Anajitegeme Mwenyewe, Anachangia Katika Futari, Je Anawajibika Kutoa Zakaatul-Fitwr?
SWALI:
salam alaykum.
Swali
langu ni kwamba. Mimi nataka kutoa zaka ni msichana ninae jitegemea
lakini nimekua nafturu kwa ndugu tofauti mwezi mzima. Na pia huko ninako
enda kufuturu nachanigia kitu katika ftar. Je zakaah yangu niitoe vipi?
Waaleykum saam.
JIBU:
Sifa
zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote,
Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu
'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum)
na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Kufuturu kwa watu au kuchangia futari haihusiani na hukmu ya kutoa Zakaatul-Fitwr kwani hikma ya kutoa Zakaatul-Fitwr ni kuitwaharisha
Swawm ya mwenye kufunga kutokana na maneno maovu, machafu ambayo
ameyatamka. Vile vile ili kuwapatia masikini nao chakula kizuri siku ya
'Iyd nao wafurahi. Dalili ifuatayo ni uthibitisho:
عَنْ ابْنِ عَبَّاس ٍقَالَ
فَرَضَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ زَكَاةَ
الْفِطْرِ طُهْرَةً لِلصَّائِمِ مِنْ اللَّغْوِ وَالرَّفَثِ وَطُعْمَةً
لِلْمَسَاكِينِ مَنْ أَدَّاهَا قَبْلَ الصَّلاةِ فَهِيَ زَكَاةٌ
مَقْبُولَةٌ وَمَنْ أَدَّاهَا بَعْدَ الصَّلاةِ فَهِيَ صَدَقَةٌ مِنْ
الصَّدَقَاتِ . " رواه أبو داود بِإِسْنَادٍ حَسَنٍ .
Kutoka
kwa Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhuma) ambaye amesema: "Mtume
amefaridhisha Zakaatul-Fitwr kuwa ni twahara ya mwenye kufunga kutokana
na maneno ya upuuzi na machafu, na kulisha masikini. Atakayeitoa kabla
ya Swalah basi hiyo ni Zakaah iliyotakabaliwa, na atakayeitoa baada ya
Swalah basi hiyo ni Sadaqah miongoni mwa Sadaqah" [Abu Daawuud kwa isnaad iliyo nzuri].
Kwa hiyo ni waajib wako kuota Zakaatul-Fitwr maadam una uwezo na unajitegemea mwenyewe.
Kwa maelezo zaidi bonyeza kiungo kifuatacho upate kusoma mas-ala mbalimbali yanayohusu Zakaatul-Fitwr:
Na Allaah Anajua zaidi
No comments:
Post a Comment