Wednesday 12 October 2016

Hiswnul Muslim - Du'aa Na Adhkaar Mbalimbali Kutoka Katika Qur-aan, Sunnah Na Athar


بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمن الرَّحيم
Kwa Jina La Allaah Mwingi Wa Rehema (Duniani) Mwenye Kurehemu (Akhera)

UTANGULIZI
Hakika sifa njema zote ni za Allaah, tunamsifu, tunamuomba msaada na tunamuomba maghfirah, tunamuomba Atuhifadhi na shari za nafsi zetu, na maovu ya matendo yetu. Anayemuongoza Allaah hapana wa kumpoteza, na Anayempoteza, hapana wa wa kumuongoza.  Nakiri kwamba, hapana apasaye kuabudiwa ila Allaah, hali ya kuwa peke Yake, hana mshirika, na ninakiri kwamba Muhammad ni mja Wake na ni Mtume Wake. Allaah Amrehemu na Awarehemu jamaa zake na Maswahaba zake na wanaowafuata hao kwa wema mpaka siku ya malipo na Amsalimishe kwa amani nyingi.
Baada ya yaliyotangulia huu ni ufupi (Mukhtasar) wa kitabu changu  kiitwacho “HISWN AL-MUSLIM MIN ADHKAAR AL-KITAAB WA SUNNAH
Ninamuomba Allaah kwa majina Yake mazuri, na sifa Zake zilizo juu, Ajaaliye kazi hii kuwa, imesafika  lengo lake, kwa kutaka radhi zake Allaah Mtukufu, na Aninufaishe kwa hayo katika uhai wangu huu, na baada ya kufa, na Amnufaishe atakayekisoma, kukichapisha, au aliyekuwa ni sababu ya kukitawanya, hakika  Yeye  Allaah Ndiye  Muweza.
Allaah Amrehemu Mtume wetu Muhammad صلى الله عليه وسلم na Aali zake na Maswahaba wake na wanaowafuata hao, kwa wema mpaka siku ya malipo.
                                      






01 Fadhila Za Kumtaja Allaah




 Amesema Allaah سبحانه وتعالى
:{ فَاذْكُرُونِي أَذْكُرْكُمْ وَاشْكُرُواْ لِي وَلاَ تَكْفُرُونِ }
“Nitajeni nami nitawataja, na nishukuruni na wala msinikufuru (Suratul Baqaraha 152)
Na akasema:
 { يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا اللَّهَ ذِكْراً كَثِيراً}
“Enyi mlioamini mtajeni Mwenyezi Mungu sana” (Suratul Ahzaab 41 )
Akasema tena:
 { وَالذَّاكِرِينَ اللَّهَ كَثِيراً وَالذَّاكِرَاتِ أَعَدَّ اللَّهُ لَهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْراً عَظِيماً}
“Nawasifu wanaume wanaomtaja Mwenyezi Mungu sana na nawasifu wanawake wanaomtaja, Mwenyezi Mungu   kawaandalia wote hao msamaha na malipo makubwa” (Suratul Ahzaab 35 )
Akasema tena :
{ وَاذْكُر رَّبَّكَ فِي نَفْسِكَ تَضَرُّعاً وَخِيفَةً وَدُونَ الْجَهْرِ مِنَ الْقَوْلِ بِالْغُدُوِّ وَالآصَالِ وَلاَ تَكُن مِّنَ الْغَافِلِينَ }
“Mtaje Mola wako  moyoni mwako kwa  unyenyekevu  na kwa uwoga, pasina kudhihirisha sauti, mtaje asubuhi  na jioni, nawala usiwe nikatika wenye kughafilika” (Suratul A’raaf 205)
Mtume صلى الله عليه وسلم amesema :
 }  وقال صلى الله عليه وسلم :" مثل الذي يذكر ربه والذي لا يذكر ربه مثل الحي والميت {
{Mfano wa anaemtaja Mola wake na asiyemtaja ni mfano wa alie hai na maiti }
Na akasema Mtume صلى الله عليه وسلم
وقال صلى الله عليه وسلم :" ألا أنبئكم بخير أعمالكم , وأزكاها عند مليككم، وأرفعها في درجاتكم ، وخير لكم من إنفاق الذهب والورق ، وخير لكم من أن تلقوا عدوكم فتضربوا أعناقهم ويضربوا أعناقكم ؟" قالوا بلى .قال : "ذكر الله تعالى
{Hivi niwaambieni khabari  yamatendo yenu bora, na ambayo ni masafi mno, mbele ya Mola wenu, na ambayo ni yajuu mno katika daraja zenu, na ambayo ni bora kwenu kuliko kutoa  dhahabu na fedha, na ambayo ni bora kuliko  kukutana  na adui zenu, mkawapiga shingo zao, nao wakakupigeni shingo zenu?))  Wakasema masahaba; Ndio . Akasema  Mtume صلى الله عليه وسلم  ((Ni kumtaja Mwenyezi Mungu))
وقال صلى الله عليه وسلم :" يقول الله تعالى : أنا عند ظن عبدي بي ، وأنا معه إذا ذكرني ، فإن ذكرني في نفسه ذكرتهُ في نفسي ، وإن ذكرني في ملأ ذكرته في ملأ خير منهم ،وإن تقرب إلى شبراً تقربت إليه ذراعاً ،وإن تقرب إلي ذراعاً تقربت إليه باعاً ، وإن أتاني يمشي أتيتهُ هرولة "
Amesema Mtume صلى الله عليه وسلم Mwenyezi Mungu  anasema “Mimi niko mbele ya dhana ya mja wangu kwangu, akinitaja moyoni nami ninamtaja moyoni  na akinitaja katika  kundi, nami namtaja  katika kundi bora zaidi ya hilo lake, na akijikurubisha kwangu paa moja, basi mimi najikurubisha kwake kiasi cha dhiraa, na akijikurubisha  kwangu kiasi cha dhiraa, basi mimi nitajikurubisha  kwake kiasi chakuyoosha mkono hadi kati ya kifuwa, na akinijia kwa mwendo mdogo basi nami nitamjia kwa mwendo wa kasi. 
وعن عبد الله بن بسرٍ رضي الله عنهُ أن رجلاً قال : يا رسول الله إن شرائع الإسلام قد كثرت علي فأخبرني بشيءٍ أتشبث به. قال :" لا يزال لسانك رطباً من ذكر الله  
Imepokelewa kutoka kwa Abdalla Bin Busr رضى الله عنه   kwamba mtu mmoja alisema :
“Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ibada za dini zimekuwa nyingi kwangu, basi nieleze kitu  ambacho nitaweza  kudumu nacho.   Mtume صلى الله عليه وسلم  akamwambia : Ulimi wako utaendelea kuwa rutuba  (yaani sio ukavu ) kwakumtaja Mwenyezi Mungu  .
وقال صلى الله عليه وسلم:" من قرأ حرفاً من كتاب الله به حسنة ،والحسنة بعشر أمثالها ، لا أقول : {الم } حرف؛ ولكن : ألف حرف ،ولام حرف ،وميم حرف
Na amesema tena Mtume صلى الله عليه وسلم  “Anaesoma harufu moja katika kitabu cha Mwenyezi Mungu  basi anapata thawabu za jema moja na jema ni kwa mema kumi, sisemi kuwa ‘Alif Laam Miim’ ni harufu moja lakini ni kwamba ‘Alif’ peke yake ni harufu moja, na ‘Laam’ ni harufu , na ‘Miim’ ni harufu”
وعن عقبة بن عامر رضي الله عنه قال : خرج رسول الله صلى الله عليه وسلم ونحن في الصفة فقال :" أيكم يحب أن يغدو كل يوم إلى بطحان أو إلى العقيق فيأتي منه بناقتين كوماوين في غير إثم ولا قطيعة رحم ؟" فقلنا : يا رسول الله نحب ذلك . قال :" أفلا يغدو أحدكم إلى المسجد فيعلم ، أو يقرأ آيتين من كتاب الله عز وجل خير له من ناقتين ، وثلاث خير لهُ من ثلاث ٍ، وأربع خير لهُ من أربع ، ومن أعدادهن من الإبل
Imepokelewa kutoka kwa Uqbah bin Aamir رضى الله عنه   amesema :  ‘Ametoka Mtume wa Mwenyezi Mungu   na sisi tuko sehemu iitwayo Assufah, akasema “Nani kati yenu anapenda aende kila siku sehemu iitwayo But-haan au Aqiq aje na ngamia  wawili walio  nenepa pasi na dhambi wala kukata udugu?”  Wakasema  maswahaba “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu tunapenda hivyo’ akasema Mtume صلى الله عليه وسلم  “Hivi haendi (asubuhi ) mmoja wenu msikitini  akajuwa  au akasoma Aya mbili, za kitabu cha Mwenyezi Mungu?    Hizo aya mbili  ni bora kwake kuliko  kupata ngamia wawili, na endapo atasoma aya tatu zitakuwa  ni bora   kwake  kuliko ngamia watatu, na aya nne ni bora kwake kuliko ngamia wanne, na vilevile zaidi ya hapo.  Aya zozote atakazo zisoma  basi ni bora kwake kuliko hisabu  yake kwa ngamia”
وقال صلى الله عليه وسلم:" من قعد مقعداً لك يذكر الله فيه كانت عليه من الله ترة ومن اضطجع مضجعاً لم يذكر الله فيه كانت عليه من الله ترة
Na Anasema Mtume صلى الله عليه وسلم  “Anaekaa kikao chochote  kile asimtaje Mwenyezi Mungu  katika kikao hicho basi ana dhambi kutoka kwa Mwenyezi Mungu,  na anaelala sehemu yeyote ile kisha asimtaje Mwenyezi Mungu   wakati wakuinuka sehemu hiyo basi ana dhambi kwa Mwenyezi Mungu” 
وقال صلى الله عليه وسلم : " ما جلس قوم مجلساً لم يذكروا الله فيه ، ولم يصلوا على نبيهم إلا كان عليهم ترة ، فإن شاء عذبهم وإن شاء غفر لهم
Amesema Mtume صلى الله عليه وسلم Hapana watu wowote  wale, wanaokaa kikao kisha wasimtaje Mwenyezi Mungu humo, wala wasimswalie Mtume wao  ila  watakuwa wana dhambi. Akipenda Atawaadhibu na Akipenda Atawaghufuria.  
وقال صلى الله عليه وسلم :" ما من قوم يقومون من مجلس لا يذكرون الله فيه إلا قاموا عن مثل جيفة حمار وكان لهم حسرة
Amesema Mtume صلى الله عليه وسلم Hapana watu wowote wale  wanaosimama katika kikao walichokaa, kisha wasimtaje  Mwenyezi Mungu  ila watakuwa wanasimama kama  mzoga wa punda, na watakuja juta kwa kutomtaja Mwenyezi Mungu”
















02 Kuamka Kutoka Usingizini

(1)
  الحَمْـدُ لِلّهِ الّذي أَحْـيانا بَعْـدَ ما أَماتَـنا وَإليه النُّـشور
“Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu  ambae ametupa uhai baada ya kutufisha na ni Kwake tu kufufuliwa “
Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu  “Mwenye kushutuka usingizini usiku akasema
 (2):
ُ لا شَـريكَ له، لهُ المُلـكُ ولهُ الحَمـد، وهوَ على كلّ شيءٍ قدير، سُـبْحانَ اللهِ، والحمْـدُ لله ، ولا إلهَ إلاّ اللهُ
   لا إلهَ إلاّ اللّهُ وَحْـدَه واللهُ أكبَر، وَلا حَولَ وَلا قوّة إلاّ باللّهِ العليّ العظيم, رب اغْفِرْ لي
“Hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu, na hali ya kuwa peke yake hana mshirika, ni Wake ufalme, na ni Zake sifa njema, na Yeye juu ya kila kitu ni muweza, Ametakasika Mwenyezi Mungu  na sifa njema zote ni zake, na hapana Mola apasae  kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu , na Mwenyezi Mungu  ni mkubwa, na hapana uwezo wala nguvu, isipokuwa vyote vinatokana na Mwenyezi Mungu aliyejuu, aliyemtukufu, Ewe Mola (Mwenyezi Mungu) nisamehe :
basi atasamhewa na kama atasimama akaenda kutawadha, akaswali, basi swala yake atakubaliwa :
(3)
الحمدُ للهِ الذي عَافانِي فِي جَسَدي وَرَدّ عَليّ رُْوحِي وَأَذِنَ لِي بِذِكْرِه
“Sifa njema zote ni Zake Mwenyezi Mungu  ambae amenipa uzima wa mwili wangu, na akanirudishia  roho yangu, na akaniruhusu kumtaja”
(4)
) إِنّ فِي خَلْقِ السّمَوَاتِ وَالأرْضِ واخْتِـلافِ اللّيلِ والنّهارِ لآياتٍ لأُولي الألباب (…
(سورة آل عمران 190-200






03 Dua'a Ya Kuvaa Nguo


(5)
الْحَمْدُ للهِ الّذِي كََسَانِي هَذا (الثّوب) وَرَزَقَنِيهِ مِنْ غَـيـْرِ حَولٍ مِنّي وَلا قُوَّة
“Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu  ambae amenivisha nguo hii, na kuniruzuku pasina uwezo kutoka kwangu wala nguvu” 





04 Dua'a Ya Kuvaa Nguo Mpya

(6) 
اللّهُـمَّ لَـكَ الحَـمْـدُ أنْـتَ كَسَـوْتَنيهِ، أََسْأََلُـكَ مِـنْ خَـيرِهِ وَخَـيْرِ مَا صُنِعَ لَـه، وَأَعوذُ بِكَ مِـنْ شَـرِّهِ وَشَـرِّ مـا صُنِعَ لَـهُ.
“Ewe Mwenyezi Mungu , sifa njema ni zako, wewe ndie ulienivisha, nakuomba kheri ya nguo hii, na kheri ya kila ambacho nguo hii imetengenezewa, na najilinda Kwako kutokana na shari yake, na shari ambayo nguo hii imetengenezewa”itaendelea**************


No comments: