachanigia kitu katika ftar. Je zakaah yangu niitoe vipi?
Waaleykum saam.

JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Kufuturu kwa watu au kuchangia futari haihusiani na hukmu ya kutoa Zakaatul-Fitwr kwani hikma ya kutoa Zakaatul-Fitwr ni kuitwaharisha Swawm ya mwenye kufunga kutokana na maneno maovu, machafu ambayo ameyatamka. Vile vile ili kuwapatia masikini nao chakula kizuri siku ya 'Iyd nao wafurahi. Dalili ifuatayo ni uthibitisho:     
عَنْ ابْنِ عَبَّاس ٍقَالَ فَرَضَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ زَكَاةَ الْفِطْرِ طُهْرَةً لِلصَّائِمِ مِنْ اللَّغْوِ وَالرَّفَثِ وَطُعْمَةً لِلْمَسَاكِينِ مَنْ أَدَّاهَا قَبْلَ الصَّلاةِ فَهِيَ زَكَاةٌ مَقْبُولَةٌ وَمَنْ أَدَّاهَا بَعْدَ الصَّلاةِ فَهِيَ صَدَقَةٌ مِنْ الصَّدَقَاتِ . " رواه أبو داود  بِإِسْنَادٍ حَسَنٍ .

Kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhuma) ambaye amesema: "Mtume amefaridhisha Zakaatul-Fitwr kuwa ni twahara ya mwenye kufunga kutokana na maneno ya upuuzi na machafu, na kulisha masikini. Atakayeitoa kabla ya Swalah basi hiyo ni Zakaah iliyotakabaliwa, na atakayeitoa baada ya Swalah basi hiyo ni Sadaqah miongoni mwa Sadaqah" [Abu Daawuud kwa isnaad iliyo nzuri].

Kwa hiyo  ni waajib wako kuota Zakaatul-Fitwr maadam una uwezo na unajitegemea mwenyewe.

Kwa maelezo zaidi bonyeza kiungo kifuatacho upate kusoma mas-ala  mbalimbali yanayohusu Zakaatul-Fitwr:

Na Allaah Anajua zaidi
 
Mwenye Ugongwa Wa Ukimwi Anaweza Kufunga Ramadhaan?

SWALI

Assalaam aleykum wa rahmatullahi wabaraakat.Nduzanguni waislamu,shukrani sana kwenu kwa kuweza kuwasiliana nanyi na imetupa wingi wa elimu ambazo hatukuwa nazo.
swali langu ni.
-Kuna ndungu wetu ambaye anaugua na huu ugonjwa wa ukimwi,alhamdulillah ameweza kupata dawa.je, anaweza kufunga Ramadhani ama yumo katika wangonjwa wasie funga kwa ajili ya afya zao?Ramadhaan Karim

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Swawm katika hali ya ugonjwa inategemea  uwezo wa mtu. Ikiwa ataweza kufunga bila ya taklifu yoyote ya siha yake basi imewajibika kwake kufunga. Na ikiwa hawezi kufunga kwa vile italeta madhara katika siha yake basi atakuwa miongoni mwa waliopewa udhuru wa kutokufunga kutokana na kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) :

(Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine))  [Al-Baqarah:185]

Ni Rahma ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwamba Hamkalifishi mtu na jambo asiloliweza:

((Allaah haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo. Faida ya iliyoyachuma ni yake, na hasara ya iliyoyachuma ni juu yake pia)) [2: 286].

Atakalopasa kufanya ni  ima alipe siku za mbele ikiwa pia atakuwa na uwezo wa kufunga bila ya kuathiri siha yake au kumfanyia taklifu, ikishindikana itabidi alipe kafara kwa kulisha masikini mmoja kwa kila siku moja ya Swawm. Na Anaweza kulipa ima kulisha maskini 30 siku mbali mbali au kulisha wote kwa pamoja kwa maana wote 30 kwa siku moja. Vyovyote atakavyofanya inajuzu kwani Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ‘anhu) alifanya hivyo alipokuwa na umri mkubwa na aliposhindwa kufunga alilisha masikini siku ya mwisho ya Ramadhaan.

Tunamuombea Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ampe shifaaun ya haraka.

Na Allah Anajua zaidi

Wasiwasi Wa Shaytwaan Unamfanya Afikirie Mambo Ya Kufru, Afanyeje?

SWALI:
ASALAMU ALAYKUM.

Swali Langu hili, kwa kawaida huwa ninaposoma, mambo ya dini kwa mfano makala ua ninapo sikiliza mawaidha au kusoma Qur-ani hutokezea ndani ya nafsi yangu kusema jambo hili ni uongo yaani huwa sitamki mdomoni mwangu moyo tu hunipiga paa nakusema iwe Mtume Swala lwahu Alayhi Wasalamu amesema hivi haiwezekani. Halafu hushtuka na kusema ASTAHAFIRULLAH. Naomba jawabu ndugu zanguni Waislamu.  NIFANYE NINI MIE JAMANI? Kwa sababu hujihisi ibada zangu zote zinaharibika

JIBU:
 
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kutiwa katika wasiwasi. Hakika wasiwasi huu unaingizwa bila ya kuwa na haja katika hilo. Hata hivyo, wanadamu huwa wanaingia katika mtego huo kwa sababu moja au nyingine. Wasiwasi huu huingia kwa mwanaadamu, hasa akiwa:
  1. Hakupata malezi mazuri ya Kiislamu.
  2. Hasomi adhkaar zinazotakiwa kusomwa kila siku.
  3. Kusoma Qur-aan bila kuelewa.
  4. Marafiki wabaya ambao wanamuamrisha maovu na mabaya.
  5. Kufuata matamanio yake mwenyewe.
Kitu ambacho unatakiwa kufanya ni kama ifuatavyo:
  1. Kujiweka katika kundi la watu wema wenye kufanya ‘Ibaadah inavyotakiwa.
  2. Kusoma Qur-aan kila wakati pamoja na kujua maana yake na kufanya juhudi ya kufuata yaliyo ndani yake.
  3. Kusoma adhkaar za asubuhi na jioni. Ingia katika kiungo kifuatacho: 

Na du’aa zote nyinginezo unazohitaji katika hali yako utazipata katika kitabu kifuatacho:

  1. Kusoma asubuhi, jioni na hata wakati wa kulala Suratul Iklaasw na Mu'awadhdhatayn (Qul A’udhu birabbil Falaq, na Qul A’uudhu birabbin Naas) mara tatu tatu.
  2. Kusema A'udhu Billaahi unapoingia wasiwasi.
  3. Kuzidisha ‘Ibaadah kama ya Swalah na funga.
Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Akuondoshe katika wasiwasi ulionao na akuweke katika hali ya Imani ya daima na Akuongoze wewe na sisi katika njia Yake nyoofu.

Na Allaah Anajua zaidi

Ishara Za Mtoto Wa Kiume Kubaleghe Na Nini Jukumu La Mzazi Kwa Hali Hiyo Ya Mwanae?

SWALI:
Ningependa kuuliza suala moja
Mimi nina mtoto wa kiume lakini bado hajabaleigh natakuka kujuwa kuna inshara ngani akibaeigh na vipi mtu utajuwa kama baleigh na vipi umafahamishe ili ajuwa kuwa keshakuwa mkubwa aanze kusali na kufunga naona kusaidiwa.
Muislamu mwenzenu

JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa muulizaji. Ishara ya kijana wa kiume kubaleghe ni kama zifuatazo:
  • Kumea nywele za kwapani.
  • Kubadilika kwa sauti yake na kuwa nene na nzito.
  • Kuota kwa mara ya kwanza na kutokwa na maji (manii).
  • Kufikia miaka kumi na tano (15).
Wazazi hawafai kungoja mpaka mtoto abaleghe ndio waanze kumwambia kuhusu Swalah na Funga. Bali malezi yanatakiwa yawe mazuri kuanzia anapoanza kujua na kufahamu mambo, kutofautisha baina ya baya na zuri, ukweli na uongo.
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anatuelekeza kuhusu malezi ya kiibada ya watoto wetu pale alipotufahamisha:
Waamrisheni watoto wenu kuswali wakiwa na miaka saba na wapigeni kwa kutoswali wakiwa na miaka kumi” (Abu Daawuud).
Na kufunga nayo ni hivyo hivyo wawe ni wenye kufundishwa na kuzowezeshwa kuanzia mtoto akiwa na miaka hiyo saba na Ibaadah nyingine ni hivyo hivyo.

Taratibu Za Ruqyah Na Yapasayo Kufanywa Kabla Ya Kusoma Ruqyah

SWALI:
Nimepitia website yenu nzuri mashAllaah, Mungu awazidishie na kazi hiyo nzuri. Tafadhali kuhusu suala la Rukyah, tafadhali nitumie utaratibu kamili, yaani ayas na sura za rukyah zote na utaribu wa kuzisoma hizo sura. Pia nielimishe vipi nitajiyarisha ninapo jisomea rukyah, yaani kuhusu udhu, mavazi na kadhalika. Shukran

JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola   wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako hilo kuhusu Ruqyah. Katika mas-ala ya Ruqyah zipo Aayah za kusomwa na mtu mwenyewe za kutaka kinga kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) na zipo zile za kumsomea mtu aliyekumbwa na jini au kufanyiwa sihri.
Ama njia ya kujikinga mwenyewe ni kuwa uwe unasoma Aayah zifuatazo asubuhi na jioni. Nazo ni kama zifuatazo:
 
  1. Al-Faatihah (Surah ya kwanza).
  2. Al-Baqarah (Aayah nne za mwanzo, Ayatul Kursiy na Aayah mbili baada yake na Aayah tatu za mwisho).
  3. Aal-‘Imraan (3: 1 – 2).
  4. Suratut Tawbah (9: 129 mara saba).
  5. Al-Israa’ (17: 110 – 111).
  6. Al-Mu’minuun (23: 115 – 118).
  7. Al-Hashr (59: 22 – 24).
  8. Al-Kaafiruun (109).
  9. Al-Ikhlaasw, al-Falaq na an-Naas (mara tatu tatu).
 
Ama kipengele cha pili cha kumsomea mwengine inafaa usome Aayah zifuatazo:
Mwanzo unaanza na A’udhu Billaahi minash Shaytwaanir Rajiym.
  1. Al-Faatihah (Surah ya kwanza).
  2. Al-Baqarah (ayah 1 – 5, 102, 163 – 164, 255, 285 - 286).
  3. Aal-‘Imraan (3: 18 – 19).
  4. Suratut al-A‘raf (7: 54 – 56, 117 - 122).
  5. Yunus (10: 81 – 82).
  6. Twaaha (20: 69).
  7. Al-Hajj (22: 19 – 22).
  8. Al-Mu’minuun (23: 115 – 118).
  9. An-Naml (27: 30 – 31).
  10.  Asw-Swaaffaat (37: 1 – 10).
  11.  Ad-Dukhkhaan (44: 43 – 48).
  12.  Al-Ahqaaf (46: 29 – 32).
  13.  Al-Fath (48: 29).
  14.  Ar-Rahmaan (55: 33 – 36).
  15.  Al-Hashr (59: 21- 24).
  16.  Al-Jinn (72: 1 – 9,
  17.  Al-Buruuj (85).
  18.  Zilzalah (99).
  19.  Al-Humazah (104).
  20.  Al-Ikhlaasw, al-Falaq na an-Naas.
Ama unapokuwa unasoma unafaa uwe twahara (nguo na mwili) na umejisitiri kwa kujifunika vizuri sehemu zipasazo kusitiriwa na pia usome kwa unyenyekvu.