Vipi Aswali Tarawiyh Akiwa Safarini?
SWALI:
Assalam
alaykum warahmatullah,baada ya salam ya kheri na baraka,nilikua naomba
kufaham namna ya kuswali taraweh nikiwa safarini,nawatakieni wepesi
katika kazi zenu,Allah awalipe pepo,amin
JIBU:
Sifa
zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote,
Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu
'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum)
na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Muislamu
anapokuwa safarini ameruhusiwa kupunguza Swalah zake za fardhi, kwa
hiyo hata Swalah za Sunnah anaweza kuziacha. Yote inategemea na hali
yake ilivyo huko safarini. Ikiwa unahisi kuwa huwezi kuswali basi ni
ruhusa kwako, ama ikiwa unao uwezo wa kuswali basi ni vyema kuzitekeleza
ili upate fadhila na thawabu zake.
No comments:
Post a Comment