Wednesday 29 July 2015

Mawaridi Kumi Ya Kupata Mapenzi Ya Allaah

 سبحانه وتعالى Na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم


 
 
 
WARIDI LA: 1
 
Omba Tawbah sana kwa Allaah سبحانه وتعالى   Na  jiweke katika Twaharah daima
}}...إِنَّ اللّهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ{{
{{…… Hakika Allaah huwapenda wanao tubu na huwapenda wanao jisafisha}}
Al-Baqarah:222 
 

WARIDI LA:  2 
 Mfuate Mtume صلى الله عليهو آله  وسلم   kwa kutimiza Sunnah zake na fuata tabia na mwendo wake  ili  uthibitishe  mapenzi yako kwa Allaah سبحانه وتعالى
 
}}قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللّهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللّهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَاللّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ    {{
{{Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Allaah basi nifuateni mimi, Allaah Atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu. Na Allaah ni Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu}}
Al-Imraan:31
 
Vile vile  fuata  Sunnah za Makhalifa Wanne waliongoka, Abubakar, 'Umar, 'Uthmaan na 'Aliy
عنهما  رضي الله

WARIDI LA : 3
Timiza Fardhi yako kwanza vizuri, kisha ongeza na Sunnah zaidi za Swalah, kutoa sadaqa, kwenda Umra, kufanya kila aina ya wema kwa wazazi na Waislamu wenzako
((‏عن ‏ ‏أبي هريرة رضي الله عنه ‏ ‏قال ‏
‏قال رسول الله ‏ ‏صلى الله عليه وآله وسلم ‏ ‏إن الله قال ‏ ‏من عادى لي وليا فقد ‏‏ آذنته ‏‏ بالحرب وما تقرب إلي عبدي بشيء أحب إلي مما افترضت عليه وما يزال عبدي يتقرب إلي بالنوافل حتى أحبه فإذا أحببته كنت سمعه الذي يسمع به وبصره الذي يبصر به ويده التي يبطش بها ورجله التي يمشي بها وإن سألني لأعطينه ولئن استعاذني لأعيذنه وما ترددت عن شيء أنا فاعله ترددي عن نفس المؤمن يكره الموت وأنا أكره مساءته))
 
((Inatoka kwa Abu Hurayrah رضي الله عنه ambaye alisema: Mtume ‏صلى الله عليه وآله وسلم  amesema: Hakika Allaah Amesema: Yeyote yule afanyae uadui kwa walii (rafiki) wangu nitatangaza vita dhidi yake.  Mja wangu hanikaribii na kitu chochote ninachokipenda kama amali nilizomuwajibisha, na mja wangu huzidi kunikaribia kwa amali njema za Sunnah ili nimpende. Ninapompenda huwa (Mimi ni) masikio yake anayosikilizia, macho yake anayoonea, mikono yake anayopigania, miguu yake anayokwendea, lau angeniomba kitu bila shaka ningempa, lau angeniomba himaya bila shaka ningempa, sisiti juu ya kitu chochote kama ninavyosita  (kuichukua) roho ya mja wangu muumin.  Anachukia mauti nami nachukia kumuumiza.))
 
(Al-Bukhariy)
 

WARIDI LA:  4
 
Fanya mema mengi Allaah Aridhike na wewe na wewe uridhike na uwe tayari kuondoka duniani hali ya kupenda kwenda kuonana naye.
 
((عن ‏ ‏أبي بردة ‏ ‏عن ‏ ‏أبي موسى ‏
‏عن النبي ‏ ‏صلى الله عليه وآله وسلم ‏ ‏قال ‏ ‏من أحب لقاء الله أحب الله لقاءه ومن كره لقاء الله كره الله لقاءه))
((Kutoka kwa Abu Musa kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم  kasema:  Atakayependa kuonana na Allaah basi Allaah Naye Atapenda kuonana naye, na atakayechukia kuonana na Allaah, basi Naye Allaah Atachukia kuonana naye))
 (Muslim)
 

WARDI LA:   5
 
Ukipendwa na Allaah سبحانه وتعالى basi utapendwa na Jibriyl na wakaazi wa mbinguni na watu wa duniani pia
 
((عن ‏ ‏أبي هريرة ‏
‏عن النبي ‏ ‏صلى الله عليه وآله وسلم ‏ ‏قال ‏ ‏إذا أحب الله العبد نادى ‏ ‏جبريل ‏ ‏إن الله يحب فلانا فأحببه فيحبه ‏ ‏جبريل ‏ ‏فينادي ‏ ‏جبريل ‏ ‏في أهل السماء إن الله يحب فلانا فأحبوه فيحبه أهل السماء ثم يوضع له القبول في الأرض))
((Imetoka kwa Abu Hurayrah kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم  amesema: AllaahAkimpenda mja Wake) Humuita Jibriyl na Husema: Nampenda fulani kwa hivyo (nawe) mpende.  Kisha Jibriyl humpenda.  Kisha Jibriyl huwaita wakaazi  wa mbinguni: Hakika Allaah Anampenda fulani basi na nyinyi mpendeni.  Basi hupendwa na wakaazi  wa mbinguni, kisha kupendwa kwake hujengwa duniani))
(Al-Bukhariy)
 

WARIDI LA:  6
 
Fanya wema, toa sadaka, jizuie na ghadhabu, wasamehe wenzako wanapokukosea  upate daraja ya Muhsiniyn na upendwe na Allaah سبحانه وتعالى    
}}الَّذِينَ يُنفِقُونَ فِي السَّرَّاء وَالضَّرَّاء وَالْكَاظِمِينَ الْغَيْظَ وَالْعَافِينَ عَنِ النَّاسِ وَاللّهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ{{
{{Ambao hutoa wanapo kuwa na wasaa na wanapo kuwa na dhiki, na wanajizuia ghadhabu, na wasamehevu kwa watu; na Allaah huwapenda wafanyao wema}}
 
(Al-'Imraan 134)
 

WARDI LA: 7
 
 Penda kusoma Suratul-Ikhlaas upate mapenzi ya Allaah سبحانه وتعالى 
 
((عن ‏ ‏أنس ‏أن رجلا قال والله إني لأحب هذه السورة ‏ ‏قل هو الله أحد ‏ ‏فقال رسول الله ‏صلى الله عليه وآله وسلم ‏‏ حبك إياها أدخلك الجنة
الترمذي وصححه الألباني
 
Imetoka kwa Anas ambaye alisema: Mtu mmoja alimwambia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم "Mimi naipenda sura hii  قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَد akasema Mtume صلى الله عليه وآله وسلم  “Mapenzi yako kwayo yatakuingiza peponi”
 
At-Tirmidhiy na  Imesahihishwa na Albaaniy
(Hapa tufahamu kuwa Suratu Ikhlaas ni sehemu ya Qur’an, na ni vizuri kuisoma Qur’an yote na usitosheke na Surah moja au baadhi na ukaacha zingine kwa kuichukua hadiyth hiyo peke yake bila kutazama na zingine).
 

WARIDI LA: 8
  Mpende Allaah سبحانه وتعالى  , Mtume صلى الله عليه وآله وسلم  na Makhalifa wake wote Wanne Abubakar, 'Umar, 'Uthmaan na ‘Aliy رضي الله عنهما  upate kuwa nao.
 
((عن ‏ ‏أنس ‏ ‏رضي الله عنه ‏
‏أن رجلا سأل النبي ‏ ‏صلى الله عليه وآله وسلم ‏ ‏عن الساعة فقال متى الساعة قال وماذا أعددت لها قال لا شيء إلا أني أحب الله ورسوله ‏ ‏صلى الله عليه وسلم ‏ ‏فقال ‏ ‏أنت مع من أحببت قال ‏ ‏أنس ‏ ‏فما فرحنا بشيء فرحنا بقول النبي ‏ ‏صلى الله عليه وسلم ‏ ‏أنت مع من أحببت
‏قال ‏ ‏أنس ‏ ‏فأنا أحب النبي ‏ ‏صلى الله عليه وسلم ‏ ‏وأبا بكر ‏ ‏وعمر ‏ ‏وأرجو أن أكون معهم بحبي إياهم وإن لم أعمل بمثل))
((Imetoka kwa Anas ‏رضي الله عنه ambaye alisema:
Alikuja mtu mmoja akamuuliza Mtume صلى الله عليه وآله وسلم  kuhusu saa (Qiyaamah) akauliza: Lini Qiyaamah? Akamuulize je, Kwani umekitayarishia nini?  Akasema: sikutayarisha kitu isipokuwa mimi nampenda Allaah na Mtume wake صلى الله عليه وسلم
Akasema: basi wewe uko pamoja na unayempenda.  Anas akasema: Hatukufurahiwa na jambo kama tulivyofurahiwa na usemi huu wa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم "wewe uko pamoja na unayempenda" Akasema Anas: "Basi mimi nampenda Mtume صلى الله عليه وآله وسلم na Abu Bakr, na 'Umar na natumai niwe pamoja nao kwa mapenzi yangu juu yao japo kama sikufanya kama walivyofanya wao"))
 
(Al Bukhariy)
 

WARIDI LA: 9
 
Kuwa na Tawakkul katika mambo yako yote, umuweke Allaah سبحانه وتعالى   mbele ya kila jambo, na unapotaka kufanya jambo, kwanza tafuta ushauri kwa watu wema, kisha swali istikhaara, kisha Tawakkal kwa Allaah سبحانه وتعالى   
 
}}شَاوِرْهُمْ فِي الأَمْرِ فَإِذَا عَزَمْتَ فَتَوَكَّلْ عَلَى اللّهِ إِنَّ اللّهَ يُحِبُّ الْمُتَوَكِّلِينَ{{
 
{{ Shauriana nao katika mambo. Na ukisha kata shauri basi mtegemee Allaah. Hakika Allaah huwapenda wanaomtegemea}}
 
Al-Imraan: 159
 

WARIDI LA: 10
 
Kuwa na tabia njema na watu kama, upole, ukarimu, heshima, ucheshi, adabu nzuri upate kuwa karibu na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم siku ya Qiyaamah.
  (( عن أبي جده ‏أنه سمع النبي ‏ ‏صلى الله عليه وآله وسلم ‏ ‏يقول ‏ ‏ألا أخبركم بأحبكم إلي وأقربكم مني مجلسا يوم القيامة فسكت القوم فأعادها مرتين ‏ ‏أو ثلاثا ‏ ‏قال القوم نعم يا رسول الله قال أحسنكم خلقا))
(احمد) 
((Imetoka kwa Abi Jidduh   kwamba amemsikia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akisema:  Je, nikujulisheni nani kipenzi kwangu na nani atakayekuwa karibu yangu siku ya Qiyaama?  Wakanyamaza watu wote, akarudia mara mbili au tatu, wakasema watu: "ndio ewe Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema: mwenye tabia njema katika nyinyi))
(Ahmad)
 

No comments: