Tafsir ya Qruan

Juzuu: 1
الم ذَلِكَ الْكِتَابُ
    سُورَةُ  الْبَقَرَة   
Al-Baqarah:   2
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
  
  الم ﴿١﴾

1. Alif Laam Miym.

ذَٰلِكَ الْكِتَابُ لَا رَيْبَ ۛ فِيهِ ۛ هُدًى لِّلْمُتَّقِينَ ﴿٢﴾

2. Hiki ni Kitabu kisicho na shaka, ndani yake ni Hidaaya kwa  wenye taqwa.

 الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِالْغَيْبِ وَيُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ ﴿٣﴾

3. Ambao huamini ya ghayb na husimamisha Swalaah na katika vile Tulivyowaruzuku hutoa.

 وَالَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ وَبِالْآخِرَةِ هُمْ يُوقِنُونَ ﴿٤﴾

4. Na ambao huamini yaliyoteremshwa kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na yale yaliyoteremshwa kabla yako na ni wenye yakini na Aakhirah.

 أُولَـٰئِكَ عَلَىٰ هُدًى مِّن رَّبِّهِمْ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿٥﴾

5. Hao wako juu ya Hidaaya kutoka kwa Mola wao, na hao ndio wenye kufaulu.

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا سَوَاءٌ عَلَيْهِمْ أَأَنذَرْتَهُمْ أَمْ لَمْ تُنذِرْهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿٦﴾

6. Hakika wale waliokufuru ni sawa kwao, ukiwaonya au usiwaonye wao hawatoamini.

خَتَمَ اللَّـهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ وَعَلَىٰ سَمْعِهِمْ ۖ وَعَلَىٰ أَبْصَارِهِمْ غِشَاوَةٌ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿٧﴾

7. Allaah Amepiga mhuri juu ya nyoyo zao, na juu ya masikio yao; na juu ya macho yao pana kifuniko; na watapata adhabu kubwa.

 وَمِنَ النَّاسِ مَن يَقُولُ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَبِالْيَوْمِ الْآخِرِ وَمَا هُم بِمُؤْمِنِينَ ﴿٨﴾ 

8. Na miongoni mwa watu wako wasemao: ”Tumemuamini Allaah na Siku ya Mwisho” hali ya kuwa si wenye kuamini.

يُخَادِعُونَ اللَّـهَ وَالَّذِينَ آمَنُوا وَمَا يَخْدَعُونَ إِلَّا أَنفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ ﴿٩﴾

9. Wanamhadaa Allaah na wale walioamini na hawahadai ila nafsi zao na wala hawahisi.

فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ فَزَادَهُمُ اللَّـهُ مَرَضًا ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْذِبُونَ ﴿١٠﴾

10. Ndani ya nyoyo zao mna maradhi na Allaah Akawazidishia maradhi, na watapata adhabu iumizayo kwa waliyokuwa wakiyakadhibisha.

 وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ قَالُوا إِنَّمَا نَحْنُ مُصْلِحُونَ ﴿١١﴾

11. Na wanapoambiwa: “Msifanye uharibifu katika ardhi”. Husema: “Hakika sisi ni watengenezaji.”

 أَلَا إِنَّهُمْ هُمُ الْمُفْسِدُونَ وَلَـٰكِن لَّا يَشْعُرُونَ ﴿١٢﴾

12. Tanabahi! Hakika wao ndio mafisadi lakini hawahisi.

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ آمِنُوا كَمَا آمَنَ النَّاسُ قَالُوا أَنُؤْمِنُ كَمَا آمَنَ السُّفَهَاءُ ۗ أَلَا إِنَّهُمْ هُمُ السُّفَهَاءُ وَلَـٰكِن لَّا يَعْلَمُونَ ﴿١٣﴾

13. Na wanapoambiwa: “Aminini kama walivyoamini watu”. Husema: “Je, tuamini kama walivyoamini masafihi.” Tanabahi! Hakika wao ndio masafihi lakini hawajui.

 وَإِذَا لَقُوا الَّذِينَ آمَنُوا قَالُوا آمَنَّا وَإِذَا خَلَوْا إِلَىٰ شَيَاطِينِهِمْ قَالُوا إِنَّا مَعَكُمْ إِنَّمَا نَحْنُ مُسْتَهْزِئُونَ ﴿١٤﴾

14. Na wanapokutana na wale walioamini husema: “Tumeamini.” Na wanapokuwa peke yao pamoja na shayaatwiyn wao, husema: “Hakika sisi tuko pamoja nanyi, hakika sisi ni wenye kuwadhihaki tu.”

  اللَّـهُ يَسْتَهْزِئُ بِهِمْ وَيَمُدُّهُمْ فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ ﴿١٥﴾

15. Allaah Anawadhihaki wao (kuwalipiza istihzai zao) na Atawaendeleza katika hali yao ya ukiukaji mipaka wakitangatanga ovyo.


 أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ اشْتَرَوُا الضَّلَالَةَ بِالْهُدَىٰ فَمَا رَبِحَت تِّجَارَتُهُمْ وَمَا كَانُوا مُهْتَدِينَ ﴿١٦﴾

16. Hao ndio wale walionunua upotofu (badala) ya Hidaaya Basi haikupata  faida  biashara yao na wala hawakuwa wenye kuongoka.

 مَثَلُهُمْ كَمَثَلِ الَّذِي اسْتَوْقَدَ نَارًا فَلَمَّا أَضَاءَتْ مَا حَوْلَهُ ذَهَبَ اللَّـهُ بِنُورِهِمْ وَتَرَكَهُمْ فِي ظُلُمَاتٍ لَّا يُبْصِرُونَ ﴿١٧﴾

17. Mfano wao ni kama mfano wa aliyekoka moto, ulipoyaangaza yaliyopo pembezoni mwake Allaah Akawaondoshea nuru yao na Akawaacha katika viza hawaoni.

 صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لَا يَرْجِعُونَ ﴿١٨﴾

18. Viziwi, mabubu, vipofu basi hawatorejea (katika njia iliyonyooka).

 أَوْ كَصَيِّبٍ مِّنَ السَّمَاءِ فِيهِ ظُلُمَاتٌ وَرَعْدٌ وَبَرْقٌ يَجْعَلُونَ أَصَابِعَهُمْ فِي آذَانِهِم مِّنَ الصَّوَاعِقِ حَذَرَ الْمَوْتِ ۚ وَاللَّـهُ مُحِيطٌ بِالْكَافِرِينَ ﴿١٩﴾

19. Au ni kama mvua kubwa kutoka mbinguni, ndani yake mna viza na radi na umeme, wanatia vidole vyao katika masikio yao kutokana na mingurumo wakihofu mauti, na Allaah ni Muhiytw (Mwenye kuwazunguka kwa ujuzi Wake) makafiri.

يَكَادُ الْبَرْقُ يَخْطَفُ أَبْصَارَهُمْ ۖ كُلَّمَا أَضَاءَ لَهُم مَّشَوْا فِيهِ وَإِذَا أَظْلَمَ عَلَيْهِمْ قَامُوا ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَذَهَبَ بِسَمْعِهِمْ وَأَبْصَارِهِمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٠﴾

20. Unakaribia umeme kunyakua macho yao, kila unapowaangazia (njia) huenda ndani yake, na unapowafanyia kiza husimama; na lau Allaah Angelitaka basi Angeliwaondoshea kusikia kwao na kuona kwao. Hakika Allaah juu ya kila kitu ni Qadiyr (Muweza).

 يَا أَيُّهَا النَّاسُ اعْبُدُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُمْ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿٢١﴾

21. Enyi watu! Mwabuduni Mola wenu Ambae Amekuumbeni na wale wa kabla yenu mpate kuwa na taqwa.

الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ فِرَاشًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً وَأَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجَ بِهِ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِزْقًا لَّكُمْ ۖ فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٢٢﴾

22. Ambaye Amewafanyieni ardhi kuwa ni tandiko na mbingu kuwa ni paa, na Akateremsha kutoka mbinguni maji, Akawatolea kwayo matunda kuwa ni riziki zenu. Basi msimuwekee Allaah waliolingana naye (washirika) na hali ya kuwa nyinyi mnajua (kuwa Allaah Hana Anayelingana nae).

 وَإِن كُنتُمْ فِي رَيْبٍ مِّمَّا نَزَّلْنَا عَلَىٰ عَبْدِنَا فَأْتُوا بِسُورَةٍ مِّن مِّثْلِهِ وَادْعُوا شُهَدَاءَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٢٣﴾

23. Na ikiwa mko katika shaka kutokana na Tuliyoyateremsha juu ya mja Wetu (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi leteni Suwrah mfano wake, na waiteni mashahidi wenu pasipo na Allaah mkiwa ni wakweli.

فَإِن لَّمْ تَفْعَلُوا وَلَن تَفْعَلُوا فَاتَّقُوا النَّارَ الَّتِي وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ ۖ أُعِدَّتْ لِلْكَافِرِينَ ﴿٢٤﴾

24. Msipofanya, na wala hamtaweza kufanya, basi ogopeni moto ambao kuni zake ni watu na mawe, ulioandaliwa kwa makafiri.

  وَبَشِّرِ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أَنَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۖ كُلَّمَا رُزِقُوا مِنْهَا مِن ثَمَرَةٍ رِّزْقًا ۙ قَالُوا هَـٰذَا الَّذِي رُزِقْنَا مِن قَبْلُ ۖ وَأُتُوا بِهِ مُتَشَابِهًا ۖ وَلَهُمْ فِيهَا أَزْوَاجٌ مُّطَهَّرَةٌ ۖ وَهُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢٥﴾

25. Na wabashirie wale walioamini na wakatenda mema kwamba watapata Jannaat zipitazo chini yake mito, kila watakaporuzukiwa humo katika matunda kuwa ni riziki husema: “Haya ndiyo yale tuliyoruzukiwa kabla.” Na wataletewa (matunda) hali ya kuwa yanashabihiana, na watapata humo wake waliotwaharishwa, nao humo ni wenye kudumu.

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَسْتَحْيِي أَن يَضْرِبَ مَثَلًا مَّا بَعُوضَةً فَمَا فَوْقَهَا ۚ فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا فَيَعْلَمُونَ أَنَّهُ الْحَقُّ مِن رَّبِّهِمْ ۖ وَأَمَّا الَّذِينَ كَفَرُوا فَيَقُولُونَ مَاذَا أَرَادَ اللَّـهُ بِهَـٰذَا مَثَلًا ۘ يُضِلُّ بِهِ كَثِيرًا وَيَهْدِي بِهِ كَثِيرًا ۚ وَمَا يُضِلُّ بِهِ إِلَّا الْفَاسِقِينَ ﴿٢٦﴾

26. Hakika Allaah Haoni hayaa kupiga mfano wa mbu na ulio zaidi yake (kwa udogo). Basi wale walioamini huelewa kwamba hiyo ni haki kutoka kwa Mola wao; ama wale waliokufuru husema: “Anataka nini Allaah kwa mfano huu?” (Allaah) Huwapoteza kwa mfano huu wengi na Huwahidi kwa mfano huu wengi na wala Hawapotezi kwayo ila mafasiki.

الَّذِينَ يَنقُضُونَ عَهْدَ اللَّـهِ مِن بَعْدِ مِيثَاقِهِ وَيَقْطَعُونَ مَا أَمَرَ اللَّـهُ بِهِ أَن يُوصَلَ وَيُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ ﴿٢٧﴾

27. Wale ambao wanavunja Ahadi ya Allaah baada ya kuifunga Kwake na wanayakata Aliyoamrisha kwayo Allaah kuungwa, na wanafanya ufisadi katika ardhi, hao ndio wenye khasara.

 كَيْفَ تَكْفُرُونَ بِاللَّـهِ وَكُنتُمْ أَمْوَاتًا فَأَحْيَاكُمْ ۖ ثُمَّ يُمِيتُكُمْ ثُمَّ يُحْيِيكُمْ ثُمَّ إِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٢٨﴾

28. Vipi mnamkanusha Allaah na hali mlikuwa wafu Akakuhuisheni, kisha Atakufisheni, kisha Atakuhuisheni, kisha Kwake mtarejeshwa?

هُوَ الَّذِي خَلَقَ لَكُم مَّا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا ثُمَّ اسْتَوَىٰ إِلَى السَّمَاءِ فَسَوَّاهُنَّ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ ۚ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٢٩﴾ 

29. Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbieni vyote vilivyomo ardhini kisha Istawaa (Yuko juu kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah) kuzielekea mbingu na Akazifanya timilifu mbingu saba, Naye kwa kila kitu ni ‘Aliym  (Mjuzi).   

 وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي جَاعِلٌ فِي الْأَرْضِ خَلِيفَةً ۖ قَالُوا أَتَجْعَلُ فِيهَا مَن يُفْسِدُ فِيهَا وَيَسْفِكُ الدِّمَاءَ وَنَحْنُ نُسَبِّحُ بِحَمْدِكَ وَنُقَدِّسُ لَكَ ۖ قَالَ إِنِّي أَعْلَمُ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٣٠﴾

30. Na (taja) Mola wako Alipowaambia Malaika: “Hakika Mimi Nitaweka katika ardhi khaliyfah.” Wakasema: “Utaweka humo atakayefanya ufisadi humo na kumwaga damu, na hali sisi tunakusabbih kwa Sifa Zako na tunakutukuza kwa Utakatifu Wako?” (Allaah) Akasema: “Hakika Mimi Nayajua zaidi msiyoyajua.”

 وَعَلَّمَ آدَمَ الْأَسْمَاءَ كُلَّهَا ثُمَّ عَرَضَهُمْ عَلَى الْمَلَائِكَةِ فَقَالَ أَنبِئُونِي بِأَسْمَاءِ هَـٰؤُلَاءِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٣١﴾

31. Na Akamfunza Aadam majina ya vitu vyote kisha Akayaonyesha mbele ya Malaika; Akasema: “Niambieni majina ya haya mkiwa ni wakweli.”

 قَالُوا سُبْحَانَكَ لَا عِلْمَ لَنَا إِلَّا مَا عَلَّمْتَنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ ﴿٣٢﴾

32. Wakasema: “Subhaanak (Utakasifu ni Wako!)! Hatuna elimu isipokuwa Uliyotufunza; hakika Wewe ni Al-‘Aliymul-Hakiym” (Mjuzi wa yote daima - Mwenye hikmah wa yote daima).


 قَالَ يَا آدَمُ أَنبِئْهُم بِأَسْمَائِهِمْ ۖ فَلَمَّا أَنبَأَهُم بِأَسْمَائِهِمْ قَالَ أَلَمْ أَقُل لَّكُمْ إِنِّي أَعْلَمُ غَيْبَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَأَعْلَمُ مَا تُبْدُونَ وَمَا كُنتُمْ تَكْتُمُونَ ﴿٣٣﴾

33. Akasema: “Ee Aadam, wajulishe kwa majina yao.” Basi alipowatajia majina yao; (Allaah) Akasema: “Je, Sikuwaambieni kuwa hakika Mimi Najua ghayb ya mbingu na ardhi na Najua mnayoyadhihirisha na mliyokuwa mkiyaficha.

وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ أَبَىٰ وَاسْتَكْبَرَ وَكَانَ مِنَ الْكَافِرِينَ ﴿٣٤﴾

34. Na (taja) Tulipowaambia Malaika: “Msujudieni Aadam.” Wakasujudu isipokuwa Ibliys alikataa na akatakabari na akawa miongoni mwa makafiri.

 وَقُلْنَا يَا آدَمُ اسْكُنْ أَنتَ وَزَوْجُكَ الْجَنَّةَ وَكُلَا مِنْهَا رَغَدًا حَيْثُ شِئْتُمَا وَلَا تَقْرَبَا هَـٰذِهِ الشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ الظَّالِمِينَ ﴿٣٥﴾

35. Na Tukasema: “Ee Aadam, kaa wewe na mkeo Jannah na kuleni humo maridhawa popote mpendapo na wala msiukaribie mti huu; mtakuwa miongoni mwa madhalimu.”

 فَأَزَلَّهُمَا الشَّيْطَانُ عَنْهَا فَأَخْرَجَهُمَا مِمَّا كَانَا فِيهِ ۖ وَقُلْنَا اهْبِطُوا بَعْضُكُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ ۖ وَلَكُمْ فِي الْأَرْضِ مُسْتَقَرٌّ وَمَتَاعٌ إِلَىٰ حِينٍ ﴿٣٦﴾

36. Shaytwaan akawatelezesha wote wawili kwayo, Akawatoa kutoka katika hali waliyokuwa nayo. Tukasema: “Shukeni mkiwa maadui nyinyi kwa nyinyi, na mtapata katika ardhi makazi na starehe hadi muda maalum.”

 فَتَلَقَّىٰ آدَمُ مِن رَّبِّهِ كَلِمَاتٍ فَتَابَ عَلَيْهِ ۚ إِنَّهُ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ ﴿٣٧﴾

37. Kisha Aadam akapokea maneno kutoka kwa Mola wake; na (Mola wake) Akapokea tawbah yake, hakika Yeye Ndiye at-Tawwaabur-Rahiym (Mwingi wa kupokea tawbah - Mwenye kurehemu).

 قُلْنَا اهْبِطُوا مِنْهَا جَمِيعًا ۖ فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدًى فَمَن تَبِعَ هُدَايَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٣٨﴾

38. Tukasema: “Shukeni kutoka humo nyote. Itakapokufikieni kutoka Kwangu Hidaaya, yeyote atakayefuata  Hidaaya Yangu hakutakuwa na khofu juu yao  wala hawatahuzunika.”

وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٣٩﴾

39. Na wale waliokufuru na wakakadhibisha Aayaat Zetu hao ni watu wa Motoni, wao humo ni ni wenye kudumu.

يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اذْكُرُوا نِعْمَتِيَ الَّتِي أَنْعَمْتُ عَلَيْكُمْ وَأَوْفُوا بِعَهْدِي أُوفِ بِعَهْدِكُمْ وَإِيَّايَ فَارْهَبُونِ ﴿٤٠﴾

40. Enyi wana wa Israaiyl! Kumbukeni neema Yangu Niliyokuneemesheni na timizeni ahadi Yangu Nikutimizieni ahadi yenu na Mimi (pekee) niogopeni . 

وَآمِنُوا بِمَا أَنزَلْتُ مُصَدِّقًا لِّمَا مَعَكُمْ وَلَا تَكُونُوا أَوَّلَ كَافِرٍ بِهِ ۖ وَلَا تَشْتَرُوا بِآيَاتِي ثَمَنًا قَلِيلًا وَإِيَّايَ فَاتَّقُونِ ﴿٤١﴾

41. Na aminini yale Niliyoyateremsha yenye kusadikisha yale yaliyo pamoja nanyi, na wala msiwe wa kwanza wenye kuzikanusha; na wala msiuze Aayaat Zangu kwa thamani ndogo na Mimi tu nicheni.

وَلَا تَلْبِسُوا الْحَقَّ بِالْبَاطِلِ وَتَكْتُمُوا الْحَقَّ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٤٢﴾

42. Na wala msichanganye haki kwa batili na mkaficha haki; na hali mnajua.

 وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَارْكَعُوا مَعَ الرَّاكِعِينَ ﴿٤٣﴾

43. Na simamisheni Swalaah na toeni Zakaah na rukuuni pamoja na wanaorukuu (katika ‘ibaadah na utiifu).

أَتَأْمُرُونَ النَّاسَ بِالْبِرِّ وَتَنسَوْنَ أَنفُسَكُمْ وَأَنتُمْ تَتْلُونَ الْكِتَابَ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٤٤﴾ 

44. Je, mnaamrisha watu (watende) mema na mnajisahu nafsi zenu na hali ya kuwa nyinyi mnasoma Kitabu; je hamtii akilini?


  وَاسْتَعِينُوا بِالصَّبْرِ وَالصَّلَاةِ ۚ وَإِنَّهَا لَكَبِيرَةٌ إِلَّا عَلَى الْخَاشِعِينَ ﴿٤٥﴾

45. Na tafuteni msaada kupitia subira na Swalaah; na hakika hilo ni kubwa isipokuwa kwa wanyenyekevu.

الَّذِينَ يَظُنُّونَ أَنَّهُم مُّلَاقُو رَبِّهِمْ وَأَنَّهُمْ إِلَيْهِ رَاجِعُونَ ﴿٤٦﴾

46. Ambao wana yakini kwamba hakika wao ni wenye kukutana na Mola wao na hakika wao Kwake ni wenye kurejea

يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اذْكُرُوا نِعْمَتِيَ الَّتِي أَنْعَمْتُ عَلَيْكُمْ وَأَنِّي فَضَّلْتُكُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿٤٧﴾

47. Enyi wana wa Israaiyl! Kumbukeni neema Yangu Niliyokuneemesheni na hakika Mimi Nimekufadhilisheni juu ya walimwengu.

وَاتَّقُوا يَوْمًا لَّا تَجْزِي نَفْسٌ عَن نَّفْسٍ شَيْئًا وَلَا يُقْبَلُ مِنْهَا شَفَاعَةٌ وَلَا يُؤْخَذُ مِنْهَا عَدْلٌ وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ ﴿٤٨﴾   

48. Iogopeni Siku ambayo nafsi haitaifaa nafsi nyingine kwa kitu chochote kile, na wala haitakubaliwa kutoka kwake shafaa’ah (uombezi wa aina yoyote ule), na wala hakitachukuliwa kutoka kwake kikomboleo, na wala hawatanusuriwa.

 وَإِذْ نَجَّيْنَاكُم مِّنْ آلِ فِرْعَوْنَ يَسُومُونَكُمْ سُوءَ الْعَذَابِ يُذَبِّحُونَ أَبْنَاءَكُمْ وَيَسْتَحْيُونَ نِسَاءَكُمْ ۚ وَفِي ذَٰلِكُم بَلَاءٌ مِّن رَّبِّكُمْ عَظِيمٌ ﴿٤٩﴾

49. Na (kumbukeni) Tulipokuokoeni kutoka kwa watu wa Fir’awn walipokusibuni adhabu mbaya, wakiwachinja watoto wenu (wachanga wa kiume), na wakiacha hai wanawake wenu, na katika hayo kwenu ulikuwa ni mtihani mkuu kutoka kwa Mola wenu. 


وَإِذْ فَرَقْنَا بِكُمُ الْبَحْرَ فَأَنجَيْنَاكُمْ وَأَغْرَقْنَا آلَ فِرْعَوْنَ وَأَنتُمْ تَنظُرُونَ ﴿٥٠﴾ 

50. Na (kumbukeni) Tulipoitenganisha bahari (ikawa sehemu mbili) kwa ajili yenu; Tukakuokoeni na Tukawagharikisha watu wa Fir’awn na huku nyinyi mnatazama.

وَإِذْ وَاعَدْنَا مُوسَىٰ أَرْبَعِينَ لَيْلَةً ثُمَّ اتَّخَذْتُمُ الْعِجْلَ مِن بَعْدِهِ وَأَنتُمْ ظَالِمُونَ ﴿٥١﴾

51. Na (kumbukeni) Tulipomuahidi Muwsaa siku arubaini kisha mkamchukua ndama (kumuabudu) baada yake na mkawa madhalimu.

ثُمَّ عَفَوْنَا عَنكُم مِّن بَعْدِ ذَٰلِكَ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٥٢﴾ 

52. Kisha Tukawasameheni baada ya hapo mpate kushukuru.

وَإِذْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ وَالْفُرْقَانَ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ ﴿٥٣﴾

 53. Na (kumbukeni) Tulipompa Muwsaa Kitabu na al-Furqaan[1] huenda mpate kuongoka.

 وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ يَا قَوْمِ إِنَّكُمْ ظَلَمْتُمْ أَنفُسَكُم بِاتِّخَاذِكُمُ الْعِجْلَ فَتُوبُوا إِلَىٰ بَارِئِكُمْ فَاقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ عِندَ بَارِئِكُمْ فَتَابَ عَلَيْكُمْ ۚ إِنَّهُ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ ﴿٥٤﴾

54. Na (kumbukeni wakati) Muwsaa alipowaambia kaumu yake: “Enyi kaumu yangu! Hakika nyinyi mmedhulumu nafsi zenu kwa kumchukua kwenu ndama, basi tubuni kwa Baariu (Muumbaji) wenu;  (namna ya kutubu kwenyewe) ziueni nafsi zenu, hivyo ni bora kwenu mbele ya Baariu wenu”. Akapokea tawbah yenu; hakika Yeye Ndiye At-Tawwaabur-Rahiym (Mwingi wa kupokea tawbah - Mwenye kurehemu).

وَإِذْ قُلْتُمْ يَا مُوسَىٰ لَن نُّؤْمِنَ لَكَ حَتَّىٰ نَرَى اللَّـهَ جَهْرَةً فَأَخَذَتْكُمُ الصَّاعِقَةُ وَأَنتُمْ تَنظُرُونَ ﴿٥٥﴾

55. Na (kumbukeni) mliposema: “Ewe Muwsaa! Hatutakuamini mpaka tumuone Allaah waziwazi”; ikakuchukuweni asw-swaa’iqah (mngurumo angamizi)  nanyi mnatazama.

ثُمَّ بَعَثْنَاكُم مِّن بَعْدِ مَوْتِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٥٦﴾

56. Kisha Tukakufufueni baada ya kufa kwenu mpate  kushukuru.

وَظَلَّلْنَا عَلَيْكُمُ الْغَمَامَ وَأَنزَلْنَا عَلَيْكُمُ الْمَنَّ وَالسَّلْوَىٰ ۖ كُلُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ ۖ وَمَا ظَلَمُونَا وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ ﴿٥٧﴾ 

57. Na Tukakufunikeni kwa mawingu (mlipokuwa mnasafiri jangwani mkitoka Misri), na Tukakuteremshieni al-manna na as-salwaa. (Tukakwambieni): “Kuleni katika vizuri Tulivyokuruzukuni.” Hawakutudhulumu Sisi lakini walikuwa wakizidhulumu nafsi zao.

وَإِذْ قُلْنَا ادْخُلُوا هَـٰذِهِ الْقَرْيَةَ فَكُلُوا مِنْهَا حَيْثُ شِئْتُمْ رَغَدًا وَادْخُلُوا الْبَابَ سُجَّدًا وَقُولُوا حِطَّةٌ نَّغْفِرْ لَكُمْ خَطَايَاكُمْ ۚ وَسَنَزِيدُ الْمُحْسِنِينَ ﴿٥٨﴾

58. Na (kumbukeni) Tuliposema: “Ingieni mji huu (Quds) na kuleni humo maridhawa popote mpendapo, na ingieni katika mlango (wake) huku mmeinama (kwa unyenyekevu) na semeni (wakati wa kuingia) Hittwah (tuondolee uzito wa madhambi yetu)”; Tutakughufurieni makosa yenu na Tutawazidishia (neema na thawabu)  wafanyao wema.  


 فَبَدَّلَ الَّذِينَ ظَلَمُوا قَوْلًا غَيْرَ الَّذِي قِيلَ لَهُمْ فَأَنزَلْنَا عَلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا رِجْزًا مِّنَ السَّمَاءِ بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ ﴿٥٩﴾ 

59. “Basi wale ambao wamedhulumu walibadilisha kauli (wakasema kauli) kinyume na ile waliyoambiwa, Tukateremsha juu ya waliodhulumu adhabu ya kufadhaika kutoka mbinguni kwa yale waliyokuwa wakifanya ya ufasiki.”



 وَإِذِ اسْتَسْقَىٰ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ فَقُلْنَا اضْرِب بِّعَصَاكَ الْحَجَرَ ۖ فَانفَجَرَتْ مِنْهُ اثْنَتَا عَشْرَةَ عَيْنًا ۖ قَدْ عَلِمَ كُلُّ أُنَاسٍ مَّشْرَبَهُمْ ۖ كُلُوا وَاشْرَبُوا مِن رِّزْقِ اللَّـهِ وَلَا تَعْثَوْا فِي الْأَرْضِ مُفْسِدِينَ ﴿٦٠﴾

60. Na (kumbukeni wakati) Muwsaa alipoomba maji kwa ajili ya kaumu yake. Tukasema: “Piga kwa fimbo yako jiwe.” Zikachimbuka (na kububujika) kutoka kwalo chemchem kumi na mbili. Kila watu (kabila) wakaelewa kinywaji chao. Kuleni na kunyweni kutokana na riziki ya Allaah na wala msifanye uovu katika ardhi kwani mtakuwa mafisadi.

 وَإِذْ قُلْتُمْ يَا مُوسَىٰ لَن نَّصْبِرَ عَلَىٰ طَعَامٍ وَاحِدٍ فَادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُخْرِجْ لَنَا مِمَّا تُنبِتُ الْأَرْضُ مِن بَقْلِهَا وَقِثَّائِهَا وَفُومِهَا وَعَدَسِهَا وَبَصَلِهَا ۖ قَالَ أَتَسْتَبْدِلُونَ الَّذِي هُوَ أَدْنَىٰ بِالَّذِي هُوَ خَيْرٌ ۚ اهْبِطُوا مِصْرًا فَإِنَّ لَكُم مَّا سَأَلْتُمْ ۗ وَضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الذِّلَّةُ وَالْمَسْكَنَةُ وَبَاءُوا بِغَضَبٍ مِّنَ اللَّـهِ ۗ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَانُوا يَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَيَقْتُلُونَ النَّبِيِّينَ بِغَيْرِ الْحَقِّ ۗ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ ﴿٦١﴾

61. Na (kumbukeni) mliposema: “Ee Muwsaa! Hatuwezi kusubiri kwa chakula (cha aina) moja, tuombee kwa Mola Wako Atutolee katika inavyoviotesha ardhi; kati ya mboga zake, matango yake, thomu (au ngano) yake, adesi zake na vitunguu vyake.” (Muwsaa) Akasema: “Je mnataka kubadilisha yaliyo duni kwa yaliyo bora? Shukeni mjini, hakika huko mtapata mnayoyauliza”. Na ikapigwa juu yao dhila na umaskini na wakastahiki ghadhabu kutoka kwa Allaah, hayo ni kwa kuwa wao walikuwa wakikanusha Aayaat za Allaah;  na wakiwaua Manabii bila ya haki; hayo ni kwa sababu ya kuasi kwao na walikuwa wanapindukia mipaka.

 إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَادُوا وَالنَّصَارَىٰ وَالصَّابِئِينَ مَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَعَمِلَ صَالِحًا فَلَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٦٢﴾

62. Hakika wale ambao wameamini, na wale ambao ni Mayahudi, na Manaswara na Masabai (waabudu nyota); yeyote atakayemwamini Allaah na Siku ya Mwisho, na akatenda mema basi watapata ujira wao kutoka kwa Mola wao, na hakutokuwa na khofu juu yao, na wala hawatohuzunika.

وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَكُمْ وَرَفَعْنَا فَوْقَكُمُ الطُّورَ خُذُوا مَا آتَيْنَاكُم بِقُوَّةٍ وَاذْكُرُوا مَا فِيهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿٦٣﴾

63. Na (kumbukeni) Tulipochukua ahadi yenu (mtekeleze yaliyo katika Tawraat) na Tukaunyanyua juu yenu (mlima) at-Twuwr (Tukasema): “Chukueni Tuliyokupeni kwa nguvu (azimio la kweli) na kumbukeni yaliyomo humo mpate kuwa na taqwa.”

ثُمَّ تَوَلَّيْتُم مِّن بَعْدِ ذَٰلِكَ ۖ فَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ لَكُنتُم مِّنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٦٤﴾

64. Kisha mkakengeuka baada ya hayo, na lau si fadhila za Allaah juu yenu na Rahmah Yake mngekuwa miongoni mwa wenye kukhasirika.

وَلَقَدْ عَلِمْتُمُ الَّذِينَ اعْتَدَوْا مِنكُمْ فِي السَّبْتِ فَقُلْنَا لَهُمْ كُونُوا قِرَدَةً خَاسِئِينَ ﴿٦٥﴾

65. Na kwa yakini mnaelewa (habari za) wale ambao walikiuka mipaka miongoni mwenu katika As-Sabt (Jumamosi) Tukawaambia: “Kuweni manyani waliotezwa (hakiri).”

فَجَعَلْنَاهَا نَكَالًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهَا وَمَا خَلْفَهَا وَمَوْعِظَةً لِّلْمُتَّقِينَ ﴿٦٦﴾

66. Tukaifanya kuwa ni adhabu ya kuonya kwa waliokuweko zama zao na wataokuja nyuma (baada) yao na ni mawaidha kwa wenye taqwa.

وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تَذْبَحُوا بَقَرَةً ۖ قَالُوا أَتَتَّخِذُنَا هُزُوًا ۖ قَالَ أَعُوذُ بِاللَّـهِ أَنْ أَكُونَ مِنَ الْجَاهِلِينَ ﴿٦٧﴾

67. Na (kumbukeni) Muwsaa alipowaambia kaumu wake:  Hakika Allaah Anakuamuruni mchinje ng’ombe.” Wakasema: “Unatufanyia mzaha?” Akasema: “Najikinga kwa Allaah kuwa  miongoni mwa wajinga.

 قَالُوا ادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لَّنَا مَا هِيَ ۚ قَالَ إِنَّهُ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٌ لَّا فَارِضٌ وَلَا بِكْرٌ عَوَانٌ بَيْنَ ذَٰلِكَ ۖ فَافْعَلُوا مَا تُؤْمَرُونَ ﴿٦٨﴾

68. Wakasema: “Tuombee kwa Mola wako Atubainishie ni ngo’mbe wa aina gani huyo?” (Muwsaa) Akasema: “Hakika Yeye (Allaah) Anasema kwamba ng’ombe wenyewe si mpevu (si mzee) wala si mchanga, bali ni wa (kati na kati) baina ya hao, basi fanyeni mnavyoamrishwa.”

قَالُوا ادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لَّنَا مَا لَوْنُهَا ۚ قَالَ إِنَّهُ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٌ صَفْرَاءُ فَاقِعٌ لَّوْنُهَا تَسُرُّ النَّاظِرِينَ ﴿٦٩﴾

69. Wakasema: “Tuombee kwa Mola wako Atubainishie rangi yake?” (Muwsaa) Akasema: “Hakika Yeye (Allaah) Anasema kwamba ni ng’ombe wa rangi ya njano iliyoiva mno, rangi yake huwapendeza wanaotazama.”

 قَالُوا ادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لَّنَا مَا هِيَ إِنَّ الْبَقَرَ تَشَابَهَ عَلَيْنَا وَإِنَّا إِن شَاءَ اللَّـهُ لَمُهْتَدُونَ ﴿٧٠﴾

70. Wakasema: “Tuombee kwa Mola wako Atubainishie ni ng’ombe wa aina gani huyo? Kwa hakika ng’ombe wametutatiza na hakika sisi In-shaa-Allaah  tutakuwa wenye kuongoka.”

 قَالَ إِنَّهُ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٌ لَّا ذَلُولٌ تُثِيرُ الْأَرْضَ وَلَا تَسْقِي الْحَرْثَ مُسَلَّمَةٌ لَّا شِيَةَ فِيهَا ۚ قَالُوا الْآنَ جِئْتَ بِالْحَقِّ ۚ فَذَبَحُوهَا وَمَا كَادُوا يَفْعَلُونَ ﴿٧١﴾

71. (Muwsaa) Akasema:: ”Hakika Yeye (Allaah) Anasema kwamba ni ng’ombe ambaye hakutiishwa; kwa kulima ardhi wala kwa kumwagilia (maji) shamba; ni kamilifu (yu safi) hana dosari.” Wakasema: “Sasa umekuja na haki”. Basi wakamchinja na hawakuwa wenye kukaribia kufanya hivyo (kuchinja).

 وَإِذْ قَتَلْتُمْ نَفْسًا فَادَّارَأْتُمْ فِيهَا ۖ وَاللَّـهُ مُخْرِجٌ مَّا كُنتُمْ تَكْتُمُونَ ﴿٧٢﴾

72. Na (kumbukeni) mlipoiua nafsi, kisha mkakhitilafiana kwayo, na Allaah ni Mwenye kutoa hayo mliyokuwa mkiyaficha.

فَقُلْنَا اضْرِبُوهُ بِبَعْضِهَا ۚ كَذَٰلِكَ يُحْيِي اللَّـهُ الْمَوْتَىٰ وَيُرِيكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ ﴿٧٣﴾

73. Tukasema: “Mpigeni (huyo maiti) kwa baadhi ya sehemu yake (huyo ng’ombe).” Hivyo ndivyo Allaah Anavyohuisha wafu na Anakuonyesheni Aayaat Zake huenda mkatia akilini.

ثُمَّ قَسَتْ قُلُوبُكُم مِّن بَعْدِ ذَٰلِكَ فَهِيَ كَالْحِجَارَةِ أَوْ أَشَدُّ قَسْوَةً ۚ وَإِنَّ مِنَ الْحِجَارَةِ لَمَا يَتَفَجَّرُ مِنْهُ الْأَنْهَارُ ۚ وَإِنَّ مِنْهَا لَمَا يَشَّقَّقُ فَيَخْرُجُ مِنْهُ الْمَاءُ ۚ وَإِنَّ مِنْهَا لَمَا يَهْبِطُ مِنْ خَشْيَةِ اللَّـهِ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿٧٤﴾

74. Kisha nyoyo zenu zikawa ngumu baada ya hayo, (zikawa) kama mawe au ngumu zaidi. Na kwa hakika katika mawe kuna  yanayobubujika ndani yake mito. Na hakika katika hayo (mawe) kuna yanayopasuka yakatoka ndani yake maji. Na hakika katika hayo kuna mengine yanayoporomoka kutokana na khofu ya Allaah. Na Allaah si Mwenye kughafilika na myatendayo.

أَفَتَطْمَعُونَ أَن يُؤْمِنُوا لَكُمْ وَقَدْ كَانَ فَرِيقٌ مِّنْهُمْ يَسْمَعُونَ كَلَامَ اللَّـهِ ثُمَّ يُحَرِّفُونَهُ مِن بَعْدِ مَا عَقَلُوهُ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿٧٥﴾

75. Je, mnatumai (enyi Waumini) kwamba watakuaminini na hali lilikuwa kundi miongoni mwao linasikia maneno ya Allaah kisha linayageuza baada ya kuyaelewa na hali wanajua?

وَإِذَا لَقُوا الَّذِينَ آمَنُوا قَالُوا آمَنَّا وَإِذَا خَلَا بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ قَالُوا أَتُحَدِّثُونَهُم بِمَا فَتَحَ اللَّـهُ عَلَيْكُمْ لِيُحَاجُّوكُم بِهِ عِندَ رَبِّكُمْ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٧٦﴾

76. Na wanapokutana na wale walioamini husema: “Tumeamini”. Na wanapokuwa peke yao; wao kwa wao; husema: “Mnawasimulia yale Aliyokufungulieni Allaah ili wapate kukuhojini kwayo mbele ya Mola wenu; hamtii akilini?”

 أَوَلَا يَعْلَمُونَ أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعْلِنُونَ ﴿٧٧﴾

77. Je, hawaelewi kwamba Allaah Anajua wanayoyaficha na wanayoyatangaza?

 وَمِنْهُمْ أُمِّيُّونَ لَا يَعْلَمُونَ الْكِتَابَ إِلَّا أَمَانِيَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَظُنُّونَ ﴿٧٨﴾ 

78. Na miongoni mwao wako ummiyyuwn (wasiojua kusoma wala kuandika); hawakijui Kitabu ila matamanio ya kuwaza tu, nao hawana ila kudhani tu.

 فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ يَكْتُبُونَ الْكِتَابَ بِأَيْدِيهِمْ ثُمَّ يَقُولُونَ هَـٰذَا مِنْ عِندِ اللَّـهِ لِيَشْتَرُوا بِهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۖ فَوَيْلٌ لَّهُم مِّمَّا كَتَبَتْ أَيْدِيهِمْ وَوَيْلٌ لَّهُم مِّمَّا يَكْسِبُونَ ﴿٧٩﴾

79. Basi ole kwa wale wenye kuandika kitabu kwa mikono yao; kisha wakasema: ”Haya ni kutoka kwa Allaah” ili wachume kwayo thamani ndogo. Basi ole wao kwa yale yaliyoandikwa na mikono yao, na ole wao kwa yale wanayoyachuma.

 وَقَالُوا لَن تَمَسَّنَا النَّارُ إِلَّا أَيَّامًا مَّعْدُودَةً ۚ قُلْ أَتَّخَذْتُمْ عِندَ اللَّـهِ عَهْدًا فَلَن يُخْلِفَ اللَّـهُ عَهْدَهُ ۖ أَمْ تَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٨٠﴾

80. Na walisema: “Hautatugusa Moto ila siku chache tu”. Sema: “Je, mmechukua ahadi kwa Allaah?” Basi Allaah Hakhalifu ahadi Yake, au mnasema kuhusu Allaah msiyoyajua?

 بَلَىٰ مَن كَسَبَ سَيِّئَةً وَأَحَاطَتْ بِهِ خَطِيئَتُهُ فَأُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٨١﴾

81. Ndio! Yeyote aliyechuma uovu na yakamzunguka kwayo makosa yake; basi hao ni watu wa Motoni, wao humo ni wenye kudumu.

 وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٨٢﴾

82. Na wale ambao wameamini na wakatenda mema; hao ni watu wa Jannah, wao humo ni wenye kudumu.

وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَ بَنِي إِسْرَائِيلَ لَا تَعْبُدُونَ إِلَّا اللَّـهَ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا وَذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَقُولُوا لِلنَّاسِ حُسْنًا وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ ثُمَّ تَوَلَّيْتُمْ إِلَّا قَلِيلًا مِّنكُمْ وَأَنتُم مُّعْرِضُونَ ﴿٨٣﴾  

83. Na (kumbukeni) Tulipochukua ahadi (fungamano) ya wana wa Israaiyl (Tukawaambia): “Msiabudu isipokuwa Allaah; na muwafanyie wema wazazi wawili, na jamaa wa karibu, na mayatima, na masikini; na semeni na watu kwa uzuri na simamisheni Swalaah, na toeni Zakaah;” kisha mkakengeuka ila wachache miongoni mwenu na hali nyinyi mnapuuza.

وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَكُمْ لَا تَسْفِكُونَ دِمَاءَكُمْ وَلَا تُخْرِجُونَ أَنفُسَكُم مِّن دِيَارِكُمْ ثُمَّ أَقْرَرْتُمْ وَأَنتُمْ تَشْهَدُونَ ﴿٨٤﴾

84. Na (kumbukeni) Tulipochukua ahadi yenu (Tukawaambia): “Msimwage damu zenu, wala msitoe nafsi zenu kutoka miji yenu;” kisha mkakubali nanyi mnashuhudia.

ثُمَّ أَنتُمْ هَـٰؤُلَاءِ تَقْتُلُونَ أَنفُسَكُمْ وَتُخْرِجُونَ فَرِيقًا مِّنكُم مِّن دِيَارِهِمْ تَظَاهَرُونَ عَلَيْهِم بِالْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَإِن يَأْتُوكُمْ أُسَارَىٰ تُفَادُوهُمْ وَهُوَ مُحَرَّمٌ عَلَيْكُمْ إِخْرَاجُهُمْ ۚ أَفَتُؤْمِنُونَ بِبَعْضِ الْكِتَابِ وَتَكْفُرُونَ بِبَعْضٍ ۚ فَمَا جَزَاءُ مَن يَفْعَلُ ذَٰلِكَ مِنكُمْ إِلَّا خِزْيٌ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يُرَدُّونَ إِلَىٰ أَشَدِّ الْعَذَابِ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿٨٥﴾

85. Kisha nyinyi ndio hao mnaua nafsi zenu na mnalitoa kundi miongoni mwenu kutoka miji (majumbani) yao, mnasaidiana dhidi yao kwa dhambi na uadui; na wanapokujieni mateka mnawakomboa na hali hilo limeharamishwa kwenu kuwatoa. Je, mnaamini baadhi ya Kitabu na mnakanusha baadhi yake? Basi hapana jazaa ya anayefanya hayo miongoni mwenu isipokuwa hizaya katika dunia, na Siku ya Qiyaamah watapelekwa kwenye adhabu kali zaidi, na Allaah si Mwenye kughafilika kwa myatendayo.


أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ اشْتَرَوُا الْحَيَاةَ الدُّنْيَا بِالْآخِرَةِ ۖ فَلَا يُخَفَّفُ عَنْهُمُ الْعَذَابُ وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ ﴿٨٦﴾

86. Hao ndio wale ambao wamenunua uhai wa dunia kwa Aakhirah, basi haitopunguzwa kwao adhabu wala hawatanusuriwa.

وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ وَقَفَّيْنَا مِن بَعْدِهِ بِالرُّسُلِ ۖ وَآتَيْنَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ الْبَيِّنَاتِ وَأَيَّدْنَاهُ بِرُوحِ الْقُدُسِ ۗ أَفَكُلَّمَا جَاءَكُمْ رَسُولٌ بِمَا لَا تَهْوَىٰ أَنفُسُكُمُ اسْتَكْبَرْتُمْ فَفَرِيقًا كَذَّبْتُمْ وَفَرِيقًا تَقْتُلُونَ ﴿٨٧﴾

87. Na kwa hakika Tulimpa Muwsaa Kitabu na Tukafuatisha Rasuli  baada yake. Na Tukampa ‘Iysaa mwana wa Maryam hoja bayana na Tukamtia nguvu kwa Roho Takatifu. Je, basi kila anapokujieni Rasuli (enyi wana wa Israaiyl) kwa yale yasiyoyapenda nafsi zenu, mlitakabari; basi kundi (la Rasuli) mlilikadhibisha na kundi (jengine) mnaliua.

وَقَالُوا قُلُوبُنَا غُلْفٌ ۚ بَل لَّعَنَهُمُ اللَّـهُ بِكُفْرِهِمْ فَقَلِيلًا مَّا يُؤْمِنُونَ ﴿٨٨﴾

88. Na wakasema: “Nyoyo zetu zimefunikwa.” Bali Allaah Amewalaani kwa kufuru zao; basi machache tu wanayoyaamini.

 وَلَمَّا جَاءَهُمْ كِتَابٌ مِّنْ عِندِ اللَّـهِ مُصَدِّقٌ لِّمَا مَعَهُمْ وَكَانُوا مِن قَبْلُ يَسْتَفْتِحُونَ عَلَى الَّذِينَ كَفَرُوا فَلَمَّا جَاءَهُم مَّا عَرَفُوا كَفَرُوا بِهِ ۚ فَلَعْنَةُ اللَّـهِ عَلَى الْكَافِرِينَ ﴿٨٩﴾

89. Na kilipowajia Kitabu kutoka kwa Allaah kisadikishacho yale yaliyo pamoja nao, na (japokuwa) kabla ya (hapo) walikuwa wakiomba ushindi dhidi ya wale ambao wamekufuru; basi yalipowajia yale waliyokuwa wakiyatambua waliyakanusha, basi laana ya Allaah juu ya wakanushaji.

 بِئْسَمَا اشْتَرَوْا بِهِ أَنفُسَهُمْ أَن يَكْفُرُوا بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ بَغْيًا أَن يُنَزِّلَ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۖ فَبَاءُوا بِغَضَبٍ عَلَىٰ غَضَبٍ ۚ وَلِلْكَافِرِينَ عَذَابٌ مُّهِينٌ ﴿٩٠﴾

90. Ubaya ulioje wa yale waliyojichumia nafsi zao kwamba wakanushe yale Aliyoyateremsha Allaah kwa ajili ya chuki kwa kuwa Allaah Kateremsha katika fadhila Zake juu ya Amtakae katika waja Wake. Basi wakastahiki ghadhabu juu ya ghadhabu. Na makafiri watapata adhabu ya kudhalilisha.

 وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ آمِنُوا بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ قَالُوا نُؤْمِنُ بِمَا أُنزِلَ عَلَيْنَا وَيَكْفُرُونَ بِمَا وَرَاءَهُ وَهُوَ الْحَقُّ مُصَدِّقًا لِّمَا مَعَهُمْ ۗ قُلْ فَلِمَ تَقْتُلُونَ أَنبِيَاءَ اللَّـهِ مِن قَبْلُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٩١﴾

91. Na wanapoambiwa: “Aminini yale Aliyoyateremsha Allaah”, husema: “Tunaamini yale yaliyoteremshwa kwetu” na wanayakanusha yale yaliyokuja nyuma (baada) yake, na hali ya kuwa hayo (wanayoyakanusha) ni haki yenye kusadikisha yale yaliyo pamoja nao. Sema: “Kwa nini basi mnawaua Manabii wa Allaah toka hapo kabla kama kweli mlikuwa waumini?

 وَلَقَدْ جَاءَكُم مُّوسَىٰ بِالْبَيِّنَاتِ ثُمَّ اتَّخَذْتُمُ الْعِجْلَ مِن بَعْدِهِ وَأَنتُمْ ظَالِمُونَ ﴿٩٢﴾

92. Na kwa hakika alikujieni Muwsaa kwa hoja bayana kisha mkamchukua ndama baada yake na hali ya kuwa nyinyi ni madhalimu.

 وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَكُمْ وَرَفَعْنَا فَوْقَكُمُ الطُّورَ خُذُوا مَا آتَيْنَاكُم بِقُوَّةٍ وَاسْمَعُوا ۖ قَالُوا سَمِعْنَا وَعَصَيْنَا وَأُشْرِبُوا فِي قُلُوبِهِمُ الْعِجْلَ بِكُفْرِهِمْ ۚ قُلْ بِئْسَمَا يَأْمُرُكُم بِهِ إِيمَانُكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٩٣﴾

93. Na (kumbukeni) Tulipochukua ahadi yenu (mtekeleze Tawraat) na Tukaunyanyua juu yenu (mlima) at-Twuwr; (Tukasema): “Chukueni Tuliyokupeni kwa nguvu na sikilizeni”. Wakasema: ”Tumesikia na tumeasi.” Wakanyweshwa katika nyoyo zao (mapenzi ya kumuabudu) ndama kwa kufuru yao. Sema: “Ubaya ulioje inakuamrisheni kwayo imani yenu mkiwa ni waumini”.

 قُلْ إِن كَانَتْ لَكُمُ الدَّارُ الْآخِرَةُ عِندَ اللَّـهِ خَالِصَةً مِّن دُونِ النَّاسِ فَتَمَنَّوُا الْمَوْتَ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٩٤﴾

94. Sema: ”Ikiwa nyumba ya Aakhirah iliyoko kwa Allaah ni makhsusi kwenu pekee pasi na watu wengine; basi tamanini mauti mkiwa ni wakweli.

 وَلَن يَتَمَنَّوْهُ أَبَدًا بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالظَّالِمِينَ ﴿٩٥﴾

95. Na hawatoyatamani abadani (hayo mauti) kutokana na yaliyoyatanguliza mikono yao. Na Allaah ni ‘Aliymun (Mjuzi) wa madhalimu.  

 وَلَتَجِدَنَّهُمْ أَحْرَصَ النَّاسِ عَلَىٰ حَيَاةٍ وَمِنَ الَّذِينَ أَشْرَكُوا ۚ يَوَدُّ أَحَدُهُمْ لَوْ يُعَمَّرُ أَلْفَ سَنَةٍ وَمَا هُوَ بِمُزَحْزِحِهِ مِنَ الْعَذَابِ أَن يُعَمَّرَ ۗ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِمَا يَعْمَلُونَ ﴿٩٦﴾

96. Na kwa yakini utawakuta wao (Mayahudi) ni watu wenye pupa mno kuliko yeyote juu ya uhai na kuliko wale ambao wameshirikisha. Anapenda mmoja wao lau angelipewa umri mrefu wa miaka elfu. Na wala huko hakutamuondoshea adhabu kwa kupewa umri mrefu. Na Allaah ni Baswiyrun (Mwenye kuona) wanayoyatenda.  

قُلْ مَن كَانَ عَدُوًّا لِّجِبْرِيلَ فَإِنَّهُ نَزَّلَهُ عَلَىٰ قَلْبِكَ بِإِذْنِ اللَّـهِ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَهُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ ﴿٩٧﴾

97. Sema: “Yeyote aliyekuwa adui wa Jibriyl, basi hakika yeye ameiteremsha Qur-aan katika moyo wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa idhini ya Allaah inayosadikisha yaliyo kabla yake, na Hidaaya, na bishara kwa Waumini.

 مَن كَانَ عَدُوًّا لِّلَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَرُسُلِهِ وَجِبْرِيلَ وَمِيكَالَ فَإِنَّ اللَّـهَ عَدُوٌّ لِّلْكَافِرِينَ ﴿٩٨﴾

98. Yeyote aliyekuwa adui wa Allaah na Malaika Wake, na Rasuli Wake, na Jibriyl, na Miykaala, basi hakika Allaah ni adui kwa makafiri.

 وَلَقَدْ أَنزَلْنَا إِلَيْكَ آيَاتٍ بَيِّنَاتٍ ۖ وَمَا يَكْفُرُ بِهَا إِلَّا الْفَاسِقُونَ ﴿٩٩﴾

99. Na kwa hakika Tumeteremsha kwako Aayaat bayana, na hawazikanushi isipokuwa mafasiki.

 أَوَكُلَّمَا عَاهَدُوا عَهْدًا نَّبَذَهُ فَرِيقٌ مِّنْهُم ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٠٠﴾

100. Je, ndio kila wanapochukua ahadi kundi miongoni mwao huivunja?  Bali wengi wao hawaamini.

 وَلَمَّا جَاءَهُمْ رَسُولٌ مِّنْ عِندِ اللَّـهِ مُصَدِّقٌ لِّمَا مَعَهُمْ نَبَذَ فَرِيقٌ مِّنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ كِتَابَ اللَّـهِ وَرَاءَ ظُهُورِهِمْ كَأَنَّهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿١٠١﴾ 

101. Na alipowajia Rasuli kutoka kwa Allaah mwenye kusadikisha yale yaliyo pamoja nao kundi miongoni mwa wale ambao wamepewa Kitabu walikitupa Kitabu cha Allaah nyuma ya migongo yao kana kwamba hawajui (yaliyomo humo).

 وَاتَّبَعُوا مَا تَتْلُو الشَّيَاطِينُ عَلَىٰ مُلْكِ سُلَيْمَانَ ۖ وَمَا كَفَرَ سُلَيْمَانُ وَلَـٰكِنَّ الشَّيَاطِينَ كَفَرُوا يُعَلِّمُونَ النَّاسَ السِّحْرَ وَمَا أُنزِلَ عَلَى الْمَلَكَيْنِ بِبَابِلَ هَارُوتَ وَمَارُوتَ ۚ وَمَا يُعَلِّمَانِ مِنْ أَحَدٍ حَتَّىٰ يَقُولَا إِنَّمَا نَحْنُ فِتْنَةٌ فَلَا تَكْفُرْ ۖ فَيَتَعَلَّمُونَ مِنْهُمَا مَا يُفَرِّقُونَ بِهِ بَيْنَ الْمَرْءِ وَزَوْجِهِ ۚ وَمَا هُم بِضَارِّينَ بِهِ مِنْ أَحَدٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ وَيَتَعَلَّمُونَ مَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ ۚ وَلَقَدْ عَلِمُوا لَمَنِ اشْتَرَاهُ مَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِنْ خَلَاقٍ ۚ وَلَبِئْسَ مَا شَرَوْا بِهِ أَنفُسَهُمْ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿١٠٢﴾

102. Na wakafuata yale waliyoyasoma shayaatwiyn juu ya ufalme wa Sulaymaan; na Sulaymaan hakukufuru lakini shayaatwiyn ndio waliokufuru; wanafundisha watu sihiri na yaliyoteremshwa kwa Malaika wawili (katika mji wa) Baabil Haaruwt na Maaruwt. Na (hao Malaika wawili) hawamfundishi yeyote mpaka wamueleze: “Hakika sisi ni mtihani, basi usikufuru (kufanya sihiri).” Basi wakajifunza kutoka kwa hao (Malaika) wawili yenye kupelekea kufarikisha kwayo baina ya mtu na mkewe. Na wao si wenye kumdhuru yeyote kwayo isipokuwa kwa idhini ya Allaah; na wanajifunza yanayowadhuru na wala hayawanufaishi; na kwa hakika walielewa kwamba atakayenunua (atayefanya biashara ya sihiri) hatopata katika Aakhirah fungu lolote, na ni ubaya ulioje walichouzia kwayo nafsi zao, lau wangelikuwa wanaelewa.


 وَلَوْ أَنَّهُمْ آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَمَثُوبَةٌ مِّنْ عِندِ اللَّـهِ خَيْرٌ ۖ لَّوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿١٠٣﴾

103. Na lau wangeliamini na wakawa na taqwa, basi malipo kutoka kwa Allaah yangekuwa ni kheri (kwao), lau wangekuwa wanajua.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقُولُوا رَاعِنَا وَقُولُوا انظُرْنَا وَاسْمَعُوا ۗ وَلِلْكَافِرِينَ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١٠٤﴾

104. Enyi mlioamini, msiseme (kumwambia Mtume wa Allaah) “raa’inaa” lakini semeni “un-dhwur-naa” na sikilizeni. Na makafiri watapata adhabu iumizayo.

 مَّا يَوَدُّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَلَا الْمُشْرِكِينَ أَن يُنَزَّلَ عَلَيْكُم مِّنْ خَيْرٍ مِّن رَّبِّكُمْ ۗ وَاللَّـهُ يَخْتَصُّ بِرَحْمَتِهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ ﴿١٠٥﴾

105. Hawapendi wale ambao wamekufuru miongoni mwa Ahlil-Kitaabi, wala washirikina kwamba iteremshwe kwenu kheri yoyote ile kutoka kwa Mola wenu. Na Allaah Humkhusisha kwa Rahmah Yake Amtakaye. Na Allaah ni Mwenye fadhila kuu.

 مَا نَنسَخْ مِنْ آيَةٍ أَوْ نُنسِهَا نَأْتِ بِخَيْرٍ مِّنْهَا أَوْ مِثْلِهَا ۗ أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٠٦﴾

106. Hatufuti Aayah yoyote au Tunayoisahaulisha ila Tunaleta iliyo bora kuliko hiyo au mfano wake. Je, huelewi kwamba Allaah juu ya kitu ni Qadiyr (Muweza)?

أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۗ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ ﴿١٠٧﴾

107. Je, huelewi kwamba Allaah Ana ufalme wa mbingu na ardhi. Nanyi hamna pasi na Allaah mlinzi (na msaidizi) yeyote wala mwenye kunusuru. 


 أَمْ تُرِيدُونَ أَن تَسْأَلُوا رَسُولَكُمْ كَمَا سُئِلَ مُوسَىٰ مِن قَبْلُ ۗ وَمَن يَتَبَدَّلِ الْكُفْرَ بِالْإِيمَانِ فَقَدْ ضَلَّ سَوَاءَ السَّبِيلِ ﴿١٠٨﴾

108. Au mnataka kumuuliza Rasuli wenu kama alivyoulizwa Muwsaa hapo kabla? Na yeyote atakayebadilisha iymaan kwa kufru, basi kwa yakini amepotea njia iliyo sawa.

 وَدَّ كَثِيرٌ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَوْ يَرُدُّونَكُم مِّن بَعْدِ إِيمَانِكُمْ كُفَّارًا حَسَدًا مِّنْ عِندِ أَنفُسِهِم مِّن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ الْحَقُّ ۖ فَاعْفُوا وَاصْفَحُوا حَتَّىٰ يَأْتِيَ اللَّـهُ بِأَمْرِهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٠٩﴾

109. Wengi katika Ahlil-Kitaab wametamani lau wangelikurudisheni baada ya kuamini kwenu mkawa makafiri (kutokana na) husuda iliyomo katika nafsi zao; baada ya kuwabainikia kwao haki. Basi sameheni na achilieni mbali (puuzeni); mpaka Allaah Alete Amri Yake. Hakika Allaah juu ya kila kitu ni Qadiyr (Muweza).

 وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ ۚ وَمَا تُقَدِّمُوا لِأَنفُسِكُم مِّنْ خَيْرٍ تَجِدُوهُ عِندَ اللَّـهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿١١٠﴾

110. Na simamisheni Swalaah, na toeni Zakaah, na lolote mnalolitanguliza kwa ajili ya nafsi zenu katika kheri mtalikuta kwa Allaah, hakika Allaah kwa myafanyao ni Baswiyr (Mwenye kuona).

 وَقَالُوا لَن يَدْخُلَ الْجَنَّةَ إِلَّا مَن كَانَ هُودًا أَوْ نَصَارَىٰ ۗ تِلْكَ أَمَانِيُّهُمْ ۗ قُلْ هَاتُوا بُرْهَانَكُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿١١١﴾

111. Na walisema: “Hatoingia Jannah isipokuwa aliyekuwa Yahudi au Naswara.” Hilo ni tamanio lao.  Sema: “Leteni ushahidi wenu wa wazi mkiwa ni wakweli.”

بَلَىٰ مَنْ أَسْلَمَ وَجْهَهُ لِلَّـهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ فَلَهُ أَجْرُهُ عِندَ رَبِّهِ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿١١٢﴾

112. Naam! (Hilo ni tamanio lao, bali) Yeyote aliyeusalimisha uso wake kwa Allaah, na ilhali ni mtenda mema basi atapata ujira wake kwa Mola wake, na wala haitokuwa khofu juu yao wala hawatohuzunika.

 وَقَالَتِ الْيَهُودُ لَيْسَتِ النَّصَارَىٰ عَلَىٰ شَيْءٍ وَقَالَتِ النَّصَارَىٰ لَيْسَتِ الْيَهُودُ عَلَىٰ شَيْءٍ وَهُمْ يَتْلُونَ الْكِتَابَ ۗ كَذَٰلِكَ قَالَ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ مِثْلَ قَوْلِهِمْ ۚ فَاللَّـهُ يَحْكُمُ بَيْنَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ ﴿١١٣﴾

113. Na Mayahudi wakasema: “Manaswara hawana lao jambo.” Na Manaswara wakasema: “Mayahudi hawana lao jambo,” na hali wao wanasoma Kitabu. Hivyo hivyo ndivyo walivyosema wale ambao hawaelewi mfano wa kauli yao. Basi Allaah Atawahukumu baina yao Siku ya Qiyaamah katika yale waliyokuwa wakikhitilafiana.

 وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن مَّنَعَ مَسَاجِدَ اللَّـهِ أَن يُذْكَرَ فِيهَا اسْمُهُ وَسَعَىٰ فِي خَرَابِهَا ۚ أُولَـٰئِكَ مَا كَانَ لَهُمْ أَن يَدْخُلُوهَا إِلَّا خَائِفِينَ ۚ لَهُمْ فِي الدُّنْيَا خِزْيٌ وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿١١٤﴾

114. Na ni nani aliye dhalimu zaidi kuliko yule anayezuia Misikiti ya Allaah kutajwa Jina Lake na akajitahidi katika kuiharibu? Hao haitokuwa kuingia kwako humo isipokuwa wakiwa ni wenye khofu; watapata duniani hizaya na Aakhirah watapata adhabu kubwa.

 وَلِلَّـهِ الْمَشْرِقُ وَالْمَغْرِبُ ۚ فَأَيْنَمَا تُوَلُّوا فَثَمَّ وَجْهُ اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿١١٥﴾

115. Na ni (milki) ya Allaah Mashariki na Magharibi; basi popote mnapogeuka kuna Wajhu Allaah. Hakika Allaah ni Waasi’un-‘Aliym (Mwenye wasaa - Mjuzi wa yote daima).

 وَقَالُوا اتَّخَذَ اللَّـهُ وَلَدًا ۗ سُبْحَانَهُ ۖ بَل لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ كُلٌّ لَّهُ قَانِتُونَ ﴿١١٦﴾

116. Na wakasema: “Allaah Amejichukulia waladi.” Subhaanah! (Utakasifu ni Wake!) Bali ni Vyake vilivyomo mbinguni na ardhini, vyote vinamtii.


 بَدِيعُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَإِذَا قَضَىٰ أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿١١٧﴾

117. Mwanzilishi wa mbingu na ardhi. Anapokidhia jambo basi huliambia “Kun” (kuwa!) basi nalo huwa.

وَقَالَ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ لَوْلَا يُكَلِّمُنَا اللَّـهُ أَوْ تَأْتِينَا آيَةٌ ۗ كَذَٰلِكَ قَالَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِم مِّثْلَ قَوْلِهِمْ ۘ تَشَابَهَتْ قُلُوبُهُمْ ۗ قَدْ بَيَّنَّا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يُوقِنُونَ ﴿١١٨﴾ 

118. Na wakasema wale ambao hawajui: “Lau Angetusemesha Allaah au ingetujia Aayah;” kadhalika walisema wale waliokuwa kabla yao mfano wa kauli yao hiyo. Zimeshabihiana nyoyo zao. Kwa yakini Tumekwishabainisha Aayaat kwa watu wenye yakini. 

 إِنَّا أَرْسَلْنَاكَ بِالْحَقِّ بَشِيرًا وَنَذِيرًا ۖ وَلَا تُسْأَلُ عَنْ أَصْحَابِ الْجَحِيمِ ﴿١١٩﴾

119. Hakika Tumekutuma kwa Haki ukiwa mwenye kutoa bishara njema na mwonyaji wala hutaulizwa kuhusu watu wa (Moto wa) Al-Jahiym.

 وَلَن تَرْضَىٰ عَنكَ الْيَهُودُ وَلَا النَّصَارَىٰ حَتَّىٰ تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ ۗ قُلْ إِنَّ هُدَى اللَّـهِ هُوَ الْهُدَىٰ ۗ وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءَهُم بَعْدَ الَّذِي جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ ۙ مَا لَكَ مِنَ اللَّـهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ ﴿١٢٠﴾

120. Na hawatoridhika nawe Mayahudi wala Manaswara mpaka ufuate millah zao. Sema: “Hakika Hidaaya ya Allaah ndio Hidaaya (pekee)”. Na ukifuata matamanio yao baada ya yale ambayo yaliyokujia katika elimu, basi hutopata kutoka kwa Allaah mlinzi yeyote wala mwenye kunusuru.


 الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَتْلُونَهُ حَقَّ تِلَاوَتِهِ أُولَـٰئِكَ يُؤْمِنُونَ بِهِ ۗ وَمَن يَكْفُرْ بِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ ﴿١٢١﴾

121. Wale Tuliowapa Kitabu wanakisoma kwa haki ya kukisoma kwake (ipasavyo); hao ndio wanaokiamini, na atakayekikanusha basi hao ndio waliokhasirika.


يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اذْكُرُوا نِعْمَتِيَ الَّتِي أَنْعَمْتُ عَلَيْكُمْ وَأَنِّي فَضَّلْتُكُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿١٢٢﴾

122. Enyi wana wa Israaiyl! Kumbukeni neema Yangu Niliyokuneemesheni na hakika Mimi Nimekufadhilisheni juu ya walimwengu.

وَاتَّقُوا يَوْمًا لَّا تَجْزِي نَفْسٌ عَن نَّفْسٍ شَيْئًا وَلَا يُقْبَلُ مِنْهَا عَدْلٌ وَلَا تَنفَعُهَا شَفَاعَةٌ وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ ﴿١٢٣﴾

123. Na iogopeni Siku ambayo nafsi haitoifaa nafsi nyingine kwa lolote, wala haitokubaliwa kutoka kwake kikomboleo wala haitamfaa shafaa’ah (uombezi wa aina yoyote ule) wala hawatonusuriwa.

 وَإِذِ ابْتَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ رَبُّهُ بِكَلِمَاتٍ فَأَتَمَّهُنَّ ۖ قَالَ إِنِّي جَاعِلُكَ لِلنَّاسِ إِمَامًا ۖ قَالَ وَمِن ذُرِّيَّتِي ۖ قَالَ لَا يَنَالُ عَهْدِي الظَّالِمِينَ ﴿١٢٤﴾

124. Na (taja) Alipojaribiwa Ibraahiym na Mola wake kwa maneno, naye akazitimiza. (Allaah) Akasema: “Hakika Mimi Nakufanya uwe Imaam (kiongozi) kwa watu.” (Ibraahiym) Akasema: “Na katika kizazi change?” (Allaah) Akasema: “Haiwafikii Ahadi Yangu madhalimu.”

 وَإِذْ جَعَلْنَا الْبَيْتَ مَثَابَةً لِّلنَّاسِ وَأَمْنًا وَاتَّخِذُوا مِن مَّقَامِ إِبْرَاهِيمَ مُصَلًّى ۖ وَعَهِدْنَا إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ أَن طَهِّرَا بَيْتِيَ لِلطَّائِفِينَ وَالْعَاكِفِينَ وَالرُّكَّعِ السُّجُودِ ﴿١٢٥﴾   

125. Na (taja) Tulipoifanya Nyumba kuwa ni mahali pa kurejewa (kuendewa) na watu na (mahali pa) amani, na chukueni kutoka mahali pa kusimama Ibraahiym kuwa ni pahala pa kuswalia. Na Tulichukua ahadi kwa Ibraahiym na Ismaa’iyl kwamba: “Itakaseni Nyumba Yangu kwa wanaotufu na wanaokaa i’tikaaf, na wanaorukuu na kusujudu.”

 وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّ اجْعَلْ هَـٰذَا بَلَدًا آمِنًا وَارْزُقْ أَهْلَهُ مِنَ الثَّمَرَاتِ مَنْ آمَنَ مِنْهُم بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۖ قَالَ وَمَن كَفَرَ فَأُمَتِّعُهُ قَلِيلًا ثُمَّ أَضْطَرُّهُ إِلَىٰ عَذَابِ النَّارِ ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ ﴿١٢٦﴾

126. Na (taja) aliposema Ibraahiym: “Mola wangu Ufanye mji huu kuwa wa amani na Waruzuku watu wake katika matunda atakayemwamini Allaah miongoni mwao na Siku ya Mwisho.” (Allaah) Akasema: “Na atakayekufuru pia Nitamstarehesha kidogo kisha Nitamsukumiza katika adhabu ya Moto, na ni pabaya paliyoje pahala pa kurejea (mwishoni)”.

 وَإِذْ يَرْفَعُ إِبْرَاهِيمُ الْقَوَاعِدَ مِنَ الْبَيْتِ وَإِسْمَاعِيلُ رَبَّنَا تَقَبَّلْ مِنَّا ۖ إِنَّكَ أَنتَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿١٢٧﴾

127. Na (taja) aliponyanyua Ibraahiym na Ismaa’iyl msingi wa Nyumba (al-Ka’abah); (wakaomba): “Mola wetu, Takabali kutoka kwetu, hakika Wewe ni as-Samiy’ul-’Aliym (Mwenye kusikia yote daima - Mjuzi wa yote daima).

 رَبَّنَا وَاجْعَلْنَا مُسْلِمَيْنِ لَكَ وَمِن ذُرِّيَّتِنَا أُمَّةً مُّسْلِمَةً لَّكَ وَأَرِنَا مَنَاسِكَنَا وَتُبْ عَلَيْنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ ﴿١٢٨﴾

128. “Mola wetu, Tujaalie tuwe wenye kujisalimisha Kwako pamoja na kizazi chetu wawe ummah wenye kujisalimisha Kwako na Tuonyeshe manaasik (taratibu za ‘ibaadah) zetu na Pokea tawbah zetu, hakika Wewe ni at-Tawwaabur-Rahiym (Mwingi wa kupokea tawbah - Mwenye kurehemu).  

 رَبَّنَا وَابْعَثْ فِيهِمْ رَسُولًا مِّنْهُمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِكَ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَيُزَكِّيهِمْ ۚ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١٢٩﴾

129. “Mola wetu, Peleka kwao Rasuli miongoni mwao ataewasomea Aayaat Zako na ataewafunza Kitabu na Hikmah na atakayewatakasa. Hakika Wewe ni Al-’Aziyzul-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima - Mwenye hikmah wa yote daima).”

 وَمَن يَرْغَبُ عَن مِّلَّةِ إِبْرَاهِيمَ إِلَّا مَن سَفِهَ نَفْسَهُ ۚ وَلَقَدِ اصْطَفَيْنَاهُ فِي الدُّنْيَا ۖ وَإِنَّهُ فِي الْآخِرَةِ لَمِنَ الصَّالِحِينَ ﴿١٣٠﴾

130. Na nani atakayejitenga na millah ya Ibraahiym isipokuwa anayeitia nafsi yake upumbavu? Na kwa yakini Tumemchagua duniani, naye Aakhirah ni miongoni mwa (waja) wema.


 إِذْ قَالَ لَهُ رَبُّهُ أَسْلِمْ ۖ قَالَ أَسْلَمْتُ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٣١﴾

131. Mola wake Alipomwambia: “Jisalimishe.” (Ibraahiym) Akasema: “Nimejisalimisha kwa Mola wa walimwengu.”

 وَوَصَّىٰ بِهَا إِبْرَاهِيمُ بَنِيهِ وَيَعْقُوبُ يَا بَنِيَّ إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَىٰ لَكُمُ الدِّينَ فَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ ﴿١٣٢﴾

132. Na Ibraahiym akawausia hayo wanawe na (kadhalika) Ya’quwb (akawaambia): “Enyi wanangu! Hakika Allaah Amekuchagulieni nyinyi Dini; basi msife isipokuwa nyinyi ni Waislamu.”

 أَمْ كُنتُمْ شُهَدَاءَ إِذْ حَضَرَ يَعْقُوبَ الْمَوْتُ إِذْ قَالَ لِبَنِيهِ مَا تَعْبُدُونَ مِن بَعْدِي قَالُوا نَعْبُدُ إِلَـٰهَكَ وَإِلَـٰهَ آبَائِكَ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ إِلَـٰهًا وَاحِدًا وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ ﴿١٣٣﴾

133. Je, mlikuwa mashahidi wakati mauti yalipomfikia Ya’quwb alipowaambia wanawe: “Mtaabudu nini baada yangu?” Wakasema: “Tutamwabudu Ilaah wako (Mungu Anayestahiki kuabudiwa kwa haki) na Ilaaha wa baba zako, Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq; Ilaahan-Waahidan (Mungu Mmoja) nasi Kwake tunajisalimisha.”


تِلْكَ أُمَّةٌ قَدْ خَلَتْ ۖ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَلَكُم مَّا كَسَبْتُمْ ۖ وَلَا تُسْأَلُونَ عَمَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٣٤﴾

134. Huo ni ummah kwa hakika umeshapita, una uliyoyachuma nanyi mna mliyoyachuma; na wala hamtoulizwa kuhusu waliyokuwa wakitenda.

 وَقَالُوا كُونُوا هُودًا أَوْ نَصَارَىٰ تَهْتَدُوا ۗ قُلْ بَلْ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۖ وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿١٣٥﴾

135. Na wakasema: “Kuweni Mayahudi au Manaswara mtaongoka.” Sema: (Sisi hatuna haja ya kuwa Mayahudi wala Manaswara kama mnavyotulingania kuwafuata) “Bali millah ya Ibraahiym haniyfaa (aliyejiengua na dini potofu akaelemea Dini ya haki)  na wala hakuwa katika washirikina.”

 قُولُوا آمَنَّا بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْنَا وَمَا أُنزِلَ إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ وَمَا أُوتِيَ مُوسَىٰ وَعِيسَىٰ وَمَا أُوتِيَ النَّبِيُّونَ مِن رَّبِّهِمْ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّنْهُمْ وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ ﴿١٣٦﴾

136. Semeni: “Tumemwamini Allaah na yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwa Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq na Ya’quwb na al-Asbaatw na aliyopewa Muwsaa na ‘Iysaa na waliyopewa Manabii kutoka kwa Mola wao, hatutofautishi baina ya mmoja yeyote miongoni mwao nasi Kwake tunajisalimisha.”

 فَإِنْ آمَنُوا بِمِثْلِ مَا آمَنتُم بِهِ فَقَدِ اهْتَدَوا ۖ وَّإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّمَا هُمْ فِي شِقَاقٍ ۖ فَسَيَكْفِيكَهُمُ اللَّـهُ ۚ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿١٣٧﴾

137. Basi wakiamini kama vile mlivyoyaamini nyinyi (Swahaba), basi kwa hakika watakuwa kweli wameongoka; na wakikengeuka basi hakika wao wamo katika upinzani, basi Allaah Atakutosheleza nao, Naye ni As-Samiy’ul-’Aliym (Mwenye kusikia yote daima - Mjuzi wa yote daima).

 صِبْغَةَ اللَّـهِ ۖ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّـهِ صِبْغَةً ۖ وَنَحْنُ لَهُ عَابِدُونَ ﴿١٣٨﴾

138. (Swib-ghah yetu; Dini yetu ni) Swib-ghata Allaahi (Dini ya Allaah) na Swib-ghah gani yaweza kuwa bora zaidi kuliko Swib-ghah ya Allaah? Na sisi ni wenye kumwabudu Yeye pekee.

قُلْ أَتُحَاجُّونَنَا فِي اللَّـهِ وَهُوَ رَبُّنَا وَرَبُّكُمْ وَلَنَا أَعْمَالُنَا وَلَكُمْ أَعْمَالُكُمْ وَنَحْنُ لَهُ مُخْلِصُونَ ﴿١٣٩﴾

139. Sema: “Je, mnahojiana nasi kuhusu Allaah na hali Yeye ni Mola wetu na Mola wenu; nasi tuna ‘amali zetu nanyi mna ‘amali zenu, na sisi Kwake ni wenye ikhlaas (kwa nia na vitendo).“

 أَمْ تَقُولُونَ إِنَّ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطَ كَانُوا هُودًا أَوْ نَصَارَىٰ ۗ قُلْ أَأَنتُمْ أَعْلَمُ أَمِ اللَّـهُ ۗ وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن كَتَمَ شَهَادَةً عِندَهُ مِنَ اللَّـهِ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿١٤٠﴾

140. Je, mnasema (mnadai) kwamba Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq na Ya’quwb na al-Asbaatw (vizazi) walikuwa Mayahudi au Manaswara? Sema: “Je nyinyi mnajua zaidi au Allaah?” Na ni nani dhalimu zaidi kuliko yule aliyeficha ushahidi alionao kutoka kwa Allaah? Na Allaah si Mwenye kughafilika kwa myatendayo.


تِلْكَ أُمَّةٌ قَدْ خَلَتْ ۖ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَلَكُم مَّا كَسَبْتُمْ ۖ وَلَا تُسْأَلُونَ عَمَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٤١﴾

141. Huo ni ummah kwa hakika umeshapita, una uliyoyachuma nanyi mna mliyoyachuma, na wala hamtoulizwa waliyokuwa wakitenda.
Juzuu: 2
 سَيَقُولُ السُّفَهَاءُ

 سَيَقُولُ السُّفَهَاءُ مِنَ النَّاسِ مَا وَلَّاهُمْ عَن قِبْلَتِهِمُ الَّتِي كَانُوا عَلَيْهَا ۚ قُل لِّلَّـهِ الْمَشْرِقُ وَالْمَغْرِبُ ۚ يَهْدِي مَن يَشَاءُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿١٤٢﴾

142. Watasema masafihi miongoni mwa watu: “Nini kilichowageuza kutoka Qiblah chao ambacho walikuwa wakikielekea!” Sema: “Ni (milki ya) Allaah Mashariki na Magharibi, Anamhidi Amtakaye kuelekea njia iliyonyooka.

وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِّتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا ۗ وَمَا جَعَلْنَا الْقِبْلَةَ الَّتِي كُنتَ عَلَيْهَا إِلَّا لِنَعْلَمَ مَن يَتَّبِعُ الرَّسُولَ مِمَّن يَنقَلِبُ عَلَىٰ عَقِبَيْهِ ۚ وَإِن كَانَتْ لَكَبِيرَةً إِلَّا عَلَى الَّذِينَ هَدَى اللَّـهُ ۗ وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُضِيعَ إِيمَانَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بِالنَّاسِ لَرَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿١٤٣﴾

143. Na ndivyo hivyo Tumekufanyeni ummah wa wastani ili muwe mashahidi juu ya watu na awe Rasuli shahidi juu yenu. Na Hatukukifanya Qiblah ambacho ulikuwa ukikielekea (kuwa ni Qiblah cha kudumu milele) isipokuwa Tupate kumpambanulisha yule anayemfuata Rasuli miongoni mwa mwenye kugeuka akarudi nyuma. Na hakika ilikuwa ni jambo gumu isipokuwa kwa wale ambao Allaah Amewahidi. Na Allaah Hakuwa Mwenye kupoteza iymaan yenu, hakika Allaah kwa watu ni Rauwfur-Rahiym (Mwenye huruma mno - Mwenye kurehemu).

قَدْ نَرَىٰ تَقَلُّبَ وَجْهِكَ فِي السَّمَاءِ ۖ فَلَنُوَلِّيَنَّكَ قِبْلَةً تَرْضَاهَا ۚ فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ ۚ وَحَيْثُ مَا كُنتُمْ فَوَلُّوا وُجُوهَكُمْ شَطْرَهُ ۗ وَإِنَّ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ لَيَعْلَمُونَ أَنَّهُ الْحَقُّ مِن رَّبِّهِمْ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا يَعْمَلُونَ ﴿١٤٤﴾

144. Kwa yakini Tumeona unavyogeuzageuza uso wako mbinguni. Basi Tutakuelekeza Qiblah unachokiridhia. Basi elekeza uso wako upande wa Al-Masjidil-Haraam. Na popote mtakapokuwepo basi elekezeni nyuso zenu upande wake. Na hakika wale ambao wamepewa Kitabu wanaelewa kwamba hivyo ni haki kutoka kwa Mola wao. Na Allaah si Mwenye kughafilika kwa wayatendayo.


وَلَئِنْ أَتَيْتَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ بِكُلِّ آيَةٍ مَّا تَبِعُوا قِبْلَتَكَ ۚ وَمَا أَنتَ بِتَابِعٍ قِبْلَتَهُمْ ۚ وَمَا بَعْضُهُم بِتَابِعٍ قِبْلَةَ بَعْضٍ ۚ وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءَهُم مِّن بَعْدِ مَا جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ ۙ إِنَّكَ إِذًا لَّمِنَ الظَّالِمِينَ ﴿١٤٥﴾

145. Na hata ukiwaletea wale ambao wamepewa Kitabu kila Aayah basi hawatofuata Qiblah chako. Na wewe hutofuata Qiblah chao. Na wala baadhi yao hawatofuata Qiblah cha baadhi ya wengineo. Na kama ukiyafuata matamanio yao baada ya kukufikia katika elimu; hakika hapo utakuwa miongoni mwa madhalimu.


الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَعْرِفُونَهُ كَمَا يَعْرِفُونَ أَبْنَاءَهُمْ ۖ وَإِنَّ فَرِيقًا مِّنْهُمْ لَيَكْتُمُونَ الْحَقَّ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿١٤٦﴾ 

146. Wale ambao Tumewapa Kitabu wanamtambua (Mtume Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kama wanavyowatambua watoto wao; na hakika kundi miongoni mwao wanaficha haki na hali wao wanajua.


الْحَقُّ مِن رَّبِّكَ ۖ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُمْتَرِينَ ﴿١٤٧﴾

147. Haki kutoka kwa Mola wako basi kamwe usiwe miongoni mwa wenye shaka.


وَلِكُلٍّ وِجْهَةٌ هُوَ مُوَلِّيهَا ۖ فَاسْتَبِقُوا الْخَيْرَاتِ ۚ أَيْنَ مَا تَكُونُوا يَأْتِ بِكُمُ اللَّـهُ جَمِيعًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٤٨﴾

148. Na kila (mmoja ana) upande wa kuuelekea. Basi harakieni (shindaneni kwa kutenda) mambo ya kheri. Popote mtakapokuwa Allaah Atakuleteni nyote pamoja; hakika Allaah juu ya kila kitu ni Qadiyr (Muweza).


وَمِنْ حَيْثُ خَرَجْتَ فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ ۖ وَإِنَّهُ لَلْحَقُّ مِن رَّبِّكَ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿١٤٩﴾ 

149. Na popote utokako (wendako) basi elekeza uso wako upande wa Al-Masjidil-Haraam. Na hiyo ni haki kutoka kwa Mola wako. Na Allaah si Mwenye kughafilika kwa muyatendayo.


وَمِنْ حَيْثُ خَرَجْتَ فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ ۚ وَحَيْثُ مَا كُنتُمْ فَوَلُّوا وُجُوهَكُمْ شَطْرَهُ لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَيْكُمْ حُجَّةٌ إِلَّا الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْهُمْ فَلَا تَخْشَوْهُمْ وَاخْشَوْنِي وَلِأُتِمَّ نِعْمَتِي عَلَيْكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ ﴿١٥٠﴾

150. Na popote utokako (wendako) basi elekeza uso wako upande wa Al-Masjidil-Haraam. Na popote mtakapokuwa (Waislamu) basi elekezeni nyuso zenu upande wake, ili watu wasiwe na hoja juu yenu isipokuwa wale ambao wamedhulumu miongoni mwao. Basi msiwaogope bali Niogopeni na ili Nitimize neema Yangu juu yenu na mpate kuongoka.


كَمَا أَرْسَلْنَا فِيكُمْ رَسُولًا مِّنكُمْ يَتْلُو عَلَيْكُمْ آيَاتِنَا وَيُزَكِّيكُمْ وَيُعَلِّمُكُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَيُعَلِّمُكُم مَّا لَمْ تَكُونُوا تَعْلَمُونَ ﴿١٥١﴾

151. Kama Tulivyomtuma kwenu Rasuli anayetokana na nyinyi, anawasomea Aayaat Zetu na anakutakaseni na anakufunzeni Kitabu na Hikmah, na anakufundisheni mambo ambayo hamkuwa mkiyajua.


فَاذْكُرُونِي أَذْكُرْكُمْ وَاشْكُرُوا لِي وَلَا تَكْفُرُونِ ﴿١٥٢﴾  

152. Basi nidhukuruni  na Mimi Nitakukumbukeni; na nishukuruni wala msinikufuru.


 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَعِينُوا بِالصَّبْرِ وَالصَّلَاةِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ مَعَ الصَّابِرِينَ ﴿١٥٣﴾

153. Enyi mlioamini! Tafuteni msaada kwa subira na Swalaah; hakika Allaah Yu pamoja na wanaosubiri.


 وَلَا تَقُولُوا لِمَن يُقْتَلُ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَمْوَاتٌ ۚ بَلْ أَحْيَاءٌ وَلَـٰكِن لَّا تَشْعُرُونَ ﴿١٥٤﴾ 

154. Wala msiseme kwa waliouawa katika njia ya Allaah kuwa ni wafu, bali wahai lakini hamhisi.


وَلَنَبْلُوَنَّكُم بِشَيْءٍ مِّنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِّنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنفُسِ وَالثَّمَرَاتِ ۗ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ ﴿١٥٥﴾

155. Na bila shaka Tutakujaribuni kwa kitu katika khofu na njaa na upungufu wa mali na nafsi na mazao. Na wabashirie wenye kusubiri.


 الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّـهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ ﴿١٥٦﴾

156. Wale ambao unapowafika msiba husema: “Innaa liLLaahi wa Innaa Ilayhi Raaji’uwn” (Hakika sisi ni wa Allaah na hakika sisi Kwake ni wenye kurejea).


أُولَـٰئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَوَاتٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَرَحْمَةٌ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُهْتَدُونَ ﴿١٥٧﴾

157. Hao juu yao zitakuwa Baraka kutoka kwa Mola wao na Rahmah, na hao ndio wenye kuongoka.


إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِن شَعَائِرِ اللَّـهِ ۖ فَمَنْ حَجَّ الْبَيْتَ أَوِ اعْتَمَرَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِ أَن يَطَّوَّفَ بِهِمَا ۚ وَمَن تَطَوَّعَ خَيْرًا فَإِنَّ اللَّـهَ شَاكِرٌ عَلِيمٌ ﴿١٥٨﴾

158. Hakika Swafaa na Mar-wah ni katika alama za (Dini ya) Allaah. Basi yeyote anayehiji kwenye Nyumba au akatekeleza ‘Umrah basi hakuna dhambi kwake kuvizunguka kwayo (vilima viwili hivyo). Na atakayejitolea kufanya kheri basi hakika Allaah ni Shaakirun-‘Aliym (Mwenye kupokea shukurani - Mjuzi wa yote daima).


 إِنَّ الَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَا أَنزَلْنَا مِنَ الْبَيِّنَاتِ وَالْهُدَىٰ مِن بَعْدِ مَا بَيَّنَّاهُ لِلنَّاسِ فِي الْكِتَابِ ۙ أُولَـٰئِكَ يَلْعَنُهُمُ اللَّـهُ وَيَلْعَنُهُمُ اللَّاعِنُونَ ﴿١٥٩﴾

159. Hakika wale ambao wanaficha yale Tuliyoyateremsha katika Hoja zilizo wazi na Hidaaya baada ya kuwa Tumeyabainisha kwa watu katika Kitabu, hao Anawalaani Allaah na wanalaaniwa na kila mwenye kulaani.


إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا وَأَصْلَحُوا وَبَيَّنُوا فَأُولَـٰئِكَ أَتُوبُ عَلَيْهِمْ ۚ وَأَنَا التَّوَّابُ الرَّحِيمُ ﴿١٦٠﴾ 

160. Isipokuwa wale ambao wametubu na wakatengenea na wakabainisha; basi hao Napokea tawbah zao, Na Mimi ni At-Tawwaabur-Rahiym (Mwingi wa kupokea tawbah - Mwenye kurehemu).


 إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَمَاتُوا وَهُمْ كُفَّارٌ أُولَـٰئِكَ عَلَيْهِمْ لَعْنَةُ اللَّـهِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ ﴿١٦١﴾

161. Hakika wale ambao wamekufuru na wakafa hali ya kuwa ni makafiri; hao iko juu yao laana ya Allaah na Malaika na watu wote.


 خَالِدِينَ فِيهَا ۖ لَا يُخَفَّفُ عَنْهُمُ الْعَذَابُ وَلَا هُمْ يُنظَرُونَ ﴿١٦٢﴾

162. Wenye kudumu humo, hawatopunguziwa adhabu na wala wao hawatopewa muhula wa kupumzika.


 وَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ ﴿١٦٣﴾

163. “Na Ilaah wenu (Mungu Anayestahiki kuabudiwa kwa haki) ni Ilaahun-Waahid (Mungu Mmmoja) hapana ilaaha ila Yeye. (Ar-Rahmaanur-Rahiym (Mwingi wa Rahmah - Mwenye kurehemu).”


إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَالْفُلْكِ الَّتِي تَجْرِي فِي الْبَحْرِ بِمَا يَنفَعُ النَّاسَ وَمَا أَنزَلَ اللَّـهُ مِنَ السَّمَاءِ مِن مَّاءٍ فَأَحْيَا بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا وَبَثَّ فِيهَا مِن كُلِّ دَابَّةٍ وَتَصْرِيفِ الرِّيَاحِ وَالسَّحَابِ الْمُسَخَّرِ بَيْنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ ﴿١٦٤﴾

164. Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi na kukhitilafiana usiku na mchana na merikebu zipitazo katika bahari viwafaavyo watu na Aliyoteremsha Allaah kutoka mbinguni katika maji Akahuisha kwayo ardhi baada ya kufa kwake na Akaeneza humo kila aina ya mnyama na mgeuko wa pepo na mawingu yanayotiishwa baina ya mbingu na ardhi ni Ayaat kwa watu wenye akili.


وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللَّـهِ أَندَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّـهِ ۖ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَشَدُّ حُبًّا لِّلَّـهِ ۗ وَلَوْ يَرَى الَّذِينَ ظَلَمُوا إِذْ يَرَوْنَ الْعَذَابَ أَنَّ الْقُوَّةَ لِلَّـهِ جَمِيعًا وَأَنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعَذَابِ ﴿١٦٥﴾

165. Na miongoni mwa watu wako wenye kuchukua asiyekuwa Allaah kuwa ni mungu mshirika (anaelingana na Allaah); wanawapenda kama mapenzi (yapasavyo) ya kumpenda Allaah. Na wale ambao wameamini wana mapenzi zaidi kwa Allaah. Na lau wangelitambua wale ambao wamedhulumu (yatayowakuta) watakapoona adhabu (wataelewa) kwamba Nguvu zote ni za Allaah; na kwamba hakika Allaah ni Mkali wa kuadhibu.


إِذْ تَبَرَّأَ الَّذِينَ اتُّبِعُوا مِنَ الَّذِينَ اتَّبَعُوا وَرَأَوُا الْعَذَابَ وَتَقَطَّعَتْ بِهِمُ الْأَسْبَابُ ﴿١٦٦﴾

166. (Wakumbushe wakati) Wale ambao wamefuatwa watakapowakana wale ambao wamewafuata wakiwa wameshaiona adhabu; na yatawakatikia mafungamano yao.


وَقَالَ الَّذِينَ اتَّبَعُوا لَوْ أَنَّ لَنَا كَرَّةً فَنَتَبَرَّأَ مِنْهُمْ كَمَا تَبَرَّءُوا مِنَّا ۗ كَذَٰلِكَ يُرِيهِمُ اللَّـهُ أَعْمَالَهُمْ حَسَرَاتٍ عَلَيْهِمْ ۖ وَمَا هُم بِخَارِجِينَ مِنَ النَّارِ ﴿١٦٧﴾

167. Na watasema wale ambao wamefuata: “Lau tungekuwa tunamiliki kurudi tungewakana kama walivyotukana.” Hivyo ndivyo Allaah Atakavyowaonyesha ‘amali zao kuwa ni majuto juu yao. Na wala hawatokuwa wenye kutoka Motoni.


 يَا أَيُّهَا النَّاسُ كُلُوا مِمَّا فِي الْأَرْضِ حَلَالًا طَيِّبًا وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ ۚ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ ﴿١٦٨﴾

168. Enyi watu! Kuleni katika vilivyomo ardhini vya halaal, vizuri; na wala msifuate hatua (nyayo) za shaytwaan. Hakika yeye kwenu ni adui bayana.


إِنَّمَا يَأْمُرُكُم بِالسُّوءِ وَالْفَحْشَاءِ وَأَن تَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿١٦٩﴾ 

169. Hakika (hana cha kuamrisha isipokuwa) anakuamrisheni maovu na machafu (na ubakhili) na mseme dhidi ya Allaah msiyoyajua.


وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ اتَّبِعُوا مَا أَنزَلَ اللَّـهُ قَالُوا بَلْ نَتَّبِعُ مَا أَلْفَيْنَا عَلَيْهِ آبَاءَنَا ۗ أَوَلَوْ كَانَ آبَاؤُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ شَيْئًا وَلَا يَهْتَدُونَ ﴿١٧٠﴾

170. Na wanapoambiwa: “Fuateni Aliyoyateremsha Allaah” Husema: “Bali tunafuata tuliyowakuta nayo baba zetu.” Je, japokuwa baba zao walikuwa hawaelewi kitu chochote na wala hawaongoki?


 وَمَثَلُ الَّذِينَ كَفَرُوا كَمَثَلِ الَّذِي يَنْعِقُ بِمَا لَا يَسْمَعُ إِلَّا دُعَاءً وَنِدَاءً ۚ صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لَا يَعْقِلُونَ ﴿١٧١﴾

171. Na mfano wa wale ambao wamekufuru ni kama mfano wa yule ambaye anapiga kelele kwa (yale ambayo hawezi kuyasikia) asiyesikia (hivyo huwa hana alifanyalo) ila wito na sauti tu; viziwi, mabubu, vipofu kwa hiyo hawaelewi.


يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُلُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ وَاشْكُرُوا لِلَّـهِ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ ﴿١٧٢﴾

172. Enyi mlioamini! Kuleni vizuri Tulivyokuruzukuni na mshukuruni Allaah mkiwa mnamwabudu Yeye Pekee.


إِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةَ وَالدَّمَ وَلَحْمَ الْخِنزِيرِ وَمَا أُهِلَّ بِهِ لِغَيْرِ اللَّـهِ ۖ فَمَنِ اضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٧٣﴾

173. Hakika Allaah Amekuharamishieni mzoga na damu na nyama ya nguruwe na kilichotajiwa kwacho katika kuchinjwa kwake asiyekuwa Allaah. Lakini aliyefikwa na dharura bila ya kutamani wala kupindukia mpaka; basi si dhambi juu yake. Hakika Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).


إِنَّ الَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ مِنَ الْكِتَابِ وَيَشْتَرُونَ بِهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۙ أُولَـٰئِكَ مَا يَأْكُلُونَ فِي بُطُونِهِمْ إِلَّا النَّارَ وَلَا يُكَلِّمُهُمُ اللَّـهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلَا يُزَكِّيهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١٧٤﴾

174. Hakika wale ambao wanaficha yale Aliyoyateremsha Allaah katika Kitabu na wakayanunua kwacho thamani ndogo; hao hawali katika matumbo yao isipokuwa moto, na wala Allaah Hatowasemesha Siku ya Qiyaamah na wala Hatowatakasa nao watapata adhabu iumizayo.


 أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ اشْتَرَوُا الضَّلَالَةَ بِالْهُدَىٰ وَالْعَذَابَ بِالْمَغْفِرَةِ ۚ فَمَا أَصْبَرَهُمْ عَلَى النَّارِ ﴿١٧٥﴾

175. Hao ndio wale ambao wamenunua upotofu badala ya Hidaaya na adhabu badala ya maghfirah. Basi kuvumilia gani huko kwao ndani ya Moto?


 ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ نَزَّلَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ ۗ وَإِنَّ الَّذِينَ اخْتَلَفُوا فِي الْكِتَابِ لَفِي شِقَاقٍ بَعِيدٍ ﴿١٧٦﴾

176. Hiyo ni kwa sababu Allaah Amekiteremsha Kitabu kwa haki. Na hakika wale ambao wamekhitilafiana katika Kitabu wamo katika upinzani wa mbali (na haki).


لَّيْسَ الْبِرَّ أَن تُوَلُّوا وُجُوهَكُمْ قِبَلَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ وَلَـٰكِنَّ الْبِرَّ مَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالْكِتَابِ وَالنَّبِيِّينَ وَآتَى الْمَالَ عَلَىٰ حُبِّهِ ذَوِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينَ وَابْنَ السَّبِيلِ وَالسَّائِلِينَ وَفِي الرِّقَابِ وَأَقَامَ الصَّلَاةَ وَآتَى الزَّكَاةَ وَالْمُوفُونَ بِعَهْدِهِمْ إِذَا عَاهَدُوا ۖ وَالصَّابِرِينَ فِي الْبَأْسَاءِ وَالضَّرَّاءِ وَحِينَ الْبَأْسِ ۗ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ صَدَقُوا ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُتَّقُونَ ﴿١٧٧﴾ 

177. Si wema (pekee) kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa Mashariki na Magharibi lakini wema (khasa) ni mwenye kuamini Allaah na Siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii, na akawapa mali juu ya kuipenda kwake jamaa wa karibu na mayatima na masikini na msafiri (aliyeharibikiwa) na waombao (msaada) na katika kukomboa watumwa na akasimamisha Swalaah, na akatoa Zakaah na watimizao ahadi zao wanapoahidi, na wanaosubiri katika shida na dhara na katika vita. Hao ndio ambao wamesadikisha na hao ndio wenye taqwa.


يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِصَاصُ فِي الْقَتْلَى ۖ الْحُرُّ بِالْحُرِّ وَالْعَبْدُ بِالْعَبْدِ وَالْأُنثَىٰ بِالْأُنثَىٰ ۚ فَمَنْ عُفِيَ لَهُ مِنْ أَخِيهِ شَيْءٌ فَاتِّبَاعٌ بِالْمَعْرُوفِ وَأَدَاءٌ إِلَيْهِ بِإِحْسَانٍ ۗ ذَٰلِكَ تَخْفِيفٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَرَحْمَةٌ ۗ فَمَنِ اعْتَدَىٰ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَلَهُ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١٧٨﴾

178. Enyi mlioamini! Mmeandikiwa (Shari’ah ya kulipiza) kisasi[1]  waliouawa. Muungwana kwa muungwana, na mtumwa kwa mtumwa, na mwanamke kwa mwanamke, na anayesamehewa na nduguye kwa lolote basi kufuatilizwa kwake kuwe kwa wema naye alipe kwa ihsani. Hiyo ni takhafifu kutoka kwa Mola wenu na Rahmah. Na atakayeruka mipaka baada ya hapo basi atapata adhabu iumizayo.


 وَلَكُمْ فِي الْقِصَاصِ حَيَاةٌ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿١٧٩﴾

179. Na mtapata katika (kulipiza) kisasi uhai enyi wenye akili mpate kuwa na taqwa.


 كُتِبَ عَلَيْكُمْ إِذَا حَضَرَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ إِن تَرَكَ خَيْرًا الْوَصِيَّةُ لِلْوَالِدَيْنِ وَالْأَقْرَبِينَ بِالْمَعْرُوفِ ۖ حَقًّا عَلَى الْمُتَّقِينَ ﴿١٨٠﴾

180. Mmeandikiwa kuwa anapofikiwa mmoja wenu na mauti kama ameacha mali, kufanya wasia kwa wazazi wawili, na jamaa wa karibu kwa maaruwf (namna inayoeleweka katika shari’ah). Haya ni wajibu kwa wenye taqwa.


فَمَن بَدَّلَهُ بَعْدَ مَا سَمِعَهُ فَإِنَّمَا إِثْمُهُ عَلَى الَّذِينَ يُبَدِّلُونَهُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿١٨١﴾

181. Atakayeubadilisha (huo wasia) baada ya kuusikia; basi hakika dhambi yake ni juu ya wale watakaoubadilisha. Hakika Allaah ni Samiy’un-‘Aliym (Mwenye kusikia yote daima - Mjuzi wa yote daima).


 فَمَنْ خَافَ مِن مُّوصٍ جَنَفًا أَوْ إِثْمًا فَأَصْلَحَ بَيْنَهُمْ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٨٢﴾

182. Basi mwenye kukhofu kwamba muusiaji kakosea (kenda kombo) au kapata dhambi (kwa kufanya makosa kwake makusudi) akatengeneza baina yao; basi haitokuwa dhambi juu yake. Hakika Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).


 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿١٨٣﴾

183. Enyi mlioamini! Mmeandikiwa Swawm kama ilivyoandikwa kwa walio kabla yenu mpate kuwa na taqwa.


 أَيَّامًا مَّعْدُودَاتٍ ۚ فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۚ وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ ۖ فَمَن تَطَوَّعَ خَيْرًا فَهُوَ خَيْرٌ لَّهُ ۚ وَأَن تَصُومُوا خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿١٨٤﴾

184.  (Kufunga kwenyewe ni) Siku za kuhesabika. Basi atakayekuwa mgonjwa miongoni mwenu, au yuko safarini (akafunga baadhi ya siku); basi (akamilishe) idadi (ya siku anazotakiwa kufunga) katika siku nyinginezo. Na wale wasioiweza (Swawm) watoe fidia; kulisha masikini.  Na atakayejitolea kwa jema lolote lile basi ni bora kwake. Na mkifunga ni bora kwenu mkiwa mnajua.


شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ ۚ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ۖ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۗ يُرِيدُ اللَّـهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُوا الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُوا اللَّـهَ عَلَىٰ مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿١٨٥﴾

185. Mwezi wa Ramadhaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan ili iwe Hidaaya kwa watu na hoja bayana za Hidaaya na Al-Furqaan (Upambanuzi). Basi atakayeshuhudia miongoni mwenu mwezi na afunge. Na atakayekuwa mgonjwa au safarini basi (atimize) idadi katika siku nyinginezo. Allaah Anakutakieni mepesi na wala Hakutakieni magumu; ili mkamilishe idadi na ili mumkabbiri Allaah (mseme: Allaahu Akbar) kwa kukuhidini na mpate kushukuru.


وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ ۖ فَلْيَسْتَجِيبُوا لِي وَلْيُؤْمِنُوا بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ ﴿١٨٦﴾

186. Na watakapokuuliza (Ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) waja Wangu kuhusu Mimi, basi Mimi ni Qariyb (Yu karibu daima kwa elimu Yake); Naitikia maombi ya muombaji anaponiomba. Basi waniitikie Mimi na waniamini Mimi, wapate kuongoka.


 أُحِلَّ لَكُمْ لَيْلَةَ الصِّيَامِ الرَّفَثُ إِلَىٰ نِسَائِكُمْ ۚ هُنَّ لِبَاسٌ لَّكُمْ وَأَنتُمْ لِبَاسٌ لَّهُنَّ ۗ عَلِمَ اللَّـهُ أَنَّكُمْ كُنتُمْ تَخْتَانُونَ أَنفُسَكُمْ فَتَابَ عَلَيْكُمْ وَعَفَا عَنكُمْ ۖ فَالْآنَ بَاشِرُوهُنَّ وَابْتَغُوا مَا كَتَبَ اللَّـهُ لَكُمْ ۚ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ۖ ثُمَّ أَتِمُّوا الصِّيَامَ إِلَى اللَّيْلِ ۚ وَلَا تُبَاشِرُوهُنَّ وَأَنتُمْ عَاكِفُونَ فِي الْمَسَاجِدِ ۗ تِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ فَلَا تَقْرَبُوهَا ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ آيَاتِهِ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ ﴿١٨٧﴾

187. Mmehalalishiwa usiku wa Swawm kujamiiana na wake zenu. Wao ni vazi kwenu na nyinyi ni vazi kwao. Allaah Anajua kwamba nyinyi mlikuwa mkizihini nafsi zenu hivyo Akapokea tawbah yenu na Akakusameheni. Basi sasa changanyikeni nao (waingilieni) na tafuteni Aliyokuandikieni Allaah kwenu. Na kuleni na kunyweni mpaka ibainike kwenu weupe (wa Afajiri) kutokana na weusi (wa usiku). Kisha timizeni Swawm mpaka usiku. Na wala msichanganyike nao hali ya kuwa nyinyi wenye kukaa i’tikaaf Misikitini. Hiyo ni mipaka ya Allaah basi msiikaribie. Hivyo ndivyo Allaah Anavyobainisha Aayaat Zake kwa watu wapate kuwa na taqwa.


 وَلَا تَأْكُلُوا أَمْوَالَكُم بَيْنَكُم بِالْبَاطِلِ وَتُدْلُوا بِهَا إِلَى الْحُكَّامِ لِتَأْكُلُوا فَرِيقًا مِّنْ أَمْوَالِ النَّاسِ بِالْإِثْمِ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿١٨٨﴾

188. Na wala msiliane mali zenu kwa ubatilifu na kuzipeleka kwa mahakimu ili mle sehemu katika mali ya watu kwa dhambi nanyi mnajua (kwamba ni haraam).


 يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَهِلَّةِ ۖ قُلْ هِيَ مَوَاقِيتُ لِلنَّاسِ وَالْحَجِّ ۗ وَلَيْسَ الْبِرُّ بِأَن تَأْتُوا الْبُيُوتَ مِن ظُهُورِهَا وَلَـٰكِنَّ الْبِرَّ مَنِ اتَّقَىٰ ۗ وَأْتُوا الْبُيُوتَ مِنْ أَبْوَابِهَا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿١٨٩﴾

189. Wanakuuliza kuhusu miezi (inapoandama). Sema: “Hiyo ni vipimo vya nyakati kwa watu na Hajj.” Na si wema kuingia nyumba kwa nyuma yake, lakini wema ni kuwa na taqwa. Na ingieni nyumba (majumbani) kupitia milango yake. Na mcheni Allaah mpate kufaulu.


وَقَاتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ الَّذِينَ يُقَاتِلُونَكُمْ وَلَا تَعْتَدُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ ﴿١٩٠﴾

190. Na piganeni katika njia ya Allaah (dhidi ya) wale ambao wanaokupigeni, wala msivuke mipaka. Hakika Allaah Hapendi wanaopindukia mipaka.


وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ وَأَخْرِجُوهُم مِّنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ ۚ وَالْفِتْنَةُ أَشَدُّ مِنَ الْقَتْلِ ۚ وَلَا تُقَاتِلُوهُمْ عِندَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ حَتَّىٰ يُقَاتِلُوكُمْ فِيهِ ۖ فَإِن قَاتَلُوكُمْ فَاقْتُلُوهُمْ ۗ كَذَٰلِكَ جَزَاءُ الْكَافِرِينَ ﴿١٩١﴾

191. Na wauweni popote muwakutapo, na watoeni popote walipokutoeni, na fitnah ni mbaya zaidi kuliko kuua. Na wala msipigane nao kwenye Al-Masjidil-Haraam mpaka wakupigeni humo, watakapokupigeni basi (nanyi pia) wapigeni. Namna hivi ndivyo (inavyokuwa) jazaa ya makafiri.


فَإِنِ انتَهَوْا فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٩٢﴾ 

192. Wakikoma, basi Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).


 وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ لِلَّـهِ ۖ فَإِنِ انتَهَوْا فَلَا عُدْوَانَ إِلَّا عَلَى الظَّالِمِينَ ﴿١٩٣﴾

193. Na piganeni nao mpaka kusiweko fitnah (shirki, kufru), na Dini (‘ibaadah zote) iwe kwa ajili ya Allaah Pekee, wakikoma basi kusiweko na uadui ila kwa madhalimu.


 الشَّهْرُ الْحَرَامُ بِالشَّهْرِ الْحَرَامِ وَالْحُرُمَاتُ قِصَاصٌ ۚ فَمَنِ اعْتَدَىٰ عَلَيْكُمْ فَاعْتَدُوا عَلَيْهِ بِمِثْلِ مَا اعْتَدَىٰ عَلَيْكُمْ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ ﴿١٩٤﴾

194. Mwezi mtukufu kwa mwezi mtukufu, na vitakatifu vimewekewa kisasi. Basi atakayekufanyieni uadui, nanyi mfanyieni uadui kwa kadiri alivyokufanyieni uadui. Na mcheni Allaah, na jueni kwamba Allaah Yu Pamoja na wenye taqwa.


 وَأَنفِقُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلَا تُلْقُوا بِأَيْدِيكُمْ إِلَى التَّهْلُكَةِ ۛ وَأَحْسِنُوا ۛ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿١٩٥﴾

195. Na toeni katika njia ya Allaah wala msijitupe kwa mikono yenu katika maangamizi. Na fanyeni ihsaan Hakika Allaah Anapenda watendao wema.


 وَأَتِمُّوا الْحَجَّ وَالْعُمْرَةَ لِلَّـهِ ۚ فَإِنْ أُحْصِرْتُمْ فَمَا اسْتَيْسَرَ مِنَ الْهَدْيِ ۖ وَلَا تَحْلِقُوا رُءُوسَكُمْ حَتَّىٰ يَبْلُغَ الْهَدْيُ مَحِلَّهُ ۚ فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوْ بِهِ أَذًى مِّن رَّأْسِهِ فَفِدْيَةٌ مِّن صِيَامٍ أَوْ صَدَقَةٍ أَوْ نُسُكٍ ۚ فَإِذَا أَمِنتُمْ فَمَن تَمَتَّعَ بِالْعُمْرَةِ إِلَى الْحَجِّ فَمَا اسْتَيْسَرَ مِنَ الْهَدْيِ ۚ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ فِي الْحَجِّ وَسَبْعَةٍ إِذَا رَجَعْتُمْ ۗ تِلْكَ عَشَرَةٌ كَامِلَةٌ ۗ ذَٰلِكَ لِمَن لَّمْ يَكُنْ أَهْلُهُ حَاضِرِي الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿١٩٦﴾

196. Na timizeni Hajj na ‘Umrah kwa ajili ya Allaah. Na kama mkizuilika basi (chinjeni) wanyama walio wepesi kupatikana. Na wala msinyoe vichwa vyenu mpaka mnyama afikie machinjoni pake. Na atakayekuwa miongoni mwenu mgonjwa au ana udhia kichwani mwake; basi atoe fidia kwa kufunga au kutoa sadaka au kuchinja mnyama. Na mtakapopata amani, basi mwenye kujistarehesha kwa kutekeleza ‘Umrah kisha (atekeleze) Hajj, basi achinje mnyama aliye mwepesi. Na asiyepata (mnyama), afunge siku tatu katika Hajj na (siku) saba mtakaporejea. Hizo ni (siku) kumi timilifu. Hayo ni kwa ajili ya yule ambaye watu wake hawaishi karibu na Al-Masjidil-Haraam. Na mcheni Allaah, na jueni kwamba Allaah ni Mkali wa kuakibu.


 الْحَجُّ أَشْهُرٌ مَّعْلُومَاتٌ ۚ فَمَن فَرَضَ فِيهِنَّ الْحَجَّ فَلَا رَفَثَ وَلَا فُسُوقَ وَلَا جِدَالَ فِي الْحَجِّ ۗ وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ يَعْلَمْهُ اللَّـهُ ۗ وَتَزَوَّدُوا فَإِنَّ خَيْرَ الزَّادِ التَّقْوَىٰ ۚ وَاتَّقُونِ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ ﴿١٩٧﴾

197. Hajj ni miezi maalumu. Na atakayekusudia kuhiji, basi asifanye tendo la ndoa wala ufasiki wala mabishano katika Hajj. Na lolote mlifanyalo katika ya kheri Allaah Analijua. Na jitengenezeeni akiba. Na hakika bora ya akiba ni taqwa. Na nicheni Mimi enyi wenye akili!


 لَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَن تَبْتَغُوا فَضْلًا مِّن رَّبِّكُمْ ۚ فَإِذَا أَفَضْتُم مِّنْ عَرَفَاتٍ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ عِندَ الْمَشْعَرِ الْحَرَامِ ۖ وَاذْكُرُوهُ كَمَا هَدَاكُمْ وَإِن كُنتُم مِّن قَبْلِهِ لَمِنَ الضَّالِّينَ ﴿١٩٨﴾ 

198. Hapana dhambi kwenu kutafuta fadhila toka kwa Mola wenu. Basi mtakapomiminika kutoka ‘Arafaat mdhukuruni Allaah kwenye Mash’aril- Haraam (Muzdalifah) na mdhukuruni Yeye kama Alivyokuhidini kwani hakika mlikuwa kabla ya hapo miongoni mwa waliopotea.


 ثُمَّ أَفِيضُوا مِنْ حَيْثُ أَفَاضَ النَّاسُ وَاسْتَغْفِرُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٩٩﴾

199. Kisha miminikeni kutoka pale wamiminikapo watu; na ombeni maghfirah kwa Allaah. Hakika Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).


 فَإِذَا قَضَيْتُم مَّنَاسِكَكُمْ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ كَذِكْرِكُمْ آبَاءَكُمْ أَوْ أَشَدَّ ذِكْرًا ۗ فَمِنَ النَّاسِ مَن يَقُولُ رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا وَمَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِنْ خَلَاقٍ ﴿٢٠٠﴾

200. Mtakapomaliza kutekeleza manaasik zenu (‘ibaadah za Hajj), basi mdhukuruni Allaah kama mnavyowadhukuru baba zenu au (mdhukuruni) dhikri[2] zaidi. Kwani kuna baadhi ya watu wasemao: “Mola wetu Tupe katika dunia;” naye katika Aakhirah hana sehemu yoyote.


 وَمِنْهُم مَّن يَقُولُ رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الْآخِرَةِ حَسَنَةً وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ ﴿٢٠١﴾

201. Na miongoni mwao (wako) wasemao: “Mola wetu Tupe katika dunia mema na katika Aakhirah (pia Tupe) mema na Tukinge na adhabu ya Moto.”


 أُولَـٰئِكَ لَهُمْ نَصِيبٌ مِّمَّا كَسَبُوا ۚ وَاللَّـهُ سَرِيعُ الْحِسَابِ ﴿٢٠٢﴾

202. Hao watapata pato lao kutokana na waliyoyachuma, na Allaah ni Mwepesi wa kuhesabu.


 وَاذْكُرُوا اللَّـهَ فِي أَيَّامٍ مَّعْدُودَاتٍ ۚ فَمَن تَعَجَّلَ فِي يَوْمَيْنِ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ وَمَن تَأَخَّرَ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ ۚ لِمَنِ اتَّقَىٰ ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّكُمْ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ ﴿٢٠٣﴾

203. Na mdhukuruni Allaah katika siku za kuhesabika. Atakayeharakisha (akaondoka Minaa na kurudi Makkah) katika siku mbili, basi hakuna dhambi juu yake; na atakayechelewesha (akabakia Minaa mpaka siku ya mwisho) basi hakuna dhambi juu yake; kwa mwenye kuwa na taqwa. Na mcheni Allaah na jueni kwamba Kwake mtakusanywa.


 وَمِنَ النَّاسِ مَن يُعْجِبُكَ قَوْلُهُ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيُشْهِدُ اللَّـهَ عَلَىٰ مَا فِي قَلْبِهِ وَهُوَ أَلَدُّ الْخِصَامِ ﴿٢٠٤﴾

204. Na katika watu yupo mwenye kukuvutia kauli yake katika uhai wa dunia na humshuhudisha Allaah kwa yale yaliyomo katika moyo wake na hali yeye ndiye khasimu mbaya zaidi.


 وَإِذَا تَوَلَّىٰ سَعَىٰ فِي الْأَرْضِ لِيُفْسِدَ فِيهَا وَيُهْلِكَ الْحَرْثَ وَالنَّسْلَ ۗ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ الْفَسَادَ ﴿٢٠٥﴾ 

205. Na anapotawala hujitahidi (kufanya akitakacho) katika ardhi ili afisidi humo na aangamize mimea na vizazi.  Na Allaah Hapendi ufisadi.


 وَإِذَا قِيلَ لَهُ اتَّقِ اللَّـهَ أَخَذَتْهُ الْعِزَّةُ بِالْإِثْمِ ۚ فَحَسْبُهُ جَهَنَّمُ ۚ وَلَبِئْسَ الْمِهَادُ ﴿٢٠٦﴾

206. Na anapoambiwa: “Muogope Allaah!” Hupandwa na mori kwa (kutenda) dhambi. Basi (Moto wa) Jahannam unamtosheleza na ni pabaya palioje mahali pa kupumzika.


 وَمِنَ النَّاسِ مَن يَشْرِي نَفْسَهُ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ رَءُوفٌ بِالْعِبَادِ ﴿٢٠٧﴾

207. Na katika watu yuko anayeiuza nafsi yake kutafuta Radhi za Allaah. Na Allaah ni Rauwfun (Mwenye huruma mno) kwa waja.


 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ادْخُلُوا فِي السِّلْمِ كَافَّةً وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ ۚ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ ﴿٢٠٨﴾

208. Enyi mlioamini! Ingieni katika Uislamu kikamilifu, na wala msifuate hatua za shaytwaan. Hakika yeye kwenu ni adui wa wazi.


فَإِن زَلَلْتُم مِّن بَعْدِ مَا جَاءَتْكُمُ الْبَيِّنَاتُ فَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٠٩﴾ 

209. Lakini mkiteleza baada ya kukujieni hoja bayana, jueni kwamba hakika Allaah ni ‘Aziyzun-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima - Mwenye hikmah wa yote daima).


 هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن يَأْتِيَهُمُ اللَّـهُ فِي ظُلَلٍ مِّنَ الْغَمَامِ وَالْمَلَائِكَةُ وَقُضِيَ الْأَمْرُ ۚ وَإِلَى اللَّـهِ تُرْجَعُ الْأُمُورُ ﴿٢١٠﴾

210. Je, wanangojea (nini) isipokuwa Allaah Awajie katika vivuli vya mawingu pamoja na Malaika, na itolewe hukumu? Na kwa Allaah hurudishwa mambo.


 سَلْ بَنِي إِسْرَائِيلَ كَمْ آتَيْنَاهُم مِّنْ آيَةٍ بَيِّنَةٍ ۗ وَمَن يُبَدِّلْ نِعْمَةَ اللَّـهِ مِن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُ فَإِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿٢١١﴾

211. Waulize wana wa Israaiyl, ni ngapi Tumewapa katika Aayah   zilizowazi? Na atakayebadilisha neema ya Allaah baada ya kumjia, basi hakika Allaah ni Mkali wa kuakibu.


 زُيِّنَ لِلَّذِينَ كَفَرُوا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا وَيَسْخَرُونَ مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا ۘ وَالَّذِينَ اتَّقَوْا فَوْقَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ وَاللَّـهُ يَرْزُقُ مَن يَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴿٢١٢﴾

212. Wamepambiwa wale waliokufuru uhai wa dunia na wanawakejeli wale ambao wameamini. Na wale ambao wana taqwa watakuwa juu yao Siku ya Qiyaamah. Na Allaah Humruzuku Amtakaye bila ya hesabu.


 كَانَ النَّاسُ أُمَّةً وَاحِدَةً فَبَعَثَ اللَّـهُ النَّبِيِّينَ مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ وَأَنزَلَ مَعَهُمُ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ لِيَحْكُمَ بَيْنَ النَّاسِ فِيمَا اخْتَلَفُوا فِيهِ ۚ وَمَا اخْتَلَفَ فِيهِ إِلَّا الَّذِينَ أُوتُوهُ مِن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَاتُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ ۖ فَهَدَى اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا لِمَا اخْتَلَفُوا فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بِإِذْنِهِ ۗ وَاللَّـهُ يَهْدِي مَن يَشَاءُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٢١٣﴾

213. Watu walikuwa ummah mmoja, kisha Allaah Akatuma Manabii wabashiriaji na waonyaji na Akateremsha pamoja nao Kitabu kwa haki ili kihukumu baina ya watu katika waliyokhitilafiana kwayo. Na hawakukhitilafiana katika hayo isipokuwa wale ambao walipewa hicho (Kitabu) baada ya kuwajia hoja bayana, kwa sababu ya chuki baina yao. Allaah Akawahidi wale ambao wameamini katika (kufuata na kushikamana na) haki katika waliyokhitilafiana, kwa idhini Yake. Na Allaah Humhidi Amtakaye kuelekea njia iliyonyooka.


 أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تَدْخُلُوا الْجَنَّةَ وَلَمَّا يَأْتِكُم مَّثَلُ الَّذِينَ خَلَوْا مِن قَبْلِكُم ۖ مَّسَّتْهُمُ الْبَأْسَاءُ وَالضَّرَّاءُ وَزُلْزِلُوا حَتَّىٰ يَقُولَ الرَّسُولُ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ مَتَىٰ نَصْرُ اللَّـهِ ۗ أَلَا إِنَّ نَصْرَ اللَّـهِ قَرِيبٌ ﴿٢١٤﴾

214. Je, mnadhani kwamba mtaingia Jannah na hali bado haijakufikieni (mitihani) kama ya wale ambao wamepita kabla yenu?  Iliwapata shida na dhara na wakatetemeshwa mpaka akawa Rasuli na wale ambao wameamini pamoja naye wanasema: “Lini itafika nusura ya Allaah?” Tanabahi! Hakika nusura ya Allaah iko karibu.


يَسْأَلُونَكَ مَاذَا يُنفِقُونَ ۖ قُلْ مَا أَنفَقْتُم مِّنْ خَيْرٍ فَلِلْوَالِدَيْنِ وَالْأَقْرَبِينَ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَابْنِ السَّبِيلِ ۗ وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ بِهِ عَلِيمٌ ﴿٢١٥﴾

215. Wanakuuliza nini watoe?  Sema: “Mnachotoa chochote katika kheri basi ni kwa ajili ya wazazi wawili, na jamaa wa karibu, na mayatima, na masikini, na msafiri”.  Na lolote mlifanyalo katika kheri basi hakika Allaah kwa hilo ni ‘Aliym (Mjuzi).


 كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِتَالُ وَهُوَ كُرْهٌ لَّكُمْ ۖ وَعَسَىٰ أَن تَكْرَهُوا شَيْئًا وَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ وَعَسَىٰ أَن تُحِبُّوا شَيْئًا وَهُوَ شَرٌّ لَّكُمْ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿٢١٦﴾

216. Mmeandikiwa kupigana (vita) nako ni chukizo kwenu. Na huenda mkachukia jambo na hali lenyewe ni kheri kwenu. Na huenda mkapenda jambo na hali lenyewe ni la shari kwenu. Na Allaah Anajua na nyinyi hamjui.


  يَسْأَلُونَكَ عَنِ الشَّهْرِ الْحَرَامِ قِتَالٍ فِيهِ ۖ قُلْ قِتَالٌ فِيهِ كَبِيرٌ ۖ وَصَدٌّ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ وَكُفْرٌ بِهِ وَالْمَسْجِدِ الْحَرَامِ وَإِخْرَاجُ أَهْلِهِ مِنْهُ أَكْبَرُ عِندَ اللَّـهِ ۚ وَالْفِتْنَةُ أَكْبَرُ مِنَ الْقَتْلِ ۗ وَلَا يَزَالُونَ يُقَاتِلُونَكُمْ حَتَّىٰ يَرُدُّوكُمْ عَن دِينِكُمْ إِنِ اسْتَطَاعُوا ۚ وَمَن يَرْتَدِدْ مِنكُمْ عَن دِينِهِ فَيَمُتْ وَهُوَ كَافِرٌ فَأُولَـٰئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۖ وَأُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢١٧﴾

217. Wanakuuliza kuhusu miezi mitukufu (je inafaa) kupigana humo. Sema: “Kupigana humo ni (dhambi) kubwa. Na kuzuia (watu kufuata) njia ya Allaah na kumkanusha Yeye na (kuzuia watu wasiende) Al-Masjidil-Haraam na kuwatoa watu wake humo ni (dhambi) kubwa zaidi mbele ya Allaah. Na fitnah ni mbaya zaidi kuliko kuua”. Na wala hawatoacha kukupigeni vita mpaka wakutoeni katika Dini yenu wakiweza. Na atakayeritadi miongoni mwenu kutoka Dini yake, akafariki hali ya kuwa ni mwenye kukanusha, basi hao zimeporomoka ‘amali zao katika dunia na Aakhirah. Na hao ni watu wa Motoni, wao humo ni wenye kudumu.


 إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَاجَرُوا وَجَاهَدُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أُولَـٰئِكَ يَرْجُونَ رَحْمَتَ اللَّـهِ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٢١٨﴾

218. Hakika wale walioamini na wale waliohajiri na wakapigana jihaad katika njia ya Allaah, hao wanataraji Rahmah ya Allaah, na Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).


 يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ ۖ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَإِثْمُهُمَا أَكْبَرُ مِن نَّفْعِهِمَا ۗ وَيَسْأَلُونَكَ مَاذَا يُنفِقُونَ قُلِ الْعَفْوَ ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَتَفَكَّرُونَ ﴿٢١٩﴾

219. Wanakuuliza kuhusu ulevi na kamari. Sema: “Humo (katika viwili vyote) mna dhambi kubwa na (pia mna) manufaa kwa watu. Na dhambi yake (vitu viwili hivyo) ni kubwa kuliko manufaa yake.” Na wanakuuliza nini watoe. Sema: “Al-’Afwa (yaliyokuzidieni).” Hivyo ndivyo Allaah Anavyokubainishieni Aayaat mpate kutafakari.


 فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۗ وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْيَتَامَىٰ ۖ قُلْ إِصْلَاحٌ لَّهُمْ خَيْرٌ ۖ وَإِن تُخَالِطُوهُمْ فَإِخْوَانُكُمْ ۚ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ الْمُفْسِدَ مِنَ الْمُصْلِحِ ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَأَعْنَتَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٢٠﴾

220. Katika dunia na Aakhirah. Na wanakuuliza kuhusu mayatima. Sema: “Kuwatengeneza ni kheri.  Na Allaah Anamjua fisadi na mtengenezaji. Na lau Angetaka Allaah Angelikutieni katika udhia.” Hakika Allaah ni ‘Aziyzun Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima - Mwenye hikmah wa yote daima).


 وَلَا تَنكِحُوا الْمُشْرِكَاتِ حَتَّىٰ يُؤْمِنَّ ۚ وَلَأَمَةٌ مُّؤْمِنَةٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكَةٍ وَلَوْ أَعْجَبَتْكُمْ ۗ وَلَا تُنكِحُوا الْمُشْرِكِينَ حَتَّىٰ يُؤْمِنُوا ۚ وَلَعَبْدٌ مُّؤْمِنٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكٍ وَلَوْ أَعْجَبَكُمْ ۗ أُولَـٰئِكَ يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ ۖ وَاللَّـهُ يَدْعُو إِلَى الْجَنَّةِ وَالْمَغْفِرَةِ بِإِذْنِهِ ۖ وَيُبَيِّنُ آيَاتِهِ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ﴿٢٢١﴾

221. Na wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini. Na mjakazi Muumini ni bora kuliko mshirikina japo akikupendezeni. Na wala msiwaoze wanaume washirikina mpaka waamini. Na mtumwa Muumini ni bora kuliko mshirikina japo akikupendezeni. Hao (washirikina) wanaita katika Moto na Allaah Anaita katika Al-Jannah na maghfirah kwa Idhini Yake. Na Anabainisha Aayaat Zake wapate kukumbuka.


 وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ ۖ قُلْ هُوَ أَذًى فَاعْتَزِلُوا النِّسَاءَ فِي الْمَحِيضِ ۖ وَلَا تَقْرَبُوهُنَّ حَتَّىٰ يَطْهُرْنَ ۖ فَإِذَا تَطَهَّرْنَ فَأْتُوهُنَّ مِنْ حَيْثُ أَمَرَكُمُ اللَّـهُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ ﴿٢٢٢﴾ 

222. Na wanakuuliza kuhusu hedhi. Sema: “Hiyo ni adha (uchafu); basi waepukeni Wanawake (wanapokuwa) katika hedhi. Wala msiwakaribie (kujimai nao) mpaka watwaharike. Watapotwaharika basi waendeeni (waingilieni jimai) kupitia pale Alipokuamrisheni Allaah”. Hakika Allaah Anapenda wenye kutubia na Anapenda wenye kujitwaharisha.


 نِسَاؤُكُمْ حَرْثٌ لَّكُمْ فَأْتُوا حَرْثَكُمْ أَنَّىٰ شِئْتُمْ ۖ وَقَدِّمُوا لِأَنفُسِكُمْ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّكُم مُّلَاقُوهُ ۗ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٢٢٣﴾

223. Wake zenu ni konde kwenu. Basi ziendeeni konde zenu vyovyote mpendavyo. Na tangulizeni kwa ajili ya nafsi zenu. Na mcheni Allaah na jueni kwamba hakika nyinyi ni wenye kukutana Naye. Na wabashirie Waumini.


  وَلَا تَجْعَلُوا اللَّـهَ عُرْضَةً لِّأَيْمَانِكُمْ أَن تَبَرُّوا وَتَتَّقُوا وَتُصْلِحُوا بَيْنَ النَّاسِ ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٢٤﴾

224. Wala msimfanye Allaah kuwa ni kinga kwa viapo vyenu katika kutimiza wajibu na kumcha na kupatanisha baina ya watu. Na Allaah ni Samiy’un-‘Aliym (Mwenye kusikia yote daima - Mjuzi wa yote daima).


 لَّا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّـهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ وَلَـٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا كَسَبَتْ قُلُوبُكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ حَلِيمٌ ﴿٢٢٥﴾

225. Allaah Hatokuchukulieni kwa viapo vyenu vya upuuzi lakini Atakuchukulieni kwa yaliyochuma nyoyo zenu. Na Allaah ni Ghafuwrun-Haliym (Mwingi wa kughufuria - Mpole wa kuwavumilia waja).


 لِّلَّذِينَ يُؤْلُونَ مِن نِّسَائِهِمْ تَرَبُّصُ أَرْبَعَةِ أَشْهُرٍ ۖ فَإِن فَاءُوا فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٢٢٦﴾

226. Kwa wale ambao wameapa kujitenga na wake zao (kutokujamiiana) wangojee miezi minne. Wakirejea; basi hakika Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).


 وَإِنْ عَزَمُوا الطَّلَاقَ فَإِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٢٧﴾

227. Na wakiazimia talaka, basi hakika Allaah ni Samiy’un-‘Aliym (Mwenye kusikia yote daima - Mjuzi wa yote daima).


 وَالْمُطَلَّقَاتُ يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ ثَلَاثَةَ قُرُوءٍ ۚ وَلَا يَحِلُّ لَهُنَّ أَن يَكْتُمْنَ مَا خَلَقَ اللَّـهُ فِي أَرْحَامِهِنَّ إِن كُنَّ يُؤْمِنَّ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ وَبُعُولَتُهُنَّ أَحَقُّ بِرَدِّهِنَّ فِي ذَٰلِكَ إِنْ أَرَادُوا إِصْلَاحًا ۚ وَلَهُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ وَلِلرِّجَالِ عَلَيْهِنَّ دَرَجَةٌ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٢٨﴾

228. Na wanawake waliotalakiwa wangojee kwa nafsi zao (wasiolewe) quruu (twahara au hedhi) tatu. Na wala si halaal kwa hao wanawake kuficha Aliyoumba Allaah katika matumbo yao ikiwa wao ni wenye kumwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Na waume zao wana haki kuwarejea katika muda huo ikiwa wakitaka suluhu. Na hao wanawake wana kama ile (haki) iliyo juu yao kwa ma’aruwf (mujibu wa shari’ah). Na kwa wanaume juu ya hao wanawake wana daraja. Na Allaah ni ‘Aziyzun-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima - Mwenye hikmah wa yote daima).


 الطَّلَاقُ مَرَّتَانِ ۖ فَإِمْسَاكٌ بِمَعْرُوفٍ أَوْ تَسْرِيحٌ بِإِحْسَانٍ ۗ وَلَا يَحِلُّ لَكُمْ أَن تَأْخُذُوا مِمَّا آتَيْتُمُوهُنَّ شَيْئًا إِلَّا أَن يَخَافَا أَلَّا يُقِيمَا حُدُودَ اللَّـهِ ۖ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا يُقِيمَا حُدُودَ اللَّـهِ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا فِيمَا افْتَدَتْ بِهِ ۗ تِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ فَلَا تَعْتَدُوهَا ۚ وَمَن يَتَعَدَّ حُدُودَ اللَّـهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٢٢٩﴾

229. Talaka ni mara mbili. Hivyo kuzuia kwa ma’aruwf au kuachia kwa ihsaan. Wala si halaal kwenu kuchukua chochote katika mlivyowapa hao wanawake, isipokuwa wote wawili (mume na mke) wakikhofu kuwa hawatoweza kusimamisha mipaka ya Allaah. Mtakapokhofu kuwa wote wawili hawatoweza kusimamisha mipaka ya Allaah; basi hakuna dhambi juu yao katika atakachojikombolea kwacho mke. Hiyo ni mipaka ya Allaah basi msiivuke. Na atakayevuka mipaka ya Allaah basi hao ndio madhalimu.


 فَإِن طَلَّقَهَا فَلَا تَحِلُّ لَهُ مِن بَعْدُ حَتَّىٰ تَنكِحَ زَوْجًا غَيْرَهُ ۗ فَإِن طَلَّقَهَا فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا أَن يَتَرَاجَعَا إِن ظَنَّا أَن يُقِيمَا حُدُودَ اللَّـهِ ۗ وَتِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ يُبَيِّنُهَا لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿٢٣٠﴾

230. Na akimtalaki (mara ya tatu) basi hatokuwa halaal kwake baada ya hapo mpaka aolewe na mume mwengine. Akimtalaki (huyo mume mwengine) hapatokuwa dhambi juu yao wawili (mwanamke na mumewe wa kwanza) kurejeana wakidhani kwamba watasimamisha mipaka ya Allaah. Na hiyo ni mipaka ya Allaah Anaibainisha kwa watu wanaojua.


 وَإِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَبَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَأَمْسِكُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ أَوْ سَرِّحُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ ۚ وَلَا تُمْسِكُوهُنَّ ضِرَارًا لِّتَعْتَدُوا ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَقَدْ ظَلَمَ نَفْسَهُ ۚ وَلَا تَتَّخِذُوا آيَاتِ اللَّـهِ هُزُوًا ۚ وَاذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَمَا أَنزَلَ عَلَيْكُم مِّنَ الْكِتَابِ وَالْحِكْمَةِ يَعِظُكُم بِهِ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٢٣١﴾

231. Na mtakapowatalaki wanawake wakafikia muda (wa kukaribia kumaliza eda) zao; basi wazuieni (warejeeni) kwa ma’aruwf (wema) au waacheni (talaka) kwa ma’aruwf (mujibu wa shari’ah). Na wala msiwazuie kuwapa dhara kwa kuvuka mipaka (kuwafanyia uadui). Na atakayefanya hiyvo basi kwa yakini amejidhulumu nafsi yake. Na wala msizifanyie mzaha Aayaat za Allaah. Na kumbukeni neema za Allaah juu yenu na Aliyokuteremshieni katika Kitabu na Hikmah Anakuwaidhini kwayo. Na mcheni Allaah na jueni kwamba Allaah kwa kila kitu ni ‘Aliym (Mjuzi).


 وَإِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَبَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَلَا تَعْضُلُوهُنَّ أَن يَنكِحْنَ أَزْوَاجَهُنَّ إِذَا تَرَاضَوْا بَيْنَهُم بِالْمَعْرُوفِ ۗ ذَٰلِكَ يُوعَظُ بِهِ مَن كَانَ مِنكُمْ يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۗ ذَٰلِكُمْ أَزْكَىٰ لَكُمْ وَأَطْهَرُ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿٢٣٢﴾

232. Na mtakapowatalaki wanawake kisha wakafikia muda wao; basi msiwazuie kuolewa na waume zao (wa awali) ikiwa wameridhiana baina yao kwa ma’aruwf (mujibu wa ada). Hayo anawaidhiwa kwayo yeyote miongoni mwenu mwenye kumwamini Allaah na Siku ya Mwisho.  Hivyo kwenu ni utakaso zaidi na usafi zaidi. Na Allaah Anajua nanyi hamjui.


وَالْوَالِدَاتُ يُرْضِعْنَ أَوْلَادَهُنَّ حَوْلَيْنِ كَامِلَيْنِ ۖ لِمَنْ أَرَادَ أَن يُتِمَّ الرَّضَاعَةَ ۚ وَعَلَى الْمَوْلُودِ لَهُ رِزْقُهُنَّ وَكِسْوَتُهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ لَا تُكَلَّفُ نَفْسٌ إِلَّا وُسْعَهَا ۚ لَا تُضَارَّ وَالِدَةٌ بِوَلَدِهَا وَلَا مَوْلُودٌ لَّهُ بِوَلَدِهِ ۚ وَعَلَى الْوَارِثِ مِثْلُ ذَٰلِكَ ۗ فَإِنْ أَرَادَا فِصَالًا عَن تَرَاضٍ مِّنْهُمَا وَتَشَاوُرٍ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا ۗ وَإِنْ أَرَدتُّمْ أَن تَسْتَرْضِعُوا أَوْلَادَكُمْ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ إِذَا سَلَّمْتُم مَّا آتَيْتُم بِالْمَعْرُوفِ ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٢٣٣﴾  

233. Na wazazi wa kike wanyonyeshe waladi wao miaka miwili kamili, kwa mwenye kutaka kutimiza kunyonyesha. Na ni juu ya mzazi wa kiume kuwapatia chakula chao na nguo kwa ma’aruwf (mujibu wa ada). Hailazimishwi nafsi ila kwa liliwezalo. Asidhuriwe mzazi wa kike kwa ajii ya waladi wake, na wala mzazi wa kiume (pia) kwa ajili ya waladi wake. Na juu ya mrithi mfano wa hivyo. Watakapotaka (wote wawili) kumwachisha (kunyonya) kwa maridhiano baina yao (wawili) na mashauriano basi hapana dhambi juu ya wawili hao. Na mtakapotaka kutafuta wa kuwayonyesha waladi wenu, basi si dhambi kwenu ikiwa mtatoa (kuwalipa) mlichoahidi kwa ma’aruwf. Na mcheni Allaah na jueni kwamba hakika Allaah kwa myatendayo ni Baswiyr (Mwenye kuona).


 وَالَّذِينَ يُتَوَفَّوْنَ مِنكُمْ وَيَذَرُونَ أَزْوَاجًا يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَعَشْرًا ۖ فَإِذَا بَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا فَعَلْنَ فِي أَنفُسِهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿٢٣٤﴾

234. Na wale wanaofishwa miongoni mwenu na wakaacha wake, (hao wake) wangojee nafsi zao miezi minne na siku kumi (eda ya mfiwa). Watakapofikia muda wao, si dhambi kwao katika yale waliyoyafanya katika nafsi zao kwa ma’aruwf. Na Allaah kwa myatendayo ni Khabiyr (Mjuzi wa  vilivyodhahiri na vilivyofichikana).


 وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا عَرَّضْتُم بِهِ مِنْ خِطْبَةِ النِّسَاءِ أَوْ أَكْنَنتُمْ فِي أَنفُسِكُمْ ۚ عَلِمَ اللَّـهُ أَنَّكُمْ سَتَذْكُرُونَهُنَّ وَلَـٰكِن لَّا تُوَاعِدُوهُنَّ سِرًّا إِلَّا أَن تَقُولُوا قَوْلًا مَّعْرُوفًا ۚ وَلَا تَعْزِمُوا عُقْدَةَ النِّكَاحِ حَتَّىٰ يَبْلُغَ الْكِتَابُ أَجَلَهُ ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا فِي أَنفُسِكُمْ فَاحْذَرُوهُ ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ حَلِيمٌ ﴿٢٣٥﴾

235. Wala si dhambi juu yenu katika mliyotolea ishara kwayo ya kuposa wanawake (walio katika eda) au mliyoficha katika nafsi zenu. Allaah Anajua kwamba nyinyi mtawakumbuka lakini msifunge nao ahadi kisiri isipokuwa mseme kauli ma’aruwf (inayoeleweka kawaida). Na wala msiazimie kufunga ndoa mpaka kitabu kifikie mwisho wake (eda ifikie mwisho wake). Na jueni kwamba Allaah Anajua yaliyomo katika nafsi zenu basi tahadharini Naye. Na jueni kwamba hakika Allaah ni Ghafuwrun-Haliym (Mwingi wa kughufuria - Mpole wa kuwavumilia waja).


لَّا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ إِن طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ مَا لَمْ تَمَسُّوهُنَّ أَوْ تَفْرِضُوا لَهُنَّ فَرِيضَةً ۚ وَمَتِّعُوهُنَّ عَلَى الْمُوسِعِ قَدَرُهُ وَعَلَى الْمُقْتِرِ قَدَرُهُ مَتَاعًا بِالْمَعْرُوفِ ۖ حَقًّا عَلَى الْمُحْسِنِينَ ﴿٢٣٦﴾

236. Hakuna dhambi kwenu mkiwatalaki wanawake ambao hamkuwagusa (hamkuwaingilia) au kuwabainishia kwao mahari. Wapeni kiliwazo kwa mwenye wasaa kadiri ya uwezo wake na mwenye dhiki kadiri ya uwezo wake. Maliwaza (kitoka nyumba) kwa ma’aruwf (mujibu wa ada), ni haki kwa watendao wema.


وَإِن طَلَّقْتُمُوهُنَّ مِن قَبْلِ أَن تَمَسُّوهُنَّ وَقَدْ فَرَضْتُمْ لَهُنَّ فَرِيضَةً فَنِصْفُ مَا فَرَضْتُمْ إِلَّا أَن يَعْفُونَ أَوْ يَعْفُوَ الَّذِي بِيَدِهِ عُقْدَةُ النِّكَاحِ ۚ وَأَن تَعْفُوا أَقْرَبُ لِلتَّقْوَىٰ ۚ وَلَا تَنسَوُا الْفَضْلَ بَيْنَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٢٣٧﴾ 

237. Na mkiwatalaki kabla ya kuwagusa (kuwaingilia) na mkawa mmeshawabainishia kwao mahari, basi (wapeni) nusu ya hayo mliyobainisha isipokuwa wakisamehe (wanawake wenyewe) au asamehe yule ambaye fungamano ya ndoa liko mikononi mwake. Na mkisamehe ni ukaribu zaidi ya taqwa. Na wala msisahau fadhila baina yenu. Hakika Allaah kwa myatendayo ni Baswiyr (Mwenye kuona).


 حَافِظُوا عَلَى الصَّلَوَاتِ وَالصَّلَاةِ الْوُسْطَىٰ وَقُومُوا لِلَّـهِ قَانِتِينَ ﴿٢٣٨﴾

238. Shikamaneni na Swalaah na (khasa) Swalaah ya katikati, na simameni mbele ya Allaah katika hali ya utiifu.


 فَإِنْ خِفْتُمْ فَرِجَالًا أَوْ رُكْبَانًا ۖ فَإِذَا أَمِنتُمْ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ كَمَا عَلَّمَكُم مَّا لَمْ تَكُونُوا تَعْلَمُونَ ﴿٢٣٩﴾

239. Mkikhofu (adui basi swalini) hali mnakwenda au mmepanda (kipando). Mtakapokuwa katika amani mdhukuruni Allaah kama Alivyokufunzeni yale mliyokuwa hamuyajui.


 وَالَّذِينَ يُتَوَفَّوْنَ مِنكُمْ وَيَذَرُونَ أَزْوَاجًا وَصِيَّةً لِّأَزْوَاجِهِم مَّتَاعًا إِلَى الْحَوْلِ غَيْرَ إِخْرَاجٍ ۚ فَإِنْ خَرَجْنَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِي مَا فَعَلْنَ فِي أَنفُسِهِنَّ مِن مَّعْرُوفٍ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٤٠﴾

240. Na wale ambao wamefishwa miongoni mwenu wakaacha wake, wawausie kwa ajili ya wake zao matumizi kwa mwaka mmoja bila ya kuwatoa. Watakapotoka wanawake (wenyewe) basi hakuna dhambi juu yenu katika yale waliyofanya katika nafsi zao katika ma’aruwf (yanayokubalika na shari’ah). Na Allaah ni ‘Aziyzun-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima - Mwenye hikmah wa yote daima).


 وَلِلْمُطَلَّقَاتِ مَتَاعٌ بِالْمَعْرُوفِ ۖ حَقًّا عَلَى الْمُتَّقِينَ ﴿٢٤١﴾

241. Na wanawake waliotalakiwa wapewe matumizi kwa ma’aruwf, ni haki juu ya wenye taqwa.  


 كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ ﴿٢٤٢﴾

242. Hivyo ndivyo Allaah Anavyokubainishieni Aayaat Zake mpate kutia akilini.


أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ خَرَجُوا مِن دِيَارِهِمْ وَهُمْ أُلُوفٌ حَذَرَ الْمَوْتِ فَقَالَ لَهُمُ اللَّـهُ مُوتُوا ثُمَّ أَحْيَاهُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَذُو فَضْلٍ عَلَى النَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَشْكُرُونَ ﴿٢٤٣﴾

243. Je, hukuwaona wale ambao walitoka kutoka majumbani mwao nao wakiwa ni maelfu wakikhofu mauti, Allaah Akawaambia: “Kufeni” kisha Akawahuisha? Hakika Allaah ni Mwenye fadhila juu ya watu lakini watu wengi hawashukuru.


وَقَاتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٤٤﴾

244. Na piganeni katika njia ya Allaah, na jueni kwamba Allaah ni Samiy’un-‘Aliym (Mwenye kusikia yote daima - Mjuzi wa yote daima).

Juzuu: 3
تِلْكَ الرُّسُلُ

 تِلْكَ الرُّسُلُ فَضَّلْنَا بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۘ مِّنْهُم مَّن كَلَّمَ اللَّـهُ ۖ وَرَفَعَ بَعْضَهُمْ دَرَجَاتٍ ۚ وَآتَيْنَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ الْبَيِّنَاتِ وَأَيَّدْنَاهُ بِرُوحِ الْقُدُسِ ۗ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا اقْتَتَلَ الَّذِينَ مِن بَعْدِهِم مِّن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَاتُ وَلَـٰكِنِ اخْتَلَفُوا فَمِنْهُم مَّنْ آمَنَ وَمِنْهُم مَّن كَفَرَ ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا اقْتَتَلُوا وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَفْعَلُ مَا يُرِيدُ ﴿٢٥٣﴾

253. Hao ni Rasuli, Tumewafadhilisha baadhi yao juu ya baadhi. Miongoni mwao (yuko) aliyesemeshwa na Allaah, na Akawapandisha baadhi yao vyeo. Na Tukampa ‘Iysaa mwana wa Maryam hoja bayana na Tukamtia nguvu kwa Roho Takatifu. Na lau Angelitaka Allaah wasingelipigana wale ambao (walikuja) baada yao, baada ya kuwajia hoja bayana. Lakini walikhitalifiana, basi miongoni mwao (kuna) walioamini na miongoni mwao waliokufuru. Na lau Angelitaka Allaah wasingelipigana lakini Allaah Anafanya Ayatakayo.

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَنفِقُوا مِمَّا رَزَقْنَاكُم مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِيَ يَوْمٌ لَّا بَيْعٌ فِيهِ وَلَا خُلَّةٌ وَلَا شَفَاعَةٌ ۗ وَالْكَافِرُونَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٢٥٤﴾

254. Enyi mlioamini! Toeni katika Tulivyokuruzukuni kabla haijafika Siku (ambayo) hakutakuweko biashara humo wala urafiki wala shafaa’ah (uombezi wa aina yoyote ule). Na makafiri wao ndio madhalimu.

 اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ ۚ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ ۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ ۚ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۖ وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا ۚ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ ﴿٢٥٥﴾

255. Allaah, hapana ilaaha (mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki) ila Yeye, Al-Hayyul-Qayyuwm (Aliyehai daima, Msimamizi wa kila kitu). Haumchukuwi usingizi wala kulala. Ni Vyake pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Nani huyu ambaye anashufai (anayeombea) mbele Yake bila ya idhini Yake. Anajua yaliyo mbele yao (viumbe) na yaliyo nyuma yao. Wala hawadiriki kitu chochote kile katika Elimu Yake isipokuwa kwa Alitakalo. Imeenea Kursiyy Yake (Kiti) mbingu na ardhi. Wala hakumchoshi kuvihifadhi viwili hivyo. Naye ni Al-‘Aliyyul-‘Adhwiym (Mwenye Uluwa - Mwenye taadhima).


لَا إِكْرَاهَ فِي الدِّينِ ۖ قَد تَّبَيَّنَ الرُّشْدُ مِنَ الْغَيِّ ۚ فَمَن يَكْفُرْ بِالطَّاغُوتِ وَيُؤْمِن بِاللَّـهِ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ لَا انفِصَامَ لَهَا ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٥٦﴾

256. Hapana kulazimisha katika (kuingia) Dini, kwani imekwishabainika kati ya Uongofu na upotofu. Basi atakayemkanusha twaaghuwt (miungu ya uongo) na akamwamini Allaah kwa hakika atakuwa ameshikilia imara kishikilio madhubuti kisichovunjika, na Allaah ni Samiy’un-‘Aliym (Mwenye kusikia yote daima - Mjuzi wa yote daima).

 اللَّـهُ وَلِيُّ الَّذِينَ آمَنُوا يُخْرِجُهُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ ۖ وَالَّذِينَ كَفَرُوا أَوْلِيَاؤُهُمُ الطَّاغُوتُ يُخْرِجُونَهُم مِّنَ النُّورِ إِلَى الظُّلُمَاتِ ۗ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢٥٧﴾

257. Allaah ni Waliyyu wa wale ambao wameamini, Anawatoa kutoka katika viza na kuwaingiza katika Nuru.  Na wale ambao wamekufuru walinzi wao ni twaaghuwt (miungu ya uongo) huwatoa kutoka katika Nuru na kuwaingiza katika viza. Hao ni watu wa Motoni wao humo ni wenye kudumu.

 أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِي حَاجَّ إِبْرَاهِيمَ فِي رَبِّهِ أَنْ آتَاهُ اللَّـهُ الْمُلْكَ إِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّيَ الَّذِي يُحْيِي وَيُمِيتُ قَالَ أَنَا أُحْيِي وَأُمِيتُ ۖ قَالَ إِبْرَاهِيمُ فَإِنَّ اللَّـهَ يَأْتِي بِالشَّمْسِ مِنَ الْمَشْرِقِ فَأْتِ بِهَا مِنَ الْمَغْرِبِ فَبُهِتَ الَّذِي كَفَرَ ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿٢٥٨﴾

258. Je, hukumzingatia yule ambaye alimuhoji Ibraahiym kuhusu Mola wake kwa vile Allaah Alimpa ufalme; aliposema Ibraahiym: “Mola wangu ni Ambaye Anahuisha na Anafisha.” Akasema: “Mimi pia nahuisha na nafisha.” Ibraahiym akasema: “Hakika Allaah Analileta jua (lichomoze) kutoka Mashariki basi wewe lilete kutoka Magharibi.” Akapigwa na butwaa (na kufedheheka) yule aliyekufuru. Na Allaah Haongoi watu madhalimu.

أَوْ كَالَّذِي مَرَّ عَلَىٰ قَرْيَةٍ وَهِيَ خَاوِيَةٌ عَلَىٰ عُرُوشِهَا قَالَ أَنَّىٰ يُحْيِي هَـٰذِهِ اللَّـهُ بَعْدَ مَوْتِهَا ۖ فَأَمَاتَهُ اللَّـهُ مِائَةَ عَامٍ ثُمَّ بَعَثَهُ ۖ قَالَ كَمْ لَبِثْتَ ۖ قَالَ لَبِثْتُ يَوْمًا أَوْ بَعْضَ يَوْمٍ ۖ قَالَ بَل لَّبِثْتَ مِائَةَ عَامٍ فَانظُرْ إِلَىٰ طَعَامِكَ وَشَرَابِكَ لَمْ يَتَسَنَّهْ ۖ وَانظُرْ إِلَىٰ حِمَارِكَ وَلِنَجْعَلَكَ آيَةً لِّلنَّاسِ ۖ وَانظُرْ إِلَى الْعِظَامِ كَيْفَ نُنشِزُهَا ثُمَّ نَكْسُوهَا لَحْمًا ۚ فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُ قَالَ أَعْلَمُ أَنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٥٩﴾

259. Au (hukuzingatia mfano wa) kama yule aliyepita katika kijiji nacho ni kilichoporomoka kabisa juu ya mapaa yake (kuwa gofu); akasema (kwa mshangao): “Vipi Allaah Atahuisha hiki (kijiji) baada ya kufa kwake?” Basi Allaah Alimfisha miaka mia; kisha Akamfufua. Akasema: (kwa kumuuliza) “Umekaa muda gani?” Akasema: “Nimekaa siku (moja) au sehemu ya siku”. (Allaah) Akasema: “Bali umekaa miaka mia; basi kitazame chakula chako na kinywaji chako hakikuharibika. Na mtazame punda wako; na Tutakufanya (uwe) Aayah kwa watu. Na itazame mifupa (ya punda) jinsi Tunavyoinyanyua, kisha Tunaivisha nyama”. Basi ilipombainikia alisema: “Najua kwamba hakika Allaah juu ya kila kitu ni Qadiyr (Muweza).”


 وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّ أَرِنِي كَيْفَ تُحْيِي الْمَوْتَىٰ ۖ قَالَ أَوَلَمْ تُؤْمِن ۖ قَالَ بَلَىٰ وَلَـٰكِن لِّيَطْمَئِنَّ قَلْبِي ۖ قَالَ فَخُذْ أَرْبَعَةً مِّنَ الطَّيْرِ فَصُرْهُنَّ إِلَيْكَ ثُمَّ اجْعَلْ عَلَىٰ كُلِّ جَبَلٍ مِّنْهُنَّ جُزْءًا ثُمَّ ادْعُهُنَّ يَأْتِينَكَ سَعْيًا ۚ وَاعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٦٠﴾ 

260. Na (taja) aliposema Ibraahiym: “Mola wangu nionyeshe vipi Unahuisha wafu?” (Allaah) Akasema: “Je kwani huamini?” Akasema: “La! (Naamini) lakini (kwayo) moyo wangu upate kutulia.” (Allaah) Akasema: “Basi chukua ndege wanne wazoeshe kwako, (kisha uwachinje), kisha weka juu ya kila jabali katika hao (ndege) sehemu yao; kisha waite watakujia mbio (wakiwa wameumbika upya nawe huku unawaona wanavyojiunga viungo vyao kila mmoja); na elewa kwamba hakika Allaah ni ‘Aziyzun-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima - Mwenye hikmah wa yote daima).


مَّثَلُ الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ كَمَثَلِ حَبَّةٍ أَنبَتَتْ سَبْعَ سَنَابِلَ فِي كُلِّ سُنبُلَةٍ مِّائَةُ حَبَّةٍ ۗ وَاللَّـهُ يُضَاعِفُ لِمَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٦١﴾ 

261. Mfano wa wale ambao wanatoa mali zao katika njia ya Allaah ni kama mfano wa punje moja (ya mbegu) iliyotoa mashuke saba, katika kila shuke kuna punje mia. Na Allaah Humzidishia Amtakaye; na Allaah ni Waasi’un-‘Aliym (Mwenye wasaa - Mjuzi wa yote daima).


 الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ثُمَّ لَا يُتْبِعُونَ مَا أَنفَقُوا مَنًّا وَلَا أَذًى ۙ لَّهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٢٦٢﴾

262. Wale ambao wanatoa mali zao katika njia ya Allaah kisha hawafuatishii kwa waliyoyatoa masimbulizi wala udhia watapa ujira wao kwa Mola wao, na wala hakuna khofu juu yao na wala hawatohuzunika.

 قَوْلٌ مَّعْرُوفٌ وَمَغْفِرَةٌ خَيْرٌ مِّن صَدَقَةٍ يَتْبَعُهَا أَذًى ۗ وَاللَّـهُ غَنِيٌّ حَلِيمٌ ﴿٢٦٣﴾

263. Kauli njema na msamaha ni bora kuliko swadaqah inayoifuata udhia. Na Allaah ni Ghaniyyun-Haliym (Mkwasi - Mpole wa kuwavumilia waja).


 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُبْطِلُوا صَدَقَاتِكُم بِالْمَنِّ وَالْأَذَىٰ كَالَّذِي يُنفِقُ مَالَهُ رِئَاءَ النَّاسِ وَلَا يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۖ فَمَثَلُهُ كَمَثَلِ صَفْوَانٍ عَلَيْهِ تُرَابٌ فَأَصَابَهُ وَابِلٌ فَتَرَكَهُ صَلْدًا ۖ لَّا يَقْدِرُونَ عَلَىٰ شَيْءٍ مِّمَّا كَسَبُوا ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ ﴿٢٦٤﴾

264. Enyi mlioamini! Msibatilishe swadaqah zenu kwa masimbulizi na udhia kama yule ambaye anatoa mali yake kwa kujionyesha kwa watu, wala hamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Basi mfano wake ni kama jabali juu yake pana udongo, kisha likapigwa hilo jabali na mvua kubwa ikaliacha tupu. Hawatakuwa na uwezo juu ya lolote katika waliyoyachuma. Na Allaah Haongoi watu makafiri.

  وَمَثَلُ الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمُ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّـهِ وَتَثْبِيتًا مِّنْ أَنفُسِهِمْ كَمَثَلِ جَنَّةٍ بِرَبْوَةٍ أَصَابَهَا وَابِلٌ فَآتَتْ أُكُلَهَا ضِعْفَيْنِ فَإِن لَّمْ يُصِبْهَا وَابِلٌ فَطَلٌّ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٢٦٥﴾

265. Na mfano wa wale ambao wanatoa mali zao kutafuta Radhi za Allaah na kujithibitisha nafsi zao ni kama mfano wa bustani iliyoko pahala paliponyanyuka; ikafikiwa hiyo bustani na mvua kubwa, ikatoa mazao yake maradufu, na hata kama haikufikiwa na mvua kubwa basi mvua ndogo (huitosheleza kutoa mazao). Na Allaah kwa muyatendayo ni Baswiyr (Mwenye kuona).

 أَيَوَدُّ أَحَدُكُمْ أَن تَكُونَ لَهُ جَنَّةٌ مِّن نَّخِيلٍ وَأَعْنَابٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ لَهُ فِيهَا مِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ وَأَصَابَهُ الْكِبَرُ وَلَهُ ذُرِّيَّةٌ ضُعَفَاءُ فَأَصَابَهَا إِعْصَارٌ فِيهِ نَارٌ فَاحْتَرَقَتْ ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَتَفَكَّرُونَ ﴿٢٦٦﴾

266. Je! Anapenda mmoja wenu kuwa na (kumiliki) bustani ya mitende na mizabibu ipitayo chini yake mito; anayo humo kila aina ya matunda; ukamfikia uzee, naye ana kizazi dhaifu; kisha ikapigwa hiyo bustani na kimbunga cha moto kikaiteketeza? Hivyo ndivyo Allaah Anavyobainisha Aayaat kwenu mpate kutafakari.

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَنفِقُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا كَسَبْتُمْ وَمِمَّا أَخْرَجْنَا لَكُم مِّنَ الْأَرْضِ ۖ وَلَا تَيَمَّمُوا الْخَبِيثَ مِنْهُ تُنفِقُونَ وَلَسْتُم بِآخِذِيهِ إِلَّا أَن تُغْمِضُوا فِيهِ ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ حَمِيدٌ ﴿٢٦٧﴾

267. Enyi mlioamini! Toeni katika vizuri mlivyochuma na katika ambayo Tumekutoleeni kutoka katika ardhi. Na wala msikusudie vibaya kutoka humo mkavitoa na hali nyinyi (wenyewe) si wenye kuvichukuwa isipokuwa kuvifumbia macho. Na jueni kwamba hakika Allaah ni Ghaniyyun-Hamiyd (Mkwasi - Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote daima).

 الشَّيْطَانُ يَعِدُكُمُ الْفَقْرَ وَيَأْمُرُكُم بِالْفَحْشَاءِ ۖ وَاللَّـهُ يَعِدُكُم مَّغْفِرَةً مِّنْهُ وَفَضْلًا ۗ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٦٨﴾

268. Shaytwaan anakutishieni ufukara na anakuamrisheni al-fahshaa (ubakhili), na Allaah Anakuahidini maghfirah kutoka Kwake na fadhila. Na Allaah ni Waasi’un-‘Aliym (Mwenye wasaa - Mjuzi wa yote daima).

يُؤْتِي الْحِكْمَةَ مَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُؤْتَ الْحِكْمَةَ فَقَدْ أُوتِيَ خَيْرًا كَثِيرًا ۗ وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٢٦٩﴾  

269. Humpa hikmah Amtakaye. Na anayepewa hikmah basi kwa yakini huwa amepewa kheri nyingi. Na hawakumbuki (na kuwaidhika) isipokuwa wenye akili.

 وَمَا أَنفَقْتُم مِّن نَّفَقَةٍ أَوْ نَذَرْتُم مِّن نَّذْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُهُ ۗ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ ﴿٢٧٠﴾

270. Na chochote mtoacho katika matumizi au mkiwekacho nadhiri katika nadhiri, basi Allaah Anakijua. Na madhalimu hawana wa kuwanusuru.

 إِن تُبْدُوا الصَّدَقَاتِ فَنِعِمَّا هِيَ ۖ وَإِن تُخْفُوهَا وَتُؤْتُوهَا الْفُقَرَاءَ فَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۚ وَيُكَفِّرُ عَنكُم مِّن سَيِّئَاتِكُمْ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿٢٧١﴾

 271. Mkidhihirisha swadaqah basi ni vizuri hivyo, na mkizificha na kuwapa mafakiri, basi hilo ni kheri kwenu. Na Atakufutieni katika maovu yenu. Na Allaah kwa myatendayo ni Khabiyr (Mjuzi wa  vilivyodhahiri na vilivyofichikana)

 لَّيْسَ عَلَيْكَ هُدَاهُمْ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ ۗ وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ فَلِأَنفُسِكُمْ ۚ وَمَا تُنفِقُونَ إِلَّا ابْتِغَاءَ وَجْهِ اللَّـهِ ۚ وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ يُوَفَّ إِلَيْكُمْ وَأَنتُمْ لَا تُظْلَمُونَ ﴿٢٧٢﴾

271. Si juu yako Hidaaya yao, lakini Allaah Humhidi Amtakaye. Na mtoacho chochote katika kheri basi ni kwa ajili ya nafsi zenu. Na hamtoi ila kutaka Wajhi wa Allaah. Na chochote mtoacho katika kheri mtalipwa kamilifu nanyi hamtodhulumiwa.

 لِلْفُقَرَاءِ الَّذِينَ أُحْصِرُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ لَا يَسْتَطِيعُونَ ضَرْبًا فِي الْأَرْضِ يَحْسَبُهُمُ الْجَاهِلُ أَغْنِيَاءَ مِنَ التَّعَفُّفِ تَعْرِفُهُم بِسِيمَاهُمْ لَا يَسْأَلُونَ النَّاسَ إِلْحَافًا ۗ وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ بِهِ عَلِيمٌ ﴿٢٧٣﴾

273. (Swadaqah ni) Kwa ajili ya mafakiri ambao wamezuilika katika njia ya Allaah hawawezi kwenda huku na kule katika ardhi; asiyewajua huwadhania kuwa ni matajiri kutokana na staha, unawatambua kwa alama zao, hawaombi watu kwa ung’ang’anizi. Na chochote mtoacho katika kheri basi Allaah kwacho ni ‘Aliym (Mjuzi).

 الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُم بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ سِرًّا وَعَلَانِيَةً فَلَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٢٧٤﴾

273. Wale ambao wanatoa mali zao usiku na mchana, kwa siri na kwa dhahiri; watapata ujira wao kwa Mola wao, na wala hakuna khofu juu yao na wala wao hawatohuzunika.

الَّذِينَ يَأْكُلُونَ الرِّبَا لَا يَقُومُونَ إِلَّا كَمَا يَقُومُ الَّذِي يَتَخَبَّطُهُ الشَّيْطَانُ مِنَ الْمَسِّ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا إِنَّمَا الْبَيْعُ مِثْلُ الرِّبَا ۗ وَأَحَلَّ اللَّـهُ الْبَيْعَ وَحَرَّمَ الرِّبَا ۚ فَمَن جَاءَهُ مَوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّهِ فَانتَهَىٰ فَلَهُ مَا سَلَفَ وَأَمْرُهُ إِلَى اللَّـهِ ۖ وَمَنْ عَادَ فَأُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢٧٥﴾

275. Wale ambao wanakula ribaa hawatosimama (Siku ya Qiyaamah) ila kama anavyosimama yule aliyezugwa na shaytwaan kwa kuguswa. Hivyo kwa sababu wao wamesema: “Hakika biashara (kuuza na kununua) ni kama ribaa.” Na Allaah Amehalalisha biashara na Ameharamisha ribaa. Basi atakayefikiwa na mawaidha kutoka kwa Mola wake akakoma (kula ribaa); basi ni yake yale yaliyopita, na hukumu yake iko kwa Allaah. Na atakayerudia (ribaa) basi hao ni watu wa Motoni, wao humo ni wenye kudumu.

 يَمْحَقُ اللَّـهُ الرِّبَا وَيُرْبِي الصَّدَقَاتِ ۗ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ كَفَّارٍ أَثِيمٍ ﴿٢٧٦﴾

276. Allaah Huifuta (baraka mali ya) ribaa na Huzibariki swadaqah. Na Allaah Hapendi kila kafiri apapiae madhambi.

 إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ لَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٢٧٧﴾

 277. Hakika wale ambao wameamini na wakatenda mema na wakasimamisha Swalaah na wakatoa Zakaah; watapata ujira kutoka kwa Mola wao na wala hakuna khofu juu yao na wala wao hawatohuzunika.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَذَرُوا مَا بَقِيَ مِنَ الرِّبَا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٢٧٨﴾

 278. Enyi mlioamini! Mcheni Allaah na acheni yaliyobakia katika ribaa ikiwa nyinyi ni Waumini.

 فَإِن لَّمْ تَفْعَلُوا فَأْذَنُوا بِحَرْبٍ مِّنَ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ ۖ وَإِن تُبْتُمْ فَلَكُمْ رُءُوسُ أَمْوَالِكُمْ لَا تَظْلِمُونَ وَلَا تُظْلَمُونَ ﴿٢٧٩﴾

279. Na msipofanya basi tangazeni vita kutoka kwa Allaah na Rasuli Wake. Na mkitubu basi mtapata rasilmali zenu msidhulumu na wala msidhulumiwe.


 وَإِن كَانَ ذُو عُسْرَةٍ فَنَظِرَةٌ إِلَىٰ مَيْسَرَةٍ ۚ وَأَن تَصَدَّقُوا خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٢٨٠﴾

280. Na ikiwa (mdaiwa) ni mwenye hali ngumu, basi (mdai) angoje muda wa kufarijika (anayemdai).  Na mkitoa swadaqah (deni mnalodai) basi ni kheri kwenu mkiwa mnajua.

  وَاتَّقُوا يَوْمًا تُرْجَعُونَ فِيهِ إِلَى اللَّـهِ ۖ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿٢٨١﴾

281. Na iogopeni Siku mtayorejeshwa humo kwa Allaah, kisha kila nafsi italipwa kamilifu iliyoyachuma nao hawatodhulumiwa.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا تَدَايَنتُم بِدَيْنٍ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى فَاكْتُبُوهُ ۚ وَلْيَكْتُب بَّيْنَكُمْ كَاتِبٌ بِالْعَدْلِ ۚ وَلَا يَأْبَ كَاتِبٌ أَن يَكْتُبَ كَمَا عَلَّمَهُ اللَّـهُ ۚ فَلْيَكْتُبْ وَلْيُمْلِلِ الَّذِي عَلَيْهِ الْحَقُّ وَلْيَتَّقِ اللَّـهَ رَبَّهُ وَلَا يَبْخَسْ مِنْهُ شَيْئًا ۚ فَإِن كَانَ الَّذِي عَلَيْهِ الْحَقُّ سَفِيهًا أَوْ ضَعِيفًا أَوْ لَا يَسْتَطِيعُ أَن يُمِلَّ هُوَ فَلْيُمْلِلْ وَلِيُّهُ بِالْعَدْلِ ۚ وَاسْتَشْهِدُوا شَهِيدَيْنِ مِن رِّجَالِكُمْ ۖ فَإِن لَّمْ يَكُونَا رَجُلَيْنِ فَرَجُلٌ وَامْرَأَتَانِ مِمَّن تَرْضَوْنَ مِنَ الشُّهَدَاءِ أَن تَضِلَّ إِحْدَاهُمَا فَتُذَكِّرَ إِحْدَاهُمَا الْأُخْرَىٰ ۚ وَلَا يَأْبَ الشُّهَدَاءُ إِذَا مَا دُعُوا ۚ وَلَا تَسْأَمُوا أَن تَكْتُبُوهُ صَغِيرًا أَوْ كَبِيرًا إِلَىٰ أَجَلِهِ ۚ ذَٰلِكُمْ أَقْسَطُ عِندَ اللَّـهِ وَأَقْوَمُ لِلشَّهَادَةِ وَأَدْنَىٰ أَلَّا تَرْتَابُوا ۖ إِلَّا أَن تَكُونَ تِجَارَةً حَاضِرَةً تُدِيرُونَهَا بَيْنَكُمْ فَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَلَّا تَكْتُبُوهَا ۗ وَأَشْهِدُوا إِذَا تَبَايَعْتُمْ ۚ وَلَا يُضَارَّ كَاتِبٌ وَلَا شَهِيدٌ ۚ وَإِن تَفْعَلُوا فَإِنَّهُ فُسُوقٌ بِكُمْ ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ وَيُعَلِّمُكُمُ اللَّـهُ ۗ وَاللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٢٨٢﴾ 

282. Enyi mlioamini! Mtakapokopeshana deni kwa muda maalumu basi liandikeni. Na aandike baina yenu mwandishi kwa uadilifu. Na wala asikatae mwandishi kuandika kama Allaah Alivyomfunza. Basi aandike na atamke (maneno yanayoandikwa) yule ambaye ana haki (mdai) na amuogope Allaah Mola wake, na wala asipunguze humo kitu chochote. Basi ikiwa yule ambaye ana haki amepumbaa (hajakomaa kiakili) au dhaifu (mnyonge), au hawezi kuandikisha mwenyewe, basi aandikishe msimamizi wake kwa uadilifu. Na mshuhudishe mashahidi wawili wanaume miongoni mwenu. Na ikiwa hakuna wanaume wawili, basi mwanamume mmoja na wanawake wawili katika wale mnaowaridhia miongoni mwa mashahidi, ili kama mmoja wao (hao wanawake wawili) akipotea, basi mmoja wao atamkumbusha mwengine. Na mashahidi wasikatae watapoitwa. Na wala msichukie kuliandika (deni likiwa) dogo au kubwa mpaka muda wake. Hivyo kwenu ndiyo aqswatw (uadilifu upasavyo) mbele ya Allaah na ndio imara (unyoofu) zaidi kwa ushahidi; na ni karibu zaidi ili msiwe na shaka; isipokuwa itakapokuwa biashara taslimu (mkono-kwa-mkono) mnayoiendesha baina yenu, basi si dhambi kwenu msipoiandika. Na shuhudisheni mnapouziana. Na wala asidhuriwe mwandishi wala shahidi; na mkifanya basi hakika huo ni ufasiki kwenu. Na mcheni Allaah, na Allaah Anakufunzeni, na Allaah kwa kila kitu ni ‘Aliym (Mjuzi).

 وَإِن كُنتُمْ عَلَىٰ سَفَرٍ وَلَمْ تَجِدُوا كَاتِبًا فَرِهَانٌ مَّقْبُوضَةٌ ۖ فَإِنْ أَمِنَ بَعْضُكُم بَعْضًا فَلْيُؤَدِّ الَّذِي اؤْتُمِنَ أَمَانَتَهُ وَلْيَتَّقِ اللَّـهَ رَبَّهُ ۗ وَلَا تَكْتُمُوا الشَّهَادَةَ ۚ وَمَن يَكْتُمْهَا فَإِنَّهُ آثِمٌ قَلْبُهُ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌ ﴿٢٨٣﴾

283. Na mkiwa safarini na hamkumpata mwandishi, basi (mdai) akabidhiwe rahani. Na ikiwa mmoja wenu amewekewa amana na mwengine, basi airudishe yule ambaye ameaminiwa amana ya mwenzake; na amche Allaah Mola wake; na wala msifiche ushahidi; na mwenye kuuficha basi hakika moyo wake ni wenye kutenda dhambi. Na Allaah kwa mnayoyatenda ni ‘Aliym (Mjuzi).

لِّلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَإِن تُبْدُوا مَا فِي أَنفُسِكُمْ أَوْ تُخْفُوهُ يُحَاسِبْكُم بِهِ اللَّـهُ ۖ فَيَغْفِرُ لِمَن يَشَاءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٨٤﴾

 284. Ni vya Allaah Pekee vyote viliomo mbinguni na viliomo ardhini. Na mkidhihirisha yale yaliyomo ndani ya nafsi zenu au mkiyaficha; basi Allaah Atakuhesabuni kwayo. Humghufuria Amtakaye na Humuadhibu Amtakaye. Na Allaah juu ya kila kitu ni Qadiyr (Muweza).

آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مِن رَّبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ ۚ كُلٌّ آمَنَ بِاللَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّن رُّسُلِهِ ۚ وَقَالُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۖ غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ ﴿٢٨٥﴾

 285. Rasuli ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola wake na Waumini (pia wameamini). Wote wamemwamini Allaah, na Malaika Wake, na Vitabu Vyake, na Rasuli Wake. (Nao husema): “Hatutafautishi baina ya yeyote kati ya Rasuli Wake”. Na wakasema:  “Tumesikia na tumetii, tunakuomba maghfirah Mola wetu na Kwako ni marejeo (ya mwisho).”

 لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۚ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا اكْتَسَبَتْ ۗ رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تُحَمِّلْنَا مَا لَا طَاقَةَ لَنَا بِهِ ۖ وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا ۚ أَنتَ مَوْلَانَا فَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ ﴿٢٨٦﴾  

286. Allaah Hakalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya uwezo wake. Itapata iliyoyachuma, na ni dhidi yake iliyojichumia. “Mola wetu Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Mola wetu Usitubebeshe mzigo kama Ulivyoubebesha juu ya wale ambao waliokuwa kabla yetu. Mola wetu Usitutwike tusiyoyaweza, na Tusamehe, na Tughufurie na Turehemu, Wewe ni Mawlaa wetu, basi Tunusuru dhidi ya watu makafiri.

مَّن ذَا الَّذِي يُقْرِضُ اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا فَيُضَاعِفَهُ لَهُ أَضْعَافًا كَثِيرَةً ۚ وَاللَّـهُ يَقْبِضُ وَيَبْسُطُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٢٤٥﴾

245. Ni nani atakayemkopesha Allaah mkopo mzuri kisha (Allaah) Amzidishie mzidisho mwingi. Na Allaah Anakunja na Anakunjua, na Kwake mtarejeshwa.


 أَلَمْ تَرَ إِلَى الْمَلَإِ مِن بَنِي إِسْرَائِيلَ مِن بَعْدِ مُوسَىٰ إِذْ قَالُوا لِنَبِيٍّ لَّهُمُ ابْعَثْ لَنَا مَلِكًا نُّقَاتِلْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۖ قَالَ هَلْ عَسَيْتُمْ إِن كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِتَالُ أَلَّا تُقَاتِلُوا ۖ قَالُوا وَمَا لَنَا أَلَّا نُقَاتِلَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَقَدْ أُخْرِجْنَا مِن دِيَارِنَا وَأَبْنَائِنَا ۖ فَلَمَّا كُتِبَ عَلَيْهِمُ الْقِتَالُ تَوَلَّوْا إِلَّا قَلِيلًا مِّنْهُمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالظَّالِمِينَ ﴿٢٤٦﴾

246. Je, hukuwazingatia wakuu katika wana wa Israaiyl baada ya Muwsaa walipomwambia Nabii kwao: “Tutumie mfalme tupigane katika njia ya Allaah.” (Nabii) Akasema: “Je, huenda mkaandikiwa kupigana kisha msipigane?”  Wakasema: “Tuna nini hata tusipigane katika njia ya Allaah na hali tumekwishatolewa kutoka majumbani mwetu na watoto wetu?” Walipoandikiwa kupigana juu yao walikengeuka isipokuwa wachache miongoni mwao. Na Allaah ni ‘Aliym (Mjuzi) wa madhalimu.


 وَقَالَ لَهُمْ نَبِيُّهُمْ إِنَّ اللَّـهَ قَدْ بَعَثَ لَكُمْ طَالُوتَ مَلِكًا ۚ قَالُوا أَنَّىٰ يَكُونُ لَهُ الْمُلْكُ عَلَيْنَا وَنَحْنُ أَحَقُّ بِالْمُلْكِ مِنْهُ وَلَمْ يُؤْتَ سَعَةً مِّنَ الْمَالِ ۚ قَالَ إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَاهُ عَلَيْكُمْ وَزَادَهُ بَسْطَةً فِي الْعِلْمِ وَالْجِسْمِ ۖ وَاللَّـهُ يُؤْتِي مُلْكَهُ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٤٧﴾ 

247. Na Nabii wao akawaambia: “Hakika Allaah Amekutumieni Twaaluwt kuwa ni mfalme”.  Wakasema: “Vipi yeye atakuwa na ufalme juu yetu, na hali sisi tuna haki zaidi ya ufalme kuliko yeye, na wala hakupewa wasaa katika mali?” (Nabii) Akasema: “Hakika Allaah Amemchagua juu yenu na Akamuongezea ukunjufu katika elimu na mwili, na Allaah Humpa Amtakaye ufalme Wake”. Na Allaah ni Waasi’un-‘Aliym (Mwenye wasaa - Mjuzi wa yote daima).


 وَقَالَ لَهُمْ نَبِيُّهُمْ إِنَّ آيَةَ مُلْكِهِ أَن يَأْتِيَكُمُ التَّابُوتُ فِيهِ سَكِينَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَبَقِيَّةٌ مِّمَّا تَرَكَ آلُ مُوسَىٰ وَآلُ هَارُونَ تَحْمِلُهُ الْمَلَائِكَةُ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٢٤٨﴾

248. Na Nabii wao akawaambia: “Hakika ishara ya ufalme wake ni kwamba litakujieni sanduku ndani yake mna sakiynah (kituliza nyoyo) kutoka Mola wenu na mabaki katika yale waliyoacha watu wa Muwsaa na watu wa Haaruwn, (sanduku hilo) watalibeba Malaika.” Hakika katika hayo mna Aayah kwenu mkiwa ni Waumini.


فَلَمَّا فَصَلَ طَالُوتُ بِالْجُنُودِ قَالَ إِنَّ اللَّـهَ مُبْتَلِيكُم بِنَهَرٍ فَمَن شَرِبَ مِنْهُ فَلَيْسَ مِنِّي وَمَن لَّمْ يَطْعَمْهُ فَإِنَّهُ مِنِّي إِلَّا مَنِ اغْتَرَفَ غُرْفَةً بِيَدِهِ ۚ فَشَرِبُوا مِنْهُ إِلَّا قَلِيلًا مِّنْهُمْ ۚ فَلَمَّا جَاوَزَهُ هُوَ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ قَالُوا لَا طَاقَةَ لَنَا الْيَوْمَ بِجَالُوتَ وَجُنُودِهِ ۚ قَالَ الَّذِينَ يَظُنُّونَ أَنَّهُم مُّلَاقُو اللَّـهِ كَم مِّن فِئَةٍ قَلِيلَةٍ غَلَبَتْ فِئَةً كَثِيرَةً بِإِذْنِ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ مَعَ الصَّابِرِينَ ﴿٢٤٩﴾

249. Alipoondoka Twaaluwt na jeshi akasema: “Hakika Allaah Atakujaribuni kwa mto; atakayekunywa humo, hatokuwa pamoja nami; na asiyekula hakika huyu yu pamoja nami, isipokuwa atakayeteka mteko kwa mkono wake.” Basi wakanywa kutoka humo isipokuwa wachache miongoni mwao. Alipouvuka yeye na wale ambao wameamini pamoja naye; wakasema: “Leo hatuna nguvu kabisa dhidi ya Jaaluwt na jeshi lake.” Wakasema wale ambao wana yakini kwamba wao ni wenye kukutana na Allaah: “Makundi mangapi machache yameshinda makundi mengi kwa idhini ya Allaah? Na Allaah Yu pamoja na wenye kusubiri.”


وَلَمَّا بَرَزُوا لِجَالُوتَ وَجُنُودِهِ قَالُوا رَبَّنَا أَفْرِغْ عَلَيْنَا صَبْرًا وَثَبِّتْ أَقْدَامَنَا وَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ ﴿٢٥٠﴾

250. Na walipojitokeza kupambana na Jaaluwt na jeshi lake wakasema:  “Mola wetu Tumiminie subira na ithibitishe miguu yetu na Tunusuru dhidi ya watu makafiri.


 فَهَزَمُوهُم بِإِذْنِ اللَّـهِ وَقَتَلَ دَاوُودُ جَالُوتَ وَآتَاهُ اللَّـهُ الْمُلْكَ وَالْحِكْمَةَ وَعَلَّمَهُ مِمَّا يَشَاءُ ۗ وَلَوْلَا دَفْعُ اللَّـهِ النَّاسَ بَعْضَهُم بِبَعْضٍ لَّفَسَدَتِ الْأَرْضُ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ ذُو فَضْلٍ عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿٢٥١﴾

 251. Wakawashinda kwa idhini ya Allaah na Daawuwd akamuua Jaaluwt; na Allaah Akampa (Daawuwd) ufalme na hikmah, na Akamfunza katika Aliyoyataka. Na lau Allaah Asingelizuia watu baadhi yao kwa wengine, basi ingelifisidika ardhi lakini Allaah ni Mwenye fadhila juu ya  walimwengu.


 تِلْكَ آيَاتُ اللَّـهِ نَتْلُوهَا عَلَيْكَ بِالْحَقِّ ۚ وَإِنَّكَ لَمِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿٢٥٢﴾

252. Hizo ni Aayaat za Allaah Tunakusomea (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa haki. Na hakika wewe ni miongoni mwa waliotumwa.

1 comment:

Anonymous said...

Allah akulipe kila la kheri