Taratibu Za Ruqyah Na Yapasayo Kufanywa Kabla Ya Kusoma Ruqyah
SWALI:
Nimepitia
website yenu nzuri mashAllaah, Mungu awazidishie na kazi hiyo nzuri.
Tafadhali kuhusu suala la Rukyah, tafadhali nitumie utaratibu kamili,
yaani ayas na sura za rukyah zote na utaribu wa kuzisoma hizo sura. Pia
nielimishe vipi nitajiyarisha ninapo jisomea rukyah, yaani kuhusu udhu,
mavazi na kadhalika. Shukran
JIBU:
Sifa
zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote,
Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako hilo
kuhusu Ruqyah. Katika mas-ala ya Ruqyah zipo Aayah za kusomwa na mtu
mwenyewe za kutaka kinga kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) na
zipo zile za kumsomea mtu aliyekumbwa na jini au kufanyiwa sihri.
Ama njia ya kujikinga mwenyewe ni kuwa uwe unasoma Aayah zifuatazo asubuhi na jioni. Nazo ni kama zifuatazo:
- Al-Faatihah (Surah ya kwanza).
- Al-Baqarah (Aayah nne za mwanzo, Ayatul Kursiy na Aayah mbili baada yake na Aayah tatu za mwisho).
- Aal-‘Imraan (3: 1 – 2).
- Suratut Tawbah (9: 129 mara saba).
- Al-Israa’ (17: 110 – 111).
- Al-Mu’minuun (23: 115 – 118).
- Al-Hashr (59: 22 – 24).
- Al-Kaafiruun (109).
- Al-Ikhlaasw, al-Falaq na an-Naas (mara tatu tatu).
Ama kipengele cha pili cha kumsomea mwengine inafaa usome Aayah zifuatazo:
Mwanzo unaanza na A’udhu Billaahi minash Shaytwaanir Rajiym.
- Al-Faatihah (Surah ya kwanza).
- Al-Baqarah (ayah 1 – 5, 102, 163 – 164, 255, 285 - 286).
- Aal-‘Imraan (3: 18 – 19).
- Suratut al-A‘raf (7: 54 – 56, 117 - 122).
- Yunus (10: 81 – 82).
- Twaaha (20: 69).
- Al-Hajj (22: 19 – 22).
- Al-Mu’minuun (23: 115 – 118).
- An-Naml (27: 30 – 31).
- Asw-Swaaffaat (37: 1 – 10).
- Ad-Dukhkhaan (44: 43 – 48).
- Al-Ahqaaf (46: 29 – 32).
- Al-Fath (48: 29).
- Ar-Rahmaan (55: 33 – 36).
- Al-Hashr (59: 21- 24).
- Al-Jinn (72: 1 – 9,
- Al-Buruuj (85).
- Zilzalah (99).
- Al-Humazah (104).
- Al-Ikhlaasw, al-Falaq na an-Naas.
Ama
unapokuwa unasoma unafaa uwe twahara (nguo na mwili) na umejisitiri kwa
kujifunika vizuri sehemu zipasazo kusitiriwa na pia usome kwa
unyenyekvu.
Na Allaah Anajua zaidi
No comments:
Post a Comment