Saturday, 11 April 2015

Ishara Za Mtoto Wa Kiume Kubaleghe Na Nini Jukumu La Mzazi Kwa Hali Hiyo Ya Mwanae?


SWALI:
Ningependa kuuliza suala moja
Mimi nina mtoto wa kiume lakini bado hajabaleigh natakuka kujuwa kuna inshara ngani akibaeigh na vipi mtu utajuwa kama baleigh na vipi umafahamishe ili ajuwa kuwa keshakuwa mkubwa aanze kusali na kufunga naona kusaidiwa.
Muislamu mwenzenu


JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa muulizaji. Ishara ya kijana wa kiume kubaleghe ni kama zifuatazo:
  • Kumea nywele za kwapani.
  • Kubadilika kwa sauti yake na kuwa nene na nzito.
  • Kuota kwa mara ya kwanza na kutokwa na maji (manii).
  • Kufikia miaka kumi na tano (15).
Wazazi hawafai kungoja mpaka mtoto abaleghe ndio waanze kumwambia kuhusu Swalah na Funga. Bali malezi yanatakiwa yawe mazuri kuanzia anapoanza kujua na kufahamu mambo, kutofautisha baina ya baya na zuri, ukweli na uongo.
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anatuelekeza kuhusu malezi ya kiibada ya watoto wetu pale alipotufahamisha:
Waamrisheni watoto wenu kuswali wakiwa na miaka saba na wapigeni kwa kutoswali wakiwa na miaka kumi” (Abu Daawuud).
Na kufunga nayo ni hivyo hivyo wawe ni wenye kufundishwa na kuzowezeshwa kuanzia mtoto akiwa na miaka hiyo saba na Ibaadah nyingine ni hivyo hivyo.

No comments: