Mwenye Ugongwa Wa Ukimwi Anaweza Kufunga Ramadhaan?
SWALI
Assalaam aleykum wa rahmatullahi wabaraakat.Nduzanguni waislamu,shukrani sana kwenu kwa kuweza kuwasiliana nanyi na imetupa wingi wa elimu ambazo hatukuwa nazo.
swali langu ni.
-Kuna
ndungu wetu ambaye anaugua na huu ugonjwa wa ukimwi,alhamdulillah
ameweza kupata dawa.je, anaweza kufunga Ramadhani ama yumo katika
wangonjwa wasie funga kwa ajili ya afya zao?Ramadhaan Karim
JIBU:
Sifa
zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote,
Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum)
na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Swawm
katika hali ya ugonjwa inategemea uwezo wa mtu. Ikiwa ataweza kufunga
bila ya taklifu yoyote ya siha yake basi imewajibika kwake kufunga. Na
ikiwa hawezi kufunga kwa vile italeta madhara katika siha yake basi
atakuwa miongoni mwa waliopewa udhuru wa kutokufunga kutokana na kauli
ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) :
(Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine)) [Al-Baqarah:185]
Ni Rahma ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwamba Hamkalifishi mtu na jambo asiloliweza:
((Allaah
haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo. Faida ya
iliyoyachuma ni yake, na hasara ya iliyoyachuma ni juu yake pia)) [2: 286].
Atakalopasa
kufanya ni ima alipe siku za mbele ikiwa pia atakuwa na uwezo wa
kufunga bila ya kuathiri siha yake au kumfanyia taklifu, ikishindikana
itabidi alipe kafara kwa kulisha masikini mmoja kwa kila siku moja ya
Swawm. Na Anaweza kulipa ima kulisha maskini 30 siku mbali mbali au
kulisha wote kwa pamoja kwa maana wote 30 kwa siku moja. Vyovyote
atakavyofanya inajuzu kwani Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ‘anhu)
alifanya hivyo alipokuwa na umri mkubwa na aliposhindwa kufunga alilisha
masikini siku ya mwisho ya Ramadhaan.
Tunamuombea Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ampe shifaaun ya haraka.
Na Allah Anajua zaidi
No comments:
Post a Comment